Social Icons

Loading...

Nyie ni watu wabaya: Mtoto wa miaka 4 awaambia magaidi

Mtoto wa miaka minne ambaye ni raia wa Uingereza, Elliott Prior ameonyesha ushujaa wa hali ya juu baada ya kuweza kuwatolea maneno makali na ya kugusa magaidi waliovamia jengo la maduka la Westgate.
Baada ya maneno hayo, baadhi ya taarifa zilizochapishwa kwenye vyombo mbalimbali vya kimataifa, vinasema magaidi hao waliomba mtoto huyo awasamehe kwa maelezo kuwa wao siyo watu wabaya.
Inaelezwa kuwa, kitendo cha mtoto huyo kilikuwa cha kishujaa kwani aliweza kuwaeleza magaidi hao maneno hayo, bila kuogopa silaha nzito walizokuwa wameshika mkononi huku baadhi ya watu wakiwa wameshauuawa.
Mtandao wa Daily Mail unasema mtoto huyo alimwambia mmoja wa magaini hao kuwa ‘Nyie ni watu wabaya sana’.
Mtandao huo unasema mtoto huyo aliyasema maneno hayo kama njia ya kumkinga mama yake Amber, aliyekuwa amepigwa risasi mguuni pamoja na dada yake Amelie, mwenye umri wa miaka sita ambaye walikuwa wote ndani ya duka hilo.
Chanzo http://www.mwananchi.co.tz/habari/habari-ya-ndani/Nyie-ni-watu-wabaya--Mtoto-wa-miaka-4-awaambia-magaidi/-/1724700/2007674/-/rejief/-/index.html

NBC BOSS named to be Business Woman of the Year 2013.

 
Managing Director Ms. Mizinga Melu
The National Bank of Commerce (NBC) Managing Director Ms. Mizinga Melu was named Business Woman of the Year 2013 at the All Africa Business Leaders Awards (AABLA) which was held in Johannesburg, South Africa.

The All Africa Business Leaders Awards (AABLA) aims to identify and honour those leaders who are making a difference through innovation and inspiration in their industry sectors. It is organized and overseen by ABN Productions.
AABLA was successfully launched in South Africa in 2011 with the first awards ceremony which took place in October the same year. As one of the most prominent award ceremonies in Africa, the AABLA ceremony is televised across the African continent annually. The Business Leaders Awards was originally conceived by CNBC Worldwide.
There are four categories through which participants can be nominated namely Business Leader of the year 2013, Business Woman of the year 2013, Entrepreneur of the Year 2013 and Young Business Leader of the year 2013.
The winner of the Southern Africa Business Woman of the Year category exemplifies outstanding leadership in business. She showcases positive financial results, increased shareholder value, and provided sound management, proven corporate governance, and demonstrated innovation, best business practices and accountability, together with intangible qualities such as integrity and vision.
Ms. Melu was appointed to the role of Managing Director at NBC with effect from 20th May 2013. She is an exceptional banker having worked in 6 African countries and equipped with more than 20 years of experience in the Banking Industry. Mizinga is an expert in formulating, implementing and developing Business Strategies; one such example is the award winning USD500m Microfinance Bill Clinton pledge of banking the unbanked.
Among some of the recent recognitions awarded to Mizinga include, CEO of the year across all industries by the Zambia Institute Chartered Accountants in 2012 and Leaders and Achievers Outstanding CEO performance by PMR of South Africa in 2013. Mizinga is

KIBONZO


JEE HII NI KWELI - Faida za umbea kiafya kwa mujibu wa wataalamu.

Katika jamii yoyote mtu mwenye tabia ya umbea huchukiwa, hutengwa na hata wakati mwingine hupigwa kwa kuonekana kuwa ni chanzo cha migogoro na huku viongozi wa dini wakimwona mtu wa aina hiyo kuwa ni mtenda dhambi.
Watu wanaopenda tabia ya umbea huenda wakawa wamepata mtetezi. Ripoti iliyotolewa hivi karibuni kuhusu tabia ya watu kupenda kutumia muda mwingi kusema mambo ya watu wengine, inasema tabia ya umbea ina manufaa kiafya.
Ripoti hiyo iliyotolewa na watafiti kutoka chuo kikuu cha Rhode Island cha Marekani, inasema kuwa watu wanaonufaika zaidi za tabia hiyo ni wale wanaopenda kuongea mambo mabaya wa watu wengine kuliko wenzao wanaopenda kuzungumza kuhusu mambo mazuri.
Wataalamu hao wamebaini kuwa iwapo mtu atatumia dakika 20 kuzungumzia mambo mabaya ya watu wengine, anaweza kuimarisha afya yake kwa kupunguza msongo wa mawazo, woga na mashaka kwa asilimia 96 kwa muda wa masaa manne mfululizo.
Hata hivyo, wamebainisha kuwa mtu akitumia muda huo huo kuzungumza mambo mazuri ya watu wengine, atapunguza msongo wa mawazo kwa asilimia 72 ikimaanisha kuwa watu wenye kuzungumza mambo mabaya ndio wenye kunufaika zaidi.
Watafiti hao, wakifafanua hali hiyo wameelezwa kuwa mtu anapoongea habari nzuri zinazowahusu watu wengine huuchochea ubongo kutaka kujiunganisha na mtu anayezungumzwa, wakati yule anayezungumza habari mbaya huwa kinyume chake.
Mtu anayezungumza habari mbaya anatabia ya kutokuhifadhi alichokisema, bali huendelea na mambo yake kama kawaida, wakati anayezungumza habari nzuri hukaa nazo moyoni kwa kipindi cha muda fulani.
Mtaalamu wa Saikolojia kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Lusajo Kajula anasema binadamu wote huongea kuhusu watu wengine, lakini umbea ni zaidi ya maongezi.
Lusajo anasema asili ya mwanadamu ni kuzungumza japokuwa wakati mwingine hujikuta akiishia kutoa mifano halisi ya maisha ya watu wengine na hivyo kuingia katika mgogoro wakati mtu aliyesemwa anaposikia.
“Umbea ni kawaida na hauzuiliki, tatizo ni yaliyomo ndani ya umbea ambayo mara nyingi hutegemea na mawazo mtu aliyonayo. Kama ana mawazo hasi, ataongea mambo mabaya,” anasema Kajula.
Hata hivyo, Kajula anapingana na dhana iliyopo miongoni mwa watu kuwa mwanamke ndiyo anayependa zaidi tabia ya kuzungumza mambo ya watu wengine kuliko mwanaume.
“Kuna tafiti nyingi zinazoonyesha kuwa wanaume ni wambea zaidi kuliko wanawake, ila wao hawasutani na pia hawawezi kujieleza vizuri kama wanawake,” anasema Kajula na kuongeza kuwa kwa kawaida tabia ya kuongea mambo mazuri yanayowahusu watu wengine hukusudia kukuza heshima ya mtu anaezungumziwa.
Mwanasaikolojia na mwandishi wa kitabu kiitwacho ‘Nguvu ya Umbea’, Maria Konnikova anasema hakuna mtu anaeweza kuukwepa umbea na kushauri kuwa mtu asihangaike kutaka kuwazuia wambea kusema wayatakayo.
Anasema wataalamu mbalimbali wa masuala ya saikolojia wamebaini kuwa umbea ni njia muhimu katika kuleta umoja na mshikamano katika jamii kwani kwa kufanya hivyo husaidia kueneza taarifa ambazo wanajamii wasingeweza kuzifahamu.
“Pia imebainika kuwa umbea ni zana nzuri ya kuifundisha jamii mtu gani anafaa kuwa rafiki na yupi anastahili kuepukwa,” anasema Konnikova.
Mwanasaikolojia Homer Simpson wakati fulani aliwahi kusema: “Kama hatutakiwi kula nyama kwanini wanyama waliumbwa kwa nyama? Kama kila mtu anafahamu kuwa umbea ni mbaya kwa nini anasema? Jibu ni rahisi; katika ubongo wetu kuna sehemu inayopenda umbea.”
Anasema kila mtu ananufaika na mambo mazuri yanayosemwa juu yake anapoyasikia. “Wapi ungependa kufanya kazi, sehemu ambayo watu wanakusema vibaya au vizuri?”anahoji Simpson.
Mchungaji wa Kanisa la Free Pentekosti Tanzania (FPCT) Njia Panda ya Himo, Kilimanjaro, Elisante Ngailo, akizungumzia utafiti huo anasema watu wanaotumia muda mwingi kuzungumza mambo mabaya yanayowahusu watu wengine husema tu bila kufiria.
“Watu wa aina hii hawaumizi kichwa kufiri sana, wao husema mambo walioyasikia au kuyaona, kisha kuendelea na maisha yao,” anasema Ngailo.
Anaongeza: “Lakini hawa watafiti wanataka kutuambia kwamba sasa tuwaseme sana watu kusudi tupunguze msongo wa mawazo? Hili haliwezekanianasema Ngailo.
Kwa maoni yake si sahihi kwa watu kuwasema watu wengine vibaya na kwamba tafiti kama hizi hazijengi jamii kwa kuwa tabia ya umbea inapingwa na makundi mbalimbali ya watu.
Maoni ya watu mbalimbali
Roda Mgimwa mkazi wa Vingunguti anasema matokeo ya utafiti uliofanywa kuhusu tabia ya umbea anakubaliana nao kwasababu watu wa aina hiyo hawana hofu ya jambo wanalolizungumza.
“Wakati mwingine unaweza kumsikia mtu anasema umbea kuhusu mtu fulani ndani ya daladala bila kujua iwapo yule anayesemwa ana ndugu yake hapo au la. Kwa namna hii watu hawa hawawezi kusumbuliwa na msongo wa mawazo,” anasema Roda.
Elia Mwamwaja mkazi wa Kongowe anasema matokeo ya utafiti huo yanaweza kuwapa nguvu wambea kuwasema vibaya watu wengi zaidi hasa kila wakati wanapohisi wanamsongo wa mawazo.
“Sasa kuna watu watatumia umbea kama dawa, wakihisi wanamsongo wa mawazo watakuwa wanaanza kusema mambo mabaya hata kama sio ya kweli,” anasema Mwamwaja.
Hata hivyo, Mwamwaja anatoa angalizo: “Kwa mtu ambaye hakuwa na tabia ya umbea hawezi kuianza tabia hiyo leo kwasababu tu amesikia wanaofanya hivyo wanaweza kupunguza msongo wa mawazo.”.

UPINZANI WATAKA JK ASISAINI MUSWADA

Mshikamano wa vyama vya upinzani katika kupinga Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa 2013 umehamia nje ya Bunge na sasa vyama hivyo vimetangaza kuanza kampeni ya kuuhamasisha umma kudai maridhiano kabla ya kuendelea na mchakato wa Katiba Mpya.
Jana wenyeviti wa vyama hivyo; James Mbatia (NCCR-Mageuzi), Freeman Mbowe (Chadema) na Profesa Ibrahim Lipumba (CUF) walikutana na waandishi wa habari na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kutosaini muswada huo kuwa sheria, hadi pale kutakapokuwa na maridhiano ya pande zote husika.
Walisema muungano wao ni mwanzo wa kuunganisha umma wa Watanzania kufanya uamuzi wa kunusuru walichokiita “utekaji madaraka na mamlaka ya nchi kutoka kwa wananchi” hivyo wanaitaka Serikali kurekebisha kasoro zinazojitokeza katika mchakato huo.
Akitoa tamko la pamoja kwa niaba ya viongozi wenzake, Profesa Lipumba alisema wanachopigania ni kuurejesha mchakato wa Katiba Mpya mikononi mwa umma, kwa maelezo kwamba suala hilo kwa sasa limehodhiwa na CCM.
“Rais Kikwete asisaini muswada huu, aurejeshe bungeni ufanyiwe marekebisho yenye kujenga kuaminiana na mwafaka wa kitaifa kwenye mchakato wa mabadiliko ya Katiba. Hatutakwenda kumwona ila aurejeshe bungeni,”alisema Lipumba na kuongeza:
“Mchakato huu unahitaji uvumilivu, staha na hekima na usitawaliwe na nia mbaya, ubabe, mabavu, kejeli na dharau hasa kutoka kwa watawala. Misingi hii ikipuuzwa mchakato mzima unaweza kutumbukiza taifa letu katika mpasuko, migogoro na hata machafuko.”
Mwenyekiti huyo wa CUF alisema nchi ni mali ya watu, hivyo mchakato huo haupaswi kuhodhiwa na chama kimoja, badala yake  unapaswa kuwa shirikishi na jumuishi ili kuwezesha kuandikwa kwa Katiba katika msingi wa maridhiano.
Kuna madai kwamba muswada ulipitishwa ukiwa na marekebisho ambayo yalifanyika kinyume na maoni ya wadau na kinyume hata na makubaliano ya awali ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusu mamlaka ya Rais kuteua wajumbe Bunge Maalumu la Katiba.
Madai mengine ni kwamba wabunge wa CCM waliongeza baadhi ya mambo kupitia majedwali ya marekebisho, hivyo kutoa mwanya kwa Serikali inayoongozwa na chama hicho kupitia kwa Rais kuwa na mamlaka zaidi ya uteuzi wa wajumbe husika.
Itakumbukwa kuwa Septemba 6 mwaka huu, wabunge wa CCM walitumia wingi wao kupitisha muswada huo katika mkutano wa Bunge ambao ulisababisha tafrani kiasi cha Mbowe na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi kutolewa nje ya Bunge kwa amri ya Naibu Spika, Job Ndugai.
Katika tafrani hiyo, baadhi ya wabunge wa upinzani walirushiana makonde na maofisa usalama, huku wabunge wote wa upinzani, isipokuwa Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema, wakiususia.
 Chanzo  kutoka  gazeti  la  mwananchi.

KP Leo.


Mapya yafichuka kuhusu ghorofa refu karibu na Ikulu ya Dar.

SHAHIDI wa  tatu katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka katika ujenzi wa jengo la ghorofa 18, lililo karibu na Ikulu, Saimon Maembe ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Manispaa ya Ilala iliwanyima kibali washtakiwa katika kesi hiyo cha kuongeza idadi ya ghorofa kwenye juu.
Kesi hiyo inawakabili vigogo wawili wa Wakala wa Majengo (TBA) ambao ni aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa TBA, Makumba  Togolai Kimweri na Msanifu Mkuu wa TBA, Richard John Maliyaga.
Washtakiwa hao wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya kwa kutoa kibali cha kupanua jengo hilo kwa kuongeza ghorofa tatu zaidi kutoka 15 hadi 18, bila idhini ya mamlaka husika na bila kufuata Sheria za mipango miji.
Jengo hilo linalomilikiwa kwa ubia kati ya kampuni ya Royalle Orchard Inn na TBA, liko katikati ya Jiji la Dar es Salaam, katika mtaaa wa Chimara,  kitalu namba 45 na 46, karibu na Taasisi ya Saratani Ocean Road, katika  Manispaa ya Ilala.
Akitoa ushahidi wake jana Mchunguzi  wa kesi hiyo toka  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), alidai wakati anafanya uchunguzi wake aligundua kuwa  Manispaa ya Ilala ilikataa maombi ya washtakiwa hao  kujenga ghorofa 15.
Maembe alidai   licha ya kuwa Wizara ya Ujenzi kutoa waraka kwa TBA ikielekeza kuwa ni lazima ishirikishwe katika mchakato wa uendelezaji wa viwanja vinavyomilikiwa na TBA kwa niaba ya Serikali, hata hivyo washtakiwa hao hawakuishirikisha wizara hiyo katika mradi huo.
Maembe aliyekuwa akiongozwa na  Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leonard Swai, kutoa ushahidi wake alieleza kuwa alianza kufanya uchunguzi wa ujenzi wa jengo hilo   baada ya  Rais Jakaya Kikwete  na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutoa maelekezo kwa  Takukuru, na kwamba alikabidhiwa jukumu hilo na Kaimu Mkurugenzi wa Takukuru.
Alidai  wakati akifanya uchunguzi wake  alikwenda TBA ambako alipata nyaraka mbalimbali za mradi huo kama vile tangazo la zabuni ya ubia wa ujenzi wa jengo hilo, maombi ya wazabuni na taarifa ya tathmini ya zabuni hiyo.
Alizitaja nyaraka nyingine kuwa ni mihtasari ya vikao na uamuzi wa Bodi ya Zabuni ya TBA, mkataba wa ujenzi wa jengo hilo na vibali vya ujenzi, na kwamba kampuni ya Royalle Orchard Inn ndio ilishinda zabuni hiyo na kwamba  nilibaini kuwa vibali vya ujenzi vilitolewa na TBA, jambo ambalo lilimshangaza nikuona   kuwa vibali vya ujenzi vilitolewa na TBA wenyewe, kwa sababu haikuwa kawaida kwani kuna mamlaka zinazohusika na vibali vya ujenzi.
Maembe alidai kuwa katika  makubaliano ya ubia kati ya TBA na kampuni hiyo, walikuabaliana kujenga jengo kwa ajili ya makazi na biashara na kwamba jengo litakuwa ni la ghorofa 15.
Alidai kuwa kibali cha kwanza kilikuwa ni cha ujenzi wa ghorofa 15 na cha pili kikiwa ni cha upanuzi wa mradi kutoka ghorofa 15 hadi 18 na kwamba vyote vilitolewa na kusainiwa na mshtakiwa wa pili, Maliyaga.
Shahidi huyo alidai kuwa baadaye alikwenda Manispaa ya Ilala ambayo kwa mujibu wa Sheria namba  8 ya Mipango Miji ya mwaka 2007 ndio yenye mamlaka ya kutoa vibali, ili kuona kama walihusika kutoa vibali vya ujenzi huo.
“Kiongozi wa Idara ya Mipango Miji alieleza kuwa waliwahi (washtakiwa) kupeleka maombi ya kibali cha  kujenga ghorofa 15 lakini wakayakataa, kwa sababu hayakuendena na ramani ya mchoro wa eneo husika.”
Maembe alidai   baadaye alikwenda Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambayo ndio yenye uamuzi wa mwisho ya matumizi ya ardhi, na kwamba katika Idara ya Mipango Miji alipata ramani ya eneo husika ya mwaka 2000.

Bilionea wa Afrika awekeza sekta ya madini Kenya.


Miongoni mwa mabilionea wakubwa  Afrika ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa  Nigeria, Aliko Dangote amesema atawekeza dola za kimarekani milioni 400 katika sekta ya madini nchini Kenya.
Dangote ambaye aliwasili Kenya wiki iliyopita pamoja na  Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria, alisema yuko tayari kuwekeza katika sekta ya madini ya Kenya ili kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.
Waziri wa madini wa Kenya, Najib Balala alipongeza hatua hiyo ya Dangote na kufurahia ushirikiano wake na tume iliyoundwa na Serikali ya Kenya ya kuchunguza utaratibu wa utoaji leseni za kuwekeza katika sekta ya madini nchini Kenya. Balala  alitumia pia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji wengine katika sekta hiyo ya Madini,ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi.
“Namshukuru sana Dangote kwa kukubali kuwekeza katika sekta hii ya madini hapa Kenya kwani atatusaidia kukuza uchumi wa nchi yetu, pia natumia fursa hii kuwakaribisha wengine,’’ alisema  Balala.
Awali Kenya ilisema kwamba  itafuata moja kwa moja sera na mfumo wa udhibiti wa madini kama unaotumiwa na Tanzania kwa sababu mageuzi yaliyofanywana Serikali katika sekta ya madini ni dhahiri kuwa yameanza kuzaa matunda.
Kenya iliiwashauri Watanzania kuwa  ni vyema kupata Katiba Mpya, lakini Katiba peke yake haiwezi kuleta maendeleoya wananchi kwani maendeleo yataletwa na juhudi za wananchi wenyewe.
Chanzo   gazeti  la  mwananchi

JK na PK uso kwa uso leo UGANDA.

KP Leo


Rais Kikwete aongoza mazishi ya Askofu Kulola.

Rais Jakaya Kikwete ameongoza maelfu ya waombolezaji kumzika aliyekuwa Askofu Mkuu Moses Kulola wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT). Kiongozi huyo alizikwa jana nje ya Kanisa la Calvary Bugando.Licha ya kuongoza mazishi hayo, Rais Kikwete pia alitoa ushuhuda kwamba licha ya kuwa muumini wa dini ya Kiislamu, Askofu Kulola wakati wa uhai wake mara kadhaa alikwenda Ikulu kumfanyia maombi.
Rais Kikwete katika salamu zake za rambirambi, alisema amekwenda kushiriki msiba huo kuungana na waombolezaji kutokana na kumfahamu Askofu Kulola ambaye alikuwa mtu wa watu.
“Tuzidi kuwaombea kwa Mungu, familia katika kipindi hiki kigumu, kwa jinsi nilivyomfahamu marehemu alikuwa mpenda watu, hakujali kabila wala hali zao, alijali utu na heshima hii ndiyo sababu na mimi alikuwa rafiki yangu,” alieleza Rais Kikwete.
Alibainisha kwamba licha ya kuwa Muislamu mara kadhaa Askofu huyo alifika kumwombea Ikulu na katika maombezi yake alisisitiza kuwa alikuwa akiwaombea Watanzania na nchi nzima kwa ujumla, hivyo aliwahimiza walio hai kumuenzi Askofu kwa vitendo.

Liverpool , Arsenal zatakata EPL

Liverpool  1     Man  U  0



Arsenal    1   Spurs  0

More   results  visit :  http://www.premierleague.com/en-gb/matchday.html

Rais Obama achelewesha uamuzi wa kuivamia Syria


Rais Barack Obama amechelewesha kutoa uamuzi wa kuivamia Syria kijeshi baada ya kuazimia kulipeleka suala hilo bungeni ili liidhinishwe.Obama amechukua hatua hiyo wakati huu ambapo shinikizo la kuishambulia Syria na kumwondoa madarakani Rais Bashar al-Assad likizidi kushika kasi, kwa kile kinachodaiwa kuwa amekuwa akitumia silaha za sumu dhidi ya raia.

Mchakato huo unaendelea huku Rais wa Urusi, Vladmir Putin akimuonya Obama na kusema uvamizi wa kijeshi wa Syria ni suala lisilokubalika.Tayari Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amezishutumu Urusi na China kwa kushindwa kushirikiana na nchi za Magharibi kumaliza umwagaji damu nchini Syria na kuzilaumu kwa kudhoofisha jukumu la Umoja wa Mataifa.
Katika mahojiano na gazeti moja la Ujerumani yaliyochapishwa juzi,  Merkel alizishutumu Urusi na China kwa kutatiza juhudi za nchi za Magharibi za kuutatua mzozo wa Syria.
Nchi hizo mbili ambazo ni wanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walitumia kura yao ya turufu kupinga maazimio mara tatu kuihusu Syria tangu vita vizuke nchini humo zaidi ya miaka miwili iliyopita.
Urusi na China zinatarajiwa pia wakati huu kupinga azimio linaloungwa mkono na Marekani na Uingereza lililowasilishwa katika baraza hilo ambalo ndilo lenye mamlaka ya kuidhinisha hatua za kijeshi dhidi ya utawala wa Syria kutokana na  madai ya matumizi ya silaha za kemikali siku kumi zilizopita viungani mwa Mji Mkuu Damascus.
Chanzo  mwananchi

Mzee MANDELA arejeshwa nyumbani toka hospitali.




RAIS wa zamani wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela amerejea nyumbani kwake mjini Johannesburg kimya kimya baada ya kulazwa hospitali mjini Pretoria kwa muda mrefu.
Mandela mwenye umri wa miaka 95 alilazwa hospitali tangu Juni 8 mwaka huu baada ya kupata maambukizi katika mapafu.
Hali ya afya yake wiki iliyopita ilitajwa kuwa ‘mbaya lakini imara’ na haikutolewa taarifa tena kuhusiana na afya yake.
Maambukizi ya ugonjwa wake yanasemekana kuhusishwa na kipindi cha karibu miongo mitatu aliyokaa gerezani baada ya kufungwa kutokana na harakati zake za kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo.
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top