Rais wa China, Xi Jinping aliwasili nchini jana saa 10:5
akitumia ndege Boeng 747 ya Shirika la Ndege la China na leo atazungumza
kwa mara ya kwanza na Afrika akitumia jukwaa la Tanzania.
Jinping atatoa hotuba yake kwenye jengo jipya la
kisasa la Mwalimu Nyerere ambalo limejengwa na Serikali ya China likiwa
na uwezo wa kuchukua watu 1,800 kwa mara moja lilipo jijini.Rais huyo ambaye ameambatana na mkewe pamoja na
maofisa mbalimbali wa Serikali yake,anatajiwa kutambulisha sera kwa Bara
la Afrika huku wachunguzi wa mambo wakisema kuwa hotuba yake hiyo
huenda itazingatia juu ya uimarisha uhusiano mwema baina ya pande zote
mbili.
China ndiyo dola inayotajwa kuwa na ushawishi
mkubwa barani Afrika na katika kipindi cha muongo mmoja uliopita kiwango
cha ufanyaji biashara baina ya pande hizo mbili kinatajwa kukua kwa
asilimia 70. China pia ndiyo mshirika pekee kwa Afrika ambaye misaada
yake inaambatana na masharti nafuu.
Hata hivyo ushawishi wa China barani Afrika
unakosolewa na baadhi ya nchi za Magharibi zinazoituhumu China kwamba
inazinyonya nchi za Afrika.
Alipowasili jana kwenye Uwanja wa Kimataifa wa
Mwalimu Nyerere, Rais huyo alipokewa na mwenyeji wake Rais Jakaya
Kikwete na kisha alipigiwa mizinga 21 na baadaye alikagua gwaride. Baada
ya mapokezi hayo ya uwanjani, Rais Jinping na mwenyeji wake walioogoza
kwenda jijini ambapo jioni ya jana walikuwa na mazungumzo ya faragha na
baadaye walijumuika na halaika kwa ajili ya kushiriki dhifa ya taifa.
Taarifa kwa hisani ya : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1729660/-/128rxxi/-/index.html
Taarifa kwa hisani ya : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1729660/-/128rxxi/-/index.html
Post a Comment