Social Icons

Loading...

New Year Resolutions.

A year passed by, the world enters another year. It is a universal trend for people of all ages to start a new year with resolutions.

      The first day of the year will witness many new diaries purchased to start penning their plans. Resolutions vary amongst masses, getting better with savings, getting  married, getting or  adding more baby owning a  house,  quitting smoking, improving health, looking for better job, new car et al are some familiar resolutions that we often know individuals commit to. 
        Many go about speaking about the resolutions to everybody while others keep such commitment to themselves and review them at the conclusion of the year. Resolutions and New Year definitely arrive with hope and aptitude.
 Happy  new  year.
Management.
Net Media Group .

Mbowe:Ni Dk Slaa 2015.

CHAMA  cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kuwa Katibu Mkuu wake, Dk Willbrod Slaa atapewa fursa ya kuwania nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, mwaka 2015.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza hatua hiyo jana, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mpira, mjini Karatu mkoani Arusha, huku yeye akijiweka kando kuwania nafasi hiyo.Hata hivyo, Dk Slaa mwenyewe alipoulizwa iwapo ana nia ya kugombea urais mwaka 2015, alisema: “Kwani mwaka 2010 nilijitangaza mwenyewe?, Iwapo wanachama wa Chadema watanipendekeza, nitafikiria kufanya hivyo.”
   Katika maelezo yake Mbowe alisema: “Kama Mwenyezi Mungu atampa uhai na afya njema hadi mwaka 2015, Dk Slaa anatosha na Chadema, tutampa fursa nyingine ya kupeperusha bendera ya chama kwenye nafasi ya urais.”
         Huku akishangiliwa na umati wa wana chama wa Chadema Mbowe aliongeza: “Ninataka wanaotumia ugombea Urais kama kete ya kuleta mtafaruku ndani ya Chadema watambue hivyo.”
Alibainisha kuwa, binafsi hana nia ya kuwania urais na badala yake atatumia nguvu, uwezo na kila kilicho ndani ya uwezo wake, kukijenga Chadema ili kushinde uchaguzi na kushika dola.
Mbowe alisema kwa muda mrefu kumekuwapo mbinu na jitihada za kumgombanisha yeye na Dk Slaa kuhusu nafasi ya urais na kutamba kwamba njama hizo kamwe hazitafanikiwa.
Mwenyekiti huyo wa Chadema alitumia pia mkutano huo kutangaza kumalizika kwa mgogoro uliokuwapo kati ya viongozi wa chama hicho wilayani Karatu.
Hata hivyo, awali katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Mbowe alisema: “ Kikao cha CC (Kamati Kuu), kitakachofanyika Januari mwakani ndicho kitakachoweka utaratibu rasmi wa watu wanaotaka kuwania kiti cha udiwani, ubunge na urais mwaka 2015 na kutangaza nia zao na vigezo vya uteuzi.”
Alisema chama hicho kinakusudia kuwapa nafasi wenye nia kujitokeza mapema, ili kutoa fursa ya kuwaelewa, kuwaandaa, kuwapa mafunzo, kuwaeleza majukumu na wajibu wao, kuwaeleza sera, misimamo na malengo ya chama hicho.Mbowe alisema kuwa mpango huo utakihakikishia Chadema wagombea wenye uwezo na uhakika wa kushinda mwaka 2015.
“Nia ya mpango huu ni kuepuka watu wanaodandia kuomba uteuzi wa kugombea dakika za mwisho,” alisema Mbowe.Aliweka wazi kuwa chama hicho kitakuwa makini katika uteuzi wa nafasi ya urais kwa sababu ni nafasi nyeti, isiyohitaji kujaribu wala mzaha.
Alisema kwamba chama hicho hakitasubiri wala kupokea waliokosa fursa za uteuzi katika vyama vingine, kikiwemo Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao wanaokimbilia Chadema dakika za mwisho akisema kuwa uzoefu umeonyesha wengi wao wanaendelea kuwa mamluki.
Chanzo :  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/-/1597332/1654154/-/bpbv9xz/-/index.html

Dar switches over to digital broadcasting.

Dar es Salaam. At midnight today analogue television broadcasting will be switched off to pave the way for digital terrestrial broadcasting in line with the December 31, deadline agreed to by the East Africa Community Partner States.This is way ahead of the June 17, 2015 deadline set by the International Telecommunications Union (ITU), as per Geneva 2006 agreement.
   The country was the last in the region to adopt public TV broadcasting in 1994 - with the exception of Zanzibar that established a public television in 1973. But now, it has become the first to achieve the switch over from analogue to digital broadcasting in East Africa.Uganda and Kenya had earlier planned a phase by phase switchover from midnight today, starting with Kampala and Nairobi, but lack of preparation and disputes would definitely not make that possible.
      A Kenyan court has ordered the Communications Commission of Kenya (CCK) and the Information and Communication ministry to delay migration until January 11 when the Court would deliver a ruling on a case filed by a consumer lobby. The countrywide migration was earlier this year pushed to March 2013 after the countryís General Election.
The Uganda Communications Commission wanted to start progressive switchover from analogue to digital broadcasting at midnight on December 31 in Kampala and its suburbs. The transmission would have been dual illumination also called simulcast, meaning the two systems would have run parallel to each other until 2015.But, according to reports, the deadline has been silently postponed to July 17, 2015 ñ the global deadline.
Burundi has set June 17, 2015 as the deadline for migration while in Rwanda, the minister of Youth and ICT, Jean Philbert Nsengimana, announced in September that Kigaliís final switch to digital transmission was yet to be decided.
The Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) says everything is in place for the switchover at midnight.Three companies were licensed to provide digital terrestrial television (DTT) ëmultiplexing, signal distribution and transmission services.í These include Agape Associates Limited, Star Media Tanzania Limited, and Basic Transmissions Limited.
Agape, owned by a religious organisation, broadcasts through the TING brand, which sells decoders to viewers. Star Media, a private-public venture, uses Star Times brand.
Basic Transmission hasnít yet started operations.
   The Public Relations manager of TCRA, Mr Innocent Mungy, says the digital migration will be effected at midnight in all seven major urban centres where analogue broadcasting was officially available. These include Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya and Dodoma.
Communications, Science and Technology minister Makame Mbarawa said at a recent conference that early migration is better than a late one.
Switching to digital broadcasting three years before the International Telecommunication Union deadline in 2015, helps us to equip with technical skills and experience ready to face any challenge arising, as we head to the deadline,î said Prof Mbarawa.
 According to the TCRA, implementation of the digital migration roadmap started on June 15, 2006. The past six years have been a ësimulcast periodí where both analogue and digital transmission were being carried out.Prof Mbarawa told a news conference yesterday in Dar es Salaam that the complete switch-over will be effected step by step, starting with Dar es Salaam City today midnight, followed by Dodoma and Tanga on January 31, 2013; Mwanza February 28; Moshi and Arusha March 31 and Mbeya April 30.
Prof John Nkoma, director general of TCRA cautioned, ìLet Tanzanians not think that we will push forward the deadline as we did for the mobile phone number registration.
    The main benefits television viewers will get in digital broadcasting include better sound and picture quality.
Also, the country will experience efficient use of spectrum through multichannel functionalities.
ìDigital transmitter equipment are energy efficient, hence consumption of energy is low unlike the analogue transmitter,î Mr Mungy said.Mr Mungy told The Citizen in an interview last week that a minimum of 400 channels would be available for broadcasting.This is a huge opportunity for content producers and entrepreneurs who would wish to invest in TV broadcastingí and is a very big employment potential.
He said the country in the long run was expected to witness the rise of specialised channels and TV programmes like those specialising in business promotion, advertisement, nature and environment, science and technology, agriculture and others.According to Mr Mungy, Tanzania has a total of six million TV sets out of which only 2.6 million subscribers were expected to migrate.Commenting on the digital switchover, an independent business and finance consultant, Dr Donald Olomi, said that the technology was expected to bring more competition in the broadcasting and ICT business arena.

Vigogo EPL vyauaga mwaka 2012 kwa kugawa DOZI.

 Man  City  Vs  Norwich


Man U    2   West Bromwich  Albion  0

Arsenal   7   New  Castle 3


Chelsea  2   Eveton  1

Liverpool    3  QPR  0
 


Christmas & 2013 Greatings!!!!

  On  behalf  of   NET MEDIA Group   I  wish  you   Joyous Holiday   and  Happy  New  Year. Please  continue  visit  our online  web  portal   next year   and more year  to come, you  encouraged   us much   this  year  and   we  promise  you  to  keep  on moving  forward  to  serve  you  better and  improving our services.
MERRY CHRISTMAS &  HAPPY NEW  YEAR.
 Best  Regards,
Daniel  Alex.
Technical  Director.
NET  MEDIA.


 

LEMA kulamba mil 85, Bungeni.

MBUNGE wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema, huenda akazoa kitita cha Sh85 milioni ambazo ni malimbikizo ya mishahara na posho mbalimbali ambazo hakulipwa wakati alipokuwa nje ya Bunge.
Lema amekuwa nje ya Bunge kwa miezi minane, kuanzia Aprili 5 mwaka huu wakati alipovuliwa ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, hadi aliporejeshewa ubunge wake Ijumaa wiki iliyopita na Mahakama ya Rufani ambayo ilikubali rufaa yake iliyopinga uamuzi huo.Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah jana alisema baada ya kurejea bungeni, Lema atalipwa stahili zake zote anazostahili kwa muda wote wa siku 260 ambao alikwa nje ya Bunge.Ingawa ofisi hiyo ya bunge haikusema atalipwa shilingi ngapi, uchambuzi wa malipo na stahili za wabunge umebaini kuwa mbunge huyo kupitia Chadema, atalipwa kitita cha Sh85 milioni ikiwa ni mshahara wake na posho kwa kipindi cha miezi nane alichokuwa nje ya Bunge.
Hata hivyo, Lema mwenyewe aliliambia gazeti hili jana kuwa, malipo yake yanaweza kufikia Sh60 milioni.
Lema aliyeibuka mshindi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, alivuliwa wadhifa huo na Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, April 5, 2012, kufuatia kesi iliyofunguliwa na makanda watatu wa CCM; Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agness Mollel, wakipinga ushindi wake.  Hata hivyo, Desemba 21,2012, Mahakama ya Rufani ilimrejesha bungeni, baada ya kushinda rufaa yake aliyokata mahakamani hapo kupinga hukumu na tuzo ya Mahakama Kuu Arusha iliyomvua wadhifa huo.
Tangu alipovuliwa ubunge hadi Mahakama ya Rufani ilipomrejesha tena bungeni, Lema alikuwa amekosa mikutano mitatu ya Bunge yenye jumla ya vikao 84.
Mikutano hiyo ni ule wa mwezi Aprili, mkutano wa Bunge la Bajeti Juni hadi Agosti na mkutano wa Novemba.
Vyanzo vya kuaminika kutoka ndani ya Bunge na wakiwamo wabunge wa upinzani na wale wa CCM vilisema kwamba malipo ya mbunge kwa mwezi ni Sh10.7 milioni, yakijumuisha Sh2.3 milioni za mshahara, Sh2.5 milioni za mafuta, posho ya jimbo inayokaribia Sh5 milioni na malipo mengineyo.
Kwa muda wa miezi zaidi ya minane ambao amekuwa nje ya Bunge, malimbikizo ya mshahara wake yanafikia Sh18.4 milioni, posho ya jimbo Sh40 milioni, mafuta Sh20 milioni na posho nyingine Sh6.6 milioni.
Kauli ya Lema
Hata hivyo akizungumza na Mwananchi jana, Lema alisema kuwa ingawa hajui kwa hakika kuwa malipo yake ni kiasi gani, lakini kwa hesabu za haraka, yanafikia Sh60 milioni.
Alisema wakati wa kesi hiyo ikiendelea hakuwahi kuwaza kwamba angerejeshwa bungeni, hivyo hakuwahi atalipwa kiasi gani na Bunge.
“Sijui kwanza nitalipwa nini kwani sikuwahi kukaa na kupiga hesabu za malipo haya, maana  najua ubunge  siyo faraja bali ni kuongoza harakati  za kuwasaidia wananchi kutetea haki zao mbalimbali,” alisema Lema.
Alisema alichokuwa akijua ni kwamba  kama akishinda basi, atarejeshewa gharama za kesi yake na makada wa CCM ambao walimfungulia kesi kwani ni malipo yanayotambulika kisheria.
“Najua lazima hawa makada wa CCM, walipe gharama zangu za kesi.Baada ya wao kushinda kesi Mahakama Kuu, Arusha, waliniletea madai ya kuwalipa Sh139 milioni na sasa mimi nawadai zaidi ya milioni 250,” alisema Lema na kuongeza:
Chanzo :    http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/-/1597332/1650844/-/bpei3bz/-/index.html

Man U yabanwa mbavu na Swansea, Chelsea yaua 8 - 0 Aston Villa

  Chelsea  8   Aston Villa  0

STARS Yaiadhibu CHIPOLOPOLO 1- 0


Timu  ya  Taifa   ya  Tanzania   maarufu  kama Taifa Stars imeifunga timu  ya  taifa  la  Zambia  ambayo  ni  mabingwa  wa  Afrika  kwa  bao 1-0 katika  mchezo  wa  kirafiki ,  goli  hilo  pekee  lililopatikana dakika ya 45 ya mchezo. Bao hilo limefungwa na Mrisho Ngassa, kwa shuti la mbali akimalizia pasi ya  kiungo mchezeshaji  Mwinyi Kazimoto.

Vikosi  : 
Stars-Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Kelvin Nyondani,Frank Domayo,Amir Kiemba,Salum Abubakar,Mrisho Ngassa,Mwinyi Kazimoto, Hamis Mcha/Simon Msuva. 

Zambia- Danny Munyao, Chintui Kapamba,Hichani Himonde,Chisamba Lungu,Jame Chamanga/Shadrack
Malambo,Christopher Katondo/Stoppila Sunzu,Felix Katongo,Nathan Sinkala/Evans Kangwa,Roderick Kabwe/Francis Kasonde na Issac Chansa.


Pata  picha   zaidi    katika  pambano  hilo:





 

Real Madrid yazodolewa 3 -2 na Malaga - LALIGA

Barcelona  yaitwanga   Villadolid   3 -  1

Majina 16 vigogo wa TPA walipigwa stop na Dr Mwakyembe.



Idadi hiyo inafanya waliosimamishwa kazi katika bandari hiyo hadi sasa kufikia 23.Dk Mwakyembe alisema vigogo hao wamesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbalimbali.“ Bodi imewasimamisha kazi kutokana na tuhuma mbalimbali za wizi na migongano ya kimaslahi, hawa wamesimamishwa baada ya bodi kuichambua ripoti ya uchunguzi iliyotolewa na tume niliyoiunda,” alisema.Waliosimamishwa kazi na nyadhifa zao kwenye mabano ni Bakari Kilo (Mkurugenzi Uhandisi), Raymond Swai (Meneja Uhandisi), Frolence Nkya (Mkurugenzi wa Mipango) na Mahebe Machibya (Meneja Ununuzi na Ugavi).

Wengine ni Teophil Kimaro (Meneja Ununuzi), Mary Mhayaya (Afisa Uhandisi Mkuu), Ayoub Kamti (Mkurugenzi wa Tehama), Mathew Antony (Meneja Kitengo cha Kontena) Maimuna Mrisho (Mkurugenzi wa Mifumo wa Menejimenti).Wengine ni Fortunatus Sandalia (Askari kitengo cha Ulinzi), Fadhili Ngolongo (Kitengo cha Marine), Mathew Antony (Meneja Kontena), Mohamed  Abdullah (Kitengo cha Mafuta), Kilimba (Idara ya ulinzi) na Owen Rwebu.

Mwakyembe alisema katika ripoti ya uchunguzi imegundulika kwamba baadhi ya vigogo wa Bandari wanamiliki kampuni ambazo zinafanya kazi za TPA.

“Tumebaini kuwa kuna mgongano mkubwa wa kimaslahi ndani ya bandari, kuna wafanyakazi wengine wana kampuni za mkononi ambazo hazijasajiliwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) lakini zimepewa kazi za TPA,” alisema.Alisema kampuni hizo zinapomaliza muda wa mikataba yao huongezewa muda wa mikataba mingine.
Dk Mwakyembe alisema kuna mtandao mkubwa unaofanywa kwa watu mbalimbali kwa kushirikiana na vigogo wa bandari ili kufanikisha wizi katika bandari.“Kontena zinayeyuka, zinaibwa kama Twiga walivyopandishwa kwenye ndege, ninaapa mtandao huu nitaumaliza hapa bandarini,” alisema Mwakyembe huku akishangiliwa na wafanyakazi.
Aidha Mwakyembe amepiga marufuku utaratibu wa kuingia bandarini na kulipia kiingilio cha Sh200 unaojulikana kama potipasi.

UEFA DRAW


BREAKING NEWS!! Godbless Lema ashinda kesi

Godbless Lema ashinda kesi yake ya rufaa na kurudishiwa Hadhi yake ya Ubunge - Jimbo la Arusha Mjini, Wanachama wa CCM waliomfungulia mashtaka waamriwa kulipa gharama zote za kesi toka ilipoanza.


 

Hii KALI... TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA!!


Nelson Mandela Recovers, Yet Under Medical Supervision .

The 94-year-old former president of South Africa is hospitalized after undergoing surgeries to remove gall stones.He was admitted to a Pretoria hospital on December 8 after he suffered lung infection. The trouble started in 1988 when he suffered tuberculosis. He recovered from the disease then but the doctors said he shall suffer from lung problems in future too.
After dealing with his lung infection, Mandela underwent endoscopy to remove his gall stones followed by a terrible pain. The surgery was successful and he is now recovering gradually. However, the doctors said that he still needs to be at hospital.
"They occur when fluid collects in your gall and crystallizes. The stones can cause discomfort", explained Mark Sonderup, the Vice-Chairman of the South African Medical Association.
He is receiving treatment at the facility with a regular medical supervision and routine checkups. The doctors are saying that he shall recover soon and shall be fit; however they have not yet confirmed about when he shall be discharged.Nelson Mandela was the first democratically elected President of South Africa and led the nation from 1994 to 1999. In 2001, he was diagnosed with prostate cancer. He was 83 at that time and recovered successfully from the deadly disease after being treated by radiotherapy.
Source: http://topnews.us/content/252273-nelson-mandela-recovers-yet-under-medical-supervision

Waziri atia kufuli hoteli ya kitalii Dar.

Dk Terezya Huvisa
WAZIRI wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Terezya Huvisa, ameifunga Hoteli ya Kimataifa ya Double Tree, ya jijini Dar es Salaam, kutokana na kitendo cha kutiririsha maji machafu baharini.
Dk Huvisa alifanya hivyo jana baada ya ziara ya kushtukiza akiwa na Naibu wake, Charles Kitwanga.
Waziri alitembelea hoteli hiyo ili kuona utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Kitwanga mapema mwezi huu, alipofanya ziara katika viwanda na hoteli zilizoko pembezoni mwa bahari, ili kuona mfumo wa majitaka.

“Nawataka kurekebisha mara moja mfumo huo wa majina kulipa faini kwa Baraza la Hifadhi na Uhifadhi wa Mazingira (Nemc),”alisema Dk Huvisa.
Dk Huvisa alifika hatua hiyo baada ya kujiridhisha kuwa agizo lililotolewa na naibu wake wiki mbili zilizopita, halijafanyiwa kazi.
Alisema hoteli hiyo itafungwa hadi hapo itakapotekeleza agizo hilo na kuhakikisha kuwa majitaka hayatiririki baharini kama ilivyo sasa.
Chanzo :   http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1648058/-/11pwgxt/-/index.html

Chelsea Yaichapa Leeds United 5 - 1 , Yatinga Nusu fainali Capital One Cup .


KIBONZO


Shule zetu na Kilimo cha Jembe la mkono.


Magufuli apeleka bomoabomoa Morocco.

WAZIRI wa Ujenzi, Dk John Magufuli ameitaka Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), kuanza kuvunja nyumba zilizopo ndani ya hifadhi ya Barabara ya Mwenge hadi Morocco, Dar es Salaam ili kupisha ujenzi wa barabara nne za lami.Pia, ameitaka Tanroads kuacha kigugumizi katika ujenzi wa barabara za juu jijini Dar es Salaam (flyovers) kwa kuwa fedha kwa ajili ya kazi hiyo zipo.Waziri Magufuli alitoa wito huo Dar es Salaam jana, alipokuwa akizindua bodi mpya ya Mfuko wa Barabara na Bodi ya Tanroads.
“Barabara ya Mwenge- Morocco nyumba zinatakiwa kubomolewa. Zibomolewe haraka ili kupisha ujenzi. Nasema Tanroads acheni kigugumizi kwenye masuala haya,” alisisitiza Dk Magufuli.
Ingawa hakuzianisha nyumba zilizotakiwa kubomolewa katika barabara hiyo, sehemu kubwa ina nyumba za thamani kubwa hasa ghorofa jambo ambalo linatarajiwa kuwaweka katika wakati mgumu wamiliki wake.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanroads, Patrick Mfugale alisema: “Nyumba zitakazobomolewa siyo nyingi. Ni zile zilizojengwa ndani ya mita 30 ya hifadhi ya barabara. Kinachotuchelewesha ni kuondolewa kwa nyaya za umeme pamoja na mfumo mkubwa wa maji ili tuweze kuanza ujenzi.”

Waziri Magufuli alisema fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo zipo na hata za kuwalipa wamiliki wa nyumba hizo zipo, hivyo akasisitiza kuwa kazi ya kuzibomoa inapaswa kuanza mara moja.

“Wanaostahili kulipwa fidia walipwe na ambao hawastahili waondoke. Suala la kwamba mko kwenye mchakato life na libaki kuwa neno la wanasiasa tu,” alisema Magufuli.

Bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2012/13, imeonyesha kuwa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 4.3, ujenzi wake unafadhiliwa na Serikali ya Japan.
Kuhusu ujenzi wa barabara za juu, Waziri Magufuli alisema ni jambo linalowezekana na halihitaji kufanyiwa mchakato wowote.

Alisema ni muhimu bodi hiyo mpya ikasimamia ujenzi wa barabara hizo ili kupunguza msongamano wa magari Dar es Salaam.“Tengenezeni ‘flyovers’ nyingi nyingi, ni kazi ndogo lakini inashangaza kwa nini Tanroads inakuwa na kigugumizi,” alisema Magufuli na kuongeza:
“Wahandisi wa Tanroads fanyeni hivyo, mbona kule Kenya mambo yamefanyika bila tatizo? Acheni kigugumizi na siasa mfanye kazi.”

Magari ya Serikali
Waziri Magufuli pia alizungumzia mchakato wa kukamata magari ya Serikali yanayotumika vibaya na kuzitaja Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) kuwa vinara wa tatizo hilo.
Dk Magufuli alisema tangu kuanza kwa operesheni hiyo, magari 974 yalikamatwa baada ya watumishi wake kuyageuza kuwa ya kiraia kwa kubandika namba binafsi.

Alisema pamoja na kukamata kiasi hicho, bado kuna magari 746 ya Serikali ambayo hayajasajiliwa na mengi yako Wizara ya Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia pamoja na Tamisemi.
Chanzo :   Mwananchi

Messi azidi kuudhihirishia ulimwengu, afunga goli 2 , huku Barca ikiichapa Atletico Madrid 4 -1

Barcelona   4   Atletico     Madrid   1


Waziri matatani.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (pichani) anadaiwa kumiliki kampuni inayojishughulisha na masuala ya utalii kitendo ambacho kinamwingiza kwenye mgongano wa kimasilahi.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Nyalandu anamiliki Kampuni ya Nitoke Safaris Ltd jambo ambalo limeelezwa kuwa ni kinyume na Kanuni za Utumishi wa Umma hasa kwa kuwa yeye msimamizi wa sekta hiyo.Taarifa kutoka kwa Wakala wa Usajili wa Kampuni na Leseni (Brela), zinaonyesha kuwa wamiliki wa Kampuni hiyo ni L.S.Nyalandu na Faraja G. Nyalandu, huku kila mmoja akimiliki asilimia 30 ya hisa.Kampuni hiyo ilisajiliwa Aprili 24, 2009 na kupewa nambari 70735, wakati huo Nyalandu akiwa Mbunge wa Singida Kaskazini, wadhifa alioupata kuanzia mwaka 2000.
Ofisi za kampuni hiyo ziko PPF Complex Suit, namba 24 Barabara ya Mzingo, Arusha na magari ya kampuni hiyo yamekuwa yakibeba watalii mkoani Arusha.
      Alipoulizwa kuhusu madai hayo jana akiwa Mwanza, Waziri Nyalandu alikiri kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo lakini akasema tayari alishajitoa.
Katika kujenga hoja ya utetezi wake, Nyalandu alisema kama ambavyo haipendezi yeye kumiliki kampuni ya utalii akiwa waziri wa wizara hiyo, haitapendeza pia waziri wa habari kumiliki gazeti.
Chanzo  :  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1644980/-/11ptvso/-/index.html

Utafiti wamtaja mshindi wa kiti cha urais Kenya.

BADO miezi michache kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Kenya tayari mashirika mbalimbali ya utafiti yameshaanza kubashiri  washindi wa uchaguzi huo utakaofanyika mwezi  Machi mwakani watakuwa kina nani.Ni Kawaida kwa  mashirika ya utafiti ulimwenguni kote  kufanya utafiti hususan kipindi cha karibia na uchaguzi wa nchi husika.
Nchini Kenya Utafiti  uliofanywa na Kampuni ya Synovate  umebaini kwamba muungano wa Coalition for Reform and Democracy (CORD) unaoshirikisha vyama vya ODM, Wiper Democratic Movement na Ford – Kenya ungeibuka na ushindi endapo uchaguzi mkuu ungefanyika mwezi huu wa Desemba.
Hata hivyo, kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo uliofanywa kati ya tarehe 6 na 11, ushindi huo haungetambulika kikatiba kwani mgombea urais wa CORD angepata asilimia 47 dhidi ya asilimia 41 ya washindani wakuu, Muungano wa Jubilee. Hii ni endapo Waziri Mkuu Raila Odinga na Naibu wake Uhuru Kenyatta watatawazwa wagombea urais wa miungano hii huku Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka na Mbunge wa Eldoret Kaskazini William Ruto wakiwa wagombeaji wenza.
Hata hivyo, utafiti huo, uliofanywa na kudhaminiwa na Kampuni ya Ipsos Synovate, CORD ilipata asilimia 48 dhidi ya asilimia 38 ya Jubilee  iwapo Naibu Waziri Mkuu Musalia Mudavadi atateuliwa kupeperusha bendera ya muungano huo. Watu 1,625 wenye umri wa miaka 18 na zaidi walihojiwa kwa njia ya simu ya mkononi.
Mtafiti Mkuu wa kampuni hiyo Dk Tom Wolf, hata hivyo alisema kuwa bado kuna maswala mengi ambayo yanaweza kubadili matokeo hayo, ikizingatiwa kuwa miungano hiyo na vyama tanzu vina muda wa hadi Februari 11, 2013 kabla ya kuwasilisha orodha kamili ya watakaogombea nyadhifa mbali mbali kwenye uchaguzi mkuu ujao.
    Vilevile, uteuzi wa mgombea urais wa muungano wa Jubilee, unaoshirikisha vyama vya TNA, URP na UDF Jumanne ijayo, na makubaliano ya mwisho kuhusu suala hilo katika CORD jana alisema, huenda yakabadili mambo.“Matokeo hayo yanaweza kubadilika baada ya miungano mikuu kufanya teuzi zao za wagombea urais na pale teuzi za wagombezi wa nyadhifa nyingine zitakapokamilika kabla ya Februari 11 mwaka ujao, “ akaeleza Dk Wolf.
      Kumekuwa na hali ya vuta nikuvute katika muungano huo kuhusu mbinu na utaratibu wa kumteua mgombea urais kati ya Uhuru Kenyatta na Musalia Mudavadi.  Wafuasi wa Uhuru wanapendelea mfumo wa wajumbe huku wenzao wa UDF wakionekana kuegemea ule mfumo wa mwafaka.
Kulingana na umaarufu wa wawaniaji urais kibinafsi, Raila anaongoza kwa umaarufu wa asilimia 34 huku akifutwa na Uhuru kwa asilimia 27, ishara kwamba umaarufu wao umepanda kwa alama moja tangu mwezi uliopita.Hata hivyo, kutokana na dhana iliyokolea wengi kwamba Makamu wa Rais na kiongozi wa URP, William Ruto watakuwa wagombezi wenza, umaarufu wao ulishuka kwa asilimia 5 na 7 huku ule wa Mudavadi ukishuka kwa asilimia 1.  Kalonzo ana asilimia 3 kutoka 8 alioandikisha mwezi wa Novemba. Naye Ruto akiwa na umaarufu wa asilimia 2 kutoka 9 mwezi uliopita.
Chanzo   : http://www.mwananchi.co.tz/habari/afrika-mashariki/-/1597272/1645034/-/euf695/-/index.html

Chemsha Bongo, Je unakubali ukokotozi huu???


Add value to local products, JK tells manufacturers.

President Jakaya Kikwete on Thursday night urged manufacturers in the country to add value to local products to obtain international accreditation and enhance the country’s position in the world market.
He made the remark at the President’s Manufacturer of the Year Award (PMYA) ceremony at Serena Hotel in Dar es Salaam, to recognize best local manufacturers of the year 2012 from 17 selected sub-sectors, who were presented with certificates and trophies at an occasion organized by the Confederation of Tanzania Industries (CTI).
 Tanzania Distilleries Limited emerged the overall winner, while Prestige industries Ltd took the prize for small industries, DPI Simba Ltd for medium industries and Kioo Limited for large industries.
Fully sponsored by IPP Limited, it was the eighth annual event since 2005, aiming at recognizing and appreciating the manufacturing sector’s role in the development process.
In appreciation, the organizers awarded the IPP Limited executive chairman Dr. Reginald Mengi with an appreciation plaque for the sponsorship of the event. After the President’s speech, he said in his vote of thanks that the sector will strive to its best to perform.

The industrial sector, with strong backward and forward linkages, has the capacity to generate high value addition, wealth creation and employment opportunities, vital for economic growth and poverty reduction, he stated.The ceremony also enabled stakeholders to share experiences on matters affecting the industrial sector, where the president threw the challenge to manufacturers following an appeal by CTI chairman Felix Mosha. He had requested the government to seek ways in which the local manufacturing sector can be enabled to improve industrial products to higher standards.
In reply, the President reaffirmed that the government depends on local innovation and creativity in order to achieve utmost standards in manufacturing processes, despite challenges facing industrialists, including erratic power supply.
        The president assured the gathering that erratic power flow would come to an end when gas delivery by pipeline starts.He noted government recognition of the role of industries. Manufacturers provide the largest revenue contribution to the Treasury, he stated, qualifying the sector as the engine of economic development.
“The country depends entirely on decisions of members of this confederation,” the President underlined, suggesting a strategic plan for a certain period to work through to achieve specified targets.
He reminded the audience that trade competition was unavoidable, so what is needed at this juncture is to cope with emerging trends in technology to ward off obstacles to expanding market share.
         Adding value on products enables the country to become a leading producer of quality products, he said, raising the possibility of a roadmap on how to go about it.
With that spirit the country would change industrially in ten years to come, he said.
The government is working on basic infrastructure such as railway for transport, and on the availability of water, to facilitate opening of industries in many other places.
Ensuring adequate electricity supply has been a problem for years as traditionally power generation has depended on hydropower sources, he added.

Chagua Maisha Unayotaka Kuyaishi Na Uyaishi Kweli.

Na   Meshaki   Maganga  toka  IRINGA:
Wiki ya jana imekuwa wiki ya kazi nyingi na pilika za hapa na pale. Wiki hii nimebahatika kukutana na rafiki zangu ambao kwa muda mrefu tumekuwa tukiwasiliana kupitia mitandao ya kijamii na blog bila kuonana, kuna mmoja ambae aliamua kufunga safari kutoka Dar es slaam  mpaka Iringa kuja kujifunza uwekazaji kwenye mashamba ya miti na mboga mboga. Na ameamua kuwekeza kwa kununua ekari kumi za kupanda miti. Wiki hii nimejifunza kwamba, kila mtu ana uwezo wa kuchagua kufanya  yale ayatakayo  maishani, Dunia ina mengi ya kuyafanya na kuna kila nafasi kwa mwanadamu yeyote anayechagua kuwa anavyotaka maishani. Chagua maisha unayotaka kuyaishi na uyaishi kweli. 
Usiogope kujaribu kitu, maisha ya kuogopa kufanya kitu ni maisha yasiyo na maana. Usikubali maisha ya ‘ukawaida’ na ambayo yatakufanya usiishi maisha makubwa unayostahili.
Siri kubwa ya watu wenye mafanikio duniani, ni kuwa hawaogopi maisha, wapo tayari kuumia kwa kuchagua maisha wayatakayo.  Chagua kipengele mojawapo cha kijasiriamali  unachotaka kukifanya na ukifanye kweli kwa moyo wote. Jiendeleze kila siku katika ulilochagua kiasi ambacho utavunja mipaka na kuweka rekodi yako. Chagua kufanikiwa.
Wewe kama binadamu na sisi wengine wote, tuna mawazo ya aina moja tu hatuna aina zaidi ya moja. Lakini haya mawazo yetu yana sifa au tabia kuu mbili. Sifa hizi mbili zinatofautiana kabisa kana kwamba hazihusu kitu hichohicho.
Sifa hizi zimepewa majina mbalimbali tangu kufanyika kwa ugunduzi wake miaka maelfu iliyopita. Majina kama mawazo ya kawaida nay a kina, mawazo yaliyo machona yaliyolala, mawazo ya nje na ndani, mawazo yenye utashi na yasiyo na utashi, mawazo ya kike nay a kiume, mawazo razini na yasio –razini na majina mengine.Lakini katika makala hii   nitatumia maneno istilahi hizi- ‘mawazo ya kawaida na mawazo ya kina’ katika kuzungumzia jambo hili.
Ili tuweze kuelewa vizuri kuhusu tofauti ya sifa hizi mbili za mawazo yetu ni vizuri nitatoa  mfano hapa:- Tuchukulie mawazo yako kama bustani ni kile unachokifikiria  (fikra) kama mbegu ambazo unazipanda kwenye bustani hiyo. Kwenye mawazo yako ya kina, ndipo mahali ambapo mbegu hizo zinapopandwa, yaani zitakapoota. Baadae mbegu (fikra) hazaliwa kwenye miili na mazingira yanayotuzunguka.
Tunapofikiria jambo lolote. Fikira hizo huwa ziko kwenye mawazo yetu ya kawaida. Baada ya kuamini juu ya kile tunachokifikiri, ndipo ambapo fikira hizo huhifadhiwa kwenye mawazo yetu ya kina.
Wakati mwingine napengine mara nyingi huwa hatuna habari kwamba kile tunachokiamini kimehifadhiwa kwenye mawazo ya kina. Lakini kuhifadhiwa huku ni tofauti na kuhifadhiwa kwa maana ya kawaida tunayoijua. Mawazo ya kina yanapohifadhi fikira zetu huwa yanazifanyia kazi kwa kadiri zilivyokuja. Kama ambavyo tumeona kwenye mifano yetu ya awali kabisa ya mada hii, ni kile ambacho kinaombwa na mawazo  ya kawaida.
Tunaposema kile ambacho kinaombwa na mawazo  ya kawaida, tuna maana ya imani zetu, kile au yale yote tunayoyaamini. Kanuni ya ufanyaji kazi wa mawazo yetu ya kina ni imani zetu. Hakuna mtu anayeweza kuvunja kanuni hii kwani ni ya kimaumbile. Kwa hiyo, tunachokatikwa kukifahamu ni maana ya imani, kwa nini inafanya kazi na kwa namna gani.
Uzoefu wetu maishani, matukio, hali zetu za hisia na matendo yetu, vyote ni majibu ya mawazo yetu ya kina kwa mawazo yetu ya kawaida. Siyo kweli kwamba ni kile kitu au jambo tunaloliamini ndilo lene kupelekea matokeo Fulani kwenye maisha yetu, bali imani yetu kuhusu kitu au jambo hilo. Unapoamini katika ushirikina au hofu,  matokeo yake yatakuwa ni kulogwa, kuugua, hofu na kukata tamaa, lakini chenye kupelekea  hali hizo siyo ushirikina au hofu, bali inini yako kwenye hofu.
Mawazo yetu ya kina yakilishwa imani nzuri, yaani vitu au mambo mazuri, nayo hujibu vitu au mambo mazuri na yakilishwa imani mbaya nayo huzaa vitu au mambo mabaya. Mawazo haya huwa hayajui kuchuja au tunaweza kusema hayana “akili” kwani hayachambui kama imani iliyofikishwa kwake ni mbaya au nzuri, kwani zote huzifanyia kazi kwa namna moja, yakitaka kufanikisha kile ambacho kimeaminiwa na mawazo ya kawaida.
Watu ambao wana uwezo wa utumia vizuri mawazo yao ya kina wamefanikiwa sana maishani. Siyo kufanikiwa kwa mali bali zaidi kwa kuwa na furaha au vyote viwili. Wamekuwa na furaha maishani kwa sababu fikira zao siku zote zimekuea ni nzuri na wamemudu kufuta fikira mbaya kwenye mawazo yao. Kwa kufikiri kwao vizuri, mawazo yao ya kina yameweza kuzaa uzuri – mafanikio na furaha.
Wataalamu wengi wanakubali sasa kwamba, mawazo ya kina ndiyo ambayo kwa kiasi kikubwa yanabainisha aina ya maisha yetu. Hapo kabla wanasayansi wengi walikuwa wagumu sana katika kuukubali ukweli huu, lakini hivi sasa hata madaktari wa taaluma ya utabibu wanakubaliana na jambo hili.
Nimesoma utafiti wa Dr. Joseph Murphy ambaye amefanya utafiti wa kutosha kuhusu nguvu ya mawazo yetu ya kina anayaelezea mawazo haya kama nguvu kubwa alionayo binadamu katika kumwezesha kuboresha maisha yake, ingawa kwa bahati mbaya binadamu wengi hatujui kwamba tuna nguvu hiyo.Unaweza kuyapa maisha yako nguvu zaidi, uwezo zaidi, mali zaidi, afya zaidi, furaha zaidi na raha ya ziada, kwa kujifunza namna ya kuwasiliana na kutumia nguvu iliyojificha kwenye mawazo yako ya kina’,anasema kwenye kitabu chake cha The power of Subconscious Mind’.
Nguvu hiyo utaiipata vipi?  nitaeleza kwa kifupi hapa chini na kwa msomaji atakaependa anaweza kuniandikia kupitia barua pepe yangu.
Kama ambavyo tumesema ni kwamba kile ambacho hututokea kwenye maisha yetu ni matokeo ya majibu ya mawazo  yetu ya kina kwa kile amacho mawazo yetu ya kawaida yamekiamini. Tunapofikiri kwa kuamini kwamba, tumeshindwa, tuna mkosi, tumelogwa au tumekwama, taarifa hizi huenda kwenye mawazo yetu ya kina na kama tulivyobainisha, mawazo haya huwa yanaifainyia kazi imani yetu bila kujali kama ina faida kwetu au hapana. Kwa hiyo, ni wazi yataanza kufanyia kazi imani hizo na matokeo yake yataanza kuonekana sawia au baadaye kidogo, kwa nguvu au kidogo kidogo. Lakini ni lazima matokeo yatapatikana tu.
Hebu jaribu kuwatazama na kuwachunguza wale watu wanaoaini kwamba wana mkosi au wale wanaoamini kwamba, hawawezi. Mara zote utagundua kwamba, watu hawa hawatokwi na ikosi au hawafanikiwi abadani. Mikosi au kutofanikiwa huko huwajia kwa njia ambayo huwashangaza hata wao wenyewe. Hii ni nguvu ya mawazo ya kina.
Tunapoamini kuwa tuna mikosi au hatuwezi, mawazo yetu ya kina kwa kufuatana na kanuni za kimaumbile hutengeneza mazingira  ya kutupatia mikosi au kushindwa huko kwani mawazo hayo hutoa majibu kufuatana na kile kinachoenda kwenye mawazo yetu ya kawaida, yaani kile tunachokiamini.
Hebu jaribu kuwatazama na kuwachunguza wale watu wote wanaoamini kwamba wanaweza na wanaoamimi kwamba watafanikiwa. Mara zote utagundua kwamba, hatima ya watu hawa ni kufanikiwa na kumudu. Kinachowezesha hilo siyo kingine bali mawazo yao ya kina ambayo yamepokea taarifa hiyo kutoka kwenye mawazo ya kawaida ya watu hao, yaani kwenye imani zao.
Tukitaka kufanikiwa au kuanguka kwenye maisha yetu ni uamuzi wetu wenyewe. Tukizijaza fikira zetu kwa mawazo mazuri, yenye kutia moyo, ya upendo na uwezo, ni kkweli tutamudu na kufanikiwa. Tukiyajaza kwa kukata tama, hofu, kushindwa na kujibeza, matokeo yake yatakuwa ni ya kutuumiza, kutuangusha na kutuvuruga kwa kila hali.
Ni Lazima tukubali kwamba, sisi wenyewe ndiyo waumbaji wa maisha yetu kwa njia tuchaguayo kwa kuamini kwetu. Tukiamini na kujiambia kwa njia ya kutuporomosha, ni Lazima tutapotomoka. Tukiamini na kujiambia kwa njiaya kutuinua, ni Lazima tutainuka.  
Nimalizie kwa kusema “Kama unafikiri vibaya,utapata matokeo mabaya.Kama unafikiri vizuri utapata matokeo mazuri.Hii ni kwa sababu,binadamu hutenda na kuhisi kile anachokifikiri, kwani kisicho mawazoni mwake hakiwezi kumgusa kamwe”. 

Chanzo:  http://www.mjengwablog.com/2012/12/chagua-maisha-unayotaka-kuyaishi-na.html

CHELSEA washindwa kutwaa Klabu Bingwa Duniani - Yachezeshwa SAMBA na Wabrazil

  Corinthians   1   Chelsea   0




Cheka Ki- sports.


© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top