Naibu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) ambaye amemaliza muda wake, Dk.
Asha Rose Migiro, amerejea nyumbani jana na kusema kwamba anatarajia
kurudi kufundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - UDSM ambako alikuwa
akifundisha kabla ya kuingia kwenye ulingo wa siasa.
Kinyume
na matarijio ya watu wengi, Dk. Migiro amesema kuwa kwa sasa hatarajii
kujishughulisha katika mambo ya siasa na wala hana mipango ya kugombea
urais siku za mbele.
Amesema
kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amamteua kuwa Balozi
Maalum wa Malaria katika Bara la Afrika na kuongeza kuwa pamoja na
kwamba shughuli hizo atakuwa anazifanya kwa muda wake mchache, bado kuna
uwezekano mkubwa zikambana na kushindwa kujishughilisha na mambo ya
kisiasa.
Post a Comment