Social Icons

Loading...

MAGUFULI AMKANA SITTA .

Siku chache baada ya Waziri wa Afrika Mashariki Samuel Sitta kumhusisha Dk John Magufuli na kundi la urais la mwaka 2015, Waziri huyo wa Ujenzi, ameibuka na kupinga kauli hiyo, akisisitiza hafikirii kuwania nafasi hiyo.Waziri Sitta alinukuliwa na gazeti hili juzi akieleza kuwa wakati ukifika, yeye na rafiki zake Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Ujenzi, Dk Magufuli na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, watachagua mmoja wao watakayeona anafaa kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015. Alisema hayo juzi kwenye Kongamano la Mawasiliano katika Nyanja za Digitali la wanafunzi wa Idara ya Uhusiano na Masoko, Chuo Kikuu cha St. Augustine (SAUT), Mwanza.
  Kabla ya hapo alikuwa amewataja rafiki zake hao wakati wa hafla ya kuchangia Kanisa Katoliki, Josephine Bakita, Parokia ya Igoma, Mwanza, Jumapili iliyopita.
Alisema hatagombea tena ubunge mwaka 2015, baada ya kuwa katika ulingo wa siasa kwa miaka 35 na badala yake ataangalia namna nyingine ya kuwatumikia wananchi huku akigusia mchakato wa kuwania urais ambao alieleza anamwachia Mungu.
Soma  zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1866444/-/12u9pof/-/index.html

Mwalimu ajifungua watoto 5 kwa mpigo, waishi kwa saa kumi na kufariki dunia .

MWALIMU Sophia Mgaya(28) mkazi wa Ruhuwiko mjini Songea mkoani Ruvuma aliyejifungua watoto watano kwa wakati mmoja kwa njia ya upasuaji mnamo Mei 25 mwaka huu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea na watoto hao kuishi kwa muda wa masaa kumi kabla hawajafariki dunia ameruhusiwa kutoka hospitalini hapo.
Akizungumza na Demashonews kwa njia ya simu Sophia Mgaya akiwa nyumbani kwake Ruhuwiko mjini Songea alisema alilazimika kuomba kutoka wodini kwa sababu alikuwa akijisikia uchungu anapowaona wanawake wenzake wodini humo wakiwakumbatia watoto wao baada ya kujifungua huku wa kwake wote wakiwa wamefariki dunia baada ya kuzaliwa. 
           Alisema kuwa muda wote aliokuwa hospitalini hapo baada ya watoto wake kufariki huku akiwa bado anauguza kidonda cha upasuaji aliofanyiwa alikuwa akilia muda wote anapowaona wanawake wenzake waliojifungua wakiwakumbatia na kuwanyonyesha watoto wao hivyo akaamua kuomba aruhusiwe kutoka hospitalini hapo. 
 ‘’Niliomba kuruhusiwa kutoka hospitali na kwenda kujiuguza kidonda nyumbani kwa sababu ya uchungu na majonzi niiiyokuwa nikiyapata wodini hapo ninapowaona wanawake wenzangu waliojifungua wakiwakumbatia na kuwanyonyesha watoto wao huku wa kwangu wakiwa wameshazikwa”alisema Bi.Mgaya
Chanzo :  http://www.jukwaahuru.com/?p=16011

Simu zisizosajiliwa mwisho 31 Mei 2013.

Mamlaka ya Mawasilino Tanzania, TCRA, imesema watumiaji wa simu ambazo hazikusajiliwa, watakatiwa mawasiliano ifikapo Juni Mosi mwaka huu.
Tamko hilo lilitolewa jijiji Mbeya na Mkurugenzi wa Sheria na Leseni wa mamlaka hiyo, Elizabeth Nziga wakati wa semina kuhusu utekelezaji wa sheria mpya ya mawasiliano ya elektroniki na posta ya mwaka 2010 kwa wadau mbalimbali.Hiyo ni awamu nyingine katika mipango ya TCRA, kwani awali ilikuwa na kampeni za kuzima mitambo ya analogia nchi nzima na kuwataka wananchi kuingia katika mfumo wa dijitali ulioanzia katika Mkoa wa Dar es Salaam Desemba 31, mwaka jana.
Mikoa mingine iliyoingia kwenye mfumo wa dijitali ni Arusha, Tanga, Dodoma, Mbeya na Mwanza. Nziga alisema mamlaka hiyo inasisitiza kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa makubaliano kati yake na watoa huduma za mawasilino ya simu na kufikia usiku wa Juni Mosi, namba za simu ambazo hazikusajiliwa zitakoma. Mmiliki wake hataweza kuitumia kupiga wala kupokea siku.
Chanzo  gazeti  la mwananchi .

Bayern 2 Borussia Dortumond 1 - YATWAA UEFA CHAMPIONS CUP.


TAARIFA TOKA IKULU

WARSHA YA WAZI KUJADILI MATOKEO YA UCHAMBUZI WA KINA WA MAENEO YA KIPAUMBELE YA KITAIFA
MGENI RASMI MHE. RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR JAKAYA KIKWETE
Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (Ikulu) inawatangazia na kuwaalika wadau na wananchi wote kuhudhuria Warsha ya Wazi (Open Day) kupata maelezo, kujadili na kutoa maoni juu ya miradi na program zitakazotekelezwa na Serikali kwa kipindi cha miaka mitatu (2013/14 hadi 2015/16) katika maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12-2015/16). Miradi hiyo inatokana na uchambuzi wa kina uliofanywa na wataalamu wa kitanzania kwa kutumia mfumo mpya wa kimaabara (labs)
Huu ni mfumo ambao Serikali imeuanzisha ili kuhakikisha ushirikishwaji mpana wa wadau na wananchi kwa ujumla katika utekelezeaji wa miradi ya kipaumbele ya Kitaifa.
Warsha hiyo ya wazi itafanyika ijumaa tarehe 24/05/2013 katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar Es Salaam kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Wote mnakaribishwa!
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano
Ikulu
DAR ES SALAAM

STYLE MPYA YA KUJISOMEA.


Stars wamwagiwa 30Mil.


Mwenyekiti wa Kamati ya Timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars), Mohamed Dewji (wa tatu kulia) pamoja na wajumbe wengine wa kamati hiyo wakiwakabidhi Meneja wa timu hiyo, Taso Mukebesi (kushoto) na Nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja (wa pili kushoto) sh. mil. 30 kwa ajili ya kuwapa hamasa wachezaji na viongozi wa timu hiyo  kuelekea  mechi  dhidi ya  SIMBA  wa  milima  ya  ATLAS   Morroco.

Kikwete atoa msimamo mkali.

Rais Jakaya Kikwete amekemea vikali vurugu zilizotokea jana mkoani Mtwara baada ya kusomwa bungeni kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.
Akizungumza katika eneo la Kizota, Dodoma wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara ya Dodoma kwenda Iringa, Rais Kikwete alisema wote waliohusika na vurugu hizo watasakwa na kuchukuliwa hatua kali.
Rais Kikwete alisema rasilimali inayopatikana mahali popote pale nchini inatakiwa kutumiwa na Watanzania wote... “Hivi watu wa Nyarugusu wadai dhahabu ya pale au kinachopatikana Chalinze basi kisitumiwe na watu wa Morogoro! Hivi tutakuwa na taifa kweli?,” alihoji kwa ukali Rais Kikwete.
Rais Kikwete alisisitiza kuwa Serikali itawasaka wale wote wanaoongoza vurugu hizo na watawajibishwa kwa makosa hayo... “Tutawasaka hawa watu na viongozi wao hata kama wana mapembe kiasi gani, tutayakata.”
Alichosema Waziri Muhongo
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema mradi wa kusafirisha gesi kutoka mkoani Mtwara kwenda Dar es Salaam, umeanza kwa kasi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atakwenda huko wiki ijayo kuweka jiwe la msingi.
Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini jana, Waziri Muhongo alisema:
“Mradi wa kujenga bomba la gesi uko palepale na unaendelea kwa kasi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ataenda kuweka jiwe la msingi wiki lijalo.”
“Tumezungumza mengi kuhusu suala hilo na hata viongozi wa watu wa Mtwara walipelekwa nje kujifunza faida zake, lakini hata kama hawajaelewa, nimetoa kijitabu kinachozungumzia faida mbalimbali watakazopata wana Mtwara katika mradi huo.”
Profesa aliyeanza hotuba yake kwa kueleza machapisho mbalimbali yaliyotolewa na wizara yake kufafanua faida za gesi ya Mtwara kwa taifa, alisema mradi huo uliozinduliwa Novemba mwaka jana na Rais Kikwete, unahusisha ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 532 na kipenyo cha nchi 36.
“Bomba hilo lina uwezo wa kusafirisha futi za ujazo za gesi milioni 784 kwa siku. Mradi utahusisha mitambo miwili ya kusafirisha gesi asilia katika maeneo ya Mnazi Bay- Madimba (Mtwara) na Kisiwa cha Songosongo (Lindi). Utagharimu Dola za Marekani 1,225.3 milioni,” alisema.
Alisema kazi za usanifu wa mradi na ulipaji fidia kwa wananchi wapatao 3,092 waliopisha maeneo ya mradi, zimekamilika na hatua za awali za ujenzi wa mitambo ya kusafirisha gesi asilia zimeanza.

OBAMA KUZURU AFRIKA JUNE 26 MPAKA 2 JULAI 2013.

Rais  OBAMA  na  Mkewe wanatarajia  kuzuru    nchi za  Senegal, Afrika  kusini  na  Tanzania  kuanzia  June  26  mpaka  Julai 3  mwaka  huu.

IBM EAST AFRICA CONDUCTED KNOWLEDGE TRANSFER WORKSHOP @ UCC MBEZI BRANCH .

 Group  photo   involves  few  participants  from Ucc.
Mr  AMIT    DAVE  , Technical  Sales  Executive   Systems & Technology  Group   IBM  East  Africa  Ltd  briefing  during  the  workshop  on IBM  core  Products  and  Services.

Mchungaji Msigwa, wenzake 49 wapata dhamana.

Prof J ajiunga CHADEMA.



Vurugu kubwa kati ya Polisi na Wamachinga - Iringa

Mji wa Iringa uligeuka kuwa uwanja wa vita kati ya polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wafanyabiashara jana asubuhi. Watu 50 walikamatwa kutokana na tukio hilo akiwamo Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa.
Katika vurugu hizo, gari la zimamoto lilivunjwa kioo na gari lingine dogo liliharibiwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamhanda alisema Mchungaji Msigwa alikamatwa saa saba mchana kwa tuhuma za kuhusika na vurugu hizo na kwamba watu wapatao 50 walikuwa wamekamatwa katika fujo hizo zilizochukua karibu saa tatu.
“Mchungaji Msigwa amekamatwa kwa makosa ya uchochezi, kufanya maandamano bila kibali na kuhamasisha watu kufanya biashara kwenye eneo ambalo limekatazwa kisheria.
Tumemkamata na hatutamwachia hadi uchunguzi wa suala hili utakapokamilika. Pia na hao watu wengine,” alisema Kamanda Kamhanda.
Alisema waliamua kufanya doria katika eneo hilo baada ya kupata taarifa za kiitelijensia kuwa wafanyabiashara walikuwa na mpango wa kuwashambulia mgambo wa Iringa kama wangekwenda kuwazuia.
Vurugu hizo zilichangiwa na mvutano uliokuwa unafukuta kwa muda mrefu kati ya Uongozi wa Manispaa na Mbunge huyo kuhusu amri ya kuzuia watu kufanya biashara kwenye Barabara ya Mashine Tatu, Iringa.


 Chanzo  na picha  kwa  hisani  ya   http://www.kajunason.blogspot.com/

With With WhatsApp, Skype, who needs SMS?

Telecom companies are rushing to boost their internet services as the growth in mobile applications makes communication gradually cheaper.
The increased use of internet-based services, mostly social networking applications such as Facebook, Twitter, WhatsApp, Skype, Viber, Tango and MySpace, has attracted many people.“Most of the communication that I have to make is through the internet unless I really need to make an urgent call. I think that nine out of 10 times that I am on my phone I am either on twitter or Facebook or checking my e-mail. WhatsApp is one of those applications that I cannot do without. I can’t remember the last time I sent a text message,” said an internet user who declined to be named.
The trick is in the price. While it takes about Shs 130 ($0.05) to send one SMS, one is able to send far more messages using WhatsApp for the same amount of money. Since WhatsApp is internet-based, it works across all networks. And while it takes about Shs 500 ($0.19) to make a call that lasts not more than three minutes, it could easily take you more than 30 minutes on Skype.
The mobile phone applications also come with more benefits. Attaching pictures, songs and videos is made easier using these simple applications. Michael Niyitegeka, a former lecturer at Makerere University’s college of Computing and Information Sciences, who is now an IT consultant, believes telecom companies need to satisfy this market.“Users are moving faster than the telecoms. The telecoms have not yet figured out a business model (for this market),” he said.
The growth of social networking sites was largely attributed to the feel it adds to the whole idea of communication.“There is a social attribute when one goes on the social networking sites because this communication changes the SMS messaging into a kind of a monologue,” he said.
The flipside of all this is that users need to have a smart phone. However, while smart phones used to be expensive, today they go for less than Shs 400,000. And some shops are selling used smart phones at far cheaper prices. Some companies are upgrading their data systems to tap into this growing market. Huawei Technologies, the service provider for Airtel, Warid and MTN, has been upgrading its network infrastructure to provide faster and cheaper internet.

Serikali yajipanga kudhibiti viroba.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda amesema wizara yake itachukua hatua za haraka ili kudhibiti matumizi ya pombe zinazowekwa kwenye pakiti maarufu kwa jina la viroba ambazo zinaathiri afya za Watanzania wengi.Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake bungeni Dodoma jana, Dk Kigoda alisema wizara yake itawasiliana na wadau mbalimbali ili kupata ufumbuzi wa suala hilo.Dk Kigoda, ambaye pia ni Mbunge wa Handeni, aliwataja wadau hao kuwa ni Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara za Afya na Ustawi wa Jamii, Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Fedha na wamiliki wa viwanda vinavyotengeneza pombe hizo. “Tumelipokea suala la matumizi ya viroba kwa uzito wa hali ya juu na tutatoa uamuzi wa haraka baada ya kufanya mazungumzo na sekta mbalimbali,” alisema Dk Kigoda.
Alisema wizara yake kwa kushirikiana na wizara nyingine itatafuta njia mbadala kuepusha madhara kwa wanaotumia viroba ambavyo alisema vina athari kubwa kiuchumi na kijamii.
Chanzo   gazeti  la  mwananchi.

CHELSEA WATWAA EUROPA CUP , YAIFUNGA BENFICA 2 - 1

Chelsea  2    Benfica 1

 

Mengi kugawa milioni 12 kwa vijana watakao-tweet kuhusu kuondoa umasikini .

Kwa muda mrefu sana, nimekuwa nikiamini kuwa, Watanzania tumekuwa tukijidanganya kudhania na kuendelea kuamini kuwa, maendeleo ya kiteknolojia yamekuwa sababu ya kuporomoka kwa maadili ya vijana wengi wa Kitanzania.
Na leo hii, mtazamo wangu umepata msukumo mpya baada ya kusoma kuwa, kwa kipindi cha miezi 12 kuanzia sasa, kuna Mtanzania mmoja ambaye ataweza kujipatia kitita cha shilingi za kitanzania milioni moja kutokana na matumizi ya mitandao ya kijamii. Unashangaa? Hapana, usishangae, maana ni ukweli mtupu…… iko hivi:-
Mmoja kati ya Watanzania ambao wamejijengea heshima kubwa sana katika jamii ndani na nje ya mipaka ya nchi, Mzee Reginald Mengi, ameahidi kuanza kutoa kitita cha shilingi milioni moja kila mwezi kwa Mtanzania ambaye ataandika kitu au wazo ambalo litakuwa na uelekeo wa kushinda vita dhidi ya umasikini, kupitia ukurasa wake wa twitter. 
Chanzo  fuatilia : http://www.jukwaahuru.com/?p=15693

Kibonzo.


Lugola: Spika anapendelea baadhi ya wabunge.

Wakati mkutano wa 11 wa Bunge ukiendelea mjini Dodoma, Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola (CCM), ameendelea kuwa mwiba kwa Serikali yake huku akisema hakuna wa kumnyamazisha kuhusu hoja za kutetea Watanzania, kwa mambo yasiyofaa.Katika mahojiano na Mwananchi Jumapili, mbunge huyo ameeleza ya moyoni kuwa amekuwa akipingana na hoja za Serikali ikiwamo inayohusu bajeti zake ambazo alisema nyingi zimewekwa kinadharia.
“Nashukuru kwa kutaka kujua ukweli juu yangu, mara nyingi watu wamekuwa wakinituhumu mimi na wabunge wengine kuwa tunaisaliti Serikali na chama chetu, huo ni unafiki maana wanaoisaliti ni hao wakina ‘ndiyo mzee,’’anaanza kusimulia.Swali. Nini maana yake unaposema wanaoisaliti CCM ni hao wanaokubali kila kitu, kwani kukubali na kupinga huoni ni tofauti na kwamba anayepinga ndiye msaliti.
Jibu: Ngoja nikwambie (mwandishi), sisi tunaopinga baadhi ya bajeti za wizara ndiyo tunaojua uchungu wa chama chetu kwa sababu tunataka chama kiendelee kubaki madarakani, lakini hao wanaopitisha pamoja na madudu si wema kwa chama hata siku moja, watakosa majibu siku ya mwisho.
Akitetea hoja hiyo anaeleza kuwa, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzim imeainisha mambo mengi yanayotakiwa kutekelezwa.Anasema hata hivyo baadhi ya wabunge wanafanya kila kitu kwa kujipendekeza bila ya kujua kwamba kupitisha madudu hakufanyi ilani itekelezwe kwa wakati.
Swali. Kwani usipounga mkono ndiyo mambo yanatekelezwa.
Jibu. Ujue kuwa wakati wa uchaguzi mkuu vyama huenda kuomba ridhaa ya wananchi waviunge mkono, jambo hilo linakwenda sambasamba na ahadi zisizotekelezeka, sasa usipokuwa makini na hizo bajeti, unadhani utafanyaje mwisho wa siku kama si kuambulia patupu.
Anasema bajeti nyingi za Serikali huwa hazitoi majibu hata kidogo, lakini wabunge wamekuwa wakiogopa kuzikataa kwa kuhofia kuwa wataambiwa wanapingana na Serikali yao.
Chanzo gazeti  la  mwananchi.

Facebook, mitandao ya kijamii huathiri watu kisaikolojia .

Facebook, mitandao mingine ya kijamii pamoja na huduma ya ‘blackberry mesenger’ maarufu kama BBM huathiri watu kisaikolojia, husababisha ndoa kuvunjika pamoja na usaliti katika uhusiano, wanasayansi wamebaini.Utafiti huo uliofanywa mwaka 2012 na wanasayansi wa nchini Israel umebaini kuwa kwa wastani, wanawake wanatumia dakika 81 katika mitandao ya kijamii kwa siku ukilinganisha na wanaume ambao hutumia dakika 64, huku watu wasio na elimu wakionekana kuathirika zaidi na mitandao hiyo.Watafiti hao kutoka Chuo Kikuu cha Tel Aviv walihusisha matukio kadhaa ya kisaikolojia kati ya watu walioathirika na mtandao na udanganyifu uliosababishwa na uhusiano unayoanzishwa kupitia mitandao ya kijamii.Utafiti huo ulibaini kuwa wote waliohusishwa walikuwa na tatizo la upweke, ingawa hakuna aliyekuwa na historia ya matumizi ya dawa za kulevya au matatizo ya kisaikolojia.Watu wenye upweke walionekana kupendelea kutafuta uhusiano kupitia mitandao, jambo linaloelezwa kusababisha kuwaumiza watu hao na kuhisi kusalitiwa.
Kiongozi wa utafiti huo Dk Uri Nitzan kutoka Chuo Kikuu cha Sackler mchepuo wa Tiba na Afya ya Akili, Shalvata Mental Health Care Centre alisema: “Kama ilivyo matumizi ya mtandao yanazidi kuwa makubwa. Vivyo hivyo inavyozidi kuhusiana na masuala ya saikolojia. Mawasiliano ya kompyuta kama Facebook na makundi ya mawasiliano yaliyopo ndani ni sehemu muhimu ya habari hii.”
Chanzo   http://www.mwananchi.co.tz/Makala/Facebook--mitandao-ya-kijamii-huathiri-watu-kisaikolojia-/-/1597592/1849998/-/tl3712z/-/index.html

Babu Sir Alex aingoza Man U dhidi ya Swansea na wapewa Kombe lao la EPL.

Man  U       2       Swansea    1




WIGAN Yatwaa FA yainyoa Man City 1 -0

Wigan    1  Man  City  0


City Branch UCC Watembelea Kurasini Home Children Centre

Branch  Manager  wa  Ucc City  Branch  Mrs Faith Shayo  akikadhi  sehemu  ya  msaada  wa  chakula   na  vifaa    kwa    Afisa   mkuu  Mfawidhi  wa  kituo  cha  Kurasini  Home  Children Center   Ndg   Ramadhani  Yahya.Kituo   hiki  kiko  chini  ya  serikali  ya   Jamhuri  ya  Muungano  wa    Tanzania ( URT)   kimeanzishwa  mnamo  mwaka  1966  na kwa  sasa  kinatunza na kulea   watoto  wenye  kuanzia  umri wa  miaka  3  mpaka   17   wapatao    zaidi  60.

  Afisa   Mfawidhi  wa  KHCC   Mr  Ramadhani  Yahya  akipokea   moja  ya  kifurushi    kwa   niaba  ya  watoto.
  Lango   kuu  kituo cha   serikali cha   Kurasini  Home Children Center  maskani ya  watoto    ambao walio  wengi   ni  yatima,waliotelekezwa au  kukataliwa  na  wengine  hata  wazazi/walezi  wao  hawajahi  kuwatia  machoni , ukiingia  ndani  ya  ukuta huu  utajifunza  mengi   toka  kwa   viumbe  hawa  ambao   ni  Taifa  la  leo  la  Tanzania.
PICHA   ZAIDI  TEMBELEA  http://ucctznews.blogspot.com

Usafiri huu hatari.


Tanzania yapeleka kikosi DRC

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania, Rais Jakaya Kikwete amewaaga wapiganaji wa Tanzania wanaokwenda DR Congo kulinda amani kwa kuwadhibiti waasi wa vikundi mbalimbali kikiwamo cha M23 walioko Mashariki wa nchi hiyo.
Kikwete alimkabidhi bendera kiongozi wa batalioni ya wapiganaji wa JWTZ wanaokwenda kujiunga na Jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani nchini humo katika hafla iliyofanyika Msangani, Kibaha, Mkoa wa Pwani jana. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange ni miongoni mwa mashuhuda katika hafla hiyo.“Ninawatakia kila la kheri kwenye mapambano,” Amiri Jeshi Mkuu alimwambia kiongozi wa Batalioni ya Wanajeshi wa JWTZ wanaokwenda nchini humo. Tanzania inaungana na Afrika Kusini na Malawi kufanya kuwapo kwa kikosi cha askari 3,100 huku Tanzania ikipeleka askari 850 kwa ajili ya kazi hiyo.
Vikosi vya awali vya Tanzania vimekwishatangulia nchini humo vikiongozwa na Jenerali James Mwakibolwa anayeongoza Brigedi hiyo chini ya UN, na tayari amewasili kwenye Mji wa Goma, ambao ndio Mji Mkuu wa Jimbo la Kivu ya Kaskazini unaokaliwa na waasi wa M23 tangu Aprili 2012.Kwa mujibu wa Mtandao wa Monusco, vikosi vingine vya wapiganaji wa Tanzania na Afrika Kusini vitawasili wiki ijayo wakati Wanajeshi wa Malawi haijafahamika tarehe ya wao kuwasili.Msemaji wa wapiganaji wa M23, Kanali, Vianney Kazarama alikaririwa akisema: “Tuko tayari kwa mapambano, wapiganaji wako kambini Rumangabo, wakifanya mazoezi makali ya kushambulia, kujilinda na mbinu za kukabiliana na adui pamoja na kucheza kung fu.
Chanzo   mwananchi .

Sir Alex Ferguson to retire from Manchester United at the end of the season after 26 years in charge.

Mawasiliano Tower Cafeteria ; Wadau wakipata MLO.

  Blogger    mchana   wa  leo    na  wadau  wa   Ucc   SED     Mawasiliano  Tower  Cafeteria.
            Raha  ya  mlo  ni  maongezi ,   baadhi ya  wafanyakazi  toka  kitengo  cha  SED  wakipata   kinywaji   baada ya  mlo. 

Trafiki na Dreva Ngoma Inogile.


BOMU ARUSHA : PENGO AFICHUA SIRI.

Kadinali Pengo alisema amepata taarifa kutoka kwa watu ambao hana na shaka nao.
“Jana (juzi), niliongelea kwamba suala zima la tukio la Arusha halihusiani na imani yoyote ya kidini. Tamko hilo nilitamka kutokana na taarifa nilizofikishiwa na watu ambao sikuweza kuwa na shaka kwamba wanaoniambia ni kweli na sidhani kama ningekuwa na sababu ya kusema wamefika kwa kunidanganya kwa hiyo tamko litakuwa limesimama juu ya msimamo huo,” alisema Kadinali Pengo na kuongeza:“Lengo la msingi kabisa, langu na la kanisa ni kwamba tukio lolote lile liwe kwa nia mbaya au nzuri kwa upande wetu isiwe ni sababu ya kuanza mapambano na kuwa chimbuko la ukosefu wa amani katika nchi yetu,” alisema Pengo.Alisema kuwa kila anayehusika ajue amani ya kweli ya taifa lolote haiwezi ikapatikana isipokuwa ikijengwa juu ya ukweli na ukweli kabisa bila kufuta au kujaribu kupotosha ukweli kwa namna yoyote ile.
 “Tusipojua kusema ukweli ulivyo hatuwezi kufaulu kuleta amani katika taifa letu. Kwa hiyo pamoja na kuendelea kuwaomba waumini wa Katoliki pamoja na watu wenye mapenzi mema kuendelea kumwomba Mwenyezi Mungu arehemu taifa letu na mapambano ya aina yoyote ile. Tuendeleze nia yetu njema ya kusema ukweli, haidhuru ukweli huu unamgusa nani,” alisema Pengo.
Alisema kujaribu kuficha ukweli na kupotosha ni njia sahihi kwa ibilisi kuleta vurugu katika jumuiya ya watu na ieleweke hivyo.
“Naomba kila mtu akubaliane na tamko langu haidhuru pana kosa, amani ya taifa letu ni jambo la msingi na amani itajengwa tu iwapo kila mtu anayehusika atakuwa tayari kusema ukweli kama ulivyo,” alisema.
Chanzo  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1845566/-/12t0yew/-/index.html

KIBONZO


Chelsea Yatibua Sherehe za Man U yaifunga 1- 0 EPL.


Matokeo  mengine  ya   EPL    fuatilia
 http://www.premierleague.com/en-gb/matchday/results.html

Mafuriko barabara ya Mwai Kibaki eneo la May Fair Plaza.

 Mbele   ya  hospital  ya  TMJ       maji  yakiwa  yamefurika.
 Mitalo  ya  maji  ikiwa  imezidiwa   na  maji  yanayotiririka  katika  eneo  hilo
  Ngazi   maalumu  ambazo     zilikuwa  zikitumika  wakati  wa  kutoka  na  kuingia  hospitali  ya  TMJ.

Bomb Attack in Arusha Catholic Church 6 suspect arrested.

A suspected bomb attack on a new Catholic church in the northern Tanzanian town of Arusha killed at least one person and wounded dozens of others, police said.

The Vatican's ambassador to Tanzania, Archbishop Francisco Montecillo Padilla, was attending the official opening of the church when the explosion occurred, but escaped unharmed.
 
If a bomb blast is proven, it will mark an escalation in sectarian tensions in east Africa's second biggest economy.
"Some kind of explosion went off at the church. It is believed to have been a bomb but we don't know what type of bomb it was," police spokesperson Advera Senso said.
One person was arrested after the blast  and  more  5  were  arrested  later, which killed a woman and wounded 57 other people, Senso said.A Vatican embassy official said he had been in contact with Padilla. "He is personally fine," the official said.
Two Christian leaders were killed in Tanzania's semi-autonomous, predominantly Muslim islands of Zanzibar earlier this year and there have been attacks on Muslim leaders and mosques. Arusha lies near the snow-capped peak of Mount Kilimanjaro in a part of Tanzania that is predominantly Christian.

Serikali yachukua uamuzi mgumu, yafuta matokeo .

Serikali imechukua uamuzi mgumu na kuamua kuwafariji wanafunzi waliofeli mitihani ya kuhitimu kidato cha nne mwaka 2012 baada ya kufuta matokeo hayo na kuamua yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011.
Uamuzi huo wa Serikali umetokana na matokeo mabaya ya mitihani huo yaliyosababisha zaidi ya asilimia 60 ya wanafunzi kupata sifuri.
Kutokana na matokeo hayo, Serikali iliunda Tume inayoongozwa na Profesa Sifuni Mchome kuchunguza matokeo hayo ili kupata ufumbuzi wa kudumu.
Muda mfupi baada ya tamko la Serikali, baadhi ya wadau wa elimu wameeleza kufurahishwa na uamuzi huo, huku Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kikiikosoa hatua hiyo, kuwa imekiuka sheria na kupora madaraka ya Baraza la Mitihani Tanzania (Necta).
Akitoa kauli ya Serikali bungeni kuhusu taarifa ya awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Matokeo ya Mtihani wa Taifa Kidato cha nne mwaka 2012 jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisema wameagiza Necta kuweka viwango ili matokeo ya wanafunzi yalingane na juhudi zao.
“Standardization ifanyike ili matokeo ya wanafunzi yalingane na juhudi wazizoziweka katika kusoma kwa mazingira, hali halisi ya Tanzania na uamuzi wa taifa kuongeza idadi ya shule na wanafunzi wakati uwekezaji katika ubora unaendelea,” alisema Lukuvi.
Chanzo  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1841582/-/12sx76v/-/index.html

Maadhimisho ya miaka 100 ya kituo cha makumbusho ya utamaduni wa Kisukuma - BUJORA Mwanza.

                Makumbusho ya  kabila la Wasukuma eneo la Kisesa  Magu  mkoani Mwanza.
 Kanisa lililojengwa kwa ajili ya kumbukumbu ya makanisa ya kale yaliyojengwa enzi za ukoloni  yapata   miaka  100 ambapo watemi wa kabila la wasukuma walikuwa wakiabudu .
 Ni kama kigoda vile umbo la jengo hili ambako ndiko kulitumika kuhifadhi  ngoma za asili zilizotumiwa na wanasanaa wa kabila la Wasukuma katika koo mbalimbali ngoma hizi zimehifadhiwa yapata miaka 100 sasa .
   Mdau   Madata Ndelule   Charles   mhifadhi    mwandamizi  wa   makumbusho  hayo  akionyesha    mfano wa nyumba   ambayo    watemi    waliishi.
 Bagika na Bagalu ni ngoma za pande mbili ndani ya kabila la Wasukuma ambapo Bagika walikuwa wakicheza ngoma inayoshirikisha nyoka na Bagalu walikuwa wakicheza ngoma inayoshirikisha zana kama majembe ya mkono, zana za kale za kivita.
                                                             Kikundi cha sanaa cha Bujora group
 Zana na nyenzo za enzi za kale zilizotumika katika usagaji nafaka ili kupatikana unga.
       Hatua kwa hatua usagaji nafaka kwa kutumia zana na kale huku nyimbo asili zikitawala .

 Tembelea   pia   kwa  maelezo  kuhusu  kituo hiki 
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top