Social Icons

Loading...

Kibonzo - Mambo ya DIGITALI



RAI YA JENERALI : Hii ni harufu mbaya tu, Ibilisi bado hajaenda msalani

 BAADHI ya masuala ambayo nimekuwa nikiyajadili yanajitokeza hivi sasa kwa mshindo mkuu.Nimekuwa nikisema kwamba tunajitahidi mno kujenga taifa dogo ndani ya nchi kubwa. Hili linadhihirika sasa. Nimekuwa nikisema pia kwamba tunaonekana kuwa na haraka ya kufanya mambo kama vile tunakwenda kwingine, hapa si kwetu na wala hatujafika. Hili nalo linajionyesha.
    Hivi sasa tumetekwa na kelele zinazopigwa kuhusu gesi asilia inayochimbwa kusini mwa Tanzania, na tayari tumeanza kuona dalili za nchi kuparaganyika kutokana na ‘utajiri’ huo.Tunachokishuhudia si mjadala wa jinsi gani tunaweza kunufaika kama taifa kutokana na gesi inayochimbwa nchini ( na pia utajiri mwingine unaotokana na rasilimali za nchi) bali ni ghadhabu za makundi hasimu yanayokinzana kuhusu namna ya kugawana kidogo tulicho nacho.

    Kwa muda sasa, wataalamu duniani wamekuwa wakijadili kile kinachoitwa ‘resource curse’, au laana ya rasilimali. Hii ni laana ya nchi kama yetu ambazo zinajikuta zikiwa na rasilimali kubwa, lakini badala ya rasilimali hizo kuzinufaisha nchi hizo inageuka kuwa ni balaa, laaana. Hili ndilo linaelekea kutokea hapa nchini.Bado hatujui kwa uhakika ni kiasi gani cha gesi asilia tulicho nacho. Nimesoma mahali kadhaa kwamba gesi hii ni nyingi mno na inaweza ikaifanya Tanzania kuwa mojawapo ya nchi zenye machimbo ya gesi makubwa duniani. Bila shaka hilo lingekuwa jambo jema kwa nchi inayoendeshwa kwa utaratibu unaoeleweka na inayojadili masuala muhimu kwa uwazi wa kutosha.
    Kwa bahati mbaya, hii si kweli. Tumekuwa tukishuhudia usiri unaogubika mikataba juu ya rasilimali nyingine kwa muda mrefu sasa, na hakuna dalili kwamba tutaanza kesho au keshokutwa kuwa wawazi zaidi.Hadi leo serikali inakataa kuanika hadharani maudhui ya mikataba inayoingia kwa niaba ya Watanzania, na serikali  ikiulizwa inajibu kwamba mikataba hiyo ni siri baina ya serikali na ‘ wawekezaji.’

Mancini 'sad' about Balotelli sale ; IS IT TRUE??

Roberto Mancini admits a move to AC Milan was the best option for Mario Balotelli, with the striker set to join the Italian club on a four-and-a-half year deal.It appears Balotelli, 22, has completed a medical with Milan and will move to the San Siro on Wednesday, although a formal contract is yet to be signed.
Following City's 0-0 draw with QPR in the Premier League on Tuesday, Mancini conceded it was a tough decision to let Balotelli go, although he insists the Italy international will benefit from playing in his home country.
"We are also sad because Mario was an important player for us," Mancini said. "With Mario we won the Premier League and the FA Cup in two years. But it's important for him to go back to Italy.
"It will be a good chance for him to stay with his family, to play for Milan. I think he can improve and I'm happy he will become one of the best players in the world.
"We love Mario and he deserves to have this chance. For me, no [he was not a problem]. Mario was like another one of my children. But you can be upset with him sometimes, but afterwards he's a lovely lad. When he left the hotel, they [the players] were really sad. Mario is a good guy."
Read more at http://www.espn.co.uk/football/sport/story/190801.html#eRrdljv58wKio67f.99

Tanzania: It Is High Time Local Media Embraced Professionalism.

 Minister for Information, Youth, Culture and Sports, Dr Fenella Mukangara, visited the head office of Tanzania Standard (Newspapers) Limited (TSN) in Dar es Salaam where she hailed the company for operating profitably.
The minister also showered praise on TSN as among the few public entities that do not depend on the Treasury coffers to go about its business but rather generate its own income, pay requisite taxes and pay dividends to its majority and only shareholder, the government.
She was also happy that although it was operating independently without subsidies from the government, TSN has been able to stand out firm in the highly competitive media industry for many years now. On the professional front, touting the state-owned publisher as the market leader for observing high level of professionalism, she urged TSN to continue setting the pace when it comes to moral standards for others in the industry to emulate.
In today's media industry, thanks to the freedom of speech and expression, a number of newspapers, radio and television stations have been established. However, unlike the electronic media a number of newspapers end up folding shortly after few publications and this is due to the competitive nature of the market.
Thus, for a company as old as TSN to continue dominating the market it is for sure, worth praises. What is even worse for the print media is the coming into the scene of social media where information is relayed on real time basis. It is because of these factors that newspapers are now ought to be creative and adhere to professionalism.
Most of the newspapers died a natural death because they do not adhere to professionalism and thus feed readers biased information or about generally insignificant matters that have no influence in the society. Dr Mukangara did not mince words on the need to adhere to professionalism.
She was clear that even as the objective of establishing TSN was to promote and propagate government policies, publications should not avoid constructive criticisms aimed at correcting the status quo. It is thus high time for the media in the country to embrace professionalism and patriotism towards the building of better Tanzania of tomorrow.
Source :  http://allafrica.com/stories/201301300081.html

Profesa Ndulu ataka BoT isiingiliwe na wanasiasa.

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu amependekeza Katiba Mpya iweke kinga ambayo itailinda benki hiyo ili ifanye kazi zake bila kuingiliwa na mambo ya kisiasa.
Aidha, amependekeza Katiba Mpya itenganishe mamlaka zinazotoa na zile zinazotumia fedha ili kila moja ifanye kazi zake kwa kujitegemea, huku pia akitaka kinga zinazolinda shughuli za kibenki zitambulike kikatiba na si kuwepo kwenye sheria za Bunge.
Alisema benki zinapaswa kutoa fedha kwa kiwango maalumu bila kuzizidisha kwa ajili ya kuimarisha uchumi.
Akizungumza Dar es Salaam jana muda mfupi baada ya kuwasilisha maoni ya BoT kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Ndulu alisema umefika wakati BoT ikajengewa uwezo wa kufanya shughuli zake bila kuingiliwa na wanasiasa.Profesa Ndulu alisema endapo BoT itawekewa kinga itakuwa na uwezo wa kufanya kazi zake vizuri zaidi.
Soma  zaidi :  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1677998/-/11rqlh9/-/index.html

Kinana: Serikali iwasikilize wananchi wa Mtwara

SAKATA la gesi sasa limeingia hatua mpya, baada ya watendaji wakuu wa CCM; Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kuitaka Serikali ikae na wana-Mtwara ili kuona namna ya kumaliza mgogoro huo kwa amani.Kinana na Nape walitoa kauli hizo kwa nyakati tofauti jana. Wakati Kinana alisema hayo alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara mkoani Kigoma, Nape alifanya hivyo kupitia mtandaowa Twitter na baadaye kuthibitisha kauli hiyo alipoulizwa na mwandishi wetu.

Wakati watendaji hao wa CCM wakitoa matamko hayo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana alifanya vikao mfululizo mkoani Mtwara akisaka suluhu ya mgogoro huo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Uvinza, Kigoma, Kinana aliitaka Serikali isikilize hoja za wakazi wa Mtwara na kuzitafutia usumbufu sahihi.Mbali na kutoa ushauri huo, aliitaka pia Serikali kuwasaka watu wanaochochea mgogoro huo kwa kufanya vurugu na kuharibu mali za watu na kuwafikisha mbele ya sheria.

“Serikali ikae na wana-Mtwara na kuwasikiliza, wananchi hao wana hoja na Serikali inapaswa kutoa majibu sahihi kwa hoja hizo. Lakini pia iwasake na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha uvunjifu wa amani,” alisema Kinana.
Soma  zaidi :  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1678154/-/11rr4f4/-/index.html

Linux & Web Applications Training .


Kibonzo - Enzi za Mwalimu.


Vikao Vya Bunge Kuanza Kesho

WAKATI Kikao cha Kumi cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinatarajiwa kuanza kesho, Wabunge watano wamejitokeza kuwasilisha hoja binafsi katika kikao hicho.
Mbunge wa Mkanyageni (CUF), Zanzibar Habib Mnyaa anakusudia kuwasilisha maombi ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara kupinga gesi iliyogundulika mkoani humo kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam.
Naye Waziri Kivuli wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo  Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ alisema atawasilisha hoja binafsi kutaka kujua fedha zinazotumika kulipia vipindi vya runinga vinavyoelezea mafanikio ya Serikali.Mbilinyi ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) alisema atafanya hivyo ili kujua fedha hizo zinalipwa na nani kwa malengo gani.
Kwa upande wake, Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuwasilisha hoja ya kuitaka Serikali kupeleka bungeni muswada wa sheria, wa kuanzisha Mfuko wa Elimu ya Juu. Lengo kuu ni kuhakikisha kila mwanafunzi aliyepata nafasi ya kujiunga na elimu ya juu anakopeshwa kwa asilimia 100.Naye Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa anatarajiwa kuwasilisha hoja binafsi kutaka Bunge liunde Tume ya kuchunguza vitendo vya ujangili vinavyoendelea hapa nchini.
Kwa upande wake Mbunge wa Msoma Mjini (Chadema), Vincent Nyerere atawasilisha hoja binafsi kuhusu matukio ya kigaidi na mauaji holela ya raia wasio na hatia yanayotokea hapa nchini.Nyerere alisema hivi sasa vitendo vya mauaji vinaendelea, utasikia polisi kauawa na wananchi au wananchi wamemuua polisi lakini hakuna hatua zaidi.Analitaka Bunge kutoa maadhimio kuhusu vitendo hivyo vinavyohatarisha usalama wa raia na mali zao.
Chanzo  Gazeti  la  Mwananchi.

KP Leo


Chadema yajipanga kwenda Ikulu 2015

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza mkakati wa kuhakikisha kinashinda Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 ili kukiwezesha kuingia Ikulu.
Kimesema kitatekeleza hatua hiyo pia kwa kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wake wapya akiwamo mwenyekiti wa taifa, uchaguzi utakaofanyika ndani ya mwaka huu. Hata hivyo, tarehe, mwezi na ratiba kamili ya uchaguzi huo itatolewa baadaye.Kujipanga kwa chama hicho sambamba na kujenga hoja kulithibitika pia katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mwaka jana mkoani Dodoma, baada ya mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete kuwataka mawaziri na makada wa chama hicho kufanya mikutano ya hadhara na kutumia vyombo vya habari kujibu hoja za wapinzani, badala ya kutegemea nguvu za Jeshi la Polisi.Katika mkutano huo, Rais Kikwete alimtaja wazi Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk  Willibrod Slaa, akidai kuwa aliwahi kumzulia uongo pamoja na mwanaye Ridhiwani.Rais Kikwete alisisitiza kuwa hiyo ndiyo kazi ya upinzani, akiwaita watu wazima ovyo na kudai kwamba wanasema uongo mbele ya wananchi na kwamba hata wakati mwingine hunukuu takwimu za uzushi kwenye vyombo vya habari.

Nani wa kulaumiwa???


Swansea 2 Chelsea 0 ; Semi final Capital One Cup

Swansea won at Chelsea for the first time in 87 years to head into the Capital One Cup semi-final second leg with a precious two-goal advantage. Final  will  be   Bradford City  Vs  Swansea City   Capital One Cup Final at Wembley Stadium, London on 24th  February 2013.



   Does     Chelsea  Current    Team  manager  Remember  this???


Swansea  City  Vs    Bradford  City  on  24  Feb  2013    Wembley  Stadium 
                                                

Rushwa Tanzania ....


Watoto Wengine Wana Maswali Magumu...


SWAGA ZA WADADA

SWAGA ZA WADADA ZETU ILI WAONEKANE NAO WAMO HASA WAKITOKA USWAZI WAKAWA WAMENDA OUT MITAA YA USHUANI;
1. Halima………muhudumu naomba unilete salad ya moto, na chupa ya Amarula.
2. Chausiku…..nipe PIN yako niwe nakupigia
3. Siwema….nimechokaje, nimeshinda Shoprite  natengeneza nywele
4. Gulo….Boifrend wangu kanambia likizo ya  summer mwaka huu tutago London tukale Chrismas
5. Cynthia…Nimenunua  BlackBerry wamenambia PIN nikaipitie kesho
6. Fulo....Mi napendaga kusafiri na Presishen, napenda viti vya dirishani, mtu unakaa unafungua kioo chako hewa safiii mpaka mwisho wa safari.
7. Fatuma….kiukweli mi niliipenda London kuliko UK.

Tibaijuka atenganisha Mji wa Kigamboni na Temeke

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ameanzisha Wakala wa Kuendeleza Mji wa Kigamboni (KDA). Kwa maana hiyo, mji huo hautakuwa tena chini ya mamlaka ya Manispaa ya Temeke.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Profesa Tibaijuka alisema Serikali imeamua kuanzisha wakala huo ili pamoja na mambo mengine, upange na kusimamia ujenzi wa mji wa kisasa katika eneo hilo.“KDA imeanzishwa chini ya Sheria ya Wakala wa Serikali ya 1997 ili iweze kuhakikisha mji unajengwa na unakuwa bora,” alisema Profesa Tibaijuka.Alisema kutokana na kuanzishwa kwa KDA, kata zote za Kigamboni, zitaungana na madiwani wake pamoja na mbunge wao watakuwa wakikutana katika Baraza la Ushauri la KDA.“Kutakuwa na Baraza la Kigamboni ambalo madiwani na mbunge wao wataingia humo kujadili maendeleo ya mji huo na leo (jana), kutakuwa na kikao cha kwanza,” alisema Profesa Tibaijuka.
Soma  zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1673740/-/11rnri0/-/index.html

Valentine 2013 Dinner Talk @ JB Belmont Hotel


Ndege ya ATCL ikifanyiwa marekebisho na wahandisi -tayari kurudi mzigoni.

Mhandisi  akiwa  kazini  kurekebisha  kioo  cha  ndege  ya  ATCL  iliyopata  hitilafu  ikiwa  angani    kuruka   toka mkoani  Kigoma   kuelekea  Dar .
                                                       Ukarabati  ukiwa  unaendelea .

KP Leo


President Obama Inauguration Ceremony 2013

Mkapa ajitosa sakata la gesi.

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ameelezea kufedheheshwa kwake na mgogoro wa gesi, huku akiwataka wananchi na wadau wa maendeleo wa Mkoa wa Mtwara kusitisha harakati za maandamano na mihadhara.Mkapa alitaka wakazi hao kuacha kulumbana na Serikali kuhusu suala hilo, badala yake wajiandae kukaa meza moja nayo kutafuta mwafaka kwa njia ya amani.
Katika tamko lake alilolitoa Dar es Salaam jana, Mkapa alisema: “Fujo, vitisho, kupimana nguvu na malumbano siyo masharti ya maendeleo.“Nikiwa kama mwana - Mtwara na raia mwema, mpenda nchi, nimefedheheshwa sana na matukio haya ya siku za karibuni Mtwara. Kwa sababu hiyo natoa wito kwa wadau wote wa maendeleo ya Mtwara, kusitisha harakati hizi na maandamano na mihadhara.
    “Badala yake wajipange kukaa pamoja katika meza moja,  kupitia historia, kutathmini mipango, kuchambua kwa kina mikakati ya utekelezaji wake, hatimaye kufikia mwafaka wa ujia wa maendeleo. Liwezekanalo leo lisingoje kesho.”Mkapa alisema mwenendo wa mazungumzo, maandamano na mikutano ya hadhara inayoendelea mkoani Mtwara, inaelekea kuashiria kuvunjika kwa amani hali aliyosema kuwa inajenga kutokuelewana kati ya viongozi wa vyama vya siasa na Serikali, wananchi na vyama vya siasa na wananchi na viongozi wa Serikali.
Soma  zaidi :  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1672020/-/11rmwmu/-/index.html

Tanzania hailed for speedy ICT advance

South Korea Deputy Speaker, Park Byeong-Seug yesterday applauded the Tanzanian government for its effort and achievements in developing the information technology sector via the nation’s vocational institutes.Speaking in Dar es Salaam yesterday, shortly after paying an official visit to the Kipawa Institute of Communication Technology (KIICT) which is under the Vocational Education Training Authority (VETA), Byeong-Seug said he was surprised at how fast Tanzania is improving in the sector of technology.
 
“Am pleased to be in Tanzania, witnessing these subtle but fast technological developments…” he said. Despite the many challenges facing the country, he acknowledged that Tanzania has managed to provide technological education to its people in many ways.As he toured the various KIICT workshops, he pledged to convene with respective government officials in South Korea for financial support for the development of ICT in rural communities in the country.“We will also see how we can focus on instructors and management members’ training so as to increase their number and capacities… ’ pledged the deputy speaker.
 

Moto wa gesi wazidi kushika kasi Mtwara.

SAKATA la kupinga ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam limechukua sura mpya baada ya wananchi zaidi ya 30,000 kusaini katika fomu maalumu kupinga gesi hiyo kusafirishwa.Wakati wananchi hao wakikamilisha shughuli hiyo na kukabidhi fomu hizo kwa wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF), umoja wa vyama tisa vya siasa mkoani umemwomba Rais Jakaya Kikwete kusitisha mradi huo ili kuepusha uvunjifu wa amani unaoweza kujitokeza.Pia, umoja huo umewataka wabunge wote wa Mkoa wa Mtwara kutangaza msimamo wa kila mmoja juu ya gesi kwenda Dar es Salaam au kukubaliana na uamuzi wa Serikali ili wajue nani msaliti kwao.
        Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Uwanja wa Sabasaba mjini hapa, viongozi hao kwa nyakati tofauti wamemtaka Rais Kikwete kutokutumia ‘jazba na mabavu’ katika kulipatia suluhu jambo hilo, badala yake busara zitawale kwa kusitisha mradi huo.“Sisi Watanzania hatujazoea vita, bali tumezoea kupata hasara… katika hili naomba Kikwete akubali kupata hasara kama tunavyokubali hasara nyingine…Sisi wananchi tupo radhi tuingie kwenye deni kubwa kama hilo, lakini gesi haiwezi kwenda Dar es Salaam,” alisema Uledi Abdallah Makamu, Mwenyekiti wa umoja huo na kuongeza:“Hizo trilioni tatu kama anaona hawezi kuzilipa iwapo gesi itabakia Mtwara...Basi atafute njia nyingine za kulipa… Atambue kuwa hakuna fedha yenye thamani ya amani na utulivu wetu…akumbuke kuwa mafahali wawili hawakai zizi moja.”Naye Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mtwara Mjini, Mustafa Nchia aliwataka wabunge kutoa misimamo yao ili wananchi wajue ni mbunge yupi anawaunga mkono na yupi msaliti kwao.
Soma   Zaidi :  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1671038/-/11rm8cs/-/index.html

Obama Aapishwa Rasmi.

RAIS Barack Obama wa Marekani ameapishwa rasmi kushika muhula wa pili wa urais, katika sherehe maalumu iliyofanyika kwenye Ikulu ya nchi hiyo jana.
Obama ambaye ni Rais wa 44 wa Marekani, aliingia madarakani katika uchaguzi wa kihistoria mwaka 2008 uliomfanya kuwa Rais wa kwanza mwenye asili ya Afrika katika taifa hilo kubwa duniani.Sherehe za kuapishwa kwake Ikulu jana zilikuwa za faragha na zilihudhuriwa na watu wachache maalumu, leo ataapishwa katika sherehe za jumla zitakazowajumuisha watu wote kwenye Uwanja wa National Mall.
Katika kiapo chake, Obama atatumia Biblia mbili, moja iliyokuwa ikitumiwa na Martin Luther King na nyingine ilikuwa ikitumiwa na aliyekuwa Rais wa 16 wa Marekani, Abraham Lincoln.
      Lincoln aliongoza taifa hilo kuanzia Machi 1861 hadi alipouawa Aprili 1865.
Akiwa Ikulu jana, alitumia Biblia iliyowahi kutumiwa na Lincoln, katika sherehe za leo  atatumia Biblia ya Martin Luther King.Lincoln, ndiye aliyeliongoza taifa hilo kipindi kigumu cha kusimamia umoja na kufuta biashara ya utumwa.Martin Luther King ambaye alikuwa mchungaji na mwanaharakati wa haki za watu wenye asili ya Afrika nchini Marekani, aliuawa Aprili 4, 1968, muda mfupi baada ya kutoa hotuba yenye nguvu ya I have a Dream (Nimeota ndoto).Hotuba hiyo ikuwa ikieleza ndoto yake kwamba muda siyo mrefu watu wenye asili ya Afrika watapata nguvu na kupata haki yao kama raia wa Marekani.
Soma  zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kimataifa/-/1597284/1671080/-/14b41t5z/-/index.html

Wabunge waanza kujiandikisha JKT.

WABUNGE vijana katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wameanza kujiandikisha tayari kwa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa Mujibu wa Sheria kwa ajili ya mafunzo yatakayoanza Machi mwaka huu.Taarifa ambazo Mwananchi Jumamosi ilizipata juzi, zimeeleza kuwa, idadi ya wabunge ambao tayari wamejiandikisha kujiunga na JKT hadi sasa ni zaidi ya 31, huku wengine wakiendelea.
Kujiandikisha kwa wabunge hao ili wajiunge na JKT kunafuatia wito uliotolewa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, Julai mwaka uliopita, alipowasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake katika Bunge la Bajeti mjini Dodoma.
        Kwa nyakati tofauti wabunge vijana kutoka CCM, Chadema na NCCR- Mageuzi walilithibitishia gazeti hili kuwa tayari wamejiandikisha katika Ofisi ya Katibu wa Bunge kwa ajili ya mafunzo hayo.Imebainishwa kuwa, miongoni mwa wabunge waliojiandikisha, wamo pia ambao waliwahi kupitia mafunzo hayo, ikielezwa kuwa wamefanya hivyo wakitaka kwenda kujikumbushia.
Soma  Zaidi  :  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/-/1597332/1669540/-/bolrnxz/-/index.html

Barca yakwaa KISIKI yalala 3 - 2 Real Sociedad.



EPL Man U yabanwa Mbavu na Spurs, Liverpool Yaua.

Liverpool   5    Norwich  City  0



Man  City   3  Stoke  City 0

 
Chelsea  2  Arsenal 1

Man U 1  Spurs  1



KIBONZO


Marufuku wanawake kukaa kiume kwenye pikipiki

Jiji moja nchini Indonesia ambalo limekuwa likifuata sheria za kiislamu maarufu kama sharia, liko mbioni kupitisha sheria ya kuwapiga marufuku wanawake kukaa kiume kwenye pikipiki, zenye kuendeshwa na wanaume, kwa madai kuwa mkao huo huwaondolea uthamani wao
Suaidi Yahya, ambaye ni meya wa jiji hilo la Lhokseumawe, ameeleza kuwa, mpango huo umelenga katika kutunza mila na desturi za watu na tayari vipeperushi kwa ajili ya kusambaza taarifa juu ya kusudio la mpango huo, vimeshaanza kusambazwa mitaani.
      Chini ya sheria mpya, meya huyo anasema kuwa, wanawake wataruhusiwa tu kupanda pikipiki wakiwa wamekaa kiupande upande (kike), kwakuwa kukaa kiume ni ukiukwaji wa sheria za kiislamu.
“Ukimuona mwanamke amekaa kiume kwenye pikipiki, anaonekana kama mwanaume tu, lakini akikaa kike, anaonekana kama mwanamke kweli” amesema meya huyo na kuongeza pia kuwa, watu wenye kupanda pikipiki na kukaa mkao wa kike, pia hawapati ajali za kuanguka kwa urahisi.
Mamlaka za mji huo, zinatarajiwa kuanza kufanya mapitio ya muswada huo katika muda wa mwezi mmoja na ikiwa wataridhia basi utapitishwa na kuwa sheria ndogo ya jiji hilo.
     Alipoulizwa ikiwa wanawake ambao hawatatimiza sharti hilo watachukuliwa hatua, meya huyo alijibu “ndio, mara tu itakapopitishwa na kuwa sheria rasmi, hakika kutakuwa na adhabu itayotolewa”
Hata hivyo, muswada huu, umekutana na vipingamizi toka kwa watu mbalimbali akiwemo mwanaharakati wa masuala ya kiislamu, Ulil Abshar Abdalla, mwenye makazi yake kwenye mji mkuu wa Indonesia wa Jakarta.
“Uendeshaji au upakiaji wa pikipiki haujawekewa kanuni katika quran tukufu wala kwenye hadith za kiislamu ambazo ndio chimbuko la maelekezo yetu” amesema mwanaharakati huyo

Kampuni ya Tigo yagoma kupunguza gharama za simu.

WAKATI Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwasilisha rai ya kupunguza gharama za mwingiliano wa simu , Kampuni ya Tigo imekataa kufanya hivyo kwa madai kuwa itahatarisha uwekezaji wake kwa punguzo la asilimia 69.
Msimamo huo wa Tigo, umekuja baada ya TCRA kukutana na wadau wa mawasiliano jana jijini Dar es salaam, ili kukusanya maoni kuhusu mapendekezo ya kupunguza gharama ya mtandao mmoja kwenda mwingine. Hatua hiyo inalenga katika kuwasaidia wananchi kumudu gharama za mawasiliano ya simu.Naibu Mkurugenzi wa Utekelezaji wa Kanda wa TCRA, Victor Nkya, alisema punguzo hilo ni la kutoka asilimia 35 hadi asilimia 69 na kwamba litaanza kutumika Machi mosi mwaka huu na kukoma Desemba 31 mwaka 2017 .
Nkya alisema punguzo la gharama ya kupiga mtandao mmoja kwenda mwingine kwa mwaka 2013 litakuwa asilimia 34.92, mwaka 2014 asilimia 32.40, mwaka 2015 asilimia 30.18, mwaka 2016 asilimia 28.57 na mwaka 2017 ni asilimia 26.96.
Zaidi  Fuatilia  hapa  : http://www.mwananchi.co.tz/-/1597570/1668454/-/xkrt34/-/index.html

Supersport TV kurusha Mzunguko wa pili Ligi kuu Bara (Ligi kuu Vodacom )

MZUNGUKO wa pili ya Ligi Kuu ya Vodacom utaanza Januari 26 mwaka huu huku kukiwa na maombi ya televisheni ya SuperSport kuonyesha mechi za Super Week kama ilivyokuwa katika mzunguko wa kwanza.
 
Raundi tano za awali katika ratiba ya mzunguko wa pili zinabaki kama zilivyo wakati nyingine zilizobaki zitatolewa baada ya kuingiza mechi za Super Week.
 
Wakati huo huo, mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza unatarajia kuanza Januari 26 mwaka huu. Ratiba ya ligi hiyo na tarehe rasmi ya kuanza itatangazwa baada ya kupitiwa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inayotarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki.

PEP GUARDIOLA KUTUA UJERUMANI KUINOA BUYERN MUNICH

HATIMAYE  KILE  KITENDAWILI  WAPI   KOCHA   WA  ZAMANI  WA  BARCA   PEP   GUARDIOALA    WAPI   MSIMU  UJAO  WA  LIGI  BARANI  UROPA  ATASAINI   KAMA  KOCHA    KIMETEGULIWA  NA  SASA  AMEPATA   KANDARASI  YA  KUINOA    BUYERN  MUNICH  YA  UJERUMANI  KWA    MIAKA  3,  KUANZIA JUNE  2013   VILABU  AMBAVYO   VILIKUWA   VIKIMWANIA  NI  PAMOJA  NA  MAN CITY  NA CHELSEA  VYA  ENGLAND.
PEP  NI  MIONGONI  MWA  MAKACHO WENYE  MAFANIKIO  MAKUBWA  DUNIANI.

DCI Manumba alazwa Aga Khan.

HALI ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi (DCI), Kamishna Robert Manumba ni mbaya na amelazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU), Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.Habari zilizopatikana jana zilieleza kuwa Manumba amelazwa hospitalini hapo baada ya kusumbuliwa na maradhi kadhaa, ikiwamo figo.

Taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi zilisema jana kuwa tangu juzi, Manumba alikuwa hajitambui baada ya kuugua malaria ghafla na hali hiyo ilisababisha pia figo zake zote mbili kushindwa kufanya kazi.
“Alitakiwa kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu, lakini ilishindikana kwa sababu hajitambui, wakajaribu kumzindua, ikashindikana,” kilieleza chanzo hicho cha habari ndani ya jeshi hilo.
Habari  zaidi  : http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1667476/-/11r4xlt/-/index.html

Kibonzo


Okwi atua Etoile kwa Tshs : 477 mil.

Klabu  ya   Etoile du  Sahel  ya   Tunisia  imemsajili  mshambuliaji  hatari  wa    Simba   Emanuel  Okwi    t toka   Uganda kwa   kitita  cha  $300,000  sawa  na  Tshs   477 mil  , Mganda huyu   atakuwa  akikipiga  katika  klabu  hiyo , moja  ya  vigogo  kabisa  vya  soka  barani  Afrika  kwa  miaka  3.

KIBONZO


Dr Shein vows defence of the Union as Isles mark 49 of Revolution.

Zanzibaris  marked 49 years of the 12 January 1964 revolution, as Isles President Dr Ali Mohammed Shein defended the Union, describing it as the “cornerstone” of prevailing peace, unity, and harmony in both Zanzibar and the entire United Republic.
“Our Union is firm and since its founding has earned our country great esteem internationally,” remarked the soft-spoken but tough Isles leader in a speech to mark the Zanzibar revolution in festivities at Amaan Stadium.
   The celebrations were attended by ordinary people and high-profile figures from both sides of the Union, including retired President Ali Hassan Mwinyi, former Isles Presidents Abeid Amani Karume and Dr Salmin Amour, present and former prime ministers Mizengo Pinda and Frederick Sumaye, and senior government officials.
Also in attendance were members of the diplomatic corps, representatives of political parties, civil societies and ordinary people.
      In his address, Dr Shein said despite some challenges facing it, the Union has registered significant strides—in terms of political, economic and social development and strengthening of peace and stability.He, however, admitted that last year Zanzibar witnessed incidents sowing chaos and violence that were later on controlled by defence and security organs, which painted a bad picture on the history of Tanzania as a haven of peace.
But he warned that Isles government will continue taking punitive and firm measures against perpetrators of violence and destructive elements, noting that “we will not tolerate such activities at all.”

UTAFITI: Watoto wa kike wanaelewa haraka darasani kuliko wa kiume

UTAFITI mpya wa masuala ya elimu umebainisha kwamba wanafunzi wa kike hufanya vizuri zaidi darasani kuliko wanafunzi wa kiume.
Matokeo ya utafiti huo, uliofanywa hivi karibuni na wataalamu wa elimu kutoka vyuo vikuu vya Georgia na Columbia vya nchini Marekani, umebaini kuwa watoto wa kike wa kati ya umri wa miaka sita hadi 12, huelewa kwa haraka darasani kuliko watoto wale wa  kiume.
Wameeleza kuwa wanafunzi hao wa kike huwa makini zaidi kumsikiliza mwalimu anapokuwa akifundisha darasani, tofauti na watoto wa kiume, ambao hutumia muda mwingi kufanya mambo mengine ikiwamo kucheza, kuchokozana na pengine kugombana wao kwa wao.
Matokeo hayo yaliyochapishwa katika Jarida la Rasilimali Watu la Marekani na kuandikwa kwenye mtandao wa Daily Mail, yanaonyesha kuwa utafiti huo uliangalia uwezo wa watoto zaidi ya 5,000 katika Kusoma, Hisabati na Sayansi.
Watafiti hao kwa kuangalia alama za majaribio mbalimbali na maoni ya walimu, waligundua kuwa hata katika hatua za awali (chekechea), alama za watoto wa kike zimekuwa juu siku zote ikilinganishwa na alama za watoto wa kiume.
Mmoja wa watafiti hao, Christopher Cornwell, anasema kuwa ujuzi wa wanafunzi hao, ndiyo njia kubwa inayotumiwa na walimu kuwapanga wanafunzi wao katika madaraja.
Aliongeza kuwa kuna vigezo sita vya kupima uwezo wa watoto, ambavyo ni: Usikivu, ufuatiliaji wa kazi anazopewa darasani, kupenda kujifunza, kusoma kwa kujitegemea, uwezo wa kubadilika kutokana na mazingira na mpangilio wa mambo yake.
Soma  zaidi :  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1664388/-/11r2tvs/-/index.html

Kura ya maoni yampa ushindi Raila Odinga uchaguzi Kenya

WAZIRI Mkuu Raila Odinga na Makamu wa Rais, Kalonzo Musyoka wamepewa ushindi wa awali katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Machi 4 nchini Kenya.
Kwa mujibu wa kura ya maoni ya Infotrak, iwapo uchaguzi ungefanyika wiki hii, Odinga anayewania wadhifa wa kuongoza nchi hiyo kupitia muungano wa Cord angeshinda kwa asilimia 51 ya kura.
Raila ambaye ni Waziri Mkuu katika Serikali inayomaliza muda wake ndiye mgombea urais kupitia muungano huo, pamoja na mgombea mwenza, Musyoka ambaye ni makamu wa Rais katika Serikali hiyo.
       Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo uliofanywa na kampuni ya Infotrak and Consulting, Raila na Kalonzo watapata asilimia 51 ya kura zote zitakazopigwa huku wapinzani wao wakuu, Uhuru Kenyatta na William Ruto wanaowania wadhifa huo kwa tiketi ya muungano wa Jubilee wakipata asilimia 39.
Hii ina maana kuwa iwapo mambo yakisalia yalivyo, uchaguzi wa urais hautaingia katika awamu ya pili.
       Kura hizo za maoni pia zinaonyesha mgombea urais wa Muungano wa Amani, Naibu Waziri Mkuu,  Musalia Mudavadi na Muungano wa Eagle unaoshirikisha na Peter Kenneth na Raphael Tuju wanashika nafasi ya tatu kwa kuzoa asilimia 3 ya kura hizo.
Wagombea wengine wanaoshiriki katika uchaguzi huo wa urais kwa tiketi za vyama vyao bila kuungana na vyama vingine,
Martha Karua na Professa James Ole Kiyiapi wamepata asilimia 0.3 na 0.1.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Angela Ambitho alisema kuwa katika utafiti huo, watu 1,500 walihojiwa.
Alisema kura hiyo ilifanyika kabla ya Mudavadi kuteuliwa rasmi kama mgombea urais wa muungano wa Amani unaoshirikisha chama chake cha United Democratic Forum (UDF), Kanu na New Ford Kenya.
Utafiti huo ulifanyika kati ya Desemba 28 mwaka jana na Januari 2 mwaka huu katika kaunti 25 kwenye mikoa yote nchini.
Chanzo  Mwananchi

EPL weekend : Chelsea, Man U & City Zatakata.

Chelsea 4   Stoke  City   0


Man   U   2   Liverpool   1





Man  City 2   Arsenal  0

 Matokeo  mengine   tembelea
http://www.premierleague.com/en-gb/matchday/results.html

Aomba asichaguliwe asipotimiza ahadi.


MBUNGE wa Jimbo la Iringa ,Mchungaji Peter Msigwa amewataka wakazi wa Kijiji cha Kigonzile, katika Manispaa ya Iringa kutomchagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ikiwa hatatimiza ahadi ya kuwapelekea maji na barabara katika kipindi hiki cha uongozi wake.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kigonzile juzi, Msigwa alisema amepania kuwafikishia maji na barabara wakazi wa kijiji hicho ili kuwapunguzia kero ya kutafuta maji na adha ya usafiri.

“Ninajua kero ya maji na barabara ndizo zinazowatesa wakazi wa kijiji hiki hususani wakina mama, lakini niseme tu kwamba suala la maji, nimefurahi kuna mfuko mnaendelea kuuchangia deni lililobaki ninalimalizia sasa na kuhusu barabara tayari nimeshaleta greda nitahakikisha barabara hii inatengenezwa, nisipotimiza ahadi hizi msinipigie kura mwaka 2015,”alisema Msigwa.
Soma  zaidi :  http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/1597578/1662934/-/vk5saf/-/index.html

SADC Summit 2013 Dar es Salaam predged to send troops to stabilise DRC.

Tanzania is among four Southern Africa Development Community (SADC) member countries, which have pledged to send troops to the Democratic Republic of Congo (DRC) in a bid to end a crisis between Kinshasa government and the rebels in the eastern part of the country. This was revealed in Dar es Salaam yesterday during a media briefing at which a communiqué was read following a two-day Extraordinary Summit of the SADC’s organ on Political Defence and Security Cooperation.The other countries that have also pledged to send troops under the Neutral International Force (NIF) are Malawi, Namibia and South Africa.
    
       Reading the communiqué, the SADC Executive Secretary, Tomaz Salomao said the regional community urged the other member countries to follow suit.
“The Summit welcomed the pledges made by Malawi, Namibia South Africa and Tanzania to contribute to the deployment of the NIF and urged those who have not yet done so, to do so as a matter of urgency,” noted Salomao.
           He added that the Summit welcomed the United Nations (UN) support for the deployment of the NIF through the proposed UN Framework concept for Intervention Brigade in the Eastern DRC and expressed its readiness to work with UN.
Salomao said the summit, attended by four heads of state and governments noted with appreciation the good collaboration between SADC and the International Conference for the   Great Lakes Region (ICGLR) on the development in the Eastern DRC ant it reiterated the call for an urgent attention to the grave humanitarian situation in the DRC.
However, when asked on the size of the contribution from countries that have made pledges, President Jakaya Kikwete who chaired the Summit said that aspect was yet to be determined.

UDSM campus to hosts Games of 40 universities

More than 40 universities will compete at the coming Eastern Africa University Games (EAUG) scheduled to take off next month in Dar es Salaam.
The organising committee chairman, Professor Yunus Mgaya, said yesterday that the games will take place from February 8 to 12.
 President Jakaya Kikwete will grace the opening ceremony of the eighth regional championship to be hosted by the University of Dar es Salaam under the auspices of the Tanzania Universities Sports Association (TUSA), he said, noting that preparations were going on well.EAUG is an event organized on a rotational basis among universities, to bring together students from scores of universities in the region.
 Mgaya said students from within the region meet and compete in various sports and exchange views on various educational and social issues.
 
Through these games, students socialise, make friends and integrate, he said, noting that the competing teams will be accommodated at Mabibo Hostel.
 Sports disciplines to be competed at the event are soccer, netball, basketball, volleyball, track and field events, swimming, chess, rugby, hockey and handball.

Sakata la gesi Mtwara, Baba wa Taifa akumbukwa


SAKATA  la wakazi wa Mkoa wa Mtwara kupinga rasilimali ya gesi ghafi asilia inayovunwa katika kijiji cha Msimbati mkoani humo kupelekwa Dar es Salaam kwa njia ya bomba limepamba moto huku viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), wakitumia hotuba na nukuu za kauli za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuhamasisha wananchi kumuenzi mwasisi huyo wa taifa kwa kuupinga mradi huo.
Katika mkutano mkubwa uliofanyika jana Mtaa wa Sinani mjini hapa viongozi wa CUFWilaya ya Mtwara Mjini, walikuja na mbinu mpya ya kuhamsisha wananchi kuendelea na msimamo huo kwa  kutoa hotuba za nukuu  ya kauli za Baba wa Taifa kuhusu mustakabali wa hali ya maisha ya wananchi katika mazingira ya wachache kuwakandamiza wengi.
Saidi Kulaga, Katibu wa CUF Wilaya ya Mtwara mjini alisema kinachotokea leo kwa wakazi wa mikoa ya Kusini ni kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye kwa nyakati tofauti alinukuliwa akionya viongozi kuandamiza wengi.
Katibu huyo akisoma karatasi ya nukuu hizo kutoka katika kitabu cha ‘Reflection on Leadership in Africa’ kilichopigwa chapa na VUB University Press, 2000 alisema  mwasisi huyo wa Taifa katika kitabu hicho amenukuliwa akisema
Habari  zaidi   http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1663260/-/11r24q6/-/index.html

Kibonzo


Depression in Children: A silent killer.

According to the Diagnostic Statistical Manual for Mental Health, an online medical journal, depression is a mood disorder characterised by either sadness or loss of interest in pleasurable activities accompanied by at least four additional symptoms drawn from a list which may include changes in appetite or weight, or in sleep and psychomotor activity, decreased energy, feelings of worthlessness or guilt, difficulty in thinking, concentrating or making decisions, recurrent thoughts of death or suicidal ideation/ plans/ attempts.
   In children and adolescents, one’s mood may seem more irritable or cranky as opposed to being sad or of a depressed nature. The child may also feel that life is hopeless, could be discouraged or “down in the dumps”.
In noting the causes of depression, the journal indicates that children are faced by different psychosocial stressors within the environment. However, from a bio psychosocial perspective, these psychosocial stressors could be biological, psychological and social.
It states: “Every child has the resources necessary to deal with these stressors. A breakdown in these resources, say failure for one to cope adequately, results into depression or depressive symptoms. Stressors include death of a parent, divorce, poor grades, and bullying, low self-esteem, among others.
Read  more : http://www.monitor.co.ug/Magazines/Health---Living/Depression-in-Children--A-silent-killer/-/689846/1661780/-/12xq2h3z/-/index.html
© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top