Social Icons

Loading...

UEFA CHAMPION LEAGUE GROUP DRAW.

JK ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA ASKOFU DR KULOLA.

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

Coat of Arms
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameshtushwa na kuhuzunishwa na taarifa za kifo cha Kiongozi wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Askofu Mkuu Moses Kulola ambaye ameaga dunia , Alhamisi, Agosti 29, 2013 katika Hospitali ya AMI iliyoko Masaki mjini Dar Es Salaam akiwa na umri wa miaka 84.
Rais kikwete ameelezea mshtuko na huzuni yake katika Salamu za Rambirambi alizomtumia Katibu Mkuu wa Kanisa hilo Bwana Brown Mwakipesile kufuatia kifo cha Askofu Mkuu Kulola. 
“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana na taarifa za kifo cha Mtumishi wa Mungu wa muda mrefu na Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Marehemu Moses Kulola kutokana na maradhi yaliyomfanya wakati fulani apelekwe hadi India kupatiwa matibabu” amesema Rais Kikwete.
Rais Kikwete amesema alimfahamu Marehemu Askofu Moses Kulola kwa miaka mingi wakati wa enzi za uhai wake, kama Mtumishi Hodari wa Kiroho aliyejitoa vilivyo katika kuwahudumia Waumini wa Kanisa lake ambapo mahubiri yake yametoa mchango mkubwa katika kuimarisha imani za Waumini wake na kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kudumisha amani na utulivu wa nchi yetu.
Aidha Rais Kikwete amesema kifo cha Askofu Mkuu, Moses Kulola kimeacha pengo kubwa siyo tu kwa Waumini wa Kanisa lake hapa nchini, bali pia miongoni mwa wapenda amani kote nchini na kwingineko duniani kwa vile enzi za uhai wake, Marehemu aliweza kufikisha ujumbe muhimu wa kiimani kupitia mahubiri yake kwa watu wa mataifa mbalimbali ndani na nje ya  Bara la Afrika.
“Kwa niaba yangu mwenyewe na Serikali ninayoingoza, ninakutumia wewe Katibu Mkuu wa Kanisa la Evangelical Assembies of God Tanzania, Bwana Brown Mwakipesile na Waumini wote wa Kanisa hilo Salamu za Rambirambi  kutoka dhati ya moyo wangu kwa kumpoteza Kiongozi muhimu wa Kiroho.  Ninawajulisha kuwa niko nanyi katika wakati huu mgumu kwa sababu msiba wenu ni msiba wetu pia. Sala na mioyo yetu iko nanyi wakati wa maombolezo ya kifo cha Kiongozi huyo shupavu wa dini. Nawaomba wote muwe wavumilivu na wenye subira kwani yote ni Mapenzi yake Mola”, amesema Rais Kikwete.

“Vilevile kupitia kwako, naomba unifikishie Salamu zangu za Rambirambi na pole nyingi kwa familia, ndugu na jamaa wa Marehemu, Askofu Mkuu, Moses Kulola kwa kumpoteza Baba, Kiongozi Shupavu na Mhimili wa familia.  Natambua fika kwamba hiki ni kipindi kigumu sana kwao cha maombolezo.  Natambua machungu yenu wakati huu na naungana nanyi katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aiweke peponi roho ya Marehemu Moses Kulowa. Amina.”
Mazishi ya Marehemu, Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) yatafanyika mjini Mwanza Jumatano ijayo tarehe 4 Septemba, 2013.  Heshima za mwisho kwa mwili wa Kiongozi huyo zitatolewa siku ya Jumamosi tarehe 31 Agosti, 2013 katika Kanisa laEAGT karibu na Hospitali ya Temeke kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana.   
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
29 Agosti, 2013

ASKOFU Dr: KOLOLA AFARIKI

 
Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania,   Dr.Moses Kulola amefariki dunia
leo tarehe 28/08/2013 katika hospital ya AMI (African Medical Investments) iliyopo
Slipway jijini Dar es Salaam.
Askofu ana watoto wengi wa kiroho nchini Tanzania, Kanisa  linahuzinishwa na habari
hizi, Bwana awape faraja kwa kipindi hiki,  "Kuishi ni Kristo na kufa ni faida"
Jina la Bwana libarikiwe.

LUKUVI: Wabunge wengi wamo orodha ya dawa za kulevya.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi amesema baadhi ya majina ya wabunge yametajwa miongoni mwa watu wanaoshukiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya lakini Serikali haiwezi kuwataja hadharani kwa haraka.
Majibu hayo ya Waziri Lukuvi yamekuja baada ya wabunge kumbana na wengine wakizomea baada ya kueleza ugumu wa kutaja majina ya washukiwa pasi na ushahidi wa kutosha.
“Serikali haiwezi kutaja majina haraka kiasi hicho kwani inaogopa kukurupuka na kushindwa mahakamani, hivyo lazima tuwe makini sana na jambo hilo. Hatuwezi kukurupuka tu eti ni fulani wakati hatuna vithibitisho.
“Kumbukeni wengine mpo humu ndani ya Bunge na tukianza wengi mtakwisha maana katika orodha hiyo kubwa na ninyi mmo na orodha ni kubwa kweli ambayo wakati mwingine inatakiwa umakini wa hali ya juu,” alisema Lukuvi alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Karatu (Chadema), Mchungaji Israel Natse.Katika swali lake ambalo lilisababisha kelele za kuzomea, Natse alitaka majina hayo yatajwe hadharani. Hata hivyo, hali ilitulia baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuingilia kati na kusema: “Hii tabia ya zomeazomea siitaki humu ndani, acheni tabia hiyo lazima mumsikilize mtu kwa kile anachokisema kwanza lakini mtindo huu si mzuri...”
Patashika hiyo ilitokana na swali la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Catherine Magige aliyetaka kujua iwapo Serikali inaweza kuwaambia Watanzania ukubwa wa biashara hiyo nchini na kama haioni kama kuna tatizo katika ukaguzi wa abiria na mizigo katika viwanja vya ndege na juhudi za Serikali kumaliza tatizo hilo.
Akijibu swali hilo, Lukuvi alisema ukubwa wa biashara hiyo hapa nchini unadhihirishwa na idadi ya Watanzania 274 waliokamatwa kati ya mwaka 2008 hadi Julai mwaka huu kwa kosa la kujihusisha na dawa za kulevya katika nchi mbalimbali za nje.
Alisema Serikali inafahamu ukubwa wa tatizo la matumizi ya biashara hiyo haramu ya dawa za kulevya nchini na alitaja takwimu za ukamataji wa dawa hizo katika kipindi cha kuanzia mwaka 2000 hadi Machi, 2012.
Alisema pamoja na kukamatwa kwa Watanzania hao nje ya nchi, wageni 31 wanashikiliwa mahabusu katika Magereza ya Keko na Ukonga, Dar es Salaam ambao ni raia wa Iran, Pakistan, Senegal na Afrika Kusini.
Hata hivyo, katika swali lake la nyongeza, Magige alisema uteketezaji wa dawa zinazotajwa kukamatwa umekuwa wa siri kiasi cha kutiliwa shaka kuwa huenda zinachukuliwa na maofisa waliozikamata ndiyo maana hakuna uwazi.
Chanzo: mwananchi

UDSM: No taking back students who sued us.

Students who filed a law suit against the University of Dar es Salaam have not being allowed back but seven of their counterparts who did not go to court and also offered official apologies have been permitted to resume classes in the academic year of 2013/2014.
This development adds to the on going saga that was sparked last year when the university’s management expelled 15 students and suspended 86 others for boycotting classes demanding 43 of their expelled colleagues be unconditionally reinstated.
But instead of rescuing their class mates, they too were expelled and the university ahas refused to allow them back short of an apology, several behavioural reports from their immediate supervisors and for those who seeked justice through the court system, they are not to return to class until the courts gives its ruling.
those who provided the reports and offered official apologies will resume classes but those who went to court will remain expelled because we cant intervene the court proceeding” said the University Deputy vice Chancellor (administration) Prof. Yunus Mgaya during an exclusive interview held yesterday in Dar es Salaam.
Among them were leaders of the students’ organization (Daruso) which include the speaker, Minister for Education and Academics Deputy Minister.

Earlier in January 2012, 15 students were expelled, apparently only seven offered apologies and received the clean reports from the Dean of students, the relevant Academic units and also official recognition from their District Administration recognising who they are and their residency.
Prof. Mgaya, a Marine Biology professor, made it clear that the University would not tolerate any behaviour that breaches their codes of conduct and threaten the campuses peace and tranquility in any way or form.
Affirming that the institute will not reinstate the students who filed the law suit to contest their expulsion, Prof. Mgaya remained adamant that they will not receive any leniency short of the court proceeding running their due course and then also for the students to provide the required behaviour reports.
what the university wants is for the students to provide behaviour reports from the Dean of students, heads of their various Academic units and also from their local government district officials as to authenticate their residency and communal profiles,” he asserted.
As for the seven who resume class following their apologies, the professor had this to say: “We will prepare conditions for them to meet. They will have to make sue they don’t breach our conditions otherwise they are out,”
He maintained that both continuing and incoming students must keep a peaceful environment to ensure education and other activities conducted by the university continue to run smoothly. As implicated by the don, any who would, for a reason or another, derail from this norm will be faced with stringent repercussions and that includes expulsion. 
SOURCE: THE GUARDIAN

KIBONZO


JK ataka vyuo vikuu nchini kudahili wanafunzi wengi.

Rais Jakaya Kikwete amevitaka vyuo vikuu nchini kuweka nguvu zaidi, kuhakikisha vinadahili wanafunzi wa shahada za juu ili kupata wahadhiri.
Akizungumza baada ya kutoa hati idhini kwa Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki vinane, Rais Kikwete alisema kufanya hivyo vitakabiliana na tatizo la uhaba wa wahadhiri linalovikabili hivi sasa.
“Pale kwenye upungufu tusisite kutafuta wataalamu wengine kutoka nje ya nchi. Wakati wa miaka ya 1970 tulipokuwa tunasoma pale Chuo Kikuu (Mlimani), tulikuwa na wahadhiri wengi kutoka nje,” alisema Rais Kikwete.Licha ya suala hilo, Rais Kikwete alisisitiza umuhimu wa vyuo hivyo kuwekeza kwenye utoaji elimu bora.“Ikumbukwe idadi kubwa ya wanafunzi haitoshi, lazima tuzingatie ubora. Tunataka mwanafunzi anayepata shahada nchini ajulikane popote anapokwenda,” alisema Rais Kikwete na kuongeza
Taarifa  kwa hisani  ya  mwananchi.

CAG apewa maagizo ya kukagua ufisadi wa bil 13.

Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC), imeiagiza ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalumu wa matumizi ya Sh13 bilioni, katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo Afrika (ADB) uliofanyika Mei mwaka 2012.
Uamuzi huo umekuja baada ya kubainika kwa matumizi mabaya ya fedha hizo, yaliyofanywa na Hazina kwa ajili ya ununuzi wa samani za ofisini na kompyuta ndogo 200.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zitto Kabwe alisema mbali na vituo hivyo, Hazina pia imenunua, seti za televisheni za ukutani, mashine za kuchapishia karatasi, viti na makochi ya sebuleni.
Alisema ingawa vifaa hivyo vimenunuliwa kwa fedha za Serikali, baadhi yake vimeachwa katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha, bila ya kuwapo kwa makabidhiano ya kisheria.
“Kamati imepata mashaka kuhusu matumizi ya Sh13 bilioni katika mkutano wa ADB, jambo lililotufanya tumuombe CAG kufanya ukaguzi maalumu wa matumizi ya fedha hizi za Serikali,” alisema Zitto.
zaidi  soma 

Huyu ndiye Trafiki Feki aliyekamatwa.

Wazo la LEO


Dr Mwakyembe aahidi kula sahani moja na wauza UNGA.

Siku moja baada ya kufanya ziara ya ghafla Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema leo ataweka hadharani majina ya watu wanaosafirisha dawa za kulevya nchini.
Dk Mwakyembe juzi alifanya ziara hiyo JNIA kukagua utendaji kazi kwenye uwanja huo ikiwa ni siku chache baada ya kutokea kashfa ya kupitishwa kwa dawa za kulevya na baadhi ya Watanzania wakiwamo wasanii kukamatwa sehemu mbalimbali duniani.
Aidha, hatua ya waziri huyo imekuja siku tatu baada ya ahadi aliyotoa akiwa Mwanza kwamba katika kipindi cha wiki mbili kuanzia juzi, atahakikisha anawakamata vigogo wote walio katika mtandao wa usafirishaji na uingizaji wa dawa za kulevya kupitia viwanja vyote vya ndege nchini.
Akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Vijana iliyoandaliwa na Taasisi ya Jitambue Foundation, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Nyamagana, Dk Mwakyembe alisema yuko tayari kufa katika vita hivyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake jana, Dk Mwakyembe alisema: “Kesho (leo) nitawataja wanaojihusisha na dawa za kulevya. Kwa sasa nakamilisha ushahidi wa kutosha ikiwa ni pamoja na picha za wahusika.”
Aliwaonyesha waandishi wa habari picha ya mtuhumiwa mmoja ambaye alisema alikamatwa saa nane baada ya waziri huyo kufanya ziara uwanjani hapo. “Ninataka watu wafahamu wanaoliingiza taifa hili katika aibu hii, ambayo inasababisha Watanzania wasiaminike katika viwanja vya ndege vya mataifa mengine.”
“Hatuwezi kuwa taifa la kuogopaogopa, hii ni vita ya kusafisha nchi yetu, kwani ni nani mwenye mkataba na Mungu kuwa ataishi milele?” alihoji Waziri huyo alipokuwa akijibu swali kuwa suala la kuwataja watu wanaowafichua wasafirisha unga linaweza likaweka rehani maisha yake.
“Kama hupendi joto usiingie jikoni”, alisema.
Akizungumzia watendaji wa JNIA kuhusiana na dawa za kulevya, alisema: “Mfanyakazi yeyote atakayebainika kuhusika kuwasaidia wasafirisha unga atafukuzwa kazi na ambaye atafanya juhudi ya kuwakamata wasafirishaji hao atapewa zawadi.”
“Kuna watu wanadhani tunafanya mzaha katika jambo hili. Jana baada ya mimi kuondoka usiku wa saa 2:30 huyu (kijana aliyekamatwa) akaingia na mzigo,” alisema Dk Mwakyembe na kuongeza kuwa alikamatwa na kete 86 za dawa aina ya heroini na misokoto 34 ya bangi aliyokuwa akiisafirisha kwenda Italia kupitia Zurich.
Aliiagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuwatunuku wafanyakazi waliofanikisha kukamatwa kwa kijana huyo.
Akizungumzia hali ya Uwanja wa JNIA baada ya kufanya ziara juzi, Dk Mwakyembe alisema tatizo halipo kwenye vitendea kazi, bali wafanyakazi wasiokuwa waaminifu.
Chanzo  gazeti    la mwananchi.

KP leo


Dr. Ndalichako aichanachana Elimu ya Tanzania.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Nchini (Necta), Dk Joyce Ndalichako amesema karatasi za majibu ambazo wamekuwa wakizipata kutoka kwa wanafunzi zinaonyesha kuwa, watoto wengi wanahudhuria shuleni lakini hakuna wanachojifunza.
Dk Ndalichako aliyasema hayo jana jijini hapa alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa mabaraza ya mitihani ya Afrika, ambao umejikita kujadili suala la tathimini ya elimu kwa nchi za Afrika.
Hii ni mara ya kwanza kwa Dk Ndalichako kuzungumza tangu Serikali itangaze kufuta matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 na kutaka yapangwe upya, suala ambalo lilipingwa na wadau wengi wa elimu.
Alisema kuwa wakati nchi nyingi za bara hili zikiwa zimejitahidi kuongeza upatikanaji wa elimu kwa watu, ubora wa elimu unaendelea kuwa tishio kwa watu wa bara hili kwa vizazi vijavyo.“Kama mabaraza ya mitihani, tumekuwa tukiona karatasi za majibu kutoka kwa wanafunzi ambazo zinaonyesha kwa uwazi kabisa kuwa watoto wanahudhuria shuleni lakini hakuna wanachojifunza,” alisema Dk Ndalichako.
Chanzo   gazeti  la mwananchi

TAARIFA YA POLISI KUHUSU TUKIO LA SHEIHK PONDA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI

JESHI LA POLISI TANZANIA 
DAR ES SALAAM AGOSTI 10, 2013.
1.  MNAMO TAREHE 10, AGOSTI ,2013 MAJIRA YA SAA 8 MCHANA, MAENEO YA SHULE YA MSINGI KIWANJA CHA NDEGE MANISPAA YA MOROGORO, KULIFANYIKA KONGAMANO LA BARAZA LA EID LILILOANDALIWA NA UMOJA WA WAHADHILI MKOANI MOROGORO. DAKIKA KUMI KABLA YA KONGAMANO HILO KUMALIZIKA  ALIFIKA SHEKHE PONDA ISSA PONDA AMBAYE ALIZUNGUMZA KWA MUDA MFUPI.
2. KONGAMANO HILO LILIFUNGWA  MAJIRA YA SAA 12:05 JIONI AMBAPO WATU WALIANZA KUTAWANYIKA, BAADHI YAO WAKIWA WAMEZINGIRA GARI DOGO ALILOKUWA AMEPANDA SHEKHE PONDA. BAADA YA KUTOKA KATIKA  ENEO HILO, ASKARI WA JESHI LA POLISI WALIZUIA GARI HILO KWA MBELE KWA NIA YA KUTAKA KUMKAMATA SHEKHE PONDA AMBAYE MPAKA SASA ANATUHUMIWA KWA KOSA LA KUTOA MANENO YA UCHOCHEZI SEHEMU MBALIMBALI HAPA NCHINI YENYE MLENGO WA KUSABABISHA UVUNJIVU WA AMANI.
3. BAAADA YA ASKARI KUTAKA KUMKAMATA, WAFUASI WAKE WALIZUIA UKAMATAJI HUO KWA KUWARUSHIA  MAWE ASKARI.  KUFUATIA PURUKUSHANI HIYO, ASKARI WALIPIGA RISASI HEWANI KAMA ONYO LA KUWATAWANYA.
4. KATIKA VURUGU HIZO, WAFUASI HAO WALIFANIKIWA KUMTOROSHA MTUHUMIWA.  HIVI SASA IMETHIBITIKA KUWA SHEKHE PONDA YUKO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI AKITIBIWA JERAHA KATIKA BEGA LA MKONO WA KULIA LINALODAIWA ALILIPATA KATIKA PURUKUSHANI HIZO.
5. KUFUATIA TUKIO HILO, TIMU INAYOSHIRIKISHA WAJUMBE KUTOKA JUKWAA LA HAKI JINAI IKIONGOZWA NA KAMISHINA WA JESHI LA POLISI  CP ISSAYA MNGULU IMEANZA KUFANYA UCHUNGUZI WA TUKIO HILO.
6. AIDHA, JESHI LA POLISI LINATOA  WITO KWA  WANANCHI KUWA WATULIVU WAKATI SUALA HILI LINASHUGHULIKIWA KISHERIA.
Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Jomo Kenyatta airport closed after major fire.

A major fire at Jomo Kenyatta International Airport (JKIA) has forced authorities to close it as fire crews attempt to put it out, kenya's airport authority says.No reports of casualities have been established yet and the actual cause of the Wednesday morning fire remains unclear.Kenya Airways tweeted: Esteemed Guests, JKIA is closed due to the unfortunate fire incident, all flights cancelled please don't come until we update soon.Images posted on Twitter and local TV show smoke and flames gushing from one of the main buildings.
Kenya Airports Authority (KAA) confirmed that the airport would be closed and passengers evacuated.
The airport authority sent out a statement confirming "reports of a fire at JKIA affecting part of [the] international arrivals building and Unit 1 departures.
"KAA Fire and Rescue Team is on [the] ground being assisted by G4S and Nairobi Fire Brigade. Passengers have been evacuated to safety."
One of the local media, Citizen TV, posted on Twitter that fire engines were "running dangerously low on water. Please give way to bowsers ferrying water to the airport".
 The fire at east Africa's busiest airport started at around 5.00am local time (EAT) in the immigration section of the departure lounge and spread to the international arrivals area, a Kenya Civil Aviation Authority official said on condition of anonymity. 
Source: http://www.newvision.co.ug/news/645819-jomo-kenyatta-airport-closed-after-major-fire.html

FAHAMU Salim Kikeke wa BBC wapi kapitia hadi kufika pale alipo.

Mtangazaji  wa  idhaa ya kiswahili BBC  Ndg Salim Kikeke.
Penye nia pana njia na mtafutaji makini huwa hachoki, ndivyo anavyosema mtaalamu wa masuala ya uchumi, Dk Wayne Dyer wa Marekani katika kitabu chake cha ufanye nini kupata unachokiazimia.
Licha ya kauli hii ya Dk Dyneer, kuna vijana wengi nchini wanaonekana wamekata tamaa; Wengine hufikiri kwamba kama umezaliwa katika familia duni, maana yake utakuwa na maisha duni milele, huku wale ambao wamezaliwa katika familia tajiri, wanafikiri wataendelea kuwa tajiri.Hata hivyo ukweli ni kwamba mtu yeyote anaweza kuwa na maisha bora, kama anavyosema msomi Hope Clark katika kitabu chake Fedha za Waandishi cha hivi karibuni nchini Ireland, kwamba siri ya kufanikiwa katika maisha ni kuishi kwa malengo, kuishi vizuri na watu na kupenda kuwa karibu na wasiokata tamaa.
Mwalimu Julius Nyerere wakati fulani amewahi kunukuliwa akisema  ‘Uchumi mnao, mmeukalia’. Kila mtu alitafsiri alivyoweza, lakini ukweli hasa ni kwamba mtu yeyote akijipanga vizuri kwa maana ya kutuliza akili yake, kukaa na watu wa kumshauri vizuri na kufanyia kazi mambo au mipango anayoipanga, anaweza kufanikiwa anachotaka...Ni ukweli kuwa kuna wengi wana maisha duni kwa sababu pamoja na mambo mengine ya tabia zao za kukata tamaa, waoga wa kuthubutu.

Kati ya vijana ambao wanaonekana kupambana hadi kuweza kujenga majina na heshima zao Duniani ni Salim Kikeke; Ni mtu ambaye kama angekata tamaa hakika asingefika aliko sasa.
Sasa amekuwa ni mtu wa kujadiliwa na umaarufu wake hauko tu Tanzania, bali maeneo mengi ya Dunia hasa kunakozungumzwa Kiswahili. Huyu mtu ni kati ya watangazaji wakongwe na kivutio cha watu wengi kutoka barani Afrika na duniani kote, lakini katokea wapi?
Taarifa  kamili   bofya   kikeke  

AMBAVYO WENGER HATOMSAHAU DROGBA ALIYEKATAA KUMSAINI KWA PAUNI 100,00 TU AKIWA KINDA TENA UFARANSA

KAMA Arsene Wenger alihitaji ukumbusho wowote wa kosa alilofanya katika usajili akiwa kazini Arsenal, Didier Drogba alifanya hivyo Uwanja wa Emirates Jumapili.
Mabao mawili ya Drogba ya dakika za lala salama dhidi ya Arsenal yaliyowezesha Galatasaray kubeba Kombe la Emirates yameendeleza rekodi ya mshambuliaji huyo dhidi ya The Gunners na kufika mabao 15 katika mechi 15.
Kwamba, katika dakika 1175 ambazo Drogba amecheza dhidi ya Arsenal, amefunga wastani wa bao moja katika kila dakika 78 na sekunde 20.
Ulikuwa usiku wa pigo kwa Wenger, ambaye alikataa kumsajili Drogba kwa Pauni 100,000.
Akiwa anachipukia nyota huyo wa Ivory Coast katika miaka yake minne Le Mans kati ya mwaka 1998 na 2002, jicho la skauti wa Wenger lilimnasa mchezaji huyo.
Wenger alikataa kumsajili, na Drogba akahamia timu nyingine ya Ligue 1, Guingamp akiwa ana umri wa miaka 23 kwa Pauni 80,000.
Wenger alisema mwaka 2009: "Tumemuangalia kwa umakini alipokuwa Le Mans. Siyo sisi tu tuliomuangalia. Lakini tulifikiri hawezi tayari kiasi cha kutosha. "Lilikuwa ni kosa, lakini ukiwa kwenye soka, kila mmoja anaweza kuelewa. Tulikuwa na Thierry Henry. Tulisema tutafuatilia maendeleo ya Drogba. Hatukuwahi kumkataa,"
Mwaka 2004, kufuatia msimu wa mafanikio makubwa akiwa Marseille, Drogba alisaini Chelsea kwa ada ya Pauni Milioni 24.
Kana kwamba hilo halikuwa pigo tosha katika jino la Wenger, Drogba aliifanyizia ile mbaya timu yake uwanjani.Alifunga mabao 13 katika mechi 14 dhidi ya Arsenal enzi zake akiwa Stamford Bridge, mengi kati yao akifunga katika mechi muhimu.
Wenger alipata ahueni wakati Drogba alipoondoka Chelsea kuhamia Shanghai Shenhua mwaka jana, akisema wakati huo: "Sijui ni kiasi gani Chelsea wamempoteza, lakini hatumkumbuki. Amefanya madhara mengi dhidi yetu katika kila mechi,".
Drogba anaweza kuwa ukingoni mwa soka yake akiwa na umri wa miaka 35 sasa, lakini kwa Emirates atabakia kukumbukwa kama kiboko ya timu ya Wenger hadi siku atakapotungika daluga zake.
Mfaransa huyo sasa atakuwa anaomba dua Arsenal isipagwe kundi moja na Galatasaray katika Ligi ya Mabingwa katika droo inayotarajiwa kupangwa mjini Monaco Agosti 29.
Taarifa  na  picha  kwa   hisani  ya bin Zubeiry.   
 

KP LEO


Tanzanian relations with Rwanda in 'difficult'.

Relations between Tanzania and neighbour Rwanda are strained, Tanzanian President Jakaya Kikwete has acknowledged against a backdrop of conflict in eastern Democratic Republic of Congo.
"Since the end of May, our relations with Rwanda have gone through difficult times," Kikwete said in a frank speech to the nation late Friday, criticising "statements by the leaders of Rwanda against myself and against our country".
At an African Union summit meeting in Ethiopia in May, Kikwete advised Rwanda, Uganda and DR Congo to open negotiations with rebel forces.
But in response, Kigali angrily suggested that Kikwete was speaking for the Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR), a Rwandan Hutu rebel group based in DR Congo.
"The relationship (with Rwanda) became difficult after my advice to the Rwandan government to talk to his opponents," said Kikwete, speaking in Swahili.
"I gave the same advice to the governments of Congo and Uganda," Kikwete added.
Tanzania has sent troops to join the UN peacekeeping force in eastern DR Congo, taking part in a special brigade to target multiple rebel forces there, including the FDLR as well as the M23, a mainly Tutsi group founded last year.
UN experts have accused Kigali of backing M23 fighters, claims that Rwanda strongly denies.
But Kikwete said he wanted to ensure "good relations" with Kigali.
"I would like to reiterate that I and the Tanzanian government have no bad intentions against Rwanda," Kikwete said.
Some accuse Tanzania of being close to the Rwandan opposition in exile, including Colonel Patrick Karegeya, Kigali's former intelligence chief now based in South Africa.
Karegeya and former army chief of staff Faustin Kayumba Nyamwasa, also exiled in South Africa, formed the opposition Rwanda National Congress three years ago, which calls for their former comrade President Paul Kagame to step down.
source : http://www.globalpost.com/dispatch/news/afp/130804/tanzanian-relations-rwanda-difficult

Rais Clinton atua nchini

Rais wa Mstaafu wa Marekani, Bill Clinton jana alifanya ziara katika makazi ya watu duni eneo la Vingunguti, wilayani Ilala Dar es Salaam, ambapo alikagua miradi midogomidogo ya wananchi inayofadhiliwa na mfuko wake (Bill Clinton Foundation).
Clinton alitembelea eneo hilo akitokea moja kwa moja Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam (JNIA), alipowasili akiwa katika ziara ya nchi mbalimbali za Afrika kukagua miradi inayoendeshwa na mfuko wake.
Katika eneo hilo rais huyo mstaafu alipokewa kwa shamrashamra mbalimbali ikiwamo ngoma za kiasili huku baadhi ya wananchi wakipigwa butwaa na kutoamini macho yao kwa kiongozi huyo kutembelea makazi yao.
Aidha, Clinton alipata wasaa wa kusalimiana na wakazi wa Vingunguti wakiwamo watoto ambao walishindwa kuzuia hisia zao wakijaribu kumsogelea, hali iliyomsukuma Clinton kuwasogelea na kuwasalimia kwa kuwashika mikono.
Maneno ya ‘Welcome Vingunguti Clinton‘ yalisisika kutoka kwa wananchi kuashiria kumkaribisha rais huyo wa 42 wa Marekani wakati alipowasalimia akitumia takriban dakika 15.
Clinton alikagua miradi ya midogomodogo ya wananchi iliyo chini ya mfuko wake ikiratibiwa na kutekelezwa na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (Plan) pamoja na Benki ya Barclays kupitia Vikoba.
Miradi aliyokagua ni pamoja na saluni za kinamama, ushonaji na chips ambapo pia alishuhudia mmoja wa wanachama wa vikundi hivyo akikabidhiwa mkopo wa Sh100,000 ambaye alieleza mbele ya Clinton kuwa atazitumia kwa mradi wa maandazi, hali iliyomfanya rais huyo na umati wa watu uliohudhuria kucheka.
Akizungumza katika ziara hiyo Clinton alizishauri benki nchini, kuwekeza kwenye vikundi vya kuweka na kukopa (Vikoba) akieleza kuwa ndiyo mkombozi kwa wananchi hasa wanawake.
“Nimekuwa kwenye miradi hii kwa miaka 30 kabla sijawa rais, hivyo basi najua umuhimu wake. Benki zinatakiwa zisaidie Vikoba kwani vikundi hivyo huwafikia wananchi kwa haraka na wepesi hivyo basi kunahitajika njia mbadala za kuhakikisha vinakuwa imara,” alisema Clinton na kuongeza;
“ Raha ya maendeleo ni kuona watu wanajitegemea wenyewe katika shughuli za kujiingizia kipato.”
Mmoja wa wananchi walionufaika, Zainab Paul ambaye ni mwanachama wa Kikundi cha Amani Hisa alisema kuwa kupitia Mfuko wa Bill Clinton na Vikoba ameweza kujikwamua kimaisha ikiwamo kumlipa mtoto wake karo ya shule.
“Kikundi chetu kina wanachama 30 na huwa tunanunua hisa kwa Sh2000 na kila mwanachama anaruhusiwa kukopa zaidi ya mara tatu,” alisema Paul.
Chanzo   Mwananchi
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top