Social Icons

Loading...

MSAMA AIPONGEZA BASATA KWA KUANZISHA MAFUNZO YA SANAA KWA WATOTO .

 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo ya sanaa kwa watoto yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Basata na kudhaminiwa na Kampuni ya Msama Promotions. Kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza na Ofisa Tawala wa Kampuni ya Msama Promotions, Hamis Mussa.
 
MKURUGENZI wa Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama amepongeza hatua ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kuanzisha mafunzo maalumu kwa watoto wa shule za msingi.
 
Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa kufunga mafunzo maalumu
yanayolenga kuwajenga watoto katika fani ya sanaa na kushirikisha watoto wapatao 200 kutoka shule tano za wilaya ya Ilala, Msama alisema ni jambo zuri kuandaa vipaji vya kesho.
 
Mafunzo haya yataweza kuwajenga watoto wetu ambao ndio taifa la kesho, pia kupunguza tatizo la watoto kujiingiza katika mambo mabaya kama matumizi ya bangi, dawa za ulevya, hivyo kuwa mzigo na janga kwa taifa,” alisema Msama.
 
Shule zilizonufaika na mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Msama kupitia
kampuni yake ya Msama Promotions, waratibu wa Matamasha ya Pasaka na Krismas, ni Buguruni Moto, Buguruni Visiwi, Ilala Boma, Uhuru Wasichana na Msimbazi.
 
Aidha, Msama alihimiza umuhimu wa somo la sanaa shuleni akitaka lipewe msisitizo mkubwa katika kuandaa vijana bora ambao hata kama wakifeli masomo mengine, wanaweza kuwa wasanii bora. “Somo hili la sanaa mashuleni lipewe uzito unaostaili kama masomo mengine kwa sababu, mtoto akifeli masomo mengine, fani ya sanaa yaweza kuwa msaada kwake,” alisema.
 
Msama aliwashauri pia Basata kuyapeleka mafunzo hayo hadi mikoani na
kupendekeza kwa hatua ya awali waanzie katika mikoa ya Pwani na Morogoro, akiamini kuna vipaji vingi vya sanaa.
 
Naye Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza alisema mafunzo hayo yaliyoanza Machi 1, wanafunzi walikuwa wakifanya mazoezi ya sanaa katika fani utambaji, hadithi, ngoma za asili na maigizo katika maeneo ya shule zao chini ya usimamizi wa walimu wao na waratibu kutoka Basata.

Mngereza alimshukuru mgeni rasmi Msama kwa kudhamini mafunzo hayo
akisema amefanya hivyo kwa kutambua umuhimu wa elimu ya sanaa katika maisha ya kila siku.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top