Mamlaka ya
Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imesema, meli
iliyozama jana katika kisiwa cha Chumbe, Zanzibar ilikuwa na abiria 248
wakiwemo watoto 31.
Kwa
mujibu wa Sumatra, meli hiyo, inamilikiwa na Kampuni Seagul Transport,
imasajiliwa na Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) na kwamba,
Cheti cha Ubora kimeanza tarehe 24 Agosti, 2011 na kinamalizika 23
Agosti, 2012. Imesema, meli hiyo ilikuwa imeruhusiwa kubeba abiria
wanaoruhusiwa 300 na tani 26 za mizigo.
SUMATRA
kupitia Kituo cha Utafutaji na Uokoaji (MRCC) ilipata taarifa kuwa meli
ya MV Skagit iliyokuwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea Zanzibar
ilikuwa inazama katika eneo la karibu na kisiwa cha Chumbe, Zanzibar,
eneo ambalo lipo umbali wa Kilomita za Bahari 13.8 kutoka Bandari ya
Zanzibar.
Zoezi
la uokoaji linaendelea katika eneo la tukio kutoka kwa Mv Flying Horse,
Mv Kilimanjaro III, Tug Bandari ya Zanzibar, KMKM, Mv Zanzibar I,
Police Patrol Boat, Navy.
Source: Mjengwa blog
Waokoaji wakiwa kazini kwenye Meli ya Kilimanjaro
Raia wa kigeni wakiwasili Bandarini baada ya kuokolewa
Hapa ikiwa Dar es Salaam tayari kuelekea Unguja.
Meli ya MV SEAGULL iliyozama na abiria wanaokadiriwa kufikia 250 inavyoonekena ikipakia abiria Dar.
Hapa ikiwa Dar es Salaam tayari kuelekea Unguja.
Post a Comment