Social Icons

Loading...

ASKARI ALIYEMUUA MWANDISHI DAUDI MWANGOSI ASHITAKIWA

Baada ya kelele nyingi za vilio vya huzuni na simanzi na sauti ya utetezi kwa damu isiyo na hatia ya mwandishi  Daudi Mwangosi wa kituo cha Channel 10. Mauaji hayo yalitokea katika kijiji cha Nyololo, Iringa wakati wa amshaamsha  na shamra shamra za ufunguzi wa ofisi ya CHADEMA. Jana Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia mwenye namba G2573 Bw. Pasificus Cleophace Simon (miaka 23) alisomewa mashtaka ya mauaji ya kukusudia na mwendesha mashtaka mkuu wa serikali Michael Luena mbele ya Hakimu mkuu mwandamizi wa mahakama ya hakimu mfawidhi wa wilaya ya Iringa Bw. Dyness Lyimo.
Alishtakiwa kwamba mnamo tarehe 2/9/2012 katika kijiji cha Nyilolo, Mufindi, Iringa mtuhumiwa alimuua mwandishi Daudi Mwangosi akiwa kazini kutekeleza jukumu la kuuhabarisha umma. Kosa hili ni kinyume cha kifungu cha sheria namba 148 (5A) (i) cha makosa ya jinai. Mtuhumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ya mauaji. Mtuhumiwa amerudishwa mahabusu kutokana na kesi hii kuwa haiwekewi dhamana.
Askari Pasificus Simon aliyeshikilia bunduki akimwelekezea mwandishi Duadi Mwangosi alianguka chini na kuzingirwa na maaskari wengine na muda mfupi. Askari huyo alilipua bunduki na kumwua mwandishi Mwangosi.
Barua ya waziri wa mambo ya ndani ya nchi kuhusu kushtakiwa kwa askari Pasificus Simon
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top