Social Icons

Loading...

Kibonzo


Kitaifa Dk Mvungi afariki dunia.

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi (61) amefariki dunia katika Hospitali ya Millpark Netcare, Johanesburg, Afrika Kusini.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana kutoka Afrika Kusini na kuthibitishwa na Msemaji wa Hospitali ya Millpark, Tebogo Nyembezi zinasema Dk Mvungi alifariki dunia jana mchana. “Ni kweli tulimpokea mgonjwa huyo kutoka Tanzania na alifariki 6:00 mchana (saa 7:00 kwa saa za Afrika Mashariki),”alisema Nyembezi.
Nyembezi alisema kwamba walimpokea mgonjwa huyo akiwa na majeraha ya kichwa, lakini aliahidi kueleza sababu ya kifo chake leo baada ya kuzungumza na madaktari waliokuwa wakimtibu.Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba pia alithibitisha kupokea taarifa za kifo hicho na kwamba walikuwa wakiendelea kuandaa taratibu za kuleta mwili wake nchini.
“Ni pigo kubwa kwetu, tunaangalia namna ya kuusafirisha kuja nchini na baadaye tutatoa taarifa rasmi,”alisema Jaji Warioba na kuongeza:
“Kwa kweli ni pigo kubwa siyo kwetu tu, lakini pigo kubwa kwa nchi yetu, tumepoteza mtu muhimu na kiungo muhimu sana. Dk Mvungi, wengine tulimfahamu tangu alipokuwa mwanafunzi, alikuwa mtu aliyesema kile alichokiamini, akikwambia kitu kilikuwa ni kile kilichopo moyoni mwake”.
Soma  zaidi  : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Dk-Mvungi--afariki-dunia/-/1597296/2070966/-/8ldfu2/-/index.html

JK: Hatutoki Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Rais Jakaya Kikwete amesema Tanzania haitajitoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), licha kuwapo kwa vitendo alivyoviita vya ubaguzi vinavyofanywa na wakuu wa nchi za Uganda, Kenya na Rwanda.Rais Kikwete akilihutubia Bunge jana mjini Dodoma alifichua kwamba sababu kubwa ya viongozi hao kuonekana kama wanaitenga Tanzania ni msimamo wake kuhusu masuala ya Shirikisho la Kisiasa, Uhamiaji, Ardhi na Ajira.
Rais alikuwa akirejea matukio ya hivi karibuni ya marais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Uganda, Yoweri Museveni na Rais wa Rwanda, Paul Kagame kukutana na kujadiliana kuhusu masuala kadhaa yanayohusu EAC bila Tanzania kuwapo.
“Hatuna mpango wa kuondoka, tupo na tunaendelea kuwepo na napenda niwahakikishie kwamba Tanzania haijafanya jambo lolote baya kwa jumuiya yetu au kwa nchi mwanachama mmoja mmoja na tumekuwa waaminifu na watiifu kwa jumuiya wakati wote,”alisema Rais Kikwete.
Aliwashutumu viongozi wao akisema kuwa kauli zao kwamba wanakutana kwa sababu wako tayari ni za kibaguzi kwani katika mikutano yote waliyoifanya Entebbe nchini Uganda, Mombasa – Kenya na Kigali nchini Rwanda hawakuwahi kuialika Tanzania.
“Hali hii haijawahi kuwapo na ni kwa mara ya kwanza tunaanza kuwa na makundi ndani ya jumuiya yetu; huku Kenya, Uganda na Rwanda, kule Tanzania na Burundi,”alisema Kikwete katika hotuba yake iliyochukua saa1:15 na kuongeza:
“Ikiwa itakuja kutokea jumuiya ikadhoofika au ikafa, Mungu apishilie mbali Tanzania isije ikanyooshewa kidole kwamba ndiyo chanzo cha kudhoofika huko au kufa huko”.
Alisema ataendelea kuzungumza na viongozi wa nchi hizo, na kwamba tayari ameanza ili kuhakikisha utekezaji wa mambo yote ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki unafanywa kwa kuzingatia mkataba ulioanzisha jumuiya hiyo.Rais Kikwete alisema kwa mujibu wa mkataba huo mambo yote yanapaswa kutekelezwa kwa kuzingatia kalenda ambayo inaweka bayana mambo hayo kuwa ni Umoja wa Forodha, Soko la Pamoja, Umoja wa Sarafu na hatimaye Shirikisho la Kisiasa.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/JK--Hatujitoi/-/1597296/2064458/-/jxdhd2/-/index.html
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top