Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Margaret Thatcher (87), amefariki dunia jana jijini London.
Watoto wa Thatcher, Mark na Carol walitangaza kuwa mama yao alifariki kutokana na kuugua maradhi hayo ghafla. Mwanamke huyo aliongoza chama chake cha Conservative katika chaguzi tatu na mara zote hizo kiliibuka na ushindi.
Akiwa mwanamke wa kwanza kuongoza chama kikubwa cha siasa Uingereza, alipenda kuwakosoa wanaharakati wengi akiwaambia kuwa vita ya haki za mwanamke, ilikwishamalizika na wanawake wameshinda.
Thatcher, ambaye ni mwanamke pekee kushika
nafasi hiyo Uingereza, alifariki dunia katika Hoteli ya Ritz alipokuwa
akiugulia. Habari zilizopatikana jana zimeeleza kuwa Thatcher alifariki
dunia kutokana na kuugua ghafla ugonjwa wa kiharusi jana asubuhi
nyumbani kwake.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameroon
alitangaza msiba huo akimtaja Thatcher kwamba alikuwa kiongozi shupavu,
Waziri Mkuu shupavu na mwana Uingereza shupavu.
Watoto wa Thatcher, Mark na Carol walitangaza kuwa mama yao alifariki kutokana na kuugua maradhi hayo ghafla. Mwanamke huyo aliongoza chama chake cha Conservative katika chaguzi tatu na mara zote hizo kiliibuka na ushindi.
Alishika wadhifa wa Uwaziri Mkuu kwa miaka 11 kuanzia Mei 1979 hadi Novemba 1990.
Alikubalika kwa mawazo yake bora ya kujenga uchumi, ndani na nje ya Uingereza. Pia alisifika kwa msimamo wake hasa wa kusonga mbele na kutoyumbishwa na kauli za kukata tamaa. Hata hivyo, wapinzani wake waliziita sera zake kuwa ni za kikatili ambazo zilikuza wigo kati ya wenye nacho na wasionacho.
Alikubalika kwa mawazo yake bora ya kujenga uchumi, ndani na nje ya Uingereza. Pia alisifika kwa msimamo wake hasa wa kusonga mbele na kutoyumbishwa na kauli za kukata tamaa. Hata hivyo, wapinzani wake waliziita sera zake kuwa ni za kikatili ambazo zilikuza wigo kati ya wenye nacho na wasionacho.
Akiwa mwanamke wa kwanza kuongoza chama kikubwa cha siasa Uingereza, alipenda kuwakosoa wanaharakati wengi akiwaambia kuwa vita ya haki za mwanamke, ilikwishamalizika na wanawake wameshinda.
Aliiongoza Uingereza katika vita dhidi ya
Argentina kugombea Visiwa vya Falklands pia katika kipindi cha vita
baridi kulipokuwa na msuguano kati ya mataifa ya Magharibi na yale ya
Mashariki.
Akiwa Waziri Mkuu aliwahi kunusurika kuuawa kwa bomu jijini London.
Thatcher alizaliwa Oktoba 13, 1925 hukoa Grantham, Uingereza na alijitosa rasmi katika siasa mwaka 1948.
Chanzo gazeti la mwananchi

Post a Comment