![]() | |
Mch: Gwajima |
Sintofahamu katika Sakata ya issue ya Dr. Ulimboka imechukua
sura mpya Baada ya Siku ya Ijumaa Jeshi la Polisi kujitokeza kwenye vyombo vya
habari na kueleza Kuwa Mtuhumiwa wa Sekeseke la kumkamata na Kumtesa Dr.
Ulimboka amekamatwa baada ya kwenda katika kanisa la Ufufuo na Uzima lililo
chini ya Mch. Gwajima, Mchungaji huyo wa Kanisa hilo amefunguka siku ya jana na
kueleza kuwa “Joshua The Kenyan” hakuwahi kwenda kwenye Kanisa hilo na wala
Kanisa halina Utaratibu wa Kuungama kwa kusema dhambi.
Taarifa zilizotolewa juzi na kuibua maswali katikati ya
Jamii ya Watanzania hususan Wakristo waliozipokea taarifa hizo kuwa Mtuhumiwa
huyo aliyefikishwa kizimbani siku ya Ijumaa Asubuhi Mr. Joshua Mulindi Kwa maelezo ya Kova anafanya
kazi chini ya kundi la Gun Star lililo chini ya Mkuu wa Kundi hilo Bw. Silence
kutoka Nchini Kenya Walikuwa Wamekodiwa kuja Tanzania na Kigogo Mmoja kuja
nchini kwa kazi moja ya Kutoa uhai wa Dr. Ulimboka na zoezi hilo kushindikana,
ndipo kijana huyo wa Kikenya alikwenda kunako kanisa la Pastor Gwajima na
Kukiri kuhusika na sakata zima la Dr. Ulimboka.
![]() | |
Kamanda Kova akitoa maelezo kuhusiana na kukamatwa kwa Joshua Mulindi |
Siku Ya Jana Mch. Gwajima amefunguka na kuruka Kimanga
kuhusu sakata hilo na kutaka Kanisa hilo lisihusishwe na Sakata la Dr. Ulimboka
sababu huyo mtu mwenye jina la Joshua kutoka nchini Kenya hajawahi kutubu
kwenye Kanisa hilo na kueleza kuwa Kanisa lake halina utaratibu wa Kuungama kwa
Kusema dhambi za waumini kama ilivyo katika Makanisa mengine hususan RC
(Kuungama).
Mch. Huyo ambaye anaamini ana mahasimu wengi katika Gospel
ameenda mbali zaidi na kusema kama Mkenya huyo ameeleza hayo basi atakuwa
ametumwa na baadhi ya Watu wasioitakia mema huduma hiyo maarufu kwa kurejesha
Misukule hapa Tanzania.
Source : http://samsasali.blogspot.com/2012/07/liwalo-na-liwebaada-ya-jeshi-la-polisi.html
Post a Comment