Social Icons

Loading...

Mkurugenzi wa TCRA atoa kauli kuhusu mitandao ya kijamii.

Prof  JOHN  Nkomo
Siku za hivi karibuni, ongezeko la huduma za mawasiliano nchini limekuwa kwa kasi sana. Huduma za mawasiliano nchini katika kipindi kifupi zimekuwa sana na kuwafikia Watanzania wengi zaidi. Kutoka laini za simu za mkononi  milioni tatu tu mwaka 2000 hadi kufikia laini 28,000,000.  
Watanzania walio wengi hivi sasa wanafaidika kwa huduma za mawasiliano, yakiwemo mawasiliano ya simu za mikononi, utangazaji. Vile vile huduma za ziada kama kutuma na kupokea fedha kwa kutumia mitandao na simu za mkononi zimeongezeka maradufu. Wananchi wengi wanapata huduma za kibenki kwa kutumia simu zao, wanawasiliana kwa kutumia simu zao kupitia sauti, SMS na kadhalika.
Hali kadhalika kumekuwa na ongezeko la matumizi ya intaneti kwa watanzania walio wengi kutoka watumiaji laki tatu miaka mitatu iliyopita hadi watumiaji milioni 7.6 kwa takwimu za hivi karibuni. Wengi wa watumiaji wa intaneti matumizi yao ni katika kujifunza na kujielimisha pamoja na matumizi ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, BBM, LinkedIn na blog mbalimbali zinazotoa habari mbalimbali zikiwemo za kimaendeleo, burudani pamoja na michezo.
Matumizi haya ya intaneti yamewanufaisha watanzaia walio wengi kwani ni fursa murua ya kujifunza kupitia mitandao hiyo ya kijamii kwa kupata habari mpya, kujifunza na kuelimishana kuhusu shughuli za maendeleo na kuleta amani miongoni mwa watanzania.
Hata hivyo pamoja na maendeleo haya, kumekuwepo na baadhi ya watu wachache wanaotumia mawasiliano ya simu, mitandao ya kijamii, redio, TV na mawasiliano mengine kwa lengo la kuvuruga amani, kuchocheo vurugu, kuchonganisha watu, kusababisha ugomvi, kuwaumiza wengine kwa mambo yasiyo na ukweli, kupotosha jamii na hata kuvuruga maendeleo kwa ujumla.
Leo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inazindua kampeni ya kuelimisha umma kuhusu matumizi mazuri ya mawasiliano na inawatahadharisha wananchi kwamba kutumia mawasiliano vibaya kama ilivyoainishwa katika sheria ya Mawasiliano ya Kielectroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 ni makosa. Katika kampeni hii, Mamlaka inakusudia kuwasihi wananchi kuhakikisha wanatumia mawasiliano vizuri ili kudumisha amani, mshikamano na upendo miongoni mwa watanzania.
 Katika uzinduzi huu, Mamlaka imewaalika baadhi ya watumiaji mahiri wa mitandao ya kijamii ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watanzania walio wengi wanafaidika na mawasiliano. Miongoni mwao wako wamiliki wa blog mbalimbali, wasimamizi wa makundi mbalimbali katika mtandao wa FB na mengineyo. Nia ya Mamlaka ni kuomba ushirikiano kwao ili waweze kushiriki katika kampeni hii na kuwahamasisha mashabiki wao kutumia vizuri mitandao ya kijamii ili kunufaisha Taifa letu kwa matumizi mazuri.
 Watumiaji wa simu za mkononi na wananchi wote wanashauriwa kuunga mkono juhudi zinazofanyika ili kufanikisha kampeni hii kwa ajili ya kudumisha na kuendeleza amani na usalama na kuharakisha maendeleo ya sekta ya Mawasiliano inaendelea kuchangia uchumi wa Taifa na kuiweka Tanzania katika mazingira mazuri zaidi kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Tunawasihi wananchi na watumiaji wa huduma za mawasiliano kuwa wakipokea ujumbe wowote wa kueneza chuki, unaopelekea kuvuruga amani, uchochezi na kuvuruga amani, toa taarifa kwa vyombo husika, kisha futa ujumbe huo. Usiueneze kwa wengine kwani utakuwa sehemu ya uhalifu.

Ubalozi Marekani waipongeza TCCL kwa umakini

Serikali ya Marekani imeipongeza Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL, kwa kazi nzuri ya kusimamia mawasiliano wakati wa ziara ya Rais Barrack Obama wa nchi hiyo mwanzoni mwa mwezi huu.
TTCL ilipewa dhamana ya kusimamia mawasiliano yote tangu kufika kwa kiongozi huyo hadi kuondoka.
Ofisa Ubalozi wa Marekani nchini, Jeff Shrader alitoa pongezi hizo alipoongoza ujumbe wa maofisa wa ubalozi huo kutembelea makao makuu ya TTCL na kuzungumza na viongozi na wafanyakazi waliohakikisha kuwa sekta ya mawasiliano inakwenda vizuri na kwa ufanisi.
Ujumbe huo wa Marekani umeahidi kutoa vyeti kwa kutambua mchango wa TTCL na wafanyakazi wake hivi karibuni.Mkuu wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Peter Ngota aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa kampuni hiyo imepata faraja kubwa kwa kupata mrejesho huo kutoka Serikali ya Marekani.
“Tumepata faraja…hii inaonyesha uwezo wetu kitaaluma na ubora wa vifaa tulivyonavyo katika kutoa huduma za mawasiliano,” alisema.
Alisema kuwa TTCL ilipewa sifa hasa kutokana na utaalamu, uchapaji kazi na weledi ulioonyeshwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa timu ya Wamarekani waliokuwa wakifanya kazi nayo.Ngota alisema kuwa kampuni hiyo itaendelea kufanya juhudi kuhakikisha inatoa huduma bora za kimataifa wa mawasiliano nchini.
Kampuni hiyo ya simu inaendesha na kusimamia mkongo wa taifa wa mawasiliano kwa niaba ya Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
Mkongo huo unalenga kuwezesha matumizi ya Tehama katika sekta mbalimbali hapa nchini kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

SAFARI YA STARS FAINALI ZA CHAN YAISHIA UGANDA

Ndoto ya Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kushiriki fainali za Afrika kwa wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) ‘zilipeperuka’ jana kwa kipigo cha mabao 3-1 kutoka Timu ya Taifa ya Uganda, The Cranes katika mchezo wa marudiano kwenye Uwanja wa Namboole, Kampala.
Safari ya Stars imepotea kwenye michuano hiyo itakayopigwa Afrika Kusini mwakani, baada ya kufungwa nyumbani na ugenini na kufanya matokeo ya jumla kuwa mabao 4-1.
Taifa Stars, ambayo ilishiriki fainali za kwanza za CHAN kule Senegal mwaka 2009 chini ya Kocha Mbrazil, Marcio Maximo, sasa itasubiri kucheza tena michuano hiyo mwaka 2016.Matokeo hayo yanaifanya Uganda kuendelea kuifunga Tanzania inavyotaka, kwani katika mechi 41 walizokutana, wameshinda mechi 25 dhidi ya mechi 11.
Katika mchezo huo, wenyeji Uganda wakicheza kwa kujiamini, walikuwa wa kwanza kulifikia lango la Tanzania katika dakika ya kwanza na sita baadaye waliandika bao la kwanza.
The Cranes walifunga bao hilo wakitumia makosa ya mabeki wa Stars walioshindwa kujipanga vizuri na kumruhusu Mpande Joseph kuruka juu bila kukabwa na kupiga kichwa mpira uliomkuta Kalanda Frank aliyemtungua kipa Juma Kaseja.
Uganda walirudi kwenye uongozi mwanzoni mwa kipindi cha pili kwa kufunga bao la pili lililotokana na kiki ya penalti ya Brian Majwegwa kutokana na beki wa Stars David Luhende kuucheza mpira kwa mkono alipokuwa kwenye harakati za kuondoa hatari.
Safari ya Taifa Stars kwenda Afrika Kusini ilizidi kupotea baada ya wenyeji Uganda kufunga bao la tatu kutokana na shambulizi la kushtukiza katika dakika ya 47.
Hakuna shaka, bao hilo lililofungwa na Frank Kalanda lilitokana na uzembe wa kiungo Abubakary Salum, ambaye jaribio lake la kutaka kuumiliki mpira mbele ya wachezaji wawili wa Uganda lilishindikana na hivyo kuwapa mwanya wa kufanya shambulizi la kushtukiza.
Bao pekee la Stars lilifungwa dakika ya 17 na Amri Kiemba kwa shuti la nje ya 18 akimalizia kazi nzuri ya winga Mrisho Ngasa aliyecheza vizuri kipindi cha kwanza.
Mbali na mabao hayo, Stars wangeweza kuwa mbele kwa mabao 2-1 katika dakika ya 35, kama siyo kiki kali ya umbali mrefu iliyopigwa na Ngasa na kugonga ‘paa’ la Uganda na mpira kurudi uwanjani.
Kipa na nahodha wa Stars, Kaseja alifanya kazi ya ziada kupangua shuti kali la Mpande Joseph, huku dakika ya 11 mpira wa kichwa kutoka wa beki Aggrey Morris ukipaa juu kidogo ya lango kufuatia kona ya Erasto Nyoni.

Walinzi wa amani Darfur wadaiwa hawana zana za kisasa .

Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), Dk Salim Ahmed Salim, amesema umahiri wa vikosi vya kulinda amani Darfur na kwingine Afrika unatia shaka, kwani vinakabiliwa na upungufu wa vitendea kazi ikiwamo zana za kisasa.
Kauli ya Dk Salim inakuja ikiwa ni siku chache baada ya kuuawa kwa wanajeshi saba wa Tanzania waliokuwa wakitumikia Vikosi vya Kulinda Amani vya Umoja wa Mataifa na Afrika (Unamid).
Wanajeshi hao waliuawa wakiwa katika majukumu yao na kundi la Wanamgambo, linalodaiwa kuiunga mkono Serikali ya Rais Said al-Bashar la Janjaweed.
Dk Salim alisema himizo la kutaka kubadilishwa kwa kifungu cha sita kwenda saba, liende sanjari na zana za kisasa ambazo waasi hao wanatumia ikilinganishwa na walinzi wa amani wanaotumia silaha za kawaida.
Chanzo:http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Walinzi-wa-amani-Darfur-wadaiwa-/-/1597296/1925656/-/cgb97e/-/index.html

Fuatilia VIBONZO ,Je UNAKUMBUKA NINI?




KUELEKEA UCHAGUZI 2015.

HUKU Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikiwa kimeweka bayana kwamba hakiungi mkono Serikali tatu kama Rasimu ya Katiba inavyoonyesha, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe ameibuka na kusema endapo Mabaraza ya Katiba yatawasilisha hoja za kuikubali, kuna uwezekano mkubwa wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 kukwama.
“Uwepo wa Serikali tatu utafumua mfumo mzima wa utendaji ndani ya Serikali. Hatuwezi tena kufanya uchaguzi wa Rais na wabunge 2015, hatuwezi kufanya chochote nje ya Katiba ya Serikali Tatu kwa kuwa kinachofuata ni kuunda Katiba nyingine inayohusiana na Serikali tatu.“Kama tutafanya uchaguzi, utafanyika kwa taratibu zipi, ipi itakuwa mipaka ya marais wa Serikali tatu, makamu na mawaziri wakuu, mfumo wa Mahakama, Tume ya Uchaguzi, utendaji wa Bunge na wabunge, yako mengi, sasa mpaka hayo yaingie kwenye Katiba,” alisema Chikawe juzi Dar es Salaam.
Alisema lazima CCM isimamie suala hilo kwa kuwa kukubali Serikali tatu kutaua Muungano ambao sehemu kubwa unalindwa na chama hicho tawala.
“CCM wamejipanga kama baraza na kusimamia hili la Serikali mbili ambalo lengo ni kuulinda Muungano. Litakapokuja hili la Serikali tatu, lazima Muungano uparaganyike,” alisema.Hata hivyo, kauli hiyo ya Waziri Chikawe inakinzana na ile aliyoitoa Juni 4, siku moja baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutangaza hadharani Rasimu hiyo.

TOZO YA KODI ZA LAINI YA SIMU

Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa akisisitiza jambo juu ya tozo la kodi katika laini za simu wakati alipokutana na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.Serikali yawataka wananchi kutokuwa na wasiwasi kuhusiana na mpango wa ukusanyaji wa kodi ya laini za simu.
 
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana  jijini Dar es Salaam.
 
Mgimwa amesema kuwa Serikali inaendelea kukutana na wadau mbalimbali ili kujadili na kupokea mapendekezo kuhusiana na dhamira ya Serikali kutoza kodi kutoka katika laini za simu.
Aliongeza kuwa Serikali ina nia njema ya kuongeza mapato yake ili kuongeza kasi ya kutoa huduma za msingi kwa wananchi wake hususani wa vijijini.
 
“Lengo hasa la kodi hii ni kuboresha huduma za msingi vijijini kama umeme, maji na barabara ambazo ni duni sana vijijini, hata hivyo tunafanyia kazi mapendekezo mbalimbali ya wananchi na wadau wenye mitazamo mbalimbali” alisema Dk. Mgimwa.
 
Aidha Dk. Mgimwa amesema kuwa hivi karibuni amekutana na chombo cha watoa huduma za mawasiliano (MoAT) nakujadiliana nao na kuwaahidi kuwa mapendekezo yao yatafanyiwa kazi.
 
Mkutano huo umekuja baada ya wadau mbalimbali kutoa malalamiko juu ya uwepo wa tozo ya kodi ya laini za simu ambapo mmiliki wa laini ya simu atatakiwa kulipia shilimgi 1000 kila mwezi mara kodi hiyo itakapo anza kutozwa.
Picha na Frank Shija – Maelezo

KIBONZO


VILABU TAJIRI DUNIANI TAKWIMU 2012/13


Mabomba ya kusafirisha gesi yatua Mtwara.

Meli kubwa kutoka China tayari imetua katika Bandari ya Mtwara kwa ajili ya kushusha mizigo ya mabomba ya gesi ili kuanza kwa kazi ya ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.Mmoja wa watumishi ndani ya Bandari ya Mtwara ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema zaidi ya magari 20 yanatakiwa kupakua mzigo wa mabomba zaidi ya 4,000 kutoka bandarini hapo na kusafirishwa kwenda Kiranjeranje Lindi kwa ajili ya zoezi zima la ujenzi wa bomba hilo.
“Hayo magari mliyoyaona ni miongoni mwa zaidi ya magari 20 yanayokuja kupakua mzigo wa mabomba ambayo ni zaidiya 4,000 kwa ajili ya kuyapeleka maeneo mbalimbali ikiwemo Kiranjeranje Lindi kwa ajili ya kufanikisha zoezi la ujenzi wa njia ya kusafirisha gesi, upakiaji unaendelea hapa Mtwara na Dar meli inapakuwa mzigo ili kupelekwa kwenye maeneo husika na upakuaji kwa mikoa yote unaendelea kwa amani,” alisema.Akizungumza na gazeti hili mmoja wa madereva wa magari maalumu kwa ajili ya kupakua mzigo wa mabomba,alisema wametokea Dar es Salaam na hii ni zabuni maalumu waliyoipata kwa ajili ya maandalizi ya kupokea mizigo na kupeleka yanakotakiwa hapo baadaye baadaye baada ya kukabidhiwa kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Chanzo : http://www.mwananchi.co.tz/-/1597570/1916578/-/104vy0r/-/index.html

UGANDA MWIZI AKIMATWA HUWA ANAPEWA KICHAPO NAMNA HII



Huyu  ni  mwizi  aliyenaswa  na  wanakijiji    nchini  Uganda  akijaribu    kuvunja  dirisha  la  nyumba  ili  aibe
Wanakijiji  walipomnasa  walianza  kwa  kumpa  kichapo  kikali  kabla  ya  kumfunga  miguu  na  kumburuza  barabarani  huku  wengine  wakiendelea  kumshushia  kichapo
Tizama   video  ya  kichapo
http://mwanahabariuswazi.blogspot.com/2013/07/video-huu-ndio-ukatili-na-mateso.html#ixzz2ZE2NX8Xm

Nini  maoni  yako  kwa  tukio  kama  hili  nchini  kwetu.

CHADEMA YAIBANA MBAVU CCM UCHAGUZI WA UDIWANI ARUSHA .

Chadema kimethibitisha umwamba wake katika siasa za Jimbo la Arusha Mjini, baada ya kutetea kwa kishindo kata zake nne kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika jana.
Katika uchaguzi huo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na ambao ulichukuliwa kama kipimo cha siasa za Arusha ambazo zimekuwa na mvutano mkubwa, Chadema kiliongoza katikia vituo vyote 136 vya kupigia kura Kata za Elerai, Kaloleni, Kimandolu na Themi.
Kata hizo zilikuwa wazi tangu mwaka 2011 baada ya Chadema kuwatimua wanachama wake waliokuwa madiwani Estomih Mallah(Kimandolu), John Bayo (Elerai), Reuben Ngowi (Themi) na Charles Mpanda (Kaloleni).
Matokeo
Katika matokeo yaliyotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi Kata ya Elerai, Obedi Meng’oriki mshindi alikuwa Jeremiah Mpinga wa Chadema aliyepata kura 2,047 dhidi ya 1,471 za Emmanuel Laizer wa CCM. Katika Kata hiyo kulikuwa na wagombea wengine ambao ni John Bayo (CUF; kura 302), Seif Shimba (CCK; kura 3) na Boisafi Shirima (TLP;1).
Katika Kata ya Themi, Kinabo Edmund wa Chadema aliibuka na ushindi baada ya kupata kura kupata kura 674. Msimamizi wa Uchaguzi Kata hiyo, Ezeka Mboya alisema Kinabo alifuatiwa na Victor Mkolwe aliyepata kura 326 na Lobora Ndarpoi wa CUF alipata kura 307.
Kata ya Kaloleni, Msimamizi wa Uchaguzi, Anna Ledisa alimtangaza Kessi Lewi wa Chadema kuwa mshindi kwa kura 1,470 dhidi ya Emmanuel Mliari wa CCM aliyepata kura 330 na Abbas Mkindi wa CUF aliyepata kura 275 na Ngilishi Pauli wa Demokrasia Makini aliyeambulia kura mbili.
Kata ya Kimandolu, Msimamizi wa Uchaguzi, Suleiman Kilingo alimtangaza Mchungaji Rayson Ngowi wa Chadema kuwa mshindi kwa kura 2,761 na kumshinda Edna Saul wa CCM aliyepata kura 1,163. Kwa matokeo hayo, Chadema sasa kimefikisha madiwani 12 wakati CCM kimebakiwa na kumi na moja na TLP kina wawili.
Ushindi huo wa Chadema una athari kwa nafasi ya Meya wa Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo kwani CCM kina wajumbe 14 tu kwenye Baraza la Madiwani, TLP wawili wakati Chadema sasa kimefikisha 15. Wabunge wa majimbo na wale wa viti maalumu pia ni madiwani.
Taarifa    fuatilia  hapa :  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/Chadema-yaitesa-CCM-uchaguzi-wa-udiwani-Arusha/-/1597332/1915258/-/ucnuquz/-/index.html

Daraja la Kigamboni 47 % ya ujenzi imekamilika

Ujenzi  huu  utaghalimu  zaidi  ya  Bilion 215   kati  ya  hizo  NSFF  imefadhili  kwa  60%  katika  mradi  huu wa  daraja kigamboni  jijini  Dar  es  Salaam  

GIS Course @ UDSM


Tiper yaipa Serikali gawio Sh1 bil

Kampuni  ya Kuhifadhi Mafuta ya Tanzania International Petroleum Reserves Limited (Tiper), imekabidhi hundi ya Sh1 bilioni kwa Waziri ya Fedha, Dk William Mgimwa, ikiwa ni kama gawio la Serikali mwaka unaoishia  Desemba 31, 2012.Kampuni hiyo inamilikiwa kwa pamoja kati ya Serikali yenye hisa asilimia 50  na Kampuni ya Uswisi ya Oryx Oil and Gas (OOG) yenye idadi hiyohiyo ya hisa.
Akikabidhi hundi hiyo kwa Dk Mgimwa jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Tiper, Daniel Belair, alisema gawio hilo litakuwa chachu ya maendeleo ya uchumi nchini.“Tunayo furaha kukabidhi hundi hii yenye thamani ya Sh1 bilioni,  ikiwa ni wajibu wetu kisheria kama kampuni. Tunaamini mchango wetu utasaidia kuchochea uchumi wa taifa,” alisema Belair.Alisema Tiper inatarajia kuongeza zaidi uwezo wa kuhifadhi mafuta na kufikia zaidi ya lita za ujazo 290,000 ifikapo mwaka 2015,  baada ya uwekezaji Dola 12 bilioni za Marekani.Belair alisema hivi sasa Tiper ina kituo kikubwa cha kuhifadhi mafuta nchini,  chenye uwezo wa kuhifadhi zaidi ya lita za ujazo 141,000 ikilenga kufikia lita za ujazo 215,000.“Katika uwekezaji mpya, tangi mbili zenye uwezo wa kuhifadhi lita za ujazo 36,600 zimeshaongezwa katika robo ya kwanza ya 2013,” alisema Belair na kuongeza:“Kipaumbele chetu kikubwa ni kuhakikisha kuwa bidhaa za mafuta ya petroli zinapatikana katika soko muda wote.”
Chanzo    mwananchi

Nelson Mandela 'responding to treatment' - Jacob Zuma

President Zuma's statement urged the public to continue "providing support and showering him with love".People who have seen him say he remains responsive."We are encouraged that Madiba is responding to treatment," said President Zuma, referring to Mr Mandela by his clan name.
The head of Mr Mandela's Thembu tribe, King Buyelekhaya Dalindyebo, told the AFP news agency on Wednesday that he was "conscious" when he visited his hospital in Pretoria."He could not talk, but he recognised me and made a few gestures of acknowledgement, like moving his eyes," he said.

Source:  http://www.standardmedia.co.ke/?articleID=2000088098&story_title=Kenya-mandela-responding-to-treatment

Google improves search, navigation features in map apps,

Users of mobile devices running Google's Android operating system can now expect easier search and navigation in more than 100 million places with Google's new Maps for Android app.
  Google said the latest iteration of its app promises not just a streamlined design but also the information the user will need, "when and where you need it.""The search box at the top enables you to explore more than 100 million places globally ­­ making it easy to pinpoint businesses and/or points of interest with addresses, phone numbers, and reviews from people you trust," it said.
  Users can swipe the info sheet at the bottom to scroll through each result, or tap the “list” icon for a full list of results.Also, an interactive “info sheet” at the bottom of the screen can offer complete details about each place, ranging from star ratings to store hours.
  Other features of the new map app include:
  • 3 billion miles of turn-­by-­turn directions, globally
  • 1 million transit stops in 800 cities globally
  • 1 billion square feet (and growing) of indoor floor plans of airports, malls and more
New navigation feature
  Included in the latest app is a Navigation function, though still in beta, that features voice-guided, turn­-by­-turn navigation.A user can also swipe the navigation banner at the top to preview upcoming turns on the map, or use the step-­by­-step list view.Meanwhile, multiple views can make the map more relevant to a user, who can tap the Views menu on the bottom right to add new layers of information on the map."Explore the world's terrain from afar with high­def satellite imagery, and easily find public transit routes when you're visiting a new city," Google said.
Source:

RASIMU YA KATIBA 2013

KIBONZO ; TRAFIKI AKIWA KAZINI


TAMASHA LA MATUMAINI WABUNGE WA YANGA WAIFUNGA WABUNGE WA SIMBA 4 - 3










WENGER WAMNASA GONZALO HIGUAIN .

ARSENAL jana usiku walivunja rekodi yao ya usajili baada ya kukubaliana na Madrid kulipa kiasi cha  £23million kwa ajili ya kumsaini Gonzalo Higuain.

Muargentina huyo atafanyiwa vipimo na Gunners leo na anategemewa kusaini mkataba wa miaka 3 wenye thamani ya100,000 kwa wiki.

Higuain, 25, amepewa ruhusa na Madrid kusafiri kwenda London baada ya mazungumzo marefu yaliyodumu kwa wiki kadhaa.

Dili hili ambalo limethibitishwa na baba yake Higuain linakuja kuleta nafuu kwa mashabiki wa Arsenal waliokuwa wakililia kocha wao asajili wachezaji wa daraja la dunia, ili kuweza kukata kiu ya zaidi ya miaka nane ya kutwaa kombe.

Santiago Cazorla ndio alikuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya Arsenal - akiwa amesajiliwa kwa zaidi ya paundi millioni 16 akitokea Malaga.



Golikipa Julio Ceasar ndio anatajwa kumfuatia Higuain kwenda Emirates akitokea QPR ambao wameshuka daraja.
Taarifa  kwa  hisani  ya  blog ya  Shaffih

KP LEO


Banda la Wizara ya MALIASILI na UTALII







Banda la UDSM katika maonesho ya 37 ya Kimataifa Dar es Salaam.







KIBONZO


WACHINA WAKABIDHI UWANJA WA TAIFA

   Balozi wa China, Lu Youqung akimkabithi mfano  wa ufunguo  Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara.
  Muonekano  wa  uwanja  wa  Taifa  wa  Dar  es   salaam.

Egyptian Army Overthrows President in Coup.

Egypt's first democratically elected president was overthrown by the military Wednesday, ousted after just one year in office by the same kind of Arab Spring uprising that brought the Islamist leader to power.
The armed forces announced they would install a temporary civilian government to replace Islamist President Mohammed Morsi, who denounced the action as a "full coup" by the generals. They also suspended the Islamist-drafted constitution and called for new elections.
Millions of anti-Morsi protesters around the country erupted in celebrations after the televised announcement by the army chief. Fireworks burst over crowds in Cairo's Tahrir Square, where men and women danced, shouting, "God is great" and "Long live Egypt."
Fearing a violent reaction by Morsi's Islamist supporters, troops and armored vehicles deployed in the streets of Cairo and elsewhere, surrounding Islamist rallies. Clashes erupted in several provincial cities when Islamists opened fire on police, with at least nine people killed, security officials said.
Read  more : http://www.newsmax.com/newswidget/Egypt/2013/07/03/id/513246?promo_code=F492-1&utm_source=Test_Newsmax_Feed&utm_medium=nmwidget&utm_campaign=widgetphase1

OBAMA AHITIMISHA ZIARA TZ KWA UFUNGUZI RASMI WA SYMBION POWER PLANT


OBAMA ATUA DAR.

Rais Barack  Obama   wa   Marekani aliwasili Dar es Salaam jana mchana ikiwa ni nchi ya mwisho katika ziara yake barani Afrika ikitanguliwa na Senegal na Afrika Kusini.

Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, Rais Obama alisema aliainisha mambo hayo wakati alipozungumza na mwenyeji wake huyo.

Alisema katika mazungumzo hayo, waligusia mradi wa mkubwa wa umeme uitwao Power Afrika wenye lengo la kuongeza kiwango cha umeme kinachozalishwa nchini na barani Afrika ili kupata umeme nafuu na wa uhakika utakaochagiza kuongeza uzalishaji na kukuza ajira.Nchi nyingine za Afrika ambazo zitanufaika na mpango huo ni Kenya, Ghana, Liberia, Nigeria na Ethiopia.Rais Obama alisema pia wamezungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo, ukuzaji wa demokrasia na utawala bora. Alimzungumzia pia mchezaji nyota wa mpira wa kikapu wa Tanzania, Hashimu Thabeet anayecheza katika Ligi Kuu ya Marekani (NBA), akiwa na timu ya Oklahoma Thunder ya Marekani, akisema hawakuzungumzia suala lake na kuahidi kufanya hivyo siku nyingine.Akijibu swali iwapo anaridhishwa na misaada ambayo nchi yake inatoa kwa Tanzania, Rais Obama alisema anafarijika kwa matunda yanayopatikana katika mapambano dhidi ya malaria, barabara mpya zinazojengwa na katika maeneo mbalimbali ya nchi.“Hatutoi dawa, bali tunajenga miundombinu ya afya, hatutoi chakula, bali kuwezesha nchi kujitosheleza kwa chakula pia tunasisitiza kubadilishwa kwa sheria mbalimbali ili kutoa fursa kwa sekta binafsi kuleta mitaji yao kwa wingi zaidi, lakini jambo la muhimu ni kuijenga Afrika,” alisema.



© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top