Social Icons

Loading...

Fake mobile phone handsets to be switched off next year- UCC anounced !!!

UCC's Director, Technology and Licensing, Patrick Mwesigwa
Anyone with a counterfeit phone has until July 1, 2013 to dispose of it, the Uganda Communications Commission (UCC) has said.UCC was initially set to switch off fake phones this month, but its decision to postpone for another seven months a policy directive which is bound to affect thousands of people is informed by the need to mitigate the expected impact.
"We want to sensitize people about the features of fake phones so that the public and businessmen importing phones know exactly what they are buying or importing," UCC's Director, Technology and Licensing, Patrick Mwesigwa told MPs on the Information and Communications Technology committee yesterday.
According to the spokesperson of UCC Fred Otunnu, fake mobile handsets not only contravene UCC provisions, but they also pose "a security threat since they have no clear identification in terms of serial numbers.""Equipment connected to the network is meant to be of the genuine type approved by UCC in order to achieve compatibility and avoid compromising the network," Otunnu said.
 

Otunnu noted that the ongoing registration of mobile phone sim cards is complimentary rather than connected with the need to stop the circulation of fake phones on the market.
When implemented, the policy directive will see Uganda join Kenya which switched off more than 1 million fake mobile handsets early this month.
In a related development, MPs heard that UCC is set to gazette new stringent quality of service benchmarks for telecommunication companies tomorrow, as it seeks to address complaints of plummeting quality of services. The parameters which will see licenses of repeat offenders revoked will provide for financial penalties for blocked calls, loss of network coverage and dropped calls. 


Source :   http://www.newvision.co.ug/news/636921-fake-mobile-phone-handsets-to-be-switched-off-next-year.html

YANGA SASA TISHA MBAYA, SIMBA YAZIDI KUANDAMWA NA SARE

Mabingwa   wa  Kombe  la  Kagame YANGA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuichezesha   kwata  Mgambo JKT ya Handeni, Tanga mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Ushindi huo, unaifanya Yanga sasa iwe na pointi sawa na mabingwa watetezi  SIMBA SC , Nusura     mabingwa    hao wa Vodacom  Tanzania  wachapwe  na  vibonde  wa  ligi  hii  Polisi   ya  Morogoro  baada  ya  kulazimisha  sare ya 1-1, bao   pekee    la  Polisi  lilipatikana   katika dakika ya 35 kupitia kwa Mokili Rambo kabla ya Amri Kiemba kusawazisha dakika ya 57. Kwa  Upande wa Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na mshambuliaji Didier Kavumbangu.
Cannavaro alifunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya Oscar Joshua dakika ya pili kutoka wingi ya kulia, wakati Kavumbangu alimalizia pasi ya Hamisi Kiiza dakika ya 39.Yanga dakika 34 kupata bao la tatu, mfungaji akiwa ni Jerry Tegete aliyeingia dakika ya 68 kuchukua nafasi ya Kavumbangu.Katika mechi nyingine, Simba ilitoka sare ya 1-1 Polisi kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, wenyeji wakitangulia kupata bao dakika ya 35 kupitia kwa Mokili Rambo kabla ya Amri Kiemba kusawazisha dakika ya 57. 

Mkurugenzi TANESCO Atimliwa.



TAARIFA KWA UMMA.


Mzee wa Upako ‘awapaka’ wenzake

KIONGOZI wa Kanisa la Maombezi la GRC na Ubungo, Dar es Salaam, Mchungaji Antony Lusekelo   maarufu  kama " MZEE   WA  UPAKO " amewataka viongozi wa dini na Watanzania kwa jumla, kutambua kuwa Tanzania ni bora kuliko dini zao.
Mchungaji Lusekelo pia aliwataka viongozi wa dini kuendeleza vita dhidi ya rushwa huku akisema watoa rushwa na wapokeaji, wamejificha makanisani na kwenye misikiti.
Alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  ambapo alisema viongozi wa dini lazima lazima washiriki katika mapambano ya rushwa bila woga.
Katika mazungumzo hayo, mchungaji huyo pia alisema  Serikali inapaswa kuwajibika kwa kutumia nguvu zake za kisheria katika kulinda amani, huku akinyoshea kidole tukio la hivi karibuni lililoashira kuvunja kwa amani, huku Serikali ikiwa haijachukua hatua.
Alisema hilo ni tatizo kubwa na kwamba  ni watu wengi wakiwamo viongozi wa dini kushindwa kusema ukweli kwa kuogopa maisha yao kuwa mafupi.“Ni muhimu kila mwananchi kutambua kuwa  Tanzania ni bora kuliko Ukristo na Uislamu. Watu wengi wanaogopa kusema ukweli. Hata viongozi wa dini kwani watoa rushwa wamejificha misikitini na makanisani, tuendeleze mapambano dhidi ya rushwa ipo siku tutashinda,” alisema.Kuhusu vurugu nchini, alisema chanzo ni viongozi wa dini  kuhubiri siasa za chuki misikitini  na makanisani.“Vurugu siyo asili ya binadamu inatengenezwa, Serikali ina wajibu wa kutumia nguvu yake kisheria kuilinda amani na amani haishuki kutoka mbinguni au kwa maombi, inatengenezwa pia. Tatizo cheche za kidini zilipoanza hazikudhibitiwa. Serikali ilikuwepo, aidha kwa makusudi au bahati mbaya imelea cheche hizo,” alisema Lusekelo.
Soma  zaidi  : http://www.mwananchi.co.tz/habari/kitaifa/-/1597296/1606826/-/2a4eu0z/-/index.html

Kibonzo...


Wananchi Kuchangia Maoni ya Katiba kwa SMS

 Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetangaza namba nne (04) za simu za mkononi ambazo wananchi kwa sasa wanaweza kuzitumia kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (‘sms’) kutoa maoni yao kuhusu Katiba Mpya. Kwa mujibu wa taarifa ya Tume hiyo kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo (Jumatano, Oktoba 31, 2012) namba ambazo wananchi wanaweza kutuma maoni yao kwa njia ya ‘sms’ ni 0715 (Tigo) /0767 (Vodacom) / 0787 (Airtel) / 0774 (Zantel) – 08 15 08. “Kwa kuzingatia kuwa Watanzania wengi waliopo mijini na vijijini wanamiliki simu za mkononi, Tume ya Mabadiliko ya Katiba inaamini kuwa njia hii ni fursa nyingine muhimu kwa Watanzania kuweza kuwasilisha maoni yao kwa Tume,” imesema sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na Katibu wa Tume hiyo Bw. Assaa Rashid. Ili kutuma maoni, Bw. Assaa amesema, mwananchi anapaswa kufungua ukurasa wa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (sms) katika simu yake na kuandika maoni yake pamoja na jina lake kamili, jinsia, mahali anapoishi, umri, elimu na kazi na kutuma kwenda kwenye namba yoyote kati ya zilizotolewa. Kwa mujibu wa Bw. Assaa, baada ya kutumwa, maoni hayo yatakwenda kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambapo yatafanyiwa kazi pamoja na maoni yanayokusanywa kwa njia nyingine. Uanzishwaji wa njia hii ya ujumbe mfupi wa maandishi unalenga kuwapa fursa nyingine wananchi kutoa maoni yao. Tume ya Mabadiliko ya Katiba pia inapokea maoni ya wananchi kupitia mikutano ya ana kwa ana; barua pepe (maoni@katiba.go.tz); njia za posta (S.L.P. 1681, Dar es Salaam au S.L.P. 2775, Zanzibar); ukurasa wa ‘facebook’ (Tume ya Mabadiliko ya Katiba) na tovuti (http://www.katiba.go.tz/). Katika taarifa yake hiyo, Tume imewaomba wananchi kutumia namba hizo kutuma maoni yao binafsi kuhusu Katiba Mpya bila kushawishiwa na watu, makundi, vyama au taasisi yoyote na kufafanua kuwa Tume inatarajia kuanza kupokea maoni ya makundi, vyama na taasisi mara baada ya kumaliza kukusanya maoni binafsi ya wananchi katika awamu ya nne na ya mwisho itakayomalizika mwezi Desemba, 2012. 
Taarifa kwa  hisani  ya   http://www.mjengwablog.com/

USA YAKUMBWA NA KIMBUGA "SANDY"

Kimbunga Sandy ni kimbunga ambacho Marekani haijawahi kukishuhudia kwa miaka tisa iliyopita ambapo kwa mujibu wa Sky Sports ni watu 16 wamepoteza maisha mpaka sasa na nyumba zaidi ya 50 zimewaka moto huku mamilioni ya wananchi wakikaa bila umeme majumbani mwao.
Kutokana na hiki kimbunga pia safari za ndege zaidi ya eflu zimeahirishwa ambapo kwa upande mwingine nyumba laki sita na elfu sabini kwenye jiji la New York zimeachwa bila umeme.


 Taarifa   na  picha   kwa  hisani  ya  http://millardayo.com/

BUNJAK ATIMULIWA AZAM , IKO MBIONI KUMREJESHA STEWART

KOCHA Mserbia wa Azam FC, Boris Bunjak amefukuzwa rasmi leo na sasa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Muingereza Stewart Hall anarudishwa kazini.
Habari kutoka ndani ya Azam FC zimesema kwamba, sababu za kufukuzwa kwa Mserbia huyo ni kushuka kwa kiwango cha timu, hali iliyosababisha sasa ianguke hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Tayari Bunjak amekwishapewa haki zake zote na ataondoka Alhamisi, siku ambayo Stewart atawasili kuanza tena kazi Azam FC.
Bunjak anaondoka Azam baada ya kuiongoza timu katika mechi 16, akifungwa nne tu, zote dhidi ya Simba ikiwemo ya juzi ya Ligi Kuu, waliyofungwa 3-1 na kutoa sare tatu.

IWEKEEE CAPTION , JINA LA KOCHA , NANI HUYU???


KWIKI Net Media Server.


Kuna  kwiki  inaendelea  katika  Net  Media  Server ( http://www.netmedia.co.tz )   kutokana  na  " Email Spamming "  na  kusabisha  Server  kuwa  locked   kwa  muda, tunasikitika  kwa  kukosa  huduma    kwa  kipindi  hiki  ,   wahandisi   tukiendelea  kulifanyia  kazi ,  punde  tu  tutakuwa  hewani  tena.
Utawala
Net Media
30- October  -2012

Bunge kuanza Kesho Mjini DODOMA.

MKUTANO wa Tisa wa Bunge la Muungano unatarajia kuanza kesho Mjini Dodoma, huku ripoti ya Kamati Ndogo ya Bunge iliyoundwa kuchunguza tuhuma za rushwa kwa baadhi ya wabunge ikisubiriwa kwa hamu kubwa.Tume hiyo inayoongozwa na Hassan Ngwilizi iliundwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa ajili ya kuchunguza tuhuma hizo zilizoibuka katika mkutano wa Bunge uliopita. Tuhuma hizo ndizo zilizomfanya Spika kuivunja Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.
Baada ya kuibuka kwa tuhuma hizo, Agosti mwaka huu, Makinda aliunda tume ya wabunge watano kuchunguza tuhuma hizo.Ripoti hiyo inatarajiwa kuwa mtihani mkubwa kwa Spika Makinda hasa ikizingatiwa kwamba ndiye mwenye mamlaka ya kuwasilisha ripoti hiyo bungeni hasa kutokana na kuibuka kwa maneno ya chinichini kwamba kumekuwa na jitihada za kuwasafisha wabunge hasa wa chama tawala.
Hivi karibuni, Naibu Spika, Job Ndugai alikaririwa akisema kuwa mamlaka ya namna ya kuiwasilisha ripoti hiyo yako mikononi mwa Spika Makinda.“Kwa kawaida na kanuni zetu ni kwamba Spika anaweza kuamua kama ripoti hiyo ijadiliwe au iwasilishwe kwa njia ipi, wala hawezi kuingiliwa,” alisema Ndugai.
Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/kitaifa/-/1597296/1605838/-/2a5458z/-/index.html

Four Quadrants...


Chelsea 2 Man U 3



  Chelsea   Vs  Man  U
 

KATUNI...


Michezo  ya  Utotoni  .....

ZIJUWE PASSWORD 25 ZILIZOTOMIKA SANA 2012


Miaka ya sasa suala la kuingiliwa mawasiliano binafsi kwenye mitandao limekuwa likiwaathiri wengi, kiasi kwamba wengi wamejikuta kazi zao za kiofisi zikiingiliwa, siri zao binafsi zikivuja mitaani au pengine kupoteza kabisa akaunti zao za email, na mitandao mingine kutokana na hackers kuzinasa password zao kisha wakazibadili nao watumiaji wakajikuta hawawezi kusaini in kama awali.

 

YAFUATAYO NI MANENO 25 YALIYOTUMIKA KAMA PASSWORD NA WATU WENGI KWA MWAKA 2012 KWA MUJIBU WA WADADISI WA YAHOO.

1. password
2, 123456
3. 12345678
4. abc123
5. qwerty
6. monkey
7. 
letmein
8. dragon
9. 111111
10. baseball
11. iloveyou
12. trustno1
13. 1234567
14. sunshine
15. master
16. 123123
17. welcome
18. shadow
19. ashley
20. football
21. jesus
22. michael
23. ninja  
24. mustang
25. password1 
Je wataka kuwa na Password isiyofojika? 
Hapa kuna vidokezo:
- Tumia herufi ya kwanza kwa kila neno la shairi au mstari kutoka katika wimbo. Kwa Mfano, "Hey, I just met you... And this is crazy... But here's my number... So call me maybe" herufi za mwanzo ni "hijmyaticbhmnscmm."  Of course, itakupasa kuimba kichwani kila mara unapotaka ku-log in.
- Changanya maneno mawili, mfano "hungrydog" au "choppywater." au changanya  herufi  kubwa na  ndogo au  special characters kama @, % au & ili kuweka usalama zaidi, tenganisha maneno hayo kwa kuweka alama au namba au kiwakilishi chochote kwenye keyboard ya komputa yako. Hivyo badala ya kuandika "hungrydog," tumia "hungry$d0g."  Ni mifano tu mengine fanya ubunifu ila kumbuka kuweka kumbukumbu kichwani mwako.
...More  passwd Tips 

Protect your password:

  • Memorize your password, do not write it down
  • Do not share your password. Create a new account instead
  • Avoid using one password for all your logins
  • Don't provide your password to someone for assistance unless you verify:
    • They need the password
    • They are who they say they are
  • Avoid logging in from public computers
  • Change your password frequently

Tips for choosing a password:

  • Avoid dictionary words
  • Avoid familiar items (names, phone numbers, etc.)
  • Use a combination of letters, numbers, and special characters
  • Use more characters (7+)

Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste Watoa Tamko kuhusu vurugu za Mbagala.

TAMKO LA BARAZA LA MAASKOFU  WA MAKANISA YA KIPENTEKOSTE
TANZANIA (PCT)
Tarehe 25/10/2012
Ndugu wapendwa Wakristona Watanzania wenzetu kwa ujumla,tunawasalimu katika Jina la Bwana WetuYesu Kristo.Itakumbukwa kuwasikuyaterehe 12/10/2012 sote tulishitushwa na ghasia za kuchomwa kwa makanisa, Biblia Kuchanwa, kupigwa watumishi wa Mungu, kubomolewa kwa makanisa na sehemu takatifu za ibada yaani madhabahu kukojolewa;uhalifua mbao ulifanyika huko Mbagala jijini Dar es Salaam.
Pamoja na juhudi za Serikali yetu kupitia Jeshi la Polisi kufanya kazi ya kurejesha amani na utulivu Nchini, sisi .Baraza la Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste tumesikitishwa na kitendo cha watoto waliohusika na kitendo cha kukojolea Quran (mtotowa Kikristo aliyekojolea Juzuu pamoja na mwenzake wakiislamu aliyemchochea kufanya kitendo hicho);pia tumehuzunishwa na kufadhaishwa zaidi baada ya kusikia tamko la serikali kupitia kwa waziri wa mambo ya ndani kuwa waliohusika na uvunjaji wa makanisa ni wahuni.
Kwa mtazamo wetu kama viongozi wa dini tunaona kauli ya serikali inamaanisha kuwa, SerikaliHaiamini kwamba waliohusika na uvunjaji wa makanisa,kuchoma Biblia,kubomoa na kukojolea madhabahu,kunywa na kula mikate ya meza ya BWANA pamoja na kuwapiga watumishi wa Mungu ni wanaosadikiwa kuwa ni wanaharakati wa kidini;bali ni
Wahuni tu.Kimsingi, utafiti uliofanywa na baraza letu unaonyesha kuwa vitendo hivi havikufanywa na wahuni bali wanaharakati wakidini
Kwa sababu zifuatazo:-
1. Mkusanyiko wa watu waliofanya uhalifu katika makanisa ulianzia msikitini baada ya sala ya adhuhuri, ukaelekea katika kituo cha Polisi ambapo mtuhumiwa wa kukojolea Juzuu alikuwa amehifadhiwa, na wakataka wapatiwe(kijana huyo anayetuhumiwa) ili wamwadhibu kwa mujibu wa sharia’h za kiislamu kwani walidai ameidhalilisha Qurani Tukufu.
2. Uhalifu wa Kuchomwa kwa makanisa ni moja ya utekelezwaji wa hotuba na maandishi ya wanaharakati (Fisabih Lilah) yanayowahimiza baadhi ya waislamu kudai haki zao za kutaka kujikomboa na Kanisa na Ukristo ambao wanadai ni matokeo ya ukoloni, na kwamba Tanzania inatawaliwa na mfumo wa Kikristo ambao umetapakaa kama damu mwilini kuanzia ngazi ya juu ya utawala wa nchi hadi chini kwa jina maarufu “MfumoKristo”(Tunao ushahidi wa hotuba na mafundisho ya wanaharakati katika CD, DVD na magazeti).
Inashangaza kuona serikali ambayo ndiyo yenye dhamana ya kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao; kupuuza madai haya na kushindwa kabisa kuzuia uhalifu wa matukio ya kuchomwa makanisa ambayo kimsingi ya nafanana kwani yalishatokea huko Zanzibar, Bagamoyo, Tunduru, Mwanza, Ndanda, Rufiji, Kigoma, Mto wa Mbu na sasa Mbagala;kwa kisingizio cha kuwaita wanaofanya matukio hayo kuwa ni wahuni.
Kwa kuwa ni wajibu wa serikali kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu zina heshimiwa na kuthaminiwa, Baraza la Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania tungependa kuishauri Serikali yetu mambo yafuatayo:-
1. Irejee misingi ya Katiba yetu ya Jamhuri Ya Mungano waTanzania ambayo inatamka wazi kuwa; “Tanzania ni Nchi ya Kidemokrasia isiyokuwa na Dini”[KatibaYa 1977, Ibara ya 3 (1)].Hii itasaidia kuondoa hisia za kundi moja la Dini kuona idadi kubwa ya Viongozi na watawala waliopo madarakani pamoja na wakuu wa Vyombo vya ulinzi na usalama wako upande wadini Fulani.

2. Serikali kwa kushirikisha mabaraza yote ya kidini Nchini iundeTume huru itakayo kuwa najukumu la kusimamia na kuishauri serikali juu ya uendeshwaji wa shughuli za taasisi na jumuiya za kidini nchini. Jambo hili litasadia kubainisha mipaka ya kiutendaji kati ya uendeshwaji wa shughuli za kidini na mamlaka ya Nchi ambao umetajwa kwa wazi katika Katiba Ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ya 1977, ibara 19 (2);na hivyo kuondoa dhana ya kutaka kuingiza “udini” kwenye siasa ambayo inaelekea kuota mizizi Nchini.

3. Hata hivyo,baraza la makanisa ya Kipentekoste Tanzania tunatoa tamko kulaani uvunjifu waamani ambao umejitokeza kupitia vurugu zilizojitokeza hivi karibuni Nchini, na tuna waomba waumini wetu waendelee kudumisha hali ya utulivu na amani ambao umejengwa na waasisi wetu tangu Uhuru wa Nchi yetu; japo sote tunajua kuwa haki yetu ya kufanya ibada tuliyopewa na Mungu inaelekea kuvunjwa na watu wengine wasioheshimu uhuru wa ma wazo na imani katika dini. Nawafahamu kuwa yuko aliye juu kupita walio juu ambaye anayaona haya yote yanayotendeka.
Kwa ndugu zetu wanaoitwa Wanaharakati wa Kiisalamu, sisi tunajua imani yenu na mtazamo wenu kuhusu Wakristo; pamoja na msimamo mlionao juu ya kitabu cha Quran na juu ya kupigania Dini ya allah (subhahanahu wataa’alah); lakini kwa kuwa sote ni Watanzania tunawakumbusha kuwa jukumu la kudumisha amani ya Nchi yetu ni letu wote; hivyo, tutumie busara zetu katika kudumisha stahmala inayokazia kuheshimu hisia za watu wengine katika masuala ya kiimani kwani kutokufanya hivyo ni kuhalifu sheria tuliyojiwekea sisi wenyewe.
Aidha, Baraza la Makanisa ya Kipentekoste linaitaka serikali isisite kutoa tamko kali pindi vurugu za kidini zinapojitokeza bali iendelee kushughulikia migogoro ambayo inaweza kusababisha tena vurugu za kidini kwa nguvu zake zote, na iwabane waliohusika na uvunjajiwa makanisa warejeshe mali wakizochukua na kulipafidia za uharibifu wa kuchoma makanisa 10 Tanzania bara na jukwaa moja kwani kwa kufanya hivi itawahakikishia Watanzania kuwa hali hii haijitokez atena.Kwa matukio haya ya kuchomwa makanisa Nchini, Serikali yetu itambue kuwamacho na masikio ya wapenda amani Nchini na Ulimwenguni pote wanasubiri kwa hamu kuona ni hatua gani madhubuti serikali itachukua kwa watuhumiwa wa matukio ya uvunjwaji wa makanisa yaliyofanyika huko Zanzibar na Tanzania bara.
.............................. .............................. .......
Askofu Davidi Andulile Mwasota
Katibu Mkuu PCT Taifa.
MUNGU IBARIKI TANZANIA ILI IZIDI KUWA KISIWA CHA USALAMA NA AMANI.

KIBONZO..


Kanisa la KKKT Iimetangaza Tarehe 28 October, 2012 ni Siku Ya Maombi Nchi Nzima

Kufuatia matukio ya Uvunjifu wa Amani unaofanywa na kikundi cha watu wachache kwa mwamvuli wa "dini". Kanisa La Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limetoa Waraka Elekezi Wa Wachungaji Wake Wote Tanzania kuelekeza kuwa siku ya tarehe 28 October, 2012 ni siku ya Kufunga na Kuomba kwa ajili ya Amani nchini Tanzania.
Kanisa la KKKT linakuwa kanisa la Kwanza Tanzania kupitisha siku ya Kikanisa la Kufunga na Kuomba kwa ajili ya Amani Ya Nchi ilivyo Sasa.

Blog hii ambayo imefanikiwa kuutia machoni waraka huo uliotumwa na Maaskofu Dayosisi zote KKKT Wakuu wa Vituo vya Kazi za Umoja, KKKT na nakala yake kutumwa Manaibu Katibu Mkuu,Wasaidizi wa Maaskofu, Dayosisi zote KK KT, Makatibu Wakuu Dayosisi zote kuwaelekeza kwamba tarehe 28 Octoba ni Siku ya Kufunga na Kuomba. Waraka huo umeelekeza "Kufuatia matukio ya kuchoma Makanisa yaliyotokea hivi karibuni,barua  inawataarifu kuwa siku ya Jumapili tarehe28 Oktoba 2012 imepangwa kuwa siku maalum ya kuombea amani katika nchi yetu.Pamoja na mambo mengine yaliyokwishakupangwa kufanyika siku hiyo ( 28 Oktoba2012)' tafadhali sharika, mitaa na Vituo vya Kazi za Umoja vyote vya Kanisa letu vifanye maombi  hayo"
 Kanisa la KKKT inawataka Waumini wa Kanisa hilo kuendelea Kuhimizwa Kufunga na Kuomba Kwa Kadri Roho Wa Bwana atakavyowaongoza kuombea amani ya Tanzania.
Chanzo  kwa  hisani ya  : http://samsasali.blogspot.com/2012/10/kanisa-la-kkkt-iimetangaza-tarehe-28.html

Muhongo,Sitaomba radhi kwa wezi.

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameapa kuwa kamwe hataomba radhi bunge kwa madai aliyotoa dhidi ya watu aliowatuhumu kulihujumu Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ambao amewafananisha na wezi.

Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi juzi, Profesa Muhongo alisema yote aliyoyasema kwenye kikao cha Bunge la Bajeti kilichopita ni sahihi na ana ushahidi wa kutosha kuthibitisha tuhuma hizo.
“Kamwe sitaomba radhi kwa wezi. Subirini muone na kusikiliza kwenye kikao kijacho cha Bunge nitakachoongea kwa muda wa hizo dakika tano wanazotaka kunipa niombe radhi,” alisema Profesa Muhongo.
Alitoa kauli hiyo alipotakiwa kuzungumzia kuvuja kwa ripoti ya Kamati ya Brigedia Jenerali Mstaafu, Hassan Ngwilizi iliyoundwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda kuchunguza tuhuma za rushwa kwa wabunge zilizosababisha Kamati ya Nishati na Madini kuvunjwa.
Taarifa hizo za kuvuja kwa ripoti hiyo zinaeleza kuwa, Kamati ya Ngwilizi imependekeza Waziri aombe radhi na Katibu Mkuu wa wizara yake, Eliakim Maswi achukuliwe hatua za nidhami na mamlaka zilizo juu yake.
“Yaani watu waibie taifa, tuwagundue na kuwasema, halafu nisimame kuowaomba radhi? Sitafanya hivyo. Sitaki kuzungumza mengi, lakini Watanzania wasubiri kauli yangu siku jambo hilo litakapowekwa hadharani,” alisisitiza Profesa Muhongo.
Soma  Zaidi : http://www.mwananchi.co.tz/biashara/13-biashara-za-kitaifa/26765-muhongo-sitaomba-radhi-kwa-wezi

Hii Ndio List ya walioshinda UVCCM.


MWENYEKITI UVCCM TAIFA NI Mhe. JUMA SADIFA - 2012-2017
MAKAMU MWENYEKITI UVCCM TAIFA NI Mhe.MBONI MHITA


WAJUMBE NEC
1. Jerry Silaa [Mayor wa Ilala]
2. Deo Ndejembi
3. Anthony Mavunde Sosa [Wakili Msomi]
4. Jonas Nkya [Wakili Msomi]
5. Petro Magoti [mlemavu wa viungo]


6. Fatma Jumbe [mlemavu wa Ngozi]

 Habari zaidi zinasema kwamba Uchaguzi wa UVCCM uliokuwa ukiendelea huko Dodoma ulitawala vimbwanga kwa watu kutoa Rushwa kana kwamba ni agizo la chama!! Vijana wanaosemekana kwamba wanabebwa na baadhi ya vigogo wa muda mrefu katika chama [CCM] wamemwaga Rushwa pasipo kuiogopa Takukuru!!!
Katika uhalisia Chaguzi zote za ndani ya Chama Cha Mapinduzi [CCM] zimegubikwa na rushwa ya kutisha! Sumaye alitamka hivyo siku kadhaa zilizopita. Na sasa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, amethibitisha bila shaka yoyote kuwa rushwa ndani ya chaguzi kwenye jumuiya zote za CCM, ikiwemo UWT na UVCCM, ni ya kutisha na inaelekea kukizika chama hicho kikongwe hapa nchini. 
Mimi kama mwanahabari mchanga ninayechipukia nina swali dogo tu la kumuuliza Jk: Kama hilo analijua na zaidi anajua vyema kwamba chaguzi zote za ndani ya CCM, huwa vijana wa Hoseah [Takukuru] huwa wanajaa, wakijidai kwamba wanadhibiti rushwa je kama hiyo TAKUKURU inashindwa kufanya kazi inayotakiwa kuifanya na badala yake rais anabaki kulalamika badala ya kuchukua hatua ya kuivunja je hapo sasa mh rais na Mwenyekiti wa CCM taifa anataka sisi kama Wananchi tumweleweje? Tunajua wazi kwamba Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamaba na Rushwa Tanzania [TAKUKURU] Dk Edward Hosea ameteuliwa na rais kusimamia chombo hicho muhimu cha kudhiti na kuzuia vitendo vya rushwa nchini sasa kama mhusika ameshindwa kazi basi rais anapaswa kumfukuza kazi na wala si kubaki kuwalalamika wananchi kama tulivyoweza kuthibitisha katika siku chache zilizopita, kinyume na hapo basi tuseme kwamba kama safari hii mh rais asipomfukuza kazi Dk Hosea na kubaki kulalamika tutajua wazi kwamba kinachoendelea ni maigizo ya kawaida ya Chama Cha Mapinduzi. 
Kwa  hisani by Maisha Times.

Yanga yazidi kung'ara, Azam yabanwa Mbavu na Ruvu Shooting.

  YANGA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuichapa Polisi Morogoro mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Kwa Hisani ya Bin Zubeiry Blog
Ushindi huo, unaifanya Yanga itimize pointi 17, baada ya kucheza mechi tisa na kuendelea kusimama katika nafasi ya tatu, nyuma ya Azam FC yenye pointi 18, baada ya sare ya 1-1 na Ruvu Shooting Uwanja wa Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.   
Ruvu walipata bao lao kupitia kwa Seif Abdallah na Kipre Tcheche akaisawazishia Azam.
Uwanja wa Taifa, hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyotiwa kimiani na washambuliaji Simon Msuva na Didier Kavumbangu.
Msuva alikuwa wa kwanza kuwainua vitini mashabiki wa Yanga dakika ya tano kabla ya dakika moja baadaye, Mrundi Kavumbangu naye kuwapa raha mashabiki wa timu hiyo.
Yanga ingekwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa mabao 3-0 kama mkwaju wa penalti wa Haruna Niyonzima usingegonga mwamba na kurudi uwanjani kabla ya mabeki wa Polisi kuondosha kwenye hatari.
Refa Alex Mahagi kutoka Mwanza alitoa penalti hiyo, baada ya Msuva kuangushwa na beki John Bosco kwenye eneo la hatari wakati anakwenda kufunga.     
Kipindi cha pili Yanga walirudi kwa kasi tena na kuendelea kulishambulia lango la Polisi, ingawa walipoteza nafasi nyingi na kutumia moja tu, dakika ya 58, mfungaji Hamisi Kiiza aliyeingia kuchukua nafasi ya Jerry Tegete.
Katika mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Coastal Union iliifunga 1-0 African Lyon Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, Mtibwa Sugar imelazimishwa sare ya 1-1 na Kagera Sugar Uwanja wa Manungu, Morogoro. 
Matokeo ya leo yanaziweka karibu mno, Simba, Azam na Yanga pale juu, kiasi kwamba ushindani na uhondo wa ligi hiyo unaongezeka.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Yanga kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shadrack Nsajigwa, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Nahodha), Mbuyu Twite, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Nurdin Bakari, Jerry Tegete/Hamisi Kiiza, Didier Kavumbangu na David Luhende/Nizar Khalfan.
Polisi; Manji Kulwa/Kondo Salum, Nahodha Bakari, John Bosco, Noel Msakwa, Salmin Kissi, Hamisi Mamiwa, Bantu Admin/Paul John, Paschal Maige, Mokili Rambo (Nahodha), Malimi Busungu na Nicholas Kabipe/Keneth Masumbuko.
Katika mchezo wa awali wa utangulizi, Yanga B imeifunga TMK United ya Ligi Daraja la Pili, mabao 6-1 katika mchezo wa utangulizi kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na Polisi Morogoro. 
Mabao ya Yanga yamefungwa na Georgeb Banda matatu katika dakika za 61, 70 na 72, Hussein Moshi dakika ya 12 na Rehani Rehani dakika ya 19 na 27, wakati la kufutia machozi la TMK United, lilifungwa na Abdi Hashimu dakika ya 62.
Taarifa  kwa  hisani ya  blog  ya   http://richard-mwaikenda.blogspot.com/

Wambura Aula CAF .

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda kuwataarifu kuwa Ofisa Habari wake, Boniface Wambura ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika (CAF) kuwa mmoja wa maofisa watakaoshughulikia masuala ya habari wakati wa fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake zitakazofanyika nchini Equatorial Guinea.
Uteuzi huo umefanywa na Rais wa CAF, Issa Hayatou kwa ajili ya kufanikisha uendeshaji wa fainali hizo za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake zilizopangwa kuanza Oktoba 28, 2012 na kumalizika Novemba 11, 2012.
Wambura atakuwa mmoja wa maofisa watatu watakaoshughulikia habari kwenye fainali hizo. Wengine ni ofisa kutoka makao makuu ya CAF, Mahmoud Garga na Arlindo Macedo kutoka Angola.
Wambura atakuwa ni Mtanzania pekee kwenye Kamati ya Maandalizi ya fainali hizo, kitu ambacho TFF inajivunia kutoa mwakilishi kwenye moja ya mashindanoi makubwa ya mpira wa miguu Tanzania.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga ameelezea uteuzi  huyo kuwa ni matokeo ya kazi nzuri ambayo Wambura amekuwa akiifanya tangu ajiunge na Shirikisho Januari mwaka 2011.
“Taarifa zake mbalimbali zimeifanya Tanzania iwe inang’ara CAF na hata FIFA kwa kuwa kwa sasa wanajua kila kinachoendelea kwenye soka la Tanzania,” alisema Rais Tenga na kumtakia Wambura kila la kheri kwenye kazi hiyo atakayoifanya kwa takriban siku 14.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, akizungumza kwa niaba ya Sekretarieti, amemtakia Wambura kazi njema na kwamba awe kioo cha mabadiliko makubwa yanayoendelea kwenye soka la Tanzania.
Wambura alijiunga na TFF Januari, 2011 akiwa mmoja wa waajiriwa watatu wapya kwenye Shirikisho baada ya wsatendajiu wengine wawili kumaliza muda wao wa mikataba.
Wambura ni mwandishi wa habari mwandamizi ambaye ameshafanya kazi kwenye vyombo mbalimbali kuanzia kazi ya uandishi hadi Mhariri Mtendaji wa gazeti la Jambo Leo ambalo alikuwa akifanya kazi kabla ya kujiunga na TFF
Mahmoud Garga (CAF)
Boniface Wambura (Tanzania)
Arlindo Macedo (Angola

SIMBA YAZIDI KUTENGENEZA DROO ... PUNDE ITAKUWA NA KABATI

Simba SC waendeleza drooo.(Kibonzo kwa Hisani ya Marco Tibasima)
Baada ya wiki iliyopita kushikwa shati na kagera sugar katika uwanja wa Taifa, jana tena imeendeleza droo na timu ya Mgambo JKT huko Mkwakwani Tanga. Washambuliaji wake nguli na wa bei ghali wameambulia patupu kwa timu hiyo mpya. Droo hii inakuwa ya nne tangu kuanza ligi, ingawa bado timu hiyo inaongoza kwa pointi 19 ila tofauti kati yao na watani wao Yanga imepungua kuwa pointi 2. Ushindi wa mechi za kwanza je! Ulikuwa ni nguvu ya soda? au timu zilikuwa hazijaamka?

Chelsea , Man U zapata ushindi mnono , Arsenal yachezea kichapo..

Chelsea    4     Hotspurs  2



Man  U   4   Stoke  City 2



Man  City  2   West Blomwich  Albion  1



Arsenal 0     Norwich  City  0 


Yanga Yaichapa Ruvu Shooting 3 - 2.


Sophia Simba amliza Kilango UWT

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania, Sophia Simba akishangilia ndani ya Ukumbi wa Chuo cha Mipango kwenye mkutano mkuu wa 8 wa umoja huo taifa uliofanyika jana, mjini Dodoma
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba ameendeleza ubabe wake dhidi ya hasimu wake kisiasa, Anne Kilango baada ya kumbwaga kwa idadi kubwa ya kura katika uchaguzi wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT).
Hii ni mara ya pili kwa Simba kumshinda Kilango katika kuwania nafasi ya uenyekiti wa UWT, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2008, ambapo Simba aliibuka mshindi.

Dar City Centre Mchana wa LEO.

Polisi wamefunga barabara ya hapa Posta Mpya  katikati  ya  Jiji  la  Dar  es  Salaam , na daladala zinageuza hazitumii tena kituo cha kawaida.Hali inaonekana si shwari, wanajeshi wametanda!  kariakoo  nako  hali   ni  tete,  pia  Mabomu yanasikika kutoka msikiti wa Mtambani Kinondoni. Barabara ya Kawawa kupitia Kinondoni Imefungwa kwa Muda Vijana wa Kamanda Kova wanarusha mabomu huku wengine wako juu wanazunguka.

   Eneo   la    posta    stand  kukiwa  na  doria  kuzuia   ofisi  za    jeshi  la  Polisi   makao  makuu  kuvamiwa  na  waandamanaji.
   Magari  si  mengi   na  hali  ni  ya  wasiwasi   kiasi.
   Hali  ya  Barabara   ,  utadhani  ni  jumapili   , hakuna  kabisa  mpishano  uliozoeleka.

 Hapa   ni    Haedery  Plaza, kiasi  watu  hapa  ni  wengi  na   



Kariakoo  nako   hali  ilikuwa  hivi...



Sheikh Issa Ponda Afikishwa Kortini KISUTU.

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Waislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda akishuka katika gari baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa mashtaka  yanayomkabili, jijini Dar es Salaam jana.




Hali iko hivi KENYA na UGANDA.

 Swali : Je  kwa  TZ  hali  ikoje???
  Kwa  yeyote  mwenye    kibonzo  cha    hali  ilivyo  kwa    A  Tanzanian  wife    tafadhali   kitume  kupitia   daniel@netmedia.co.tz  au  danielniji@gmail.com  kitarushwa    kwenye  blog  hii.
Ahsanteni
Utawala
Net media.

WAZEE WA JANGWANI TISHIO; VODACOM WAMEBANAAA SASA WAMEACHIA

DAR YOUNG AFRICAN SPORTS CLUB
Baada ya baraza la wazee wa Yanga kuketi na kutoa msimamo na tambo zao kwamba wao kama Yanga kamwe hawawezi kuvaa nembo au jezi yenye doa lenye rangi nyekundu na hawaogopi kufungiwa au kushushwa daraja.
Tambo hizo zilichochewa pia na maombi ya uongozi wa mabingwa hao wa CECAFA kwa VODACOM kwamba ni heri watumie nembo kama ya mwaka jana yenye rangi nyeusi na sio nyekundu.
Baada ya kilio na tambo hizo sasa VODACOM wamekubali ombi hilo na leo wamekabidhi aina tatu ambazo Yanga wanatakiwa kuchagua moja ili waitumie kama nembo ya mdhamini VODACOM.

NEMBO MPYA ZA VODACOM - YANGA

Kibarua sasa ni cha Yanga kuchagua nembo waitakayo na lazima sasa walinganishe na rangi ya nembo yao.

CHANGAMOTO KWA VODACOM NA TFF:
- Je! Timu ingine kama Toto Africa, JKT Oljoro, Africa Lyons, Kagera/Mtibwa Sugar au Azam FC nao wakisema kuwa nembo yenye kidoti chekundu nayo hairandani na rangi zao je nembo hiyo itabadilishwa?
- Je! Suala hili kisheria lina maana gani kwani tunatambua kuwa nembo huwa zinasajiliwa na kupewa copyright sasa VODACOM watakuwa wanasajili nembo kulingana na matakwa ya kila timu kila msimu wa ligi kwani timu zingine zitashuka na nyingine kupanda?

MAASKOFU WA KKKT SASA WAFUNGUKA

Sio jalala bali ni ofisi ya mchungaji jinsi ilivyoteketezwa kwa  moto

Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) takribani 15 kati ya 20 leo alhamis asubuhi wamemtembelea Mkuu wa Kanisa hilo ambaye pia ni Askofu wa KKKT: Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dr. Alex Malasusa ili kumpa pole yeye na waumini wote wa KKKT na wakristo wengine waliopata madhara ya vurugu zilizotokea na zinazoendelea kutokea hapa nchini. Maaskofu hao wakiongozwa na Askofu Dr. Martin Shao na Dr. Stephen Munga wametembelea usharika wa Mbagala ili kujionea wao wenyewe uharibifu ulivyofanywa lakini pia wametembelea hapo ili kuleta salamu za maaskofu na viongozi wengine waliokuwa katika mkutano wa Lutheran Mission Corporation (LMC). Sanjari na salamu hizo walikabidhi pia TSH. 378,000/= kama pole, fedha zilizochangwa na maaskofu hao wakati wakiwa katika mkutano huo.
Askofu Dr. Alex Malasusa akitoa shukrani kwa Maaskofu waliofika kumpa pole na kutembelea kanisa hilo.
Maaskofu hao pamoja na kutembelea kanisa hilo walifanya pia  ibada ya ghafla na kutoa neno la faraja ambapo Askofu Paul Akyoo alihubiri neno hilo toka Wafilipi 4: 6-7.
Baba Askofu Paul Akyoo akihubiri neno la faraja walipotembelea usharika wa Mbagala.
Baadhi ya wachungaji, viongozi, wazee wa kanisa na washarika wa Mbagala walihudhuria ibada hii maalum
Kabla ya neno hilo la faraja Baba Askofu Dr. Martin Shao alisoma salamu/tamko la maaskofu wote wa Dayosisi 20 za kanisa hilo la KKKT. (Blog hii imefanikiwa kupata waraka huo)
Baadhi ya maaskofu wakipozi katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kuangalia uharibifu uliofanywa


SALAAM ZA MAASKOFU WA KKKT KWA WATANZANIA WOTE KUHUSIANA NA MATUKIO YA KUCHOMA MOTO MAKANISA YA KIKRISTO ENEO LA MBAGALA – DSM.

             Wapendwa Katika Bwana,
Waumini wa KKKT, Wakristo Wote na Watanzania kwa Ujumla.

Neema na Iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu Kristo, Amina.

Sisi maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za matukio ya uchomaji wa makanisa katika eneo hili la Mbagala. Tumekuwa katika mkutano wetu wa Mwaka wa Lutheran Mission Cooperation (LMC) huko Moshi pamoja na vyama vyote vya Kimissioni vya Ulaya na Marekani. Tumelazimika kukatisha mkutano huo ili kufika hapa Mbagala. Tumekuja kwa madhumuni makubwa matatu:
  1. Tumekuja kuwapa pole na kusimama pamoja nanyi katika uchungu mkubwa mlio nao. Machozi yenu ni machozi yetu. Machozi yetu ni machozi ya Kristo mwenyewe aliye Bwana wa kanisa linaloteswa. Jipeni moyo kwa kuwa yeye aliushinda ulimwengu (Yohana 16:33).
  2. Tumekuja kuonyesha majonzi yetu makubwa kwa vitendo vya uvunjifu wa amani, kuporomoka kwa umoja na mshikamano wa watanzania. Huu ni msiba mkubwa, na wenye msiba ni watanzania wote, wenye dini na wasio na dini.
  3. Tumekuja kushiriki pamoja nanyi kupokea matumaini ya Tanzania mpya. Katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa madhabahu ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa. Majivu haya na machozi yenu ni rutuba ya Tanzania mpya itakayojali upendo, uvumilivu, ustahimilivu, umoja, mshikamano, uhuru wa kuabudu na dola isiyo na dini.

Katika ujio huu wa maaskofu hapa Mbagala, hatukuja hapa kufanya haya yafuatayo:
  1. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaokashifu dini za wenzao, wawe na ruhusa kutoka mamlaka zilizo juu au kama wanajituma wenyewe.
  2. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaodhalilisha misahafu ya dini; wawe wametumwa, kutegeshewa na mamlaka zozote au kwa misukumo ya utashi wao binafsi ili kupata kisingizo cha kugombanisha madhehebu ya dini.
  3. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaochoma makanisa na kuiba mali za makanisa kwa kisingizio cha kumtetea Mungu. Kisasi cha dhambi hiyo tunamwachia Mungu mwenyewe aliyedhihakiwa na walionajisi madhabahu yake.

Wapendwa wana KKKT na watukuka sana, wana na mabinti wa Tanzania ya Julius Kambarage Nyerere; kilichotokea Mbagala katika wiki ya kuadhimisha siku ya Baba wa Taifa, ni kebehi si kwa Baba wa Taifa bali ni kebehi kwetu sisi wenyewe tunaokalia kiti alichokalia Baba wa Taifa. Yeye amelala baada ya kazi njema. Apumzike kwa amani na tunu zake zifufuke katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa amani na mshikamano wa Tanzania aliyoijenga.

Kilichotokea Mbagala ni mateso ya kimbari, yaani mateso ya Kanisa (Persecution). Mateso haya ni matokeo ya mbegu ya magugu iliyopandwa katika bustani njema na sasa magugu hayo yanazaa matunda machungu. Dalili za mateso ya kimbari kama ilivyo kwa mateso ya kanisa; zilianza kitambo na hazikushughulikiwa na waliomrithi Baba wa Taifa. Dalili hizo ni kama hizi zifuatazo: 
  • Uchochezi wa wazi kuwa taifa hili linaendeshwa na unaoitwa “mfumo Kristo”, na kuwa Baba wa Taifa alaaniwe kwa yote aliyolitendea taifa hili.
  • Ubishi usio na tija juu ya idadi ya waumini wa dini mbalimbali hapa nchini na hata kudiriki kushawishi na kugomea zoezi la sensa ya watanzania. Lengo la ubishi huu ni mbegu inayoweza kuratibisha na kurasmisha mateso ya kimbari na mateso ya kanisa.
  • Matumizi mabaya ya baadhi vyombo vya habari, vyenye lengo la kujenga hofu ya kudumu na migawanyiko ya kidini miongoni mwa watanzania
  • Ukimya wa vyombo vya dola juu ya vitendo vya uvunjaji wa sheria ya matumizi ya vyombo vya habari. Kwa vyovyote vile, uvumilivu wa dola hauna maslahi mapana kwa mustakabali wa taifa letu na ni mateso ya kimbari, mateso kwa kanisa, na kwa wantanzania wote; wawe wengi dhidi ya wachache au wachache dhidi ya wengi.
  • Madai yasiyo ya kawaida na ya mara kwa mara kwa serikali inayodaiwa kutokuwa na dini. Madai hayo ni kama:

  1. Kulazimisha uvaaji wa alama za kidini katika taasisi za umma ili kurahisisha na kuratibisha tofauti za watanzania. Tunajiuliza: Likitokea la Mbagala katika mashule yetu na vyuo vya umma, watachomwa wangapi na kuuawa wangapi?
  2. Madai yanayojirudiarudia kutaka balozi za nchi fulani kufungwa hapa nchini. Madai haya yanaashiria kutaka balozi za nchi fulani tu ndiyo ziwe hapa nchini.
  3. Madai na mashinikizo ya Uanzishwaji wa mahakama za kidini hapa nchini
  4. Mashinikizo ya kidini yanayoingilia mifumo ya kitaaluma na kisheria.
  5. Mashinikizo ya kidini juu ya mfumo wa uteuzi wa watendaji wa serikali na katika ofisi za umma,
  6. Kuhoji na kupotosha juu ya ushirikiano wa serikali na mashirika ya dini katika utoaji wa huduma za kijamii hususan afya na elimu hapa nchini

Wapendwa wana KKKT na Wapendwa watanzania wote. Hata kama wanaofanya mambo haya ya kusikitisha wametunukiwa hadhi ya kuitwa kuwa ni “wana harakati”, tofauti na wanaharakati wanaotambuliwa na watanzania walio wengi, tunawiwa kuonya kwa uvumilivu wote kuwa uana harakati wao usitumike kuvunja nchi na sheria za nchi. Tanzania yenye amani na mshikamano ni tunda la dini zote, makabila yote, itikadi zote za vyama, rangi zote na hali zote za kiuchumi. Hata wasio na dini wanachangia amani ya nchi hii.

Kwa macho na masikio yetu, tumeendelea kushuhudia vitendo vya uchomaji makanisa huko Zanzibar, Mwanza, Mdaula, Mto wa Mbu, Tunduru, Rufiji, Kigoma na sasa Mbagala. Wakati wote uvumilivu wa wakristo huenda umetafsiriwa kuwa ni unyonge na woga. Ikumbukwe kuwa hata wanyonge na waoga, hufika wakati wakasema “sasa basi” pale wanapodhalilishwa kupita kiasi. Hatuombei wakristo wafikishwe hapo.

Tumeshuhudia wizara zetu zikivamiwa mchana kweupe na kushinikiza kuachiwa kwa watuhumiwa wa uhalifu; tumeshuhudia vituo vya polisi vikichomwa moto; mahakama zikilazimishwa kufunga shughuli zake, misikiti ikitekwa, uhai wa viongozi wa dini ukitishiwa hadharani na viongozi wastaafu wakizabwa vibao hadharani kwa sababu ya zinazoitwa harakati za kidini. Tumefikia kuhoji, watu hawa wavamie nini ndipo hatua zichukuliwe? Wachome nini ndipo viongozi wenye dhamana ya kulinda mali na uhai washtuke? Wamwue nani ndipo iaminike kuwa watu hawa ni tishio kwa usalama wa taifa letu?

Sisi tulioitwa kwa njia ya nadhiri na viapo vitakatifu, tunawasihi sana waumini wa dini zetu na watanzania kwa ujumla, wenye wajibu wa kututii na wasiolazimika kututii, kuzingatia kuwa Mwenyezi Mungu analipenda taifa hili na watu wake. Kamwe hawezi kuliacha liangamie.

Kwa Wakristo wote, huu ni wakati wa kuendelea kufunga na kuomba kwa ajili ya amani ya taifa hili. Mkristo wa kweli ni yule aliye tayari kuteswa kwa ajili ya Kristo na kanisa. Wakristo hatuko tayari kuua, kutesa, kulipiza kisasi ili kumtetea Kristo. Mungu wetu hatetewi kwa kuua wengine na kuchoma madhabahu ya dini nyingine.

Katika mateso haya, kanisa litaimarika zaidi; na katika majivu haya ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa na ukombozi wa kweli utapatikana. Tunawataka wakiristo wote kusamehe na kuendelea kuwa raia wema. Kushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko ya kweli kwa kupitia njia sahihi zilizowekwa. Wakati wengine wanaweka mikakati ya kuchoma madhabahu, wakiristo tuweke mikakati ya kuomba na kushiriki vema katika haki zetu za uraia. Pamoja na kuwa wapole kama njiwa, imetupasa pia kuwa na busara kama nyoka (Mathayo 10:16).

Daima tukumbuke kuwa, “KUSHINDANA KWETU SISI SI JUU YA DAMU NA NYAMA BALI NI JUU YA FALME NA MAMLAKA, JUU YA WAKUU WA GIZA HILI, JUU YA MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO” (Waefeso 6: 12).

Ni sisi Maaskofu wenu kwa Neema ya Mungu,
  1. Askofu Dr. Alex G. Malasusa – Mkuu, KKKT na D/Mashariki na Pwani
  2. Askofu Dr. Stephen Munga –Mkuu, D/Kaskazini Mashariki
  3. Askofu Dr. Martin Shao – Mkuu, D/Kaskazini
  4. Askofu Dr. Thomas Laizer – Mkuu- D/Kaskazini Kati
  5. Askofu Dr. Benson Bagonza- Mkuu, D/Karagwe
  6. Askofu Isaya J. Mengele – Mkuu, D/Kusini
  7. Askofu Levis Sanga – Mkuu- D/Kusini Kati
  8. Askofu Elisa Buberwa – Mkuu –D/Kaskazini Magharibi
  9. Askofu Andrew Gulle – Mkuu, D/Mashariki ya Ziwa Victoria
  10. Askofu Michael Adam –Mkuu, D/Mkoani Mara
  11. Askofu Renard Mtenji – Mkuu, D/Ulanga-Kilombero
  12. Askofu Dr. Israel-Peter Mwakyolile – Mkuu, D/Konde
  13. Askofu Job Mbwilo – Mkuu, D/Kusini Magharibi
  14. Askofu Dr. Owdenburg Mdegella- Mkuu, D/Iringa
  15. Askofu Jacob Ole Mameo- Mkuu, D/Morogoro
  16. Askofu Zebedayo Daudi – Mkuu, D/Mbulu
  17. Askofu Paulo Akyoo – Mkuu, D/Meru
  18. Askofu Charles Mjema – Mkuu, D/Pare
  19. Askofu Mteule Amon Kinyunyu- Mkuu, D/Dodoma
  20. Askofu Mteule Dr. Alex Mkumbo- Mkuu, D/Kati

Mbagala, Dar es Salaam,
Oktoba 18, 2012


© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top