Social Icons

Loading...

TATHMINI YA MCHAKATO WA UHAMAJI KUTOKA MFUMO WA UTANGAZAJI WA ANALOJIA KWENDA KIDIJITI



UTANGULIZI

Mnamo mwezi Julai, 2013, Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilikamisheni jopo la wataalamu wa Chuo Kikuu kufanya tathmini ya mchakato mzima wa uhamaji toka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda mfumo wa kidijiti pamoja na uzimaji wa mitambo hiyo kwenye miji saba ambayo ni Dar e salaam, Tanga, Moshi, Mwanza, Dodoma, Arusha na Mbeya. Uzimaji wa mitambo ya analojia ilikuwa ni kwa mujibu wa sheria, ambayo iko kwenye kanuni zinazojulikana kama “Digital Broadcasting and Other Networks 2011”

Jopo hilo lilijumuisha wataalamu wafuatao:-

Prof. Nerey Mvungi         Mtaalamu wa Mawasiliano ya ki electronic
Dr.Francis Sichona         Mtaalamu wa Takwimu
Mr.F.M Ishengoma        Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano

Wote hawa ni wafanayakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


1.1    MADHUMUNI YA TATHMINI
Madhumuni ya tahmini hii ilikuwa imejengwa kwenye maeneo Makuu manne kama ifuatavyo;

(a)    Tathmini ya utendaji na utoaji huduma za utangazaji kwenye mfumo wa kidijiti ikiwa ni pamoja na usimikaji wa miundo mbinu ya kidijiti.

(b)    Tathmini ya kuangalia jinsi Mamlaka ya Mawasiliano ilivyokuwa imejizatiti kuandaa na kusimamia zoezi zima la uhamaji toka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda kidijiti

(c)    Tathmini ya jinsi watumiaji wa huduma za utangazaji walivyopokea mabadiliko hayo na changamoto zilizopo na

(d)    Tathmini ya jinsi zoezi zima la uzimaji mitambo lilivyoendeshwa.

Katika uendeshaji wa tathmini hiyo wataalamu walizingatia mambo muhimu yafuatayo ikiwa ni pamoja na hoja zilizotolewa na taasisi na watu mbalimbali kutoka kwenye jamii kama ifuatavyo:-

(i)    Idadi ya visimbuzi vilivyokuwepo kwenye soko kabla ya uzimaji mitambo kama vinatosheleza mahitaji,

(ii)    Idadi ya watu walioweza kununua visimbuzi ilikuwa ndogo hivyo watu wengi kushindwa kununua na kukosa habari zinazopatikana kwa njia ya luninga,

(iii)    Ushirikishaji wa wadau kwenye mchakato mzima wa uhamaji toka mfumo wa analojia kwenda kidijiti kabla ya uzimaji mitambo hiyo,

(iv)    Kiwango cha Elimu kwa Umma (Public Awareness Campaign) kilichotolewa kabla na baada ya uzimaji mitambo,

(v)    Bei za visimbuzi kama zilikuwa juu kwa watu wa hali ya kawaida na kusababisha kushindwa kuvinunua,

(vi)    Ubora wa visimbuzi na upokeaji wa matangazo usioridhisha kama vile kuganda kwa picha.


1.2    NJIA ILIYOTUMIKA KUFANYA TATHMINI
Njia iliyotumika kufanya tathmini hii ni ile inayotumika kimataifa (International Best Practise) kuendesha mazoezi kama haya ijulikanayo kama “Sampling Approach” ambapo takwimu hukusanywa kwa kuzingatia uwiano wa kaya zilizopo kwenye eneo husika, jinsia, umri, elimu na kazi za kumuingizia kipato mtu anayehojiwa.

Makundi mabalimbali yanayohusika kwenye mchakato huu wa uhamaji kutoka mfumo wa analojia kwenda dijitali yalihojiwa kwa kupitia dodoso maalumu lililoandaliwa na maoni yao yalikusanywa. Makundi hayo ni kama ifuatavyo:-
(i)    Watumiaji wa huduma ya matangazo kwa mfumo wa kidijiti (Consumers)

(ii)    Watengenezaji na wasambazaji wa maudhui kwa njia ya Luninga (Content Service Providers)

(iii)    Wasimikaji wa miundo mbinu ya kidijiti (Multiplex Operators) na

(iv)    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

2.0    MATOKEO YA TATHMINI
Yafuatayo ni matokeo ya zoezi zima la tathmini hiyo kama ilivyoendeshwa kwenye maeneo tajwa hapo juu.

2.1    TATHMINI YA UTENDAJI NA UTOAJI HUDUMA ZA UTANGAZAJI KWENYE MFUMO WA KIDIJITI IKIWA NI PAMOJA NA USIMIKAJI WA MIUNDO MBINU YA KIDIJTI.

Tathmini iliyoendeshwa na jopo la wataalam kuhusu utendaji na huduma kwa walaji kwa ujumla wake zimeonyesha yafuatayo;

(a)    Asilimia 89% ya kaya za watumiaji (consumers) walikuwa wakitumia huduma ya matangazo kwa mfumo wa kidijiti mara baada ya uzimaji wa mitambo ya analojia kwenye miji saba ambayo tathmini ilikuwa ikifanyika

(b)    Asilimia 11% ya kaya za watumiaji hawakuweza kupokea matangazo ya kidijiti kwa sababu mbalimbali kama ifuatavyo:-

-    5.5% hawakununua visimbuizi

-    0.1% ya Kaya, walisema visimbuzi vilikuwa havipatikani

-    3.2% ya Kaya, walishindwa kunua visimbuzi sababu ya bei kuwa juu
-    0.2% ya Kaya visimbuzi vyao vilikuwa vibovu
-    0.3% ya Kaya, visimbuzi havikuweza kupokea matangazo ya kidijiti kwa sababu ya mawimbi hayapatikani kwa ubora zaidi (Poor signal reception)

-    0.9% ya Kaya Luninga (TV screen) zilikuwa mbovu

-    0.7% ya Kaya hawakuwa na umeme


2.2    UTAYARI WA MAMLAKA YA MAWASILIANO KUANDAA NA KUSIMAMIA ZOEZI ZIMA LA UHAMAJI TOKA UTANGAZAJI WA MFUMO WA ANALOJIA KWENDA KIDIJITI

Jopo la wataalamu lililokuwa likiendesha tathmini hii liliweza kuthibitisha kuwepo kwa mambo yafuatayo pamoja na baadhi ya nyaraka kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA):-

-    Kuwepo kwa kamati ya Kiufundi inayoundwa na wadau mbalimbali ikiwa na kazi ya kutoa ushauri wa kiufundi kwa maswala yote yanayohusu uhamaji toka utangazaji wa analojia kweda kidijiti,

-    Kuwepo kwa dira madhubuti inayoonyesha mambo muhimu ya kutekelezwa kuelekea uzimaji wa mitambo ya analojia,

-    Kuwepo kwa sheria na kanuni zinazosimamia zoezi la uhamaji toka analoja kwenda kidijiti,

-    Kuwepo kwa nyaraka mbalimbali zinazoonyesha muhtasari wa vikao mbalimbali vilivyofanywa kati ya wadau na Mamlaka ya Mawasiliano.

              Vilevile Jopo la wataalamu liliweza kuthibitisha mambo yafuatayo:-

-    Muundo bora wa leseni unaozingatia utoaji huduma za matangazo ya kidijiti,

-    Utaratibu mzuri wa ushindani kwa njia ya wazi uliotumika kuwapata “Multiplex Operators” (wajenga Miundombinu na Wsambazaji wa matangazo),

-    Waraka unaonyesha mchakato wa namna ya kupata malipo yananayotakiwa kulipwa na watengenezaji na wasambazaji wa  maudhui (Transmission fee) kwa wenye leseni ya miundo mbinu ya kidijiti (Multiplex Operators),

-    Mfano wa nyaraka itakayotumika kufikia makubaliano ya utoaji huduma na mahusiano yao kibiashara (SLA) kati ya wasimikaji wa miundo mbinu ya kidijiti na watengenezaji na wasambazaji maudhui.

Kutokana na vielelezo na nyaraka ambazo jopo la wataalamu iliweza kuzipata, jopo limeridhika kabisa kuwa Mamlaka ya Mawasiliano ilikuwa imejizatiti vizuri kuandaa na kusimamia utekelezaji wa uhamaji toka mfumo wa zamani wa analojia kwenda utangazaji wa mfumo mpya wa kidijiti.

2.3    MATOKEO YA TATHMINI KUHUSU UPATIKANAJI WA VISIMBUZI NA ELIMU KWA UMMA
Tathmini imeonyesha kuwa kati ya kaya zote zilizohojiwa kwenye miji saba, ni 0.1% ya kaya zilizodai uhaba wa visimbuzi wakati wa zoezi zima la uzimaji mitambo ya analojia. Matokeo mingine ni kama ifuatavyo:-

-    35.4% ya kaya zilizohojiwa walinunua visimbuzi kabla ya uzimaji mitambo ya analojia na kabla ya kuanza utoaji wa elimu kwa umma kuhusu mfumo mpya wa uatangazaji wa kidijiti

-    29.5% ya kaya walinunua visimbuzi kabla ya uzimaji mitambo ya analojia lakini baada ya utoaji elimu kwa umma

-    35.1% walinunua visimbuzi baada ya uzimaji mitambo
    Takwimu hizi zinaonyesha kuwa upatikanaji wa visimbuzi na bei halikuwa     tatizo kubwa lililoathiri mchakato mzima wa uhamaji kutoka mfumo wa     analojia kwenda kidijiti kwenye miji hii saba. Vilevile elimu kwa umma ilisaidia sana kuhamasisha walaji kuhamia kwenye mfumo huu mpya wa utangazaji

2.4     ZOEZI LA UZIMAJI MITAMBO YA ANALOJIA

Ilifahamika kuwa zoezi la uzimaji mitambo ya analojia lilifanyika kwenye awamu nne ambapo kila awamu ilitoa nafasi ya mwezi mmoja. Jopo la wataalam limeridhika na utaratibu huu, ambao unatoa nafasi kubwa ya kutathmini matatizo yanayojitokeza kwenye awamu ya kwanza kabla ya kwenda kwenye awamu nyingine. Vilevile ulitoa fursa ya kuhakikisha kuwa eneo linalofuata linakuwa na visimbuzi vya kutosha na elimu kwa umma inatolewa kikamilifu kwa kutumia Radio na Televissheni za eneo husika.

2.5    WATENGENEZAJI NA WASAMBAZAJI MAUDHUI (CONTENT SERVICE PROVIDERS)
65% ya watengenezaji na wasambazaji wa maudhui walikuwa wamejiunga na mfumo wa kidijiti kabla ya uzimaji wa mitambo ya analojia.
Sababu kubwa ya vituo vingine kutojiunga na mfumo huu kwa wakati ilikuwa ni sababu za kimazoea kwamba huenda mitambo isingezimwa kwa wakati uliopangwa.

Mpaka sasa vituo vyote vilivyopo Dar es Salaam vimeshajiunga na mfumo huu kasoro kituo kimoja.

3.0    MAJUMUISHO

3.1    Jopo la wataalam limeridhika kuwa watazamaji wengi waliokuwa kwenye mfumo wa analojia walijiunga kwenye mfumo wa kidijiti. 11% tu ndio ambao hawakuweza kujiunga kwa sababu mbalimbali kama nilizoelezea mwanzoni. Idadi hiyo inaweza kuwa imepungua kwa vile watu wamekua wakiendelea kununua visimbuzi,

3.2    Zoezi hili halijawanyima watanzania haki ya kupata habari kwani wengi tayari wameshajiunga na mfumo huu mpya. Jopo liliona kuwa sababu ya malalamiko mengi yalitokana na tabia halisi ya wanadamu kuogopa mabadiliko,

3.3    Kutokana na takwimu zilizokusanywa, jopo limeridhika kabisa kuwa elimu kwa umma ilitolewa kwa kiwango kikubwa kwani 90% ya kaya zilizotembelewa walikuwa na habari kuhusu mfumo huu mpya wa utangazaji kwa njia ya kidijiti,

3.4    Hatua madhubuti zilichukuliwa kuhakikisha kuwa kabla eneo husika kuzimwa mitambo ya analojia kulikuwa na visimbuzi vya kutosha,

3.5    Mfumo huu mpya wa kidijiti utatoa fursa nzuri kwa watengenezaji na wasambazaji wa maudhui kutumia muda wote kutengeneza vipindi vizuri badala ya kujihusisha na usimikaji miundo mbinu ya utangazaji,

3.6    Mfumo huu mpya wa utanagazaji kwa njia ya kidijiti umeongeza ubora wa picha na channel nyingi. Juhudi zifanyike kuwa na channel nyingi za nyumbani badala ya nje ya nchi.

3.7    Jopo limeridhika kuwa mfumo huu mpya haujapunguza idadi ya watazamaji wa luninga ila watazamaji wamegawanyika kutazama channel mbalimbali na hivyo kujenga hisia kuwa watazamaji wamepungua.

3.8    Maeneo mengi yaliyokuwa yanapokea channel moja mpaka tatu sasa wanaweza kuona channel za kinyumbani zaidi ya tano.

3.9    Uhamaji kutoka DVB-T kwenda DVB-T2 uende kwa nguvu ya soko kwani dhana nzima ilikuwa kuhama mfumo wa analojia kwenda kidijiti, na viwango vyote hivi viwili vinatoa matanagazo ya kidjiti

4.0    HITIMISHO

Kutokana na matokeo ya tathmini iliyofanyika serikali inashauriwa iendelee na zoezi la uzimaji mitambo ya analojia sehemu zilizobakia. Jopo limeridhika na uandaaaji na usimamizi wa zoezi hili na kwamba kasoro zilizojitokeza ni sababu ya hofu ya mabadiliko na uzoefu wa walaji kwenye matumizi ya visimbuzi. Vilevile kuna faida nyingi za mfumo wa kidijiti ambazo watoa huduma wanatakiwa kuzitumia ili kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.

Serikali inashauriwa kutoa punguzo la kodi kwa visimbuzi ili kuwawezesha watanzania wengi zaidi kununua visimbuzi na kupata habari kwa njia ya Luninga

Naomba niwakabidhi ripoti hii ambayo ina maelezo na taarifa za kina kuhusu zoezi tathmini hii.
 
Imetolewa na:

Prof. Nerey Mvungi        Mtaalamu wa Mawasiliano ya ki electronic
Dr.Francis Sichona         Mtaalamu wa Takwimu
Mr.F.M Ishengoma        Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano

JOPO LA WATAALAMU TOKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
19 FEBRUARI 2014

Mabasi ya majini kumaliza msongamano wa magari?

Serikali, mashirika binafsi na wadau wa usafiri ndani na nje ya nchi wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali kukabiliana na msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.
Msongamano huo ambao unachangiwa kwa kiasi kikubwa na uduni wa miundombinu ikiwemo barabara, umekuwa ni kero kwa wananchi na Serikali kwa jumla.
Serikali imewekeza katika Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (BRT) na usafiri wa treni ndani ya Jiji la Dar es Salaam kama njia mojawapo ya kumaliza tatizo la msongamano wa magari na foleni.
Msingi wa tatizo
Chanzo kikubwa cha foleni jijini Dar es Salaam si wingi wa abiria bali ni wingi wa magari binafsi na njia finyu zisizokidhi mahitaji ya watu walioko katika jiji hilo.
Njia muhimu ya kupunguza foleni na msongamano wa magari ni kupunguza wingi wa magari barabarani na kuweza kuzipanua barabara ili kuwe na uwezekano wa kupita kwa urahisi.
Kutokana na foleni na uduni wa huduma za usafiri wa umma watu wa kundi la kati, wamekuwa wakikimbilia kununua magari binafsi kwa ajili ya kwenda nayo kwenye shughuli zao kwa urahisi.
Aidha, katika kuendeleza harakati za kupambana na tatizo la usafiri, Kampuni ya Transevents Marketing ya Tanzania kwa kushirikana na Kampuni ya Dutch Amphibious Transport Vehicles (DATV) ya Uholanzi inaendelea na mchakato wa kuleta usafiri wa mabasi ya abiria yenye uwezo wa kusafiri nchi kavu na majini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Transevents, Peter Nzunda anasema teknolojia hiyo ya mabasi ya nchi kavu na majini (amphibious) ina lengo la kupunguza tatizo la foleni kwenye barabara za Dar es Salaam hususan katikati ya jiji kwa kuwa mabasi hayo huweza kupita nchi kavu na majini.
Hii ina maana kuwa hata katika maeneo yenye barabara zisizo nzuri au zenye tope, magari hayo huweza kupita hivyo kutosababisha foleni kama ambavyo hutokea sasa katika baadhi ya maeneo hasa mvua zinaponyesha na kuharibu barabara.
kwa   hisani  ya  gazeti  la  mwananchi

KP LEO


YAJUE MASWALI MAGUMU WALIYOULIZWA AKINA MHE: MEMBE

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe amesema aliulizwa maswali mazito na Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, Phillip Mangula kuhusu mbio za urais 2015.Akizungumza jana mjini Dodoma muda mfupi baada ya kuhojiwa na kamati hiyo, Membe alisema kamati hiyo inauliza maswali magumu kuhusu wanayoyafanya pamoja yanayofanywa na mashabiki wao.
“Kamati inauliza maswali mazito na magumu yanayohusiana na uvunjaji wa maadili ya uongozi wa chama chetu… Kamati ya maadili imejipanga vizuri sana wala msidanganyike, wanauliza maswali mazito,” alisema Membe.
Membe aliongeza kusema aliulizwa mambo makubwa matatu, kubwa likiwa ni kuibuka ghafla kwa makundi makubwa ambayo yanazaliwa kila wakati chama hicho kinapokaribia kwenye uchaguzi wa Rais.
“Kuna mambo makubwa matatu ambayo kamati ya maadili imeyauliza. Kubwa kabisa ni uzukaji ghafla wa makundi makubwa ambayo yanazaliwa kila wakati wanapodhani mtu fulani anafaa kuwa kiongozi.”
Alisema na kuongeza: “Suala la pili nililoulizwa ni tunafanyaje kukifanya chama chetu kiwe na kundi moja litakalokwenda mwakani kwenye uchaguzi?”
zaidi  soma   hapa 

CAR FOR SALE

  CAR   HONDA   CITY :
Year : 2001; AT, Petrol, CC: 1300; 
FOR   SERIOUS      BUYER     PLS  CALL    0767612064  or  0713612064










=================================================================
The Silver  Noah Specs:
Year : 2002; AT, Petrol, CC: 1990; SV model, TV, mileage 79,000Km
 
 


 

===========================================================
The Black Noah Specs:
Year : 2002; AT, Petrol, CC: 1990; SV model, TV, mileage 87,000Km
 


MADHARA YA SMART PHONE KWA WATOTO



Wazazi wengi hawana habari kuhusu hatari zinazowakabili watoto wao wanapotumia vifaa vya tablets na simu za mkononi almaarufu kama smartphones. Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na BBC.

Takriban mmoja kati ya watoto watano walisema kwamba waliwahi kuona kitu kwenye vifaa hivyo ambacho kiliwafadhaisha kwa kiasi maradufu zaidi ya jinsi wazazi wao walivyodhania.
Utafiti mwingine umeonyesha kwamba wazazi wapatao zaidi ya 20% hawaangalii kwa karibu yale ambayo watoto wao hufanya kwenye mtandao.

Utafiti huo ulitumika ikiwa sehemu ya siku ya kuadhimisha Usalama wa Matumizi ya Mtandao.
Huku 90% ya wazazi waliohojiwa na BBC huko Uingereza wakisema kuwa wamewahi kuwatahadharisha watoto wao kuhusu usalama kwenye mtandao wanapotumia simu zao, wengi walisema kwamba wao huwaruhusu watoto wao kutumia vifaa hivyo bila usimamizi wowote.
Vizuizi vya wazazi
"Cha kusikitisha ni kwamba hamna yeyote kati yetu wa umri wowote ambaye hawezi kupata matatizo kwenye mtandao," alisema Tonny Neate ambaye ni mkuu wa shirika la Get Safe Online.
Bila kutumia vizuizi mbali mbali vya usalama na kibinafsi watoto huenda wakakumbana na mambo ambayo hayafai kwa umri wao ama umri wowote.
Usalama wa matumizi ya mtandao katika familia.
Utafiti huo pia ulionyesha kuwa watoto kati ya umri wa miaka 13-16 wamo katika hatari zaidi za ukatili kwenye mtandao wakilinganishwa na wale wa umri wa miaka 8-12. Hata hivyo wazazi hawana hofu ikiwa watoto wao waliozidi umri huo kutumia vifaa vya tablet.

David Emm,ambaye ni mtafiti wa usalama katika maabara ya Kaspersky alisema kwamba:
''siku hizi wazazi hawana habari kuhusu hatari za kutumia mtandao kwenye tablets na simu za mkononi kama walivyokuwa hapo awali mtoto alipotumia tarakilishi.
"Watoto wanapotumia rununu na vifaa vyake kuingia kwenye mtandao hutumia mtandao ule ule wenye hatari, alisema.
"Wengi wanadhani kwamba rununu na zile tablets hazihitaji kiwango sawa cha kinga kama tarakilishi. Lakini kadri asilimia kubwa ya wazazi ambao hawachunguzi kile ambacho watoto wao hufanya kwenye mtandao, mkondo huo wa mawazo unapaswa kugeuka."
Simu za kampuni ya Apple kama iPhone na tabiti za ipad tayari zina vizuizi ambavyo mzazi anaweza weka ili mtoto asiwezie kutumia.
Ni muhimu kuzifunga tandawazi kabisa au kutia umri mwafaka wa watu wanaoruhusiwa kutumia maudhui yaliyomo.
Kuna uwezekano wa kuwa na akaunti zenye vizuizi(password) kwenye simu za Android na tablets.

Vidokezo kwa Wazazi.
Zaidi ya 50% ya wazazi walioshiriki utafiti huo wa BBC walikuwa wameweka vizuizi kwenye simu zao lakini 40% pekee ya wazazi hao walisema kuwa wamefanya hivyo kwenye simu za watoto wao pia.
Katika utafiti uliofanywa kwenye maabara ya Kaspersky, 18% a wazazi waliwahi poteza fedha au data kutoka kwa simu zao au tablets kwa sababu watoto wao walikuwa wakitumia vifaa vya wazazi bila ya kuandaliwa kwa karibu.
Watoto walio huru sana kutumia sana mtandao hununua programu za michezo kwenye internet au Apps, na hivyo kutumia pesa vibaya.
Kamapuni ya Apple hivi karibuni iliambiwa iwarejeshee wazazi kima cha dola milioni 32.5 ambao watoto wao walinunua programu hizo bila ya idhini ya wazazi.
Watu wazima pia wanaonywa kuhusu usalama wao kwenye mtandao wakati kampuni ya Microsoft ilipozindua utafiti wake wa kila mwaka kuhusu usalama wa watu kwenye mitandao.

David Emm,ambaye ni mtafiti wa usalama katika maabara ya Kaspersky alisema kwamba:
''siku hizi wazazi hawana habari kuhusu hatari za kutumia mtandao kwenye tablets na simu za mkononi kama walivyokuwa hapo awali mtoto alipotumia tarakilishi.
"Watoto wanapotumia rununu na vifaa vyake kuingia kwenye mtandao hutumia mtandao ule ule wenye hatari, alisema.
"Wengi wanadhani kwamba rununu na zile tablets hazihitaji kiwango sawa cha kinga kama tarakilishi. Lakini kadri asilimia kubwa ya wazazi ambao hawachunguzi kile ambacho watoto wao hufanya kwenye mtandao, mkondo huo wa mawazo unapaswa kugeuka."
Simu za kampuni ya Apple kama iPhone na tabiti za ipad tayari zina vizuizi ambavyo mzazi anaweza weka ili mtoto asiwezie kutumia.
Ni muhimu kuzifunga tandawazi kabisa au kutia umri mwafaka wa watu wanaoruhusiwa kutumia maudhui yaliyomo.
Kuna uwezekano wa kuwa na akaunti zenye vizuizi kwenye simu za Android na tablets.

Msigwa aibana Serikali itoe majibu ripoti ya ITV London

Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa, ameitaka Serikali kutoa majibu sahihi baada ya gazeti la Daily Mail on Sunday la Uingereza, kuchapisha habari inayoeleza kuwa Tanzania ni kinara wa ujangili, huku Rais Jakaya Kikwete akifumbia macho.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mchungaji Msigwa alisema maelezo yaliyotolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu baada ya kuchapishwa kwa taarifa hizo yamejaa siasa, uzushi na uongo.
Alisema ukweli lazima uwekwe wazi kwa sababu wanaohusika na biashara hiyo ni baadhi ya watendaji wa Serikali, wafanyabiashara na vigogo wa vikosi vya ulinzi na usalama nchini.
Wakati Mchungaji Msigwa akieleza hayo, Ikulu ya Marekani jana ilitoa taarifa ya kupiga marufuku biashara ya meno ya tembo nchini humo ikiwa ni hatua yake ya kukabiliana na ujangili ulioshika kasi katika nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania.
Pia, leo Rais Kikwete atakuwa miongoni mwa viongozi 50 watakaohudhuria mkutano wa kuokoa viumbe vilivyo hatarini kutoweka duniani, unaofanyika London, Uingereza.
Mkutano huo utakuwa chini ya wenyeji wa mwana wa Wales na Waziri wa Mkuu wa Uingereza, David Cameron.
Taarifa ya gazeti hilo ya Februari 8 mwaka huu, limeitaja Tanzania kama kinara wa ujangili kwa kuua zaidi ya tembo 11,000 kwa mwaka na kumhusisha Rais Kikwete kuwa na urafiki na wafanyabiashara ya meno ya tembo.
Pia imewahusisha wafadhili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika biashara hiyo.
Katika maelezo yake Mchungaji Msigwa alisema, “Takwimu za Serikali zinaeleza wazi mwaka 2010 tembo 10,000 waliuawa nchini sawa na wastani wa tembo 37 kwa siku. Inakuwaje taarifa hizi ziwekwe wazi halafu Serikali idai inachafuliwa.”
Alisema Serikali imewahi kukiri kuwa inawajua wanaojihusisha na ujangili lakini badala ya kuwakamata imekuwa ikiwataka kuachana na biashara hiyo.
CHANZO  gazeti  la  mwananchi

LOVE & DIVE VALENTINE DINNER 2014


© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top