Viongozi zaidi ya sabini wakiwamo wakuu wa nchi na Serikali
wanatarajiwa kushiriki hatua mbalimbali za safari ya mwisho ya Mzee
Mandela aliyefariki Alhamisi ya Desemba tano usiku.
Anatarajiwa kuzikwa Jumapili ijayo, Desemba 15,
2013 katika Kijiji cha Qunu alikokulia, mazishi ambayo yanatarajiwa
kuwavuta maelfu ya watu kutoka kona mbalimbali za dunia.
Hata hivyo hadi jana maofisa wa Serikali ya Afrika
Kusini walisema walikuwa bado hawajapata orodha kamili ya viongozi wote
watakaohudhuria, l pia wakashindwa kusema iwapo Rais Obama atakwenda
Qunu au atashiriki katika hatua nyingine za awali za msiba huo kabla ya
mazishi ya Jumapili.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Jay Carney
alinukuliwa akithibitisha kwamba Obama na mkewe Michele watashiriki
katika msiba huo lakini hakuwa tayari kueleza suala hilo kwa undani.
Habari zaidi zilizopatikana jana mjini Johanesburg zinasema Rais wa
Brazil, Dilma Rousseff atakuwa miongoni mwa wageni mashuhuri
watakaoshiriki.
Balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini, anasema kuwa: “Rais Obama, amethibitisha kushiriki mazishi ya Madiba” (akirejea) jina maarufu la Mzee Mandela, taarifa ambayo ilitiliwa na nguvu na habari zilizoinukuu Ikulu ya Washington ikithibitisha ujio wa kiongozi huyo pamoja na watanguliza wake; George W. Bush na Bill Clinton.
Post a Comment