Social Icons

Loading...

MNYAMA ANG'ANG'ANIWA, POLISI NGOMA BADO MBICHI


SIMBA ASHINDWA KUUNGURUMA, ALEWESHWA NA SUKARI YA KAGERA

KIKOSI CHA "WEKUNDU WA MSIMBAZI" SIMBA SC
Ndoto za machampioni wa kandanda nchini Simba kuendeleza ushindi kwa 100% zimeanza kufifia baada ya kung'ang'aniwa na watengeneza sukari wa Kagera Sugar wanaofundishwa na kinara wa zamani  "King Mputa" Kibaden.  Mshambuliaji wa Simba Felix Sunzu alikuwa wa kwa kwa kuwaandikia machampioni hao bao katika kipindi cha kwanza kwa bao la kichwa. Katika dakika ya 51 kipindi cha pili kiungo mshambuliaji MRISHO NGASA aliwainua wanaMsimbazi kwa kuandika bao maridadi lililoonekana kuwapa faraja Simba kuwa wataibuka na ushindi kumbe walikuwa wamtangiulia kwa baiskeli ya miti.

Kagera Sugar waliongeza kasi na kuanza kuchezea sharubu za "Mnyama" kwani katika Dakika ya 63 piga nikupige langoni mwa Simba ilimpa nafasi Themi Felix kutikisa nyavu za Simba. Na kwa kasi hiyo hiyo  Kagera wakapata penati na Salum Kanoni akaifungia bao la 2 na hivyo kuwakimbiza uwanjani mapema mashabiki wa Simba.

Beki wa Simba Nasoro Masoud Chollo alipata maumivu na kufungwa kitambaa kichwani baada ya kugongan na mshambuliaji wa Kagera Sugar.

Wakati huo huo; Azam FC na Tanzania Prisons wametoka sare ya bila kufungana. Vijana wa Prisons itabidi wajilaumu kwa kushindwa kutikisa nyavu za wauza lamblamba katika uwanja wao wa Sokoine, Mbeya.
Hivyo Simba wameendelea kushika usukani wa ligi kuu ya VODACOM , Tanzania Bara.

Maafande wa Polisi Morogoro wameendelea kupata kichapo kwa kufungwa na JKT Ruvu kwa mabao 2 kwa 0. Hivyo Polisi Morogoro kuendelea kuburuza mkia kwa kuwa wa mwisho na pointi zao 2.

Maafande wa Mgambo JKT ya Tanga wamesasambua vilivyo Toto African kwa mabao 2 yaliyofungwa na Salum Madanga na bao la pili dak 62 na Dickson odhiambo. Mgambo JKT sasa wanafikisha pointi 10 sawa na ndugu zao wa Coastal Union.

Wakati huo huo, Mchecheto wa mechi kati ya Yanga na Ruvu shooting umeshika kasi pale ambapo Ruvu Shooting wamewasimamisha wachezaji wao wanne akiwamo Hussein Swedi ambayekasimamishwa kwa miezi miwili, kapewa onyo la maandishi na atapelekwa katika kikosi cha pili cha U20, wakati Benjamin Haule kapewa onyo la mdomo na ametakiwa kujirekebisha kwa wiki 2, Ponda Uka yeye amefungiwa kwa makosa ya kutoroka kambini, kusema uongo na kutokuwa mwaminifu.



author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top