Loading...
Home » Archives for April 2014
CARS FOR SALE - AT A THROW AWAY PRICE
TWO CARS FOR SALE ...
For serious buyer pls contact us via 0784717342 or mail:audaxmujun@yahoo.com;
1. A SUZUKI SWIFT IN AN IMACULATE CONDITION.
REGISTERED RECENTLY (APRIL 2014)
YEAR:2004
CC:1320
PRICE: 7.5M NEGOTIABLE
===========================================================================
2. AN IST CAR (ATTACHED) IN AN IMACULATE CONDITION, AT A THROW AWAY PRICE.
REGISTERED RECENTLY (MARCH 2014)
YEAR:2004
CC:1300
PRICE: 9.5M NEGOTIABLE
FOR SERIOUS BUYER KINDLY CONTACT us via 0784717342
mail:audaxmujun@yahoo.com;
on
PLUIJM ,TAMBWE WAKAMIANA .
Kocha wa Yanga, Hans van Pluijm na mshambuliaji wa Simba, Amis Tambwe kila moja amejigamba kuhakikisha klabu yake inamaliza msimu kwa kupata ushindi katika mchezo wa mwisho baina ya timu hizo.
Kocha huyo Mholanzi ameipongeza Azam kwa kutwaa
ubingwa na kusema waliweka changamoto na presha kubwa hasa katika mechi
zao za mwisho ambazo wote walikuwa wakipambana bega kwa bega kuusaka
ubingwa.
Pluijm alisema anaipongeza Azam kwa kutwaa ubingwa
huo na kudai mechi tatu ziliwaharibia baada ya kutoka katika michuano
ya kimataifa.
“Hatuwezi kulaumiana kwa sasa, tunawapongeza Azam
kwa ubingwa, lakini uzembe wetu umetugharimu kwa kushindwa kutumia
nafasi tuliyokuwa nayo hasa baada ya kutoka katika Ligi ya Mabingwa
Afrika.
“Tulikuwa na michezo mingi mkononi kuliko
wapinzani wetu, lakini tukashindwa kujipanga jambo ambalo lilitugharimu
na kufanya tucheze kwa presha kubwa mechi za mwishoni ili kuusaka
ubingwa, lakini tambua kila timu ilijipanga hivyo tunakubali matokeo,”
alisema.
Pluijm alisema sasa hivi wanaangalia mechi yao ya
mwisho dhidi ya Simba ili waweze kuibuka na ushindi na kujipanga kwa
ajili ya msimu ujao na Kombe la Shirikisho.
“Tuko Moshi leo (jana) tuna mechi ya kirafiki na
baada ya hapo tutarudi Dar es Salaam kuweka kambi kwa ajili ya mechi ya
mwisho ya ligi dhidi ya Simba Jumamosi, naamini tutashinda mechi hiyo
na mambo mengine yatafuata,” alisema Pluijm.
Naye mshambuliaji wa Simba, Tambwe amekiri timu
yao haikuwa vizuri msimu huu, lakini hawatakubali kamwe wafungwe na
Yanga Jumamosi ili kuwafariji mashabiki wao.
on
BUNGE LA KATIBA LAOMBA KUONGEZEWA SIKU 60
Bunge Maalumu la Katiba limeomba kuongezewa muda wa siku 60
kuanzia Agosti 5, mwaka huu litakapokutana kwa ngwe ya pili.
Bunge hilo linahitimisha ngwe yake ya kwanza
Aprili 25, mwaka huu likiwa limekutana kwa siku 67, kati ya 70
zilizokuwa zimetengwa awali.
Kwa muda huo wa ziada 60, iwapo wajumbe wote 629
watalipwa posho ya Sh300,000 iliyopangwa kwa siku, jumla ya Sh11.322
bilioni za walipakodi zitatumika ukilinganisha na Sh13.209 bilioni
zilizotumika katika siku 70 za awali. Jumla ya fedha zote zitakazotumika
kwa posho ni Sh24.53 bilioni, bila kuingiza gharama nyingine nje ya
posho za wajumbe.
Jana, Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta
alitangaza kwamba shughuli za Bunge hilo zitakoma wakati wajumbe wake
watakapokwenda kusherehekea maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano, Aprili
26, mwaka huu.
Sitta alisema jana kwamba aliwasilisha maombi ya kuongezewa muda kwa Rais Jakaya Kikwete, ambayo yalikuwa hayajajibiwa.
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue alipoulizwa
jana alisema: “Mheshimiwa Rais (Kikwete) anachoafiki ni kama ambavyo
kila mtu anaona mwenendo wa Bunge ulivyo, kwamba siku 70 haziwatoshi,
hivyo alikubali kwamba wanahitaji kuongezewa muda. Ingawa mpaka sasa
hajaamua atawaongezea siku ngapi, atakapoamua tutawafahamisha tu.”
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick
Werema alisema upo uwezekano mkubwa wa Bunge hilo kuongezewa siku 60
lakini akaongeza kuwa hilo litategemea bajeti itakayoidhinishwa na
Serikali.i 5.
chanzo fungua link
chanzo fungua link
on
KWA HERI WINDOWS XP
Kampuni ya utengenezaji wa mitambo endeshi ya kompyuta (Operating
Systems) ya Microsoft ilisitisha utoaji wa huduma za muda mrefu kwa
mitambo ya XP, ni moja ya mitambo endeshi inayotumika na watu wengi
sana.Tangu kutoka kwa taarifa hizo, kumekuwa na maneno na mikanganyiko
mingi mno kwa wateja hususan hapa Tanzania.
Kwakuwa
ni mitambo inayotumika kwa weingi kwenye kompyuta nyingi zinazotumika
kwenye mabenki na maofisini, hivyo watu walifika mbali hata kusema eti
pesa zetu hazipo salama tena. Hivyo, ili kuondoa hofu hizi
zinazoizunguka jamii, ungana nasi Dudumizi kwenye kujua nini maana ya kikomo hiki cha huduma na jinsi gani kinaweza kuathiri biashara yako?
Kwanini XP imefikia kikomo?
XP
iliingia sokoni miaka 12 iliyopita, tangu kuingia kwake, imekuwa ni
mtambo endeshi unaotumika kwa wingi na makampuni mengi duniani kote. Na
pia ni moja ya mtambo endeshi kutoka Microsoft uliokaa kwa muda mrefu
sokoni. Ingawa katika uhai wa Windows XP, kumekuwa na matoleo mengine
mengi kama Windows Vista, Windows 7 na ya sasa ambayo ni Windows 8,
lakini kampuni ya Microfost imeendelea kutoka msaada wa kiufundi na
kimatumizi kwa wateja wake wote, hivyo kwa maneno mengine tunaweza
kusema,muda wake wa maisha umefika na ni mzigo kiutendaji na hata
kibiashara kwa Microsoft kuendelea kuhudumia Windows XP ndiyo maana
wameamua kusitisha huduma kwa Windows XP.
Je nini maana ya usisitshwaji wa Huduma?
Hapa
ndipo palitokea mkanganyiko miongoni mwa watu wengi, kusitishwa kwa
huduma hakumaanishi kuwa kompyuta zote zinazotumia XP hazitotumika tena
kama wengine walivyoifananaisha na uhamaji wa mitambo ya analog kwenda
Digital.
Kusitisha
kwa huduma kwa XP kunamaanisha, kampuni ya Microfot haitoendelea kutoa
huduma (Support) kwa watumiaji wa windows XP tena, huduma hizi ni kama
masasisho (updates) ya kiusalama, maboresho ya ufanyaji kazi (kama vile
XP SP1, 2..) na huduma nyongine za utumiaji.
Hivyo, unaweza kuendelea kuitumia XP bila shida kama una uhakika kukosa huduma hizo hakutoathiri biashara.
Je kama ninatumia Windows XP, kompyuta yangu itaendelea kutumika?
Jibu ni ndiyo ila kuwa makini. Kusitishwa kwa huduma kwa Windows XP hakumaanishi kuondolewa kwa XP toka kwenye kompyuta yako, bali ni kutoweza pata huduma, hivyo Windows iliyopo kwenye komputa yako itaendelea kutumika kama kawaida, ila kuanzia sasa uhakika wa usalama wako utaendelea kupungua siku hadi siku.
Jibu ni ndiyo ila kuwa makini. Kusitishwa kwa huduma kwa Windows XP hakumaanishi kuondolewa kwa XP toka kwenye kompyuta yako, bali ni kutoweza pata huduma, hivyo Windows iliyopo kwenye komputa yako itaendelea kutumika kama kawaida, ila kuanzia sasa uhakika wa usalama wako utaendelea kupungua siku hadi siku.
Chanzo mtandao wa dudumizi
on
MVUA ZALETA MAAFA DAR ES SALAAM.
Vifo, uharibifu wa mali, miundombinu na mafuriko, msongamano wa
magari, baadhi ya wakazi wa jiji hilo kukimbia makazi yao, wengine
kulala kwenye magari na nyumba za wageni vimewakumba wakazi wa Jiji la
Dar es Salaam na vitongoji vyake, kutokana na mvua zinazoendelea
kunyesha kwa siku ya nne mfululizo.
Uukoaji ukiendelea .
Sehemu ya barabara iliyoharibika katika Daraja la Mpiji kwenye barabara ya Dar es Salaam Bagamoyo
Timu ya waandishi wa gazeti hili walifanya
uchunguzi maeneo mbalimbali na kushuhudia hali halisi ilivyo, huku
wanawake na watoto wakionekana kupata shida zaidi kwa kukaa nje ya
nyumba zao, wengine kuhamia kwenye majengo ya shule.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam
alisema jana kuwa walikuwa wakiendelea kukusanya taarifa za maafa
ikiwamo vifo alivyosema ni vingi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik alisema kuwa yupo kwenye kikao na watatoa taarifa zaidi za maafa baadaye.
Kijana ambaye akufahamika jina lake akijaribu kuokoa maisha ya akina mama waliotaka kusombwa na mafuriko jijini Dar es salaam
Kijana ambaye akufahamika jina lake akijaribu kuokoa maisha ya akina mama waliotaka kusombwa na mafuriko jijini Dar es salaam
Tegeta, Boko na Bunju
Mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka minne,
amefariki dunia baada ya nyumba aliyokuwa akiishi kujaa maji na
kushindwa kujiokoa kutokana na ulemavu, wakati mama yake akiwa kwenye
shughuli za biashara.
Majirani wa mtoto huyo walisema tofauti na kawaida
yao kumtoa mtoto huyo mvua inaponyesha, jana walimsahau na mama yake
aliporejea alikuta maiti ya mtoto wake ikielea chumbani.
Katika mvua hizo takribani kaya 180 zimekumbwa na mafuriko huku wakazi wake wakijikuta hawana pa kwenda.
“Mimi nimekuwa hapa tangu Tanu imezaliwa, nyumba
yangu imejaa maji nimeshazeeka sina mtu wa kunisaidia, wala sijui wapi
nitakwenda. Nomba Serikali inisaidie,”alisema Hussein Ngaoma ambaye ni
mjumbe wa nyumba kumi katika eneo hilo.
Naye Husna Ally ambaye pia nyumba yake imekumbwa
na mafuriko alisema: “Nasikitika, maana nimepata hasara kubwa. Mimi ni
mfanyabiashara katika eneo hili la Boko, nina duka la kuuzia samani
limejaa maji na sijaweza kuokoa chochote. Mzigo wa Sh30 milioni
umeharibika wote.”
Jeti Lumo
Katika eneo hilo licha ya kujaa maji, mfanyabiashara ndogondogo amefariki dunia kwa kusombwa na maji Uukoaji ukiendelea .
on
RAIS KIKWETE AWA BORA AFRIKA
Rais Jakaya Kikwete amechaguliwa kuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa zaidi katika maendeleo barani Afrika kwa mwaka 2013.
Heshima hiyo kwa Rais Kikwete imetolewa na jarida
la kimataifa la African Leadership Magazine Group na tuzo yake
ilitarajiwa kutolewa jana jioni katika sherehe iliyopangwa kufanyika
kwenye Hoteli ya St.Regis, Washington D.C, Marekani.
Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais, Ikulu ilisema kuwa tuzo hiyo ilitarajiwa kupokewa
na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kwa
niaba ya Rais Kikwete.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tuzo hiyo hutolewa kwa
viongozi wa Afrika ambao hutoa mchango mkubwa wa kiuchumi na kijamii
kila mwaka kwa watu wao, kama ilivyokuwa kwa Rais Kikwete kutokana na
mwelekeo wake wenye mafanikio kwa masuala ya utawala bora.
Taarifa hiyo ilisema kuwa jarida hilo limetambua
utawala bora chini ya uongozi wa Rais Kikwete ambao limesema umeifanya
Tanzania kuwa nchi ya kupigiwa mfano na kituo cha uhakika cha uwezeshaji
kutokana na mageuzi yaliyofanywa katika sera na mifumo ya uchumi.
Ilisema kuwa, Rais Kikwete alikuwa chaguo la
kwanza la wasomaji wa jarida hilo ambao walipiga kura kupitia njia
mbalimbali za mawasiliano za jarida hilo.
“Kuhusu maoni ya wasomaji wetu juu ya kiongozi
yupi wa Afrika ambaye ni hodari zaidi kwa maendeleo ya kiuchumi na
maendeleo, matokeo ya majibu ya swali hilo yamedhihirisha bila shaka
yoyote kuhusu nafasi ya Rais Kikwete katika uongozi wa nchi yake,”
taarifa ya Ikulu imelinukuu jarida hilo na kuongeza: “Ushahidi uko kila
mahali, ameweza kusimamia uchumi ambao umekuwa kwa wastani wa asilimia
saba kwa miaka yote ya uongozi wake.”
Chanzo gazeti la mwananchi.
Chanzo gazeti la mwananchi.
on
UTAFITI : WATANZANIA WENGI BADO TUNATUNZA FEDHA NYUMBANI .
Asilimia 70 ya Watanzania wanatunza fedha zao nyumbani badala ya
mfumo rasmi ukiwamo benki na huduma nyingine za fedha, imebainika.
Hayo yamebainishwa kwenye ripoti ya FinScope
iliyotolewa jana na Mfuko wa Kuendeleza Huduma za Fedha Tanzania (FSDT),
ikionyesha kuwa benki nchini zimeongezeka na kufikia 50.
Utafiti huo uliohusisha watu 8,000 umeonyesha kuwa
asilimia 70.4 ya Watanzania milioni 24.2 wanaostahili kupata huduma za
fedha, hawazitumii kutokana na sababu mbalimbali.
Sababu hizo ni pamoja na ukosefu wa elimu ya
masuala ya fedha, umbali kufikia matawi ya benki au wakala, gharama
kubwa za uendeshaji wa huduma hizo, mazoea ya mfumo wa kijima wa
utunzaji wa fedha, kukosa imani kuhusu usalama wa fedha zao.
Akizindua ripoti hiyo, Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu alisema jana kuwa pamoja na hali
hiyo, kumekuwa na maendeleo makubwa katika sekta hiyo ukilinganisha na
hali ilivyokuwa miaka minne iliyopita.
Soma zaidi mwananchi .
Soma zaidi mwananchi .
on
Man U Vs BM , Barca Vs Atletico Madrid mechi sare.
Man U 1 Bayern Munchen 1
Atletico Madrid 1 Barca 1
Atletico Madrid 1 Barca 1
on Wednesday, April 2, 2014
Sauti za wananchi wa Dar kuhusu tatizo la foleni
Kwa wakazi wa Dar es Salaam, moja ya kero kubwa ni kukithiri kwa foleni za magari barabarani.
Hakuna asiyeguswa na atizo hilo kutokana na ubovu wa miundombinu na kutokuwepo na miundombinu ya kisasa ya usafiri ikilinganishwa na ongezeko la watu.
Ni mkoa unaoongoza kwa watu kupoteza muda mwingi
barabarani, kiasi cha kuzorotesha hata utendaji wa kila siku na
kuathiri shughuli za uchumi ambazo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Tatizo hili la foleni linaelezewa na wataalamu
kwamba husabisha matatizo mbalimbali ya kiafya, ikiwa ni pamoja na watu
kupatwa na ugonjwa wa kurukwa akili. Kisa cha haya yote ni foleni hizo
ambazo inaonekana wazi kuwa zimekosa mwarobaini wa uhakika.
Hata hivyo, kama sehemu mojawapo ya kukabiliana na
tatizo hilo, Serikali inaendelea na mradi wa mabasi yaendayo kasi.
Kukamilika kwa mradi huo kunaelezwa kuwa kutasaidia kwa kiasi kupunguza
tatizo la foleni barabarani katika baadhi ya maeneo ambayo mradi huo
umeyagusa.
Hata hivyo, baadhi ya wakosoaji wanasema kuwa
kuwapo kwa mradi huo wa mabasi yaendayo kasi hakuwezi kusaidia moja kwa
moja kuondoa tatizo hilo ambalo limeendelea kuongezeka kutokana na
ongezeko kubwa la idadi ya watu na kupanuka kwa shughuli za kiuchumi.
on
Watatu wakamatwa wakidaiwa kuvuruga Bunge.
Bunge la Katiba jana lilianza kujadili Rasimu ya Katiba kwa
misukosuko kwenye Kamati baada ya kuvamiwa na kundi la wanaharakati
waliokuwa na mabango wakidai hati halisi ya Muungano yenye saini za
Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Karume.
Msukosuko mwingine uliozikumba karibu kamati zote
zinazoanza kujadili rasimu hiyo kwa kuanzia sura mbili zinazohusu
Muungano – sura ya kwanza na ya sita na kuzua malumbano, ni maana ya
maneno dola, shirikisho, muungano na nchi.
Wakati waandamanaji wenye mabango wakiishia
mikononi mwa polisi, suala la Muungano lilitulizwa kwa kuitwa wanasheria
kutoa tafsiri sahihi kwa kila neno.
Katika kamati zote, suala la muda wa kamati
kujadili sura hizo mbili kwa siku mbili kila moja pia liliibua mjadala
mkali, hadi kuwalazimisha baadhi ya wenyeviti wa kamati kuamua
kumwandikia mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta kuomba muda uongezwe.
Hali hiyo imejitokeza Bunge hilo likiwa limeshakaa
siku 40 kabla ya kuingia katika mjadala rasmi, baada ya kupoteza muda
mwingi katika kutengeneza kanuni za uendeshaji wa chombo hicho.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Watatu-wakamatwa-wakidaiwa-kuvuruga-Bunge/-/1597296/2266274/-/tg1uauz/-/index.html
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Watatu-wakamatwa-wakidaiwa-kuvuruga-Bunge/-/1597296/2266274/-/tg1uauz/-/index.html
on