Social Icons

Loading...

Yanga yaifunga Azam, SIMBA yafungwa na MTIBWA.

Kikosi   cha  Yanga  kilichoifunga  Azam  2 -0,  magoli  yaliyofungwa  na  Didier  Kavumbangu na  Hamis  Kiiza.

Yanga  ilmewakilishwa 
Ally Mustafa Barthez, Mbuyi Twite, Oscar Joshua, Naroub Cannavaro, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza na Haruna Niyonzima.



Kikosi   cha    Azam  FC.
Azam  imewakilishwa  na   Mwadini Ali, Erasto Nyoni, Ibrahim Shikanda, Aggrey Morris, Said Morad, Kipre Balou, Salum Abubakar, Jabir Aziz, John Boko, Kipre Tchetche, Hamis Mcha ‘Viali’.

Nako  huko   Morogoro.
Kutoka mjini Morogoro Simba ya jijini Dar es Salaam leo imejikuta ikiangukia pua baada ya kuchapwa bao 2-0 na Mtibwa Sugar, mchezo litawaliwa na rabsha za mara kwa mara kutoka kwa mashabiki wa Simba waliokuwa na hasira wakidai mwamuzi Judith Gamba, alikuwa hawatendei haki.
Mtibwa ilijipatia bao dakika ya 34, kwa bao lililofungwa na Mohamed Mkopi baada ya Kipa Juma Kaseja kutema shuti kali la Vicent Barnabas.

Dakika ya 87, mshambuliaji mahiri Hussein Javu, aliipatia Mtibwa bao la pili, baada ya Kaseja kufanya mbwembwe langoni mwake.
Baada ya mchezo kumalizika, Kaseja aliangua kilio uwanjani huku mashabiki wakimzonga.
Wachezaji wa Simba waligoma kupanda basi lao, ambako baadhi ya viongozi wao walifanya kazi ya ziada kuwabembeleza, ambako walikubali kwa shingo upande, lakini baada ya muda Mrisho Ngasa alishuka akiwa kabadilisha nguo kuondoka kivyake huku akisindikizwa na mashabiki lukuki.
Kwa matokeo ya mechii za leo, Yanga imekamata usukani rasmi ikiwa na pointi 26 huku Simba ikibaki na pointi zake 23 wote wakiwa na michezo 12 huku Azam ikiwa nafasi ya tatu kwa pointi 21 huku Mtibwa ikifikisha pointi 13. 

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top