Social Icons

Loading...

Easter Monday Dinner Party.


Polisi yawaonya wanaosambaza uvumi wa Pasaka.

Msemaji wa Polisi, Advera Senso.
 Polisi imeonya kuwachukulia hatua za kisheria wote watakaojihusisha na vurugu kipindi cha Sikukuu za Pasaka, zitakazoadhimishwa mwishoni mwa wiki.
Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema wamekamilika na hafikirii kama kutakuwa na yeyote atakayevunja amani.

Senso alikuwa akizungunmzia kuhusu uwapo wa uvumi wa baadhi ya watu kutaka kuvuruga shughuli za ibada kuanzia Alhamisi hadi Jumatatu. “Taarifa hizo kwa kweli hatuna, wanaovumisha uchonganishi huo tunawaonya waache mara moja kwa sababu wanahatarisha amani, tukiwapata tutawachukulia hatua za kisheria,” alisema Senso.

Alisema Tanzania haina udini wala ukabila, ipo salama na ikiwa kuna mwenye ushahidi au taarifa kuhusu kusudio la uhalifu zipeleke polisi, kwani hiyo ndiyo polisi shirikishi. Kuhusu madai ya baadhi ya viongozi wa Kikristo kupeleka taarifa hizo polisi, Senso alisisitiza kuwa Tanzania haina udini na atakayevunja amani kwa namna yoyote atashughulikiwa kisheria kama mhalifu siyo kidini.

Alisema kila mwananchi anatakiwa kujilinda, kulinda mwenzake na taifa lake kwa jumla.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (FPCT), Askofu David Mwasota alilieleza Mwananchi jana kuwa, licha ya taarifa za maandishi zinazosambazwa katika simu za viganjani, wiki iliyopita Wasomali wengi walionekana wakiingia nchini na kwamba taarifu zimefikishwa polisi.

Imeandikwa na Editha Majura, Nuzulack Dausen na Pamela Chilongola
Naye Katibu wa Baraza la Maskofu Tanzania (TEC), Padri Anthony Makunde alikiri kuwapo taarifa za vitisho dhidi ya Wakristo katika maadhimisho ya Pasaka na kwamba, walipeleka taarifa kwenye vyombo vya usalama ili zifanyiwa kazi.
Chanzo:  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1730256/-/12985sq/-/index.html

Mhe PINDA alipokutana na Pope Francis 1.


CHINA YAAHIDI MISAADA ZAIDI KWA AFRIKA.

Rais Xi Jinping wa China ameahidi kuendelea kuipiga jeki Afrika ili kukabiliana na changamoto za kimaendeleo, huku akisema kuwa suala la utoaji misaada yenye masharti magumu siyo ajenda ya Serikali yake.Jinping akitumia jukwaa la Tanzania kutambulisha sera yake kwa nchi za Afrika alisema kwamba bara hilo limepiga hatua kubwa kimaendeleo na kwamba nchi yake itaimarisha uhusiano uliopo kwa manufaa ya pande zote mbili.

Alisisitiza kwamba ushirikiano wenye tija ni ule unaozingatia “majadiliano na maridhiano” na kwamba Serikali yake imetenga kiasi cha Dola za Marekani 20 bilioni kufadhilia miradi mbalimbali ya maendeleo Afrika.“China haitakuwa tayari kutoa masharti kwa taifa lolote… Tunataka kutoa fursa zinazofanana,” alisema Rais, ambaye alishika rasmi wadhifa huo Machi 14, mwaka huu.
Alisema China haitaingilia masuala ya ndani ya nchi, huku akisisitiza kwamba shabaha ya nchi yake ni kuendelea kupalilia ushirikiano mwema uliodumu kwa miongo kadhaa na siyo kujihusisha na migogoro.

Baadhi ya wachunguzi wa mambo wanadai kuwa, kauli ya kiongozi hiyo ni kama ujumbe wa onyo kwa baadhi ya nchi za Magharibi ambazo zinalalamikiwa kuendesha sera zinazominya ustawi wa Afrika.
Mhadhiri katika Chuo cha Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa (CFR), Dk Ahmed Mtengwa alisema: “Ni hotuba inayofungua njia kwa Afrika..., amezungumzia ushirikiano unaolingana yaani `win win situation’ (kila upande ufaidike), hivyo kwangu ninayaona matumaini.”
Rais Jinping, aliyekuwa katika ziara ya siku mbili nchini na juzi usiku alisaini mikataba 17 inayohusu sekta za kilimo, afya na miundombinu.
Mkataba wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani ni kati ya miradi mikubwa iliyomo kwenye makubaliano hayo na ujenzi wake utafanywa na Kampuni ya Merchants Holding ya China na utakwenda sanjari na ujenzi wa barabara inayounganisha bandari hiyo.

Pia katika bandari hiyo itaunganishwa na Reli ya Kati na na ile ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) ili kurahisisha usafiri wa mizigo ndani na nje ya nchi.
Mikataba mingine itahusiana na uboreshaji wa sekta ya viwanda, kilimo hasa kile cha tumbaku ikiwamo kuwatafutia soko wakulima kutoka Mikoa ya Tabora na Ruvuma ili waweze kuuza zao hilo katika soko la China pamoja na kulipatia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zana za kufanyia kazi.

Rais huyo, ambaye Tanzania ndiyo nchi ya kwanza barani Afrika kuitembelea, alizindua na kukabidhi rasmi Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere kilichoko jijini Dar es Salaam ambalo ni jengo la ghorofa tatu na lenye kumbi nne za mikutano zenye uwezo wa kuchukua watu 1,800 kwa wakati mmoja.Ujenzi wa kituo hicho uligharimu Dola za Marekani 29.7 milioni zilizotolewa na Serikali ya China kwa lengo la kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Rais huyo alisifu ushirikiano wa muda mrefu baina ya taifa lake na Tanzania na kusisitiza kuwa nchi hizo zitaendelea kusaidiana kama sehemu ya kuenzi misingi iliyowekwa na waasisi wa mataifa haya mawili, Mwalimu Julius Nyerere na Mao Tse Tung.

Rais Jinping aliondoka jana jioni kwenda Afrika Kusini kuhudhuria mkutano wa tano wa Wakuu wa Nchi zinazokua kwa kasi kiuchumi ikiwamo Brazil, Urusi, India, China na Afrika ya Kusini (BRICS).
Chanzo:  gazeti  la  mwananchi.

KIBONZO


Rais XI JINPING ATUA NCHINI.


Rais wa China, Xi Jinping aliwasili nchini jana saa 10:5 akitumia ndege Boeng 747 ya Shirika la Ndege la China na leo atazungumza kwa mara ya kwanza na Afrika akitumia jukwaa la Tanzania.
         Jinping atatoa hotuba yake kwenye jengo jipya la kisasa la Mwalimu Nyerere ambalo limejengwa na Serikali ya China likiwa na uwezo wa kuchukua watu 1,800 kwa mara moja lilipo jijini.Rais huyo ambaye ameambatana na mkewe pamoja na maofisa mbalimbali wa Serikali yake,anatajiwa kutambulisha sera kwa Bara la Afrika huku wachunguzi wa mambo wakisema kuwa hotuba yake hiyo huenda itazingatia juu ya uimarisha uhusiano mwema baina ya pande zote mbili.
 China ndiyo dola inayotajwa kuwa na ushawishi mkubwa barani Afrika na katika kipindi cha muongo mmoja uliopita kiwango cha ufanyaji biashara baina ya pande hizo mbili kinatajwa kukua kwa asilimia 70. China pia ndiyo mshirika pekee kwa Afrika ambaye misaada yake inaambatana na masharti nafuu.
Hata hivyo ushawishi wa China barani Afrika unakosolewa na baadhi ya nchi za Magharibi zinazoituhumu China kwamba inazinyonya nchi za Afrika.
       Alipowasili jana kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Rais huyo alipokewa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete na kisha alipigiwa mizinga 21 na baadaye alikagua gwaride. Baada ya mapokezi hayo ya uwanjani, Rais Jinping na mwenyeji wake walioogoza kwenda jijini ambapo jioni ya jana walikuwa na mazungumzo ya faragha na baadaye walijumuika na halaika kwa ajili ya kushiriki dhifa ya taifa.
Taarifa  kwa  hisani  ya  :  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1729660/-/128rxxi/-/index.html

STARS YAIZODOA MOROCCO 3 - 1

Timu   ya    Taifa  Stars  imeifunga    Timu  ya  Taifa   ya  Moroco( SIMBA  WA  MILIMA  YA  ATLAS)  goli  3 - 1  katika  michuano  ya  kutafuta  nafasi  ya  kushirikia  mashaindano  ya  kombe  la  Dunia.

Wakili Mawalla ajiua.

Wakili Nyaga Mawalla  amefariki baada ya kujirusha kutoka ghorofani akiwa jijini Nairobi, Kenya alikokwenda kwa matibabu.Nyaga alikufa baada ya kujirusha kutoka katika jengo la ghorofa ya hospitali aliyokuwa akitibiwa jijini Nairobi usiku wa kuamkia juzi.
Mfanyakazi wa Kampuni ya Mawalla Advocate, John Minja aliliambia gazeti hili kuwa mwili wa marehemu ulitarajiwa kurejeshwa nchini jana.
“Hali yake haikuwa mbaya, kwani juzi mchana tulizungumza naye tukitaka kwenda kumsalimia lakini, alitueleza kuwa angerejea jana nchini,”alisema Minja.Hata hivyo, bado haijajulikana sababu za kujiua, lakini baadhi ya ndugu zake wanasema ni kutokana na msongo wa mawazo.
       Taarifa za kifo cha Mawalla anayemiliki kampuni kadhaa ikiwamo Kampuni ya uwakili ya Mawalla Advocates, kimeshtua wengi akiwamo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyesema taifa limepoteza kijana mwenye maono, akili na mjasiriamali aliyetajirika bila kuiba.
      “Nimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Nyaga. Licha ya udogo wake kiumri, lakini alikuwa mshauri wangu kwenye mambo mengi kiuchumi, kibiashara na kijamii. Nyaga alikuwa kiongozi wa jamii asiye na mipaka katika huduma tofauti na wafanyabiashara wengi nchini walishirikiana naye,” alisema Mbowe.

Dar ZOO Weekend hii; UTALII WA NDANI.

Blogger        Azulu   Dar   es  Salaam   ZOO.
Raha   ya   KUTEMBELEA   ZOO   haikamiliki   pasipo    KU-  ridi     huyu  mnyama (  ana  raha  yake ).

 

KIBONZO


KWELI ULAYA NI MBALI, TUJIFUNZE KWA JIRANI ZETU RWANDA.

“Ili kuleta maendeleo Tanzania ni lazima malengo yetu yaelezwe,tusiseme ni kilimo huku ikiwa bado wakulima asilimia 70 wanatumia jembe la mkono.Tusiseme elimu huku tukitenga asilimia 1.4% ya bajeti wakati Rwanda wakitenga 5.8% na Kenya 7%? Ukienda Rwanda kila mmoja anafahamu nchi yake inelekea wapi na wajibu wake ni nini.Kila mmoja anapigana na Rushwa na Kutaka utawala bora.Nchi ambayo kila mtu na lwake haiwezi kuendelea”.
Imekuwa ni kawaida kwa viongozi wa nchi za Afrika kuwa na safari nyingi za ulaya na amerika kwenda kujifunza namna ya kuendelea.Wakirudi utasikia wakisema,”huko wameendelea sana”,”wametuacha mbali hatuwezi kuwafikia hivi karibuni”.Hata katika kujifunza kuimudu sekta ya gesi walienda Sweden na Trinidad na Tobago,lakini nchi ya jirani ya msumbiji ambako nao wanatekeleza mradi kama wa hapa kwetu hawakukanyaga kabisa.Nadhani ili tujifunze vizuri ni muhimu tujifunze pia kwa wale tunaofanana nao japo kidogo kihistoria.
Miaka 19 iliyopita tulishuhudia nchi ya Rwanda ikiwa katika mauaji makubwa yaliyotikisa dunia.Ni uadui wa kikabila kati ya walio wengi wahutu na wale walio wachache ila walibahatika kusoma na kushika madaraka katika nchi,Watutsi.
Ndani ya siku mia moja(100) yalishuhudiwa mauaji ya kimbari ya watu wapatao karibu laki nane(800,000) ikimanisha angalau kwa kila siku waliuawa watu wapatao 8000.Nchi ilijaa damu,miundo mbinu iliharibiwa;shule,hospitali,barabara na viwanda.Ilikuwa ni hali ya kukatisha tamaa kwa kila mnyarwanda.
Baada ya vurugu hizi kuisha Rais Paul kagame alichukua nchi kwa mapinduzi akiwa na chama chake cha RFP.Tangu kuingia kwakwe madarakani nchi hii imepiga hatua kubwa sana kiuchumi na katika huduma za kijamii.Wakosoaji wa maendeleo ya Rwanda wanatoa hoja kadhaa kuwa ndiyo sababu ya kuendelea kwao kwa kasi katika kukuza uchumi wao.
 Wapo wengine wanaosema nchi ya Rwanda ni ndogo sana hivyo ni rahisi kuiletea maendeleo,wanasahau hapa kwetu hata katika mikoa midogo bado maendeleo hakuna.Hata hivyo udogo haiwezi kuwa kigezo cha mandeleo kwani ziko nchi ndogo zaidi ya Rwanda kama ilivyo shelisheli yenye km za mraba 455 ukilinganisha na zile za Rwanda kilometa za mraba 26,318 au ukubwa wa Gambia wa kilomita za mraba 11,295 hizi zote ni ndogo kwa eneo kulinganisha na Rwanda lakini bado Rwanda iko juu kimaendeleo ukilinganisha na nchi hizi.
Mfano huku Rwanda ikiwa uchumi wake unakua kwa kasi ya 6.5% kwa mwaka nchi ya Gambia uchumi wake hukua kwa 5.2%. Nchini Rwanda kiwango cha elimu kiko 70.4% huku nchini Gambia ikiwa ni asilimia 40.1%.Na hapa lazima tuzingatie kuwa Rwanda ni zaidi  ya mara mbili ya ukubwa wa Gambia na pia ina idadi ya watu 10,746,300 karibuni mara kumi ya idadi ya watu wa Gambia.Kwa kuzingatia haya,udogo si hoja ya kujitetea kabisa.
Kuna wale ambao wanataka pia kuhalalisha kutoendelea kwa nchi yetu Tanzania wakidai kuwa Rwanda wanapata maendeleo yao kutokana na kupendelewa kupewa misaada lukuki hasa ikitokana na huruma za mataifa mbalimbali kwa kile kilichotokea mwaka 1994.Hii nayo ni mbinu ya wavivu wa kufikiri,kwani kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na kijitabu cha pocket world in figures kinachotolewa na jarida la The economist,ilionyesha kuwa Tanzania ni nchi ya kwanza kwa kupewa misaada Afrika mashariki,ya tatu Afrika na ya sita duniani.Wakati Rwanda ikiwa imepokea misaada ya dola za kmarekani milioni 785.9 kwa mwaka 2010,Tanzania tulipata msaada wa dola za kimarekani Bilioni 2.9.Kama misaada ingekuwa ndio chanzo cha maendeleo,Tanzania tungetakiwa kuwa mbali zaidi.
Wako watu ukianza kulinganisha maendeleo yetu na yale ya nchi zingine za ulaya au marekani wanakuwa wakali na kusema hatufanani kabisa.Nadhani watu wenye fikra hii watakubaliana na mimi kama nitailinganisha Tanzania yenye uhuru wa miaka 50 na Rwanda iliyoanza kujijenga miaka 19 iliyopita.Nchi ya Rwanda ndio inayoongoza kwa kuwa na usafi katika nchi za Afrika mashariki,hili nalo linahitaji misaada ya nje?
NINI SIRI YA MAFANIKIO YA RWANDA?
Mafanikio ya Rwanda hayatokani na Jambo moja tu,yako mambo mengi yanayochangia katika maendeleo yao ya kasi yanayotamaniwa sana na mataifa mengi,leo nitalizungumzia moja.
Siri ya mafanikio ya Rwanda imejengwa katika UONGOZI MADHUBUTI WENYE MAONO,tangu Rais kagame aingie madarakani amefanikiwa kuonyesha njia kwa vitendo.Hajaacha mipango yake iwe ndani ya makaratasi tu,amehakikisha wananchi wote wanaelewa kwa undani maono ya nchi yao ni nini,na kushikamana katika kuyatekeleza.
Suala la ukabila ambalo ndio kilikuwa chanzo kikubwa cha mauaji ya mwaka 1994 alikishughulikia bila kificho na alifanya hivyo kwa uwazi.Alikemea ukabila akiwa ndani na akiwa nje pia,hakuna mnyarwanda asiyejua kuwa kagame hakubaliani na sera za ukabila.Ameonyesha kwa vitendo katika uteuzi wake wa viongozi mbalimbali pia.Leo hii ni marufuku kwa mnyarwanda yeyote kusema mimi wa kabila Fulani,kila mmoja anatakiwa ajitambulishe MIMI NI MNYARANDWA.Viongozi wetu hapa Tanzania,ni lazima pia wafikishe wananchi wao hapo katika suala la udini kama mwalimu Nyerere alivyolisimamia ili kujenga nchi ya usawa.
Katika maono yake kwa nchi ya Rwanda ya hadi mwaka 2020,kagame ameelezea jinsi anavyokusudia kuibadilisha Rwanda kutoka katika nchi ya kutegemea kilimo uchwara na misaada na kuwa nchi yenye uchumi ulio thabiti na unaotegemea uwekezaji katika elimu na biashara.Maono haya yanaeleweka kuanzia waziri hadi dereva wa daladala.Kuanzia kiongozi hadi mwananchi wanazungumza lugha moja na kuwa na msimamo mmoja.Hivi hapa kwetu wote tunaelewa tunakoelekea?Hiyo vision 2025 inajulikana kwa kiasi gani na kila mtu.Hata wale waliofika chuo kikuu ukiuliza vision 2025 inaeleza nini asilimia kubwa watakuuliza,hicho ni kitu gani?badala ya kujadili mwelekeo wan chi yetu malumbano sasa yamejikita katika siasa na kuharibiana sifa mbele ya jamii(character assassination).
Rais kagame ametengeneza kijitabu kidogo kinachoeleza kwa undani wajibu wa serikali yake na matarajio yake kutoka kwa wananchi ikiwemo mambo ya msingi(values) ya utaifa wao.Haya yanafundishwa kwa kila mtu katika vikao vya ngazi za chini vya wananchi,ni lazima uyafahamu,uyaishi na uyasimamie.Hii hutengeneza nguvu ya pamoja kuendeleza taifa lolote.Misingi yetu kama Taifa ni ipi?
Maendeleo ya Rwanda yameanzia katika fikra na mitazamo,wananchi wamefundishwa kuchukia misaada na kujiamini kuleta maendelo yao wenyewe.Hapa kwetu kiongozi mzuri anaonekana ni Yule anayefahamiana vyema na mataifa ya kimaagharibi,dio maana ni kawaida siku hizi kwenye kampeni watu kuahidi kuwa wakichaguliwa wataenda kuomba misaada na kusaidia wanaowaongoza,wamesahahu thamani ya rasilimali zao wenyewe.Rwanda ni tofauti,ukipiga kampeni za namna hiyo,haupati cheo chochote kile.
Nakumbuka kisa kimoja kilichotokea mwaka jana 2012 ambapo wanafunzi wapatao 27 kutoka nchi za magharibi walitembelea Virunga National Park,Rwanda.John Fox ambaye alikuwa mmoja wa wanafunzi hao alisema kuwa walimpa zawadi ya peni mtoto mmoja aliyekuwa maeneo ya hifadhi ya virunga.Mtoto alipokea na kukimbia kwa furaha kupata zawadi hiyo kutoka kwa wazungu.Wakiwa wanarudi kutoka ndani ya hifadhi hiyo walisimamishwa na askari wa hifadhi na kuambiwa wamefanya kosa kubwa sana,walipouliza kosa lao Yule askari wa hifadhi akawambia”Haturuhusu kuwapa watoto zawadi kwa namna hiyo kwani unawajengea mtazamo wa kuwa ombaomba na tegemezi”.Nadhani tunamuhitaji askari huyo haje kuzungumza na viongozi wa kitaifa hapa kwetu…!
Ukuaji wa uchumi wa Rwanda na maendeleo ya huduma za kijamii yanatokana  na imani ya wananchi katika utawala bora na haki kutendeka.Wakati Kenya walishindwa kuaminiana katika kusikiliza kesi na kuhukumu waliohusika katika vurugu za baada ya uchaguzi mwaka 2008,Rwanda wameweza hilo.Mahakama za ndani zilizoimarishwa nchini Rwanda(Gachacha) zipatazo 1,200 kwa nchi nzima,zimeweza kuhukumu kesi zipatazo milioni 1.2 kwa muda mfupi na kwa haki.Amani katika nchi ni matunda ya imani ya upatikanaji wa haki katika vyombo vya sheria.Hapa kwetu Tanzania Ripoti ya Transparency international inaonyesha kuwa Tanzania polisi na mahakama ndivyo vyombo vinaovyoongoza kwa rushwa nchini.
Ili kuleta maendeleo Tanzania ni lazima malengo yetu yaelezwe,tusiseme ni kilimo huku ikiwa bado wakulima asilimia 70 wanatumia jembe la mkono.Tusiseme elimu huku tukitenga asilimia 1.4% ya bajeti wakati Rwanda wakitenga 5.8% na Kenya 7%? Ukienda Rwanda kila mmoja anafahamu nchi yake inelekea wapi na wajibu wake ni nini.Kila mmoja anapigana na Rushwa na Kutaka utawala bora.Nchi ambayo kila mtu na lwake haiwezi kuendelea.
Kweli ulaya ni mbali,basi tujifunze kwa jirani zetu Rwanda…
Mwandishi  wa  makala  hii ni  mwanaharakati  wa  masuala  ya  kijamii
Joel Nanauka
March  2013.
 

Kibonzo - MAPROSOO


Man U, Arsenal na Chelsea zang'ara, Man City yafungwa na Everton

Man  U    1     Reading   0

Arsenal  2     Swansea    0


Man  City  2   Everton  0

Chelsea  2    West Ham  0



Fuatilia     matokeo ya  mechi  mwishoni  wa  wiki   http://www.premierleague.com/en-gb/matchday/results.html

Quality Business Reporting Can Increase Investment in Africa.

Nick Blazquez, President, Diageo Africa
The President, Diageo Africa, Turkey, Russia & Eastern Europe, Mr. Nick Blazquez, has stated that improving the quantity and quality of business reporting can play a significant role in generating business interest and increasing inward investment in Africa.
Blazquez, who made this known in a statement by his company to announce its annual Africa Business Reporting Awards, said his belief was as a result of his experience as a long-term investor in Africa.
“As a result, these awards were launched in 2004 as a practical way of raising awareness of economic opportunity in Africa and to celebrate excellent business journalism. In 2013, ten years on from the Awards’ inception, Africa’s profile as a business and investment destination is higher than ever. This is reflected in the fact that the Awards have continued to grow year on year and, in 2012, attracted more than 1000 entries from 27 countries, “he said.
The statement further reads: “Diageo Africa Business Reporting Awards 2013 are already attracting high-quality entries from the best journalists around the world. The Awards celebrate their ten-year anniversary in 2013 and will once again showcase the most influential and innovative journalism from and about Africa. All journalists, writers, photographers, reporters and media houses are encouraged to apply as soon as possible. In order to provide every opportunity for submissions, we have extended the final date for entries to 22 March 2013.”
The company in the statement noted: “Diageo, the world's leading premium drinks business, today issued the final call for entries to the tenth annual Diageo Africa Business Reporting Awards. The Awards recognise the achievements of business journalists reporting on the continent and provide a prestigious forum for international recognition of their work.
“The awards are open to all journalists reporting on Africa, in any medium, and of any nationality. Submissions are accepted in English and in French. Entries will be reviewed by a high-profile judging panel –further details will be announced soon. The shortlisted finalists from each category will be flown to London for the Gala Ceremony in July. Winners will each receive £500 and a specially commissioned sculpture.
The awards are free to enter and the open period for entries has been extended to 22 March. Submissions are welcomed for the following categories: Best Information and Communication Technology (ICT) feature, Best Finance feature, Best Infrastructure feature, Best Agribusiness/Environment feature, Best Tourism feature, Best Business News story, Best Business feature, Best Newcomer, Media of the Year and Journalist of the Year.”

Pinda to Grace Easter Festival .

PRIME Minister Mizengo Pinda is expected to be the guest of honour during this year's Easter Festival to be held at the National Stadium in Dar es Salaam on March 31, this year, organizers said.
A statement issued by the festival's organizing committee chairman, Alex Msama, said they have received confirmation from Prime Minister's office that the Premier will honour the event. "We're happy that our festival this year will be graced by the Primer Minister Mizengo Pinda," said Msama.
The Minister of Foreign Affairs and International Cooperation, Bernard Membe was the guest of honour during last year's festival held at the same venue. Kenya-based Congolese gospel ace Solomon Mukubwa will headline the list of international artistes who will be performing during the annual festival to be staged at various regions around the country.
Mukubwa is currently one of the most sought after African gospel singers. He has always touched people by his music and singing. Known for his energetic stage performances and bewitching vocal, Mukubwa promises to thrill fans with some of his captivating songs, including 'Mfalme wa Amani', 'Mungu Mwenye Nguvu' and 'Uwe nami Bwana'.
He will be joined by a host of other renowned contemporary gospel musicians, including Sipho Makhabane from South Africa, Ephraim Sekeleti from Zambia and Ambassadors of Christ choir from Rwanda.
Source: http://allafrica.com/stories/201303140103.html

ARSENAL YAFA KIUME YAITANDIKA BAYERN MUNICH 2 - 0 ; YASHINDWA KUFUZU

ARSENAL   2    BAYERN  MUNICH    0




  MALAGA   2    FC  PORTO 0

Papa MPYA Apatikana ni Pope Francis wa 1 toka Argentina.

Papa  mpya  ni  Cardinal  Jorge Mario Bergoglio (  Pope   Francis  1)   aliyezaliwa   miaka   76  iliyopita    toka   Argentina   Amerika ya  kusini  ameteuliwa  kuwa  kiongozi  wa  Kanisa    Katoliki  Duniani, atatumia    jina  Papa Francis wa  1.
         Moshi ' mweupe '    kiashiria   cha  kupatikana  kwa  Pope, baada ya  makadinali  16   kufanya  kikao  cha  siri    cha  kumteua   Pope  kanisa  kuu  la  St   Peter's Squire   huko Vatican City   Rome   Italia.
                              Papa  Francis  1    Jina  halisi  Cardinal   Jorge Mario Bergoglio
Wasifu  wake    fuatilia  hapa  http://en.wikipedia.org/wiki/Jorge_Bergoglio

Kibonzo.


What do Facebook dislikes and likes to reveal?

Cambridge University has devised a statistical model that can apparently work out people's sexual orientation, religious beliefs, political views, IQ level and even drug use, with a high degree of accuracy, just by analysing their Facebook likes. Like Harley Davidson motorbikes? Then you have a low IQ. Jennifer Lopez? You're an extrovert. Wicked the Musical? If you're a man, you must be gay. Every time you click the thumbs-up button on Facebook, you are apparently revealing a bit more about yourself, information that faceless corporations can use to target you with advertising and unscrupulous governments could use to persecute you. As one privacy campaigner has warned: "We need to fundamentally re-think how much data we are voluntarily sharing."That sort of reaction is inevitable, given how many people worldwide use Facebook (one billion on the last count), but should we really be concerned we're in the clutches of an invisible puppet master? I don't think so.
     This latest research is both unsurprising and nonsensical. It should come as no surprise to anyone that indicating their likes and dislikes on Facebook helps others to form an idea about who they are. We all share information about ourselves all the time, from the way we dress to the way we talk to our likes and interests, as a way of projecting ourselves. We do it without thinking about it. A woman sitting in a cafe with her hair in dreadlocks, wearing ethnic clothes and reading Sylvia Plath, is unlikely to be mistaken for a stalwart of the local Conservative Association, and probably wouldn't want to be.
   

TCRA yakataa WAZO la kurejesha Analojia.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema haitarudi nyuma kwenye suala la kutumia mfumo wa matangazo kupitia njia ya dijitali na kwamba mfumo huo utaendelea kutumika.
Kauli ya TCRA imekuja siku moja baada ya wamiliki wa vituo vya utangazaji vya televisheni nchini kutishia kusitisha kurusha matangazo ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa kutokana na kushindwa kumudu gharama za uendeshaji.Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (Moat), Reginald Mengi juzi alisema hakuna haja ya kurusha matangazo kwa hasara kwani watangazaji wamesitisha kutoa matangazo kwa sababu wananchi wengi hawana ving’amuzi. Licha ya Moat kutoa kauli hiyo juzi, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma alisisitiza kwamba TCRA haiwezi kurudi nyuma katika suala hilo kwani mfumo huo utaendelea kutumika.
Akizungumza Dar es Salaam jana kwenye warsha ya mambo ya mionzi, alisema wao kama TCRA hawawezi kurudi nyuma katika suala hilo na kwamba msimamo wao wa kuendelea kutumia mfumo wa matangazo kwa njia ya dijitali upo palepale.
                                                          Chanzo   Mwananchi

Yule DOGO wa miaka 9 Aliyeoa Bibi wa miaka 61 Huyu HAPA.


Huyu mtoto anasema wazee wa zamani ndio walimuamrisha aoe lakini pamoja na hilo, hawajasaini cheti cha ndoa na wala hawaishi pamoja ambapo wazazi wa huyu bwana harusi walichangia harusi kwa kutoa euro 1500 ambazo walisisitiza ni kama matambiko na sio kisheria.

Mtoto huyu aitwae Sanele amekaririwa akisema “nilimwambia mama yangu, nahitaji kweli kuoa na nimefurahi nimemuoa Helen lakini nikikua nitaoa mwanamke wa umri wangu”

Mama mzazi wa Sanale anasema “babu yake ndio alimchangulia Sanale amuoe Helen kwa sababu yeye(Babu) anampenda, na wamefanya hivyo ili kutimiza maagizo ya wazee wa koo ambao wameshafariki, yani ni kama matambiko”

BARCA , GALATASARAY Zatinga Robo Fainali kwa Vishindo.

Barcelona  4    Ac  Millan 0




Gala  3   FC Shalke  2


WAMILIKI VITUO VYA TV WASHAURI ANALOJIA IFUNGULIWE SAMBAMBA NA DIJITALI.

 Wamiliki wa vituo vya utangazaji vya televisheni nchini, wamesema watasitisha kurusha matangazo ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa kutokana na kushindwa kumudu gharama za uendeshaji.
Hatua hiyo inatokana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzima mitambo ya analojia na kuhamia dijitali Desemba 31, mwaka jana kitendo walichodai kimepunguza mapato yanayotokana na matangazo.Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (Moat), Reginald Mengi alisema hakuna haja ya kurusha matangazo kwa hasara.Mengi alisema kutokana na kuanza kwa mfumo wa dijitali, watangazaji wamesitisha kutoa matangazo kwa sababu wananchi wengi hawana ving’amuzi.
“Kama mamlaka itashindwa kurudisha ule mfumo wa analojia kuwa sambamba na dijitali hadi wananchi watakapokuwa na ving’amuzi, tutazima televisheni zetu ndani ya mwezi mmoja ujao,” alisema Mengi.

“Ibara ya 18 ya Katiba imekiukwa kutokana na wananchi kunyimwa fursa ya kupata habari, hivyo hali hii hatutaki iendelee,” alisema Mengi.
Mengi ambaye pia ni mmiliki wa vituo vya televisheni vya ITV, EATV na Capital TV, alisema licha ya nchi za Afrika, Tanzania imekuwa ya kwanza kuzima mitambo ilhali wananchi hawakuwezeshwa kumudu gharama za ving’amuzi.“Nchi ambazo zimeendelea kwa kila kitu kama Uingereza, Marekani, Japan na kwingineko kuzima mitambo ya analojia walitumia zaidi ya miaka minane kwa nini sisi tumewahi hivi wakati hatujajipanga?” alihoji Mengi.
Chanzo:  http://www.mwananchi.co.tz/-/1597570/1717682/-/y1r7nm/-/index.html

Kibonzo.


FIFA Yailima Tanzania Barua ya ONYO.

Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA) limesema litaifungia Tanzania iwapo itabainika kuwa Serikali imekuwa ikiingilia shughuli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).FIFA imesema kumekuwa na shutuma kupitia taarifa mbalimbali za vyombo vya habari nchini kuwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeonesha nia ya kuingilia uendeshaji wa TFF.Kwa mujibu wa barua ya jana (Machi 10 mwaka huu) ya FIFA kwenda kwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga, vyombo vya habari vimemkariri Waziri (Dk. Fenella Mukangara) kuwa Serikali imeiagiza TFF kutumia Katiba ya mwaka 2006 katika uchaguzi wakati tayari imeshafanyiwa marekebisho.
“Pia imeelezwa kuwa TFF imetakiwa kufanya Mkutano Mkuu pamoja na ule wa uchaguzi kwa tarehe ambazo zimepangwa na Serikali. Vilevile imeelezwa kuwa Serikali inakusudia kuunda Kamati ya Muda iwapo TFF haitatekeleza maagizo yake,” imesema sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valke.
FIFA imesema iwapo yaliyoripotiwa na vyombo vya habari yatathibitika kuwa kweli, maana yake huo ni uingiliaji wa wazi wa Serikali kwa shughuli za TFF.
“Tunapenda kuwakumbusha kuwa wanachama wote wa FIFA wanatakiwa kuendesha shughuli zao kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu mwingine kama ilivyoelezwa katika ibara za 13 na 17 za Katiba ya FIFA.
“Hivyo kama maagizo hayo yanayodaiwa kutolewa na Serikali yatatekelezwa, suala hili litapelekwa katika mamlaka za juu za FIFA kwa hatua zaidi ikiwemo kuisimamisha Tanzania kama ambavyo inakuwa pale panapokuwa na uingiliaji wa Serikali,” imesema barua hiyo.
Barua hiyo ambayo nakala yake pia imetumwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) imeelezea baadhi ya athari ambazo Tanzania itakumbana nazo endapo itasimamishwa ni timu za taifa pamoja na klabu kutoshiriki mechi za kimataifa kwa mujibu wa Ibara ya 14 ya Katiba ya FIFA.
Vilevile si TFF au wanachama wake na maofisa wengine watakaoweza kunufaika na programu za maendeleo, kozi au mafunzo yanayotolewa na FIFA na CAF.
“Madai ya uamuzi uliofanywa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ni ya kusikitisha kutokana na ukweli kuwa FIFA ilishatangaza itatuma ujumbe wake kuchunguza jinsi hali ilivyo kwa sasa na kutoa mapendekezo yake. Kutokana na hali hii, ujumbe wa FIFA uliokuwa uje kuchunguza (suala la uchaguzi) itabidi usubiri kwa vile ni muhimu kushughulikia tatizo hili kwanza.
“Katika mazingira haya tunaomba ueleze msimamo huu wa FIFA kwa mamlaka zinazohusika (Serikali) na athari ambazo mpira wa miguu wa Tanzania utakumbana nazo. Tunakushuru na tunatarajia utatufahamisha kila hatua inayoendelea katika suala hili,” imesema barua hiyo.

FA CUP - Man U 2 Chelsea 2 , Mechi Kurudiwa

Man U  2     Chelsea 2




EPL   Majogoo wa  Jiji    wailipua    Spurs 

Liverpool  3         Spurs  2


New  Castle 2       Stoke    City  1 
                                                                                                                                                                         

Fuatilia  matokeo  na  ratiba   ya  EPL   hapa 

Mwinyi stresses IT training expansion, pioneer attitudes

Former President Mzee Ali Hassan Mwinyi has underscored the need for Information Technology (IT) for economic development and urged IT institutes in the country to stand out as pioneers in meeting the required demand to equip professionals with quality IT and business relevant skills.The retired second phase president expressed his concern yesterday in Dar es Salaam at the 13th graduation ceremony whereby he conferred certificates for diplomas, advanced and degrees in IT and business disciplines to about 130 IT professionals graduating at different levels including Masters Degree at the Institute of Information Technology (IIT).
 The institute is affiliated with NCC education, the University of Greenwich and Pearson Vue, which has been making it a one stop training and certification centre in the country for 23 years since its inception whereby it has trained over 12,000 graduates.
At present, the institute offers courses in two major areas of studies, international programs at the level of diploma in Computer Studies and Information Technology as well as business studies which are internationally recognized.It also offers one International Advanced Diploma in Business, Bachelor’s degrees in Business Studies as well as in business information technology, plus a Master of Science degree programs in strategic business information technology.
      In his speech, Mzee Mwinyi noted that the institute’s affiliation with outstanding centers of learning abroad has enabled it to transfer much needed knowledge and skills for the country’s social and economic development.
This affiliation with internationally renowned centers of learning means that the courses offered at IIT are also world class, he emphasized.
In a relatively brief period, IT and transfer of technology has been universally accepted as a major way through which a developing country like Tanzania could catch up with developed countries in terms of knowledge and skills.
“The knowledge and IT training skills provided by IIT is a springboard for rapid advancement of our people and the nation at large. Your graduation is just the beginning of a new journey in which you will prove your real worth at the work place,” he cautioned the graduates.
    He also counseled the graduands that in whatever they would plan to do for development they should seek out a passion for excellence and ne ready to develop and learn more ideas to grasp things better.
Earlier the IIT Executive Director Moiz Salemwalla said that the institute is fully committed to offering the highest quality, developing and introducing new courses. The major intention of the institute is to gain the right competencies for either self employment or joining the job market, he said.In July this year this institute is going to start a CBET Degree program approved by the National Council for Technical Education (NACTE), developed with assistance of senior experts from the Netherlands, he said.
The program would develop and make experts learn new innovations on teaching methodology and IT innovations to enable them acquire relevant, up to date and comprehensive skills, he added.
SOURCE: GUARDIAN ON SUNDAY

Tanzania: 'Shun Selfishness, Serve Others'

 TANZANIANS have been urged to shun selfishness in the name of religion, regionalism and other divisive factors and instead focus on using their talents towards serving others.
The call was made in Dar es Salaam by Prof Esther Mwaikambo, soon after receiving the 2013 Dr Martin Luther King Jr Drum Major for Justice Award from the US Ambassador to Tanzania, Mr Alfonso Lenhard.
Prof Mwaikambo, who is the current Vice-Chancellor of the Hubert Kairuki Memorial University of Health Sciences, received the award in recognition of her tireless efforts to promote human rights and access to education and health care for Tanzanian women and girls.
Ms Mwaikambo who is a professor of paediatrics noted that there is more turmoil in the world and in Tanzania nowadays for people seeking justice. "There is more happening, in terms of some people killing and destroying others and their property in the name of religion, regionalism and other divisive factors.
That instinct of driving for gains and for selfish interests is gaining ground faster than we can handle," she said. She added that the trend is dismantling all efforts made by the nation's founder, Mwalimu Julius Nyerere, to unite the country and motivate his countrymen and women to fight poverty, diseases and ignorance.
Read   more :  http://allafrica.com/stories/201303100051.html

JK AMJULIA HALI KIBANDA

Nachukua fursa hii kuwapa maendeleo ya tiba ya Mwenyekiti wa TEF Absalom Kibanda ambaye amelazwa Hosipitali ya Millpark, Johannesburg nchini Afrika Kusini.
1. Kibanda leo ameingizwa theater ili kuanza kufanyiwa upasuaji na kujengwa sura baada ya kupungua kwa majeraha na uvimbe vilivyokuwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake, hususan kichwani na usoni.
2. Upasuaji huo unazingatia matokeo ya uchunguzi ulifanywa kwa zaidi ya saa 48 na jopo la madaktari na kubaini kwamba mbali na madhara ya awali, Kibanda pia aliumizwa taya lake la kushoto.
3. Kuhusu jicho lake la kushoto ambalo pia lilijeruhiwa, madaktari walisema wangetoa uamuzi kuhusu aina ya upasuaji ambao wangeufanya baada ya kubaini hali halisi wakati watakapokuwa wakijenga sura yake ambayo iliharibiwa kwa majeraha.
4. Wakati akipelekwa theater ambako alikuwa akifanyia upasuaji ambao uliotarajiwa kuchukua saa zaidi ya nne, alikuwa akilalamikia maumivu kutokana na kidonda kilichopo kwenye mguu wake wa kushoto. Kidonda hicho pia ni matokeo ya unyama aliyofayiwa.
5. Jana Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ambao wako Afrika Kusini kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini kumjulia hali. Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa watafikishwa mahakamani.
Tutaendelea kufahamishana kila hatua ya tiba ya Mwenyekiti wetu, na tunaomba tuendelee kumwombea ili apone haraka.


--
Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
+255 - 753 - 555556

Kenyatta Declared Kenya's Next President.

The son of Kenya’s first post-independence president, Jomo Kenyatta, took 50.07 percent of votes cast in the March 4 election, Independent Electoral and Boundaries Commission Chairman Issack Hassan told reporters today in the capital, Nairobi. Raila Odinga, the outgoing prime minister, got 43.3 percent, he said.
Odinga “does not believe that the result the IEBC announced reflected the will of the people,” Salim Lone, his adviser, said in an e-mailed response to questions today. “He will challenge the IEBC verdict in court.”
By electing Kenyatta, 51, Kenya becomes the second nation to have a sitting president facing indictment by the International Criminal Court. Sudan’s Umar al-Bashir has refused to cooperate with The Hague-based court and is under an arrest warrant for genocide and war crimes in the western region of Darfur.
 

Happy Women's Day

     TO  ALL  WOMEN ... HAPPY   WOMEN'S     DAY  2013.

MAFURIKO POSTA MPYA

Mvua  zinazoendelea  kunyesha  Dar  es  Salaam   hasa  maeneo  ya  kati  kati  ya  jiji   , asubuhi  hii  hali  ilikuwa  hivi...
Asubuhi  hii   barabarani   viatu  vilipumzika  kidogo  na  kisha  suruali    kukunjwa  hadi  magotini  ili kuweza kuvuka  na  kuelekea   ofisini,  hali  ilikuwa  mbaya.
Boda  Boda  nazo    mwendo  mdundo.
Huyu  ni  ofisa  wa  benki  maarufu  katika  mtaa  huu   akivuka  kueleka  ofisini  kwake .
Kufa  kufaana  , kuna  vijana wa  MUJINI    nao  walikuwa  kama  kawaida  kutengeza  dili za  kuvusha  watu , ukiwa  Posta  kijana  huyo  ni  nadra  sana  kumkosa  hasa katika  dili  zake  za  kuwahi  siti katika  daladala  zinazoelekea  Mwenge  au  Mbagala   kwa  Tsh 500,  leo  asubuhi    dili    lilibadirika   ghafla  ikawa ni   kuvusha   abiria  kwa kuwabeba , Hapa  ni kama  anamwambia   MREMBO    huyo  anayepita   "  karibu upande  mgongoni  nikuvushe"  mrembo  naye  wala    haoneshi   kushawishika!  KAZI  NI  KAZI.


                                        Rami  ikiwa  imefunikwa  na  maji .

Hali si shwari Simba Sports Club … Hans Pope na Kaburu Wajiuzulu

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Zacharia Hans Poppe,  ameamua kujiuzulu nyadhifa zote hizo kwa sababu kuna mgawanyiko ndani ya uongozi unaokwamisha maendeleo.
“Ni wazi kuwa kwenye uongozi tumekuwa hatufanyi kazi kwa umoja na mgawanyiko huu unatukwaza na hatuwezi kupata maendeleo,”alisema Hans Poppe.
“Baada ya kutafakari, nimeona ni bora nijiuzulu nyadhifa hizo kupisha wengine ambao wanaweza wakawa na mawazo mapya ya kuendeleza klabu, nami nitabakia kuwa mwanachama mwaminifu daima,”alisema Hans Poppe.
Poppe amewasilisha barua ya kujiuzulu Simba SC  jana na wazi kujiuzulu kwa Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ni pigo kwa klabu hiyo, kwani alikuwa akiisaidia mno kwa hali na mali.Aidha, kujiuzulu kwa Hans Poppe wazi kutachochea zaidi mgogoro ndani ya klabu hiyo na kuongeza shinikizo la viongozi wa klabu hiyo kujiuzulu pia.
Simba SC kwa sasa haifanyi vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na tayari imekwishatolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa jumla ya mabao 5-0 na Recreativo de Libolo ya Angola katika raundi ya kwanza tu.
Ubingwa wa Ligi Kuu ni kama umekwishaota mbawa, kwani hadi sasa Wekundu hao wa Msimbazi wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 31, sawa na Coastal Union ya Tanga na Mtibwa Sugar ya Morogoro, nyuma ya Azam FC yenye pointi 36 na Yanga inayoongoza kwa pointi zake 42, zote za Dar es Salaam.
Godfrey Nyange naye ajiuzulu kwa e-mail
MAKAMU Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ inadaiwa amemuandikia barua pepe, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhaj Ismail Aden Rage kumtaarifu kujiuzulu wadhifa huo.Kaburu anakuwa kiongozi wa pili wa Kamati ya Utendaji ya Simba kujiuzulu , baada ya awali mchana, Zacharia Hans Poppe aliyekuwa Mjumbe kujiuzulu pia.
Hans Poppe, aliyekuwa pia Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, alisema kwamba ameamua kujiuzulu nyadhifa zote hizo kwa sababu kuna mgawanyiko ndani ya uongozi unaokwamisha maendeleo.
Chanzo :  Bin  Zubeiry  Blog.

KIBANDA Avamiwa na kuumizwa.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda ametekwa na watu wasiofahamika na kisha kumjeruhi vibaya kwa nondo, mapanga na kisha kumng’oa meno, kucha na kumharibu jicho la kushoto.Tukio hilo la kinyama linafanana kwa kiasi fulani na lile la alilofanyiwa Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania, Stephen Ulimboka.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea juzi usiku wakati Kibanda akirejea nyumbani kwake Goba Punguni, Kata ya Mbezi Juu, kutoka kazini.Tayari mwandishi huyo mkongwe wa habari, amesafirishwa jana kwenda Afrika Kusini kwa matibabu zaidi. Aliondoka jana akisindikizwa na daktari kutoka Taasisi ya Mifupa Muhimu (Moi).Akizungumza kwa tabu alipokuwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), hospitalini Moi, Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006), alisema:

“Nilifika nyumbani kwangu kama saa sita usiku nikitokea kazini na nilipofika kwenye lango la kuingia ndani nilipiga honi ili mlinzi anifungulie. Lakini ghafla nilivamiwa na kundi la watu ambao walivunja kioo cha gari langu upande niliokuwa nimekaa. Nilitokea kupitia mlango wa abiria lakini sikuweza kuwakimbia watu wale kwani walinikamata na kuanza kunishambulia kwa vitu vizito.”

“Baada ya kutoka kwenye gari, nahisi nilikanyaga sehemu mbaya, nikateleza na kuanguka wakanifuata...niliona kama watu watatu hivi wakaanza kunishambulia. Sikuwa nafahamu kilichojiri, lakini nilisikia mwingine akimwambia mwenzake afande ‘mshuti... mshuti’ huyo alipoelekeza mtutu na kujaribu ‘kushuti’ (kupiga risasi) ilikuwa kama vile imegoma.

“Nikiwa bado niko chini, wakanipiga kwa kitu cha ncha kali kwenye jicho la kushoto, wakaning’oa meno na kucha katika vidole vya mkono wa kulia, walinipiga sana na nilipata maumivu makali. Baada ya kunipiga na kunijeruhi waliniburuza hadi bembeni ya nyumba yangu na kunitupa na wakaondoka, baadaye majirani na wasamaria wema walikuja kuniokoa.
Chanzo  :  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1713448/-/12827ip/-/index.html

KIBONZO


MVUA IKINYESHA DAR CITY CENTRE ( POSTA MPYA ) HUWA HIVI

Miundo   mbinu    eneo  la    POSTA  MPYA  Dar  City  Center  huwa   mbedembede    mvua  inaponyesha   hasa  kwa  mitaro  kushindwa  kuhimili    wingi  wa  maji    na  takataka  zingine . Wiki  hii  siku  ya  jumanne   mvua  zinazoendelea  kunyesha   hali iko  hivi  kama  ilivyoshuhudiwa  na    mwandishi wa  blog hii  kiasi    kikubwa   kuwa   kero    na   karaha  kwa  watumiaji  wa   stendi  ya  daladala  Posta  Mpya.
 Gari    kama  zinaelea  vile ,  maji  yakiwa  yamejaa    barabarani.
 Wafanyabiashara   eneo  la  stand   nao   hali ilikuwa  si shwari  kwani  wanalazimika  kufunga  biashara  zao.
  Maji  yakiendelea  kutiririka    barabarani .
 Kituo   cha     mafuta  cha  ORYX    palikuwa  hapapitiki  kabisa  .


      
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top