Social Icons

Loading...

PHP for Beginers


Ujumbe wa Leo


Hatimaye Man U yazinduka yaifuata Chelsea hatua ya nane bora UEFA CL.




Man   u   3   Olympiakos 0



Chelsea   2   -   Gala 0



habari  zaidi    fuatilia  link  hii
http://www1.skysports.com/football/live/match/306084/report


KP leo


MSAMA AIPONGEZA BASATA KWA KUANZISHA MAFUNZO YA SANAA KWA WATOTO .

 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo ya sanaa kwa watoto yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Basata na kudhaminiwa na Kampuni ya Msama Promotions. Kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza na Ofisa Tawala wa Kampuni ya Msama Promotions, Hamis Mussa.
 
MKURUGENZI wa Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama amepongeza hatua ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kuanzisha mafunzo maalumu kwa watoto wa shule za msingi.
 
Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa kufunga mafunzo maalumu
yanayolenga kuwajenga watoto katika fani ya sanaa na kushirikisha watoto wapatao 200 kutoka shule tano za wilaya ya Ilala, Msama alisema ni jambo zuri kuandaa vipaji vya kesho.
 
Mafunzo haya yataweza kuwajenga watoto wetu ambao ndio taifa la kesho, pia kupunguza tatizo la watoto kujiingiza katika mambo mabaya kama matumizi ya bangi, dawa za ulevya, hivyo kuwa mzigo na janga kwa taifa,” alisema Msama.
 
Shule zilizonufaika na mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Msama kupitia
kampuni yake ya Msama Promotions, waratibu wa Matamasha ya Pasaka na Krismas, ni Buguruni Moto, Buguruni Visiwi, Ilala Boma, Uhuru Wasichana na Msimbazi.
 
Aidha, Msama alihimiza umuhimu wa somo la sanaa shuleni akitaka lipewe msisitizo mkubwa katika kuandaa vijana bora ambao hata kama wakifeli masomo mengine, wanaweza kuwa wasanii bora. “Somo hili la sanaa mashuleni lipewe uzito unaostaili kama masomo mengine kwa sababu, mtoto akifeli masomo mengine, fani ya sanaa yaweza kuwa msaada kwake,” alisema.
 
Msama aliwashauri pia Basata kuyapeleka mafunzo hayo hadi mikoani na
kupendekeza kwa hatua ya awali waanzie katika mikoa ya Pwani na Morogoro, akiamini kuna vipaji vingi vya sanaa.
 
Naye Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza alisema mafunzo hayo yaliyoanza Machi 1, wanafunzi walikuwa wakifanya mazoezi ya sanaa katika fani utambaji, hadithi, ngoma za asili na maigizo katika maeneo ya shule zao chini ya usimamizi wa walimu wao na waratibu kutoka Basata.

Mngereza alimshukuru mgeni rasmi Msama kwa kudhamini mafunzo hayo
akisema amefanya hivyo kwa kutambua umuhimu wa elimu ya sanaa katika maisha ya kila siku.

CCM YASHINDA UCHAGUZI JIMBO LA KALENGA

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea katika uchaguzi wa kumpata Mbunge wa jimbo la Kalenga, baada ya kuzoa kura kwa asilimia 79.4 dhidi ya wapinzani wao Chadema waliopata asilimia 20.1 na Chausta 0.51.
Kwa nafasi hiyo, Mgombea wa CCM Godfrey Mgimwa amekuwa Mbunge mpya akichukua nafasi ya Mbunge aliyefariki jimboni humo, Dr William Mgimwa.
Matokeo ya uchaguzi huo, yanatoa nafasi nyingine kwa CCM kuweka rekodi ya kushinda chaguzi ndogo za ubunge katika majimbo mbalimbali yaliyokuwa nyameachwa wazi.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, CCM imeshinda kwa kura 22,943 dhidi ya kura 5,800 za Chadema huku chausta ikiambukia 143.

EPL , Man U HOI kwa Liverpool, Arsenal yatakata.

Man    United    0 , Liverpool   3
 



Arsenal  1    Spurs  0


Msimamo   wa  ligi
http://www.premierleague.com/content/premierleague/en-gb/matchday/matches.html?paramClubId=ALL&paramComp_190=true&view=.dateSeason.html

Asante Bwana Yesu kwa hatua hii...

Jana   tarehe   16  march  2014  katika  ibada  zote   mbili  katika  kanisa  la   TAG  Kinondoni Revival  Church ( KRC )  mmliki  wa   blog hii    Bloger  Daniel  na  Mtarajiwa  wake  Bibi Penina  waliweka  mambo  hadharani    na kuwekewa  mikono  na  makuhani  katika  kanisa  hilo  na  kisha  baadaye   katika tafrija  fupi  ya  kuwapongeza  wachumba    iliyofanyika   Chichi  Hotel  kinondoni  , asante  sana  wote  kwa  kutuombea  na  tunahitaji pia  neema  na  mchango  wako  wa  mawazo na  mali  kufanikisha  jambo  hili  mwezi   wa  sita  mwishoni  mwaka   huu
Mungu   wetu  akubariki  sana .
Daniel.
Jopo  la  viongozi  wa   kanisa la  TAG   Kinondoni  revival church  likiongozwa na  Mama  Askofu   Dr Rogather Z .Swai   wakiomba maombi  ya  baraka na  ulinzi   wa  Mungu kwa   wachumba.

   Tukitakiana    kheri  na    mkono  wa  pongezi,  Asante  Yesu  kwa neema  hii.
            Tabasamu  la  ukweli ,
 Keki  maalumu..
                             Daniel  na  Penina.
    Jamaa  , ndugu  na  marafiki  katika  hafla  ya  kuwapongeza   watarajiwa.

Grab the latest iOS update



The latest update for Apple's mobile devices is rolling out now, bringing bug fixes and one major feature.The iOS 7.1 update isn't as big of an upgrade as iOS7 was, of course, but it does bring tweaks and additions to the formula anyway.For one, it brings support for Apple's CarPlay service, which essentially brings selected iPhone apps (such as maps and music player) to your car's display.
Of course, you'll need a specific 2014 car model (from the likes of Ferrari, Honda and Ford, to name a few) to actually make use of CarPlay. Other features include: the ability to manually control how long Siri listens to you, HDR mode by default for the camera and several tweaks to the user-interface.
As for bug fixes, iOS7.1 improves performance on the iPhone 4, improves Touch ID performance and fixes a homescreen crash bug.

CHAGUA KIMOJA HAPA


Why many Tanzanians now avoid paying taxes.




Two out of every 10 Tanzanians simply refused to pay tax between 2011 and 2013, it has emerged. According to a new Afrobarometer study, the number of self-reported levels of non-compliance are far higher in Tanzania than in the other 29 sub-Saharan countries surveyed.The report titled “Africa’s Willing Taxpayers Thwarted by Opaque Tax Systems, Corruption” was released on Tuesday.   Survey data reveals widespread citizen commitment to the principle of taxation and to paying up for national development. But their enthusiasm is dimmed by taxation systems across the continent that remain opaque to the majority. Perceived corruption among tax authorities remains significant and evidence suggests these perceptions undermine public commitment to the integrity of the tax system and increase the likelihood of non-compliance, according to the report.
Source: http://www.thecitizen.co.tz/News/Why-many-Tanzanians-now-avoid-paying-taxes/-/1840392/2235708/-/wcnvh3/-/index.html

AHLY : KUITOA YANGA NI BAHATI TU



Kocha wa Al Ahly, Mohamed Youssef amesifu umakini na nidhamu ya hali juu ya mchezo ilioonyeshwa na wachezaji wa Yanga na kusema ushindi wa timu yake ulikuwa wa ‘ngekewa’ na si uwezo wa uwanjani.
Al Ahly iliiondoa Yanga kwa penalti 4-3 baada ya mchezo huo kumalizika kwa mabingwa wa Afrika kushinda 1-0 hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa bao 1-1 kutokana na  Yanga kushinda bao 1-0 katka mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam.
Katika pambano hilo lililofanyika kwenye Uwanja wa Max jijini Alexandria, mabingwa wa Tanzania, Yanga walicheza kwa umakini katika kujilinda na kushambulia.
Yanga walishambulia wote na kila walipopoteza mpira haraka walirudi golini kwao kujilinda kabla ya kuruhusu bao dakika 71 lililofungwa na Sayed Moawad.
Pia, Yanga mara tatu walipoteza nafasi kushinda mchezo huo wakati wachezaji wake Said Bahanuzi, Oscar Joshua na Mbuyu Twite walipopoteza mikwaju yao ya penalti.
Kocha Youssef alisema mchezo ulikuwa mgumu sana kwetu. Tulitaka kushinda katika muda wa kawaida, lakini haikuwa rahisi kwa sababu hatukuwa makini katika kutumia nafasi.
“Watu wengi walifikiri tutawafunga kirahisi Yanga. Hiyo siyo kweli... ilikuwa timu imara, lakini cha muhimu tumefuzu,” Youssef aliuambia mtandao wa Cafonline.
“Bao letu tumelipata kama bahati ya Mungu tu, pia tunashukuru kwa kiwango cha juu cha kipa wetu Sheriff Ekramy aliyeokoa penalti tatu.”

Tizama  penalti  iliyowapatia  ushindi   mafarao  wa  Misri   :  National  Al  Ahly

Mama' s Day



Waandishi wa habari wazuiwa Kamati za Bunge la Katiba Waandishi wa habari wazuiwa Kamati za Bunge la Katiba

Bunge Maalumu la Katiba limepitisha kanuni ya kuwazuia waandishi wa habari kuingia katika vikao vya kamati za chombo hicho, hatua ambayo inaelezwa ni kinyume na Katiba inayotoa uhuru wa wananchi kupata habari.
Kanuni hiyo ilipitishwa jana baada ya malumbano makali yaliyowagawa wajumbe wa bunge hilo, baadhi wakipinga kifungu hicho kwa sababu kinavunja Katiba ya nchi inayotoa uhuru kwa waandishi kukusanya na kusambaza habari na wengine wakiunga mkono kuwazuia.
Kanuni hiyo ilipitishwa kwa mbinde huku baadhi ya wajumbe wakiendelea kushikilia msimamo wa kuikataa, hata baada ya Mwenyekiti wa Muda wa bunge hilo, Pandu Ameir Kificho kuridhia kipite. Wajumbe waliopinga kanuni hiyo ni Joshua Nasari, Moses Machali, Peter Serukamba, Ezekiah Wenje na Maria Sarungi.
Baadhi ya wajumbe akiwamo Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga walisimama kutaka kuzungumza lakini hawakupata fursa hiyo.
Mjumbe aliyekuwa mwiba kwa Tasnia ya Habari ni, Dk Harrison Mwakyembe ambaye aliwashawishi wajumbe kufunga mjadala huo ili wasonge mbele kwa madai kuwa hata yeye pia ni mwanahabari. “Hakuna upande usiotambua umuhimu wa vyombo vya habari katika mchakato huu... Tunachotofautiana ni jinsi na namna
ya ushiriki wa vyombo vya habari,” alisema Dk Mwakyembe. Alisema Taifa limeingia katika kipindi maalumu kama cha vita na kwa msingi huo, kanuni zinabadilika kulingana na mazingira na kwamba vyombo vya habari vinapaswa kulitambua hilo.
Soma  zaidi  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Waandishi-wa-habari-wazuiwa/-/1597296/2234078/-/2npu1p/-/index.html

KARIBUNI NYOOTE KATIKA UZINDUZI WA KITABU CHA BISHOP MOSES KULOLA PALE EAGT TEMEKE


© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top