Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema
haitarudi nyuma kwenye suala la kutumia mfumo wa matangazo kupitia njia
ya dijitali na kwamba mfumo huo utaendelea kutumika.
Kauli ya TCRA imekuja siku moja baada ya
wamiliki wa vituo vya utangazaji vya televisheni nchini kutishia
kusitisha kurusha matangazo ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa kutokana
na kushindwa kumudu gharama za uendeshaji.Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya
Habari Tanzania (Moat), Reginald Mengi juzi alisema hakuna haja ya
kurusha matangazo kwa hasara kwani watangazaji wamesitisha kutoa
matangazo kwa sababu wananchi wengi hawana ving’amuzi. Licha ya Moat
kutoa kauli hiyo juzi, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA), Profesa John Nkoma alisisitiza kwamba TCRA haiwezi kurudi nyuma
katika suala hilo kwani mfumo huo utaendelea kutumika.
Akizungumza Dar es Salaam jana kwenye warsha
ya mambo ya mionzi, alisema wao kama TCRA hawawezi kurudi nyuma katika
suala hilo na kwamba msimamo wao wa kuendelea kutumia mfumo wa matangazo
kwa njia ya dijitali upo palepale.
Chanzo Mwananchi
Post a Comment