Wamiliki wa vituo vya utangazaji vya televisheni
nchini, wamesema watasitisha kurusha matangazo ndani ya mwezi mmoja
kuanzia sasa kutokana na kushindwa kumudu gharama za uendeshaji.
Hatua hiyo inatokana na Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) kuzima mitambo ya analojia na kuhamia dijitali Desemba
31, mwaka jana kitendo walichodai kimepunguza mapato yanayotokana na
matangazo.Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya
Habari Tanzania (Moat), Reginald Mengi alisema hakuna haja ya kurusha
matangazo kwa hasara.Mengi alisema kutokana na kuanza kwa mfumo wa
dijitali, watangazaji wamesitisha kutoa matangazo kwa sababu wananchi
wengi hawana ving’amuzi.
“Kama mamlaka itashindwa kurudisha ule mfumo
wa analojia kuwa sambamba na dijitali hadi wananchi watakapokuwa na
ving’amuzi, tutazima televisheni zetu ndani ya mwezi mmoja ujao,”
alisema Mengi.
“Ibara ya 18 ya Katiba imekiukwa kutokana na wananchi kunyimwa fursa ya kupata habari, hivyo hali hii hatutaki iendelee,” alisema Mengi.
Mengi ambaye pia ni mmiliki wa vituo vya
televisheni vya ITV, EATV na Capital TV, alisema licha ya nchi za
Afrika, Tanzania imekuwa ya kwanza kuzima mitambo ilhali wananchi
hawakuwezeshwa kumudu gharama za ving’amuzi.“Nchi ambazo zimeendelea kwa kila kitu kama
Uingereza, Marekani, Japan na kwingineko kuzima mitambo ya analojia
walitumia zaidi ya miaka minane kwa nini sisi tumewahi hivi wakati
hatujajipanga?” alihoji Mengi.
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/-/1597570/1717682/-/y1r7nm/-/index.html
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/-/1597570/1717682/-/y1r7nm/-/index.html
Post a Comment