Kampuni ya UCC leo imefanya kikao cha 21 cha wafanyakazi wote , mkutano umefanyika katika ukumbi wa Nyerere Theater One - UDSM.
Sehemu ya umati wa wafanyakazi ukifuatilia kikao hicho kwa umakini.
Aliyeketi ni Mama kipenzi cha wana UCC,asiye na makuu ,mwingi wa upendo Mrs Calista Duwe - SPO akiweka makabrasha ya kikao vizuri, waliosimama toka kushoto ni Nongwa, Blogger ,Shomary na Bashosho.
Kazi na dawa, kinywaji nacho kilikuwa sehemu ya mkutano ili kulainisha makoo, wadau wa mkutano wakifuatlia ajenda moja baada ya nyingine,
Sehemu ya umati wa wafanyakazi ukifuatlilia kikao.
Sehemu ya umati huu ukisikiza mengineyo mkutanoni.
Duu vinywaji Jaloo, baada ya kikao vimebaki , shoo hii ya refreshment ilisimamiwa na wadau hao watatu pichani, hongereni sana kwa kuhudumia mkutano.
Ndg: John Haule ( wapili toka kulia) mkongwe akifafanua jambo kwa vijana baada ya kikao , wengine kutoka kulia ni Ndg: Gideon , Bigeni, Asante na Blogger kwa mbali kama vile anataka kurudi ni Ms Rehema Shao nadhani alikuwa anaelekea dirishani kwa Mzee Kisabo.
Duu baada ya kikao kama kawaida ya vikao ni kusaini dirishani kwa Mzee KISABO , wadau wakiwa katika line kupokea shekeli .
Post a Comment