Mtoto wa miaka minne ambaye ni raia wa Uingereza, Elliott Prior
ameonyesha ushujaa wa hali ya juu baada ya kuweza kuwatolea maneno
makali na ya kugusa magaidi waliovamia jengo la maduka la Westgate.
Baada ya maneno hayo, baadhi ya taarifa
zilizochapishwa kwenye vyombo mbalimbali vya kimataifa, vinasema magaidi
hao waliomba mtoto huyo awasamehe kwa maelezo kuwa wao siyo watu
wabaya.
Inaelezwa kuwa, kitendo cha mtoto huyo kilikuwa
cha kishujaa kwani aliweza kuwaeleza magaidi hao maneno hayo, bila
kuogopa silaha nzito walizokuwa wameshika mkononi huku baadhi ya watu
wakiwa wameshauuawa.
Mtandao wa Daily Mail unasema mtoto huyo alimwambia mmoja wa magaini hao kuwa ‘Nyie ni watu wabaya sana’.
Mtandao huo unasema mtoto huyo aliyasema maneno
hayo kama njia ya kumkinga mama yake Amber, aliyekuwa amepigwa risasi
mguuni pamoja na dada yake Amelie, mwenye umri wa miaka sita ambaye
walikuwa wote ndani ya duka hilo.
Chanzo : http://www.mwananchi.co.tz/habari/habari-ya-ndani/Nyie-ni-watu-wabaya--Mtoto-wa-miaka-4-awaambia-magaidi/-/1724700/2007674/-/rejief/-/index.html
Chanzo : http://www.mwananchi.co.tz/habari/habari-ya-ndani/Nyie-ni-watu-wabaya--Mtoto-wa-miaka-4-awaambia-magaidi/-/1724700/2007674/-/rejief/-/index.html
Post a Comment