Social Icons

Loading...

Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye Abwagwa Kwenye Uchaguzi wa Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM(NEC).

 Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye Abwagwa Kwenye Uchaguzi wa Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM(NEC)Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara na Mgombea Mwenzake Mary Nagu Kwa Kura 481 kwa 648

Chanzo: http://www.hakingowi.com/2012/09/waziri-mkuu-mstaafu-fredrick-sumaye.html

Madrid , Barca zapata ushindi LA LIGA

Madrid  Vs  Deportivo   5 -  1



Barca   3   Sevilla 2


Chelsea Yaua , Yaibamiza Arsenal 2 - 1




Man   Yapigwa  stop  na  Spurs

Man  City  Vs   Fulham

Liverpool nayo  yazinduka   yaikunguta   5 - 2  Norwich City


Visit  to  view all  results http://www.premierleague.com/en-gb/matchday/results.html

Waliotoswa CCM Wafichua Siri


FILIKUNJOMBE ADAI YEYE, MKONO, LUGOLA WALIPONZWA NA PINDA, NAPE ATAKA WASIORIDHIKA WAKATE RUFAA, WASOMI WAPONGEZA

SIKU  kadhaa baada ya Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), kutangaza majina ya wagombea, baadhi ya vigogo walioachwa kwenye uteuzi huo wameeleza ya moyoni, huku Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe akisema anaamini ametoswa kwa sababu alitia saini ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Katika Bunge la 10 lililoketi Aprili mwaka huu, baadhi ya Wabunge wa CCM akiwamo Filikunjombe, Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono na Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola, waliunga mkono hoja ya kutokuwa na imani na Pinda iliyokuwa imeanzishwa bungeni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe wa Chadema.

Wabunge hao wa chama tawala, waliungana na wenzao wa upinzani kutaka kupiga kura za kutokuwa na imani na Pinda kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ameshindwa kuisimamia Serikali kwa kuwawajibisha mawaziri wazembe. Hata hivyo, mpango huo haukufanikiwa baada ya Spika wa Bunge Anne Makinda kueleza kuwa haukufuata taratibu zinazotakiwa.

Filikunjombe alipotakiwa jana kuzungumzia kuenguliwa kwake kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa ndani ya chama, alisema anaamini yeye na wenzake hao wa CCM, wametoswa kwa sababu ya kushiriki mpango wa kumng'oa Waziri Mkuu Pinda. Hata hivyo, alisema amelazimika kukubali hali hiyo na kupokea matokeo, kwa kuwa hatua yake ya kusaini kitabu hicho ilitokana na nia njema kutaka Waziri Mkuu ajiuzulu ili mambo fulani muhimu katika jamii yafanyike.

Filikunjombe alibainisha kuwa alisaini kitabu hicho cha kutokuwa na imani na Pinda akiwa na akili timamu na alikuwa anajua kinachoweza kutokea kutokana na hatua yake hiyo. "Nimesaini kitabu kile kwa nia njema, nikiwa na akili timamu na sijutii uamuzi wangu huo, ila siwezi kuwasemea Kigwangalla (Khamis mbunge wa Nzega) na Bashe (Hussein). Lakini sisi watatu (yeye, Lugola, Mkono) tumeenguliwa kwa sababu hiyo (ya kutokuwa na imani na Pinda)." Aliendelea: "Nashangaa leo naonekana adui wa chama wakati nilikuwa nakinusuru na kusema kweli adui wa CCM ni Wabunge wa chama hicho ambao hawakusaini kitabu hicho cha kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, " alisema Filikunjombe.

Mkono Mbunge wa Musomo Vijijini, Nimrod Mkono alisema kutoswa kwake ni uamuzi wa watu aliowaita wenye chama. "Walikata jina langu nikakata rufaa, likarudishwa Dodoma, lakini walipokutana wakaona sifai. Wakaamua kunifukuza sasa hapo mimi nifanye nini?" alihoji Mkono. Mkono alisema huu ni utaratibu wa chama chao cha CCM ambao umewapa baadhi ya watu haki ya kuwafukuza wengine bila kuwapa fursa ya kujitetea. "Kama ilivyotokea kwangu wamekaa na kuona Mkono hafai, fukuza basi wakafanya hivyo na hiyo haijalishi kama nilisaini kutokuwa na imani na Waziri Mkuu au la.

Suala la msingi ni kuwa Mkono amefukuzwa na atarudi kama ilivyokuwa kwa mwana mpotevu." alisema bila kufafanua. Kigwangalla Mbunge wa Nzega, Dk Hamis Kigwangalla alisema anaheshimu uamuzi wa vikao vilivyokaa na kufikia uamuzi uliochukuliwa na kwamba, ataendelea kuwa mwanachama na kukitumikia chama pamoja na wananchi kwa nguvu zote bila kinyongo.“Nitaendelea kuheshimu vikao vya chama changu na kuwa mwanachama hai ingawa sijajua wametumia vigezo gani kuteua majina hayo,” alisema Dk Kigwangalla. Bashe Kwa upande wake Bashe alisema kilichotokea ni uamuzi wa chama na vikao halali vilivyokaa na kuchukua uamuazi huo.

“Sijui kwa nini jina langu halikupitishwa, lakini nitaendela kuwa mwanachama na kuwatumikia wananchi wenzangu wa Nzega,” alisema Bashe. Katika kuhakikisha hilo, Bashe alisema leo anakwenda Nzega kupeleka mifuko ya saruji tani 18 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za kata za chama hicho wilayani humo.

Nape ajibu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alitaka makada waliotoswa na wenye kinyongo wawasilishe malalamiko yao CCM kwa maandishi badala ya kulalamika nje ya utaratibu."Wathibitishe kwa maandishi nasi chama tutajua la kufanya, kwani wabunge hao hawakuingia katika vikao vilivyotoa maamuzi sasa nashangaa kusikia katika vikao tuliwajadili na hoja iliyowaondoa ni hiyo," alisema Nape. Maoni ya wasomi Wakizungumzia uteuzi huo wasomi na wanasiasa walitoa maoni tofauti huku baadhi wakisema chama kinatakiwa kuwa na sera na mtizamo wa kuliletea maendeleo taifa bila kujali kama chama kinaongozwa na wazee au vijana.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema uamuzi huo wa CCM umeonyesha kuwa, ndani ya chama hicho hakuna aliye juu kuliko mwenzake.“Wapo waliosema wakitoswa patachimbika, lakini wametoswa na hapajachimbika, uamuzi wa kuwatosa watu wa aina hii utarejesha nidhamu ndani ya chama hicho licha ya kuwa kazi bado ni kubwa,” alisema Dk Bana. Profesa Gaudence Mpangala alisema vijana kupewa nafasi kubwa ya kugombea nafasi mbalimbali ndani ya CCM, hakuna maana kuwa sera na mtizamo wa chama hicho utabadilika.

“Kuwa na wanachama au wagombea wenye umri wa wastani(vijana) sio kigezo cha chama kufanya vyema kwa sababu hawawezi kubadili sera na mtizamo wa chama husika,” alisema Mpangala. Dk Kitila Mkumbo alisema kuingiza vijana wengi katika mpambano huo ni hatua ya ukomavu wa kisiasa kwa kuwa chama hicho awali hakikuwa na utaratibu mzuri wa kuwapa nafasi ya uongozi vijana.“Awali Chadema ndio kilionekana chama kinachowapa nafasi zaidi vijana, lakini kwa hatua hii ya CCM ni nzuri, sasa tunasubiri utendaji wao kama utakuwa na manufaa kwa taifa,” alisema Mkumbo.

Bashiru Ally alisema kama kigezo cha kuweka vijana wengi kitazingatia msimamo, fikra na ufanisi katika utendaji kazi wao basi taifa lina kila sababu ya kuunga mkono hatua hiyo.Alisema kwa kuwa vijana ndio chachu ya maendeleo kwa mataifa mbalimbali duniani, hatua ya CCM kuwapa nafasi vijana ni nzuri kama wakiifanya kazi hiyo kwa manufaa ya taifa kwanza.

Brands Kocha Mpya Yanga

Baada  ya  kusitisha  mkataba na  Kocha Tom Saintfiet   klabu  bingwa  ya  soka ukanda  wa  afrika  mashariki  na  kati  Yanga   imesaini  mkataba  wa  mwaka  mmoja na Ernstus Brands  kwa ajili ya kuiona klabu ya Yanga, pichani kushoto ni makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga   akiwa  na  kocha    huyo, kocha huyo alikuwa akiifundisha APR ya Rwanda.

CHEKA Amtwanga KARAMA

Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.

Picha  kwa  hisani  ya :http://richard-mwaikenda.blogspot.com/

SuperSports Waanza 'Supa Wikiendi'

KITUO cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini kinatarajia kuonyesha mechi nane za watani wa jadi kutoka sehemu mbalimbali duniani mwezi Oktoba ikiwamo mechi ya Simba na Yanga.
Kati ya mechi hizo za watani wa jadi itakayoanza kuonyeshwa itakuwa ni mechi kati ya Simba na Yanga hapo Oktoba 3 kupitia chaneli ya SuperSport 9east.
Crew  ya  SuperSports iliyoko  Tanzania  wiki hii.

Meneja uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi alisema hayo wakati alipotembelea ofisi za Mwananchi Tabata Relini jijini Dar es Salaam, mechi nyingine za watani wa jadi zitakazoonyeshwa na kituo cha SuperSport mwezi Oktoba ni kati ya Barcelona dhidi ya Real Madrid (Hispania), Boca Juniors dhidi ya River Plate (Argentina) na Borussia Dortmund dhidi ya Schalke (Ujerumani).
Mechi nyingine ni kati ya Ajax Amsterdam dhidi ya Feyenoord Rotterdam (Uholanzi), Liverpool dhidi ya Everton (England), Inter Milan dhidi ya AC Milan (Italia) na CSKA dhidi ya Spartak (Russia).
Pia Kambogi alisema kuanzia leo kituo cha SuperSport kitaanza kuonyesha baadhi ya mechi za Ligi Kuu ya Tanzania, ambapo leo itaonyeshwa mechi kati ya Azam dhidi ya JKT Ruvu kuanzia saa 11:45 jioni.
Mechi nyingine zitakazoonyeshwa na SuperSport ni kati ya Simba dhidi ya Tanzania Prisons kesho, Yanga dhidi ya African Lyon siku ya Jumapili, JKT Ruvu dhidi ya Mtibwa Sugar siku ya Jumatatu kabla siku ya Jumatano kuonyesha mechi ya Simba na Yanga.
Naye mchambuzi wa soka katika kituo cha SuperSport, Thomas Mhlambo raia wa Afrika Kusini aliyekuwa ameambatana na Kambogi alisema muda siyo mrefu Tanzania itakuwa na wachezaji wa soka wengi wanaocheza soka katika nchi mbalimbali ulimwenguni.
  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga (kulia) akizungumza na watangazaji maarufu wa Kampuni ya Super Sport ya Afrika Kusini, Thomas Mlambo (kushoto) na Thomas Kwenaite wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampuni hiyo kuanza kwa majaribio kutangaza baadhi ya michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom nchini katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana

CCM Yaibwaga Chadema Uchaguzi wa Meya Jijini Mwanza

Mkurugenzi  Mtendaji  wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza  Ndg:Kabwe
KITENDAWILI cha nani atakuwa Meya wa Jiji la Mwanza kimeteguliwa jana baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kushinda kiti hicho dhidi ya wapinzani wake wakubwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).Uchaguzi huo umefanyika baada ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza kugawanywa Julai mwaka huu katika sehemu mbili. Halmashauri ya Jiji la Mwanza inakuwa katika Wilaya ya Nyamagana na sehemu ya pili inakuwa Manispaa ya Ilemela.

Wakati CCM kikiibuka na ushindi huo, uchaguzi wa Halmashauri ya Ilemela uliahirishwa baada ya Diwani wa Chadema aliyefukuzwa hivi karibuni, Henry Matata kuweka pingamizi. Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa Meya wa Jiji la Mwanza, Msimamizi wa Uchaguzi huo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya jiji hilo, Wilson Kabwe alisema kura zilizopigwa na madiwani wa CCM, Chadema na Chama cha Wananchi (CUF) ni 19.

Alisema mgombea wa CCM, Stanslaus Mabula aliibuka mshindi kwa kupata kura 11 wakati mgombea wa Chadema, Charles Chinchibela alipata kura nane.CCM pia kimeibuka na ushindi katika nafasi ya naibu meya baada ya mgombea wake, John Minja kupata kura 10 dhidi ya Daudi Mkama wa CUF aliyepata kura nane.

Chadema na CUF viliungana katika uchaguzi huo. Wakati Chadema kikisimamisha mgombea umeya, CUF kilifanya hivyo katika nafasi ya naibu meya.
Hata hivyo, kuliibuka mvutano mkali kati ya CCM na Chadema kuhusu wabunge wawili wa chama tawala ambao ilielezwa kwamba walikuwa katika Halmashauri ya Ilemela lakini wakahamishiwa Nyamagana.
Akizungumzia suala hilo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema demokrasia imezingatiwa katika uchaguzi huo na kwamba suala la kuhamisha madiwani kwenda jimbo jingine lipo katika dhamana ya chama husika.
Alisema kuwa jiografia ya mkoa huo haina pingamizi kwa mbunge wa viti maalumu kuamua wapi anahitaji kufanyia kazi na akisema Chadema kilipiga hesabu zake vibaya.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa alisema chama chake kwa sasa hakiwezi kuzungumzia matokeo ya uchaguzi huo akisema ni chama makini ambacho kinahitaji muda wa kuyatafakari kabla ya kutoa uamuzi. 
Ilemela
Uchaguzi wa Ilemela umeahirishwa baada ya Diwani wa Chadema aliyevuliwa uanachama na chama hicho, Henry Matata kuweka pingamizi.
Pingamizi hilo liliwasilishwa kwa msimamizi wa uchaguzi huo muda mfupi kabla ya uchaguzi kuanza. Alichukua hatua hiyo baada ya kubaini kwamba jina lake lilikuwa limekatwa miongoni mwa wagombea umeya.
Akisoma pingamizi hilo, Msimamizi wa Uchaguzi huo, Kabwe alisema diwani huyo alidai kwamba alikuwa na haki ya kugombea nafasi hiyo hadi shauri lake lililopo mahakamani litakapoamuliwa.
Hivi karibuni, Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chadema ilifuta uteuzi wa awali wa wagombea wa nafasi za umeya na unaibu umeya kwa madai kuwa haukufanyika kwa kuzingatia sheria wa katiba ya chama hicho.
Dk Slaa alisema ofisi yake ndiyo yenye mamlaka ya kuteua wagombea katika nafasi hizo mbili.
Uchaguzi huo ulivuta hisia za wakazi wengi wa jiji la Mwanza kwani ilipotimu saa 3:45 asubuhi kulikuwa na mikusanyiko mingi katika maeneo yake mbalimbali na kusababisha askari wa kikosi cha kutuliza ghasia kufunga baadhi ya barabara.
Barabara ambazo zilifungwa ni Sekou Toure kuingia katika lango kuu la jiji hivyo kusababisha adha kwa wagonjwa waliokuwa wakifika katika Hospitali ya Mkoa.
Watu waliokuwa wakiruhusiwa kuingia katika ofisi ya jiji ni wale waliokuwa wakihusika na uchaguzi huo ambao ni wafanyakazi wa jiji, madiwani pamoja na waandishi wa habari.
Kwa  hisani  ya http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/26333-ccm-yakibwaga-chadema-mwanza

Linux & Drupal classes @ InCo Technologies T Ltd

Join our October classes in the following sessions

1. Linux EssentialsTshs 100,000/-
    Starts on 27 Oct 2012 and lasts for 6  days
2. Linux Certific., LPI Level I @ 250,000/- per module
     Starts on 15 Oct 2012 and lasts for 8 weeks
3. Building Web Applications using Drupal @ 200,000/-
     Starts on 19 Nov 2012 last for 5 weeks

Book your seat now by depositing at least one third of the fee. For inquiry send an email to training@incotechnologies.co.tz or call us through 0754 711 071

InCo Technologies T Ltd | "Honouring Your Dream"

KIBONZO.... Matumizi ya Teknolojia IBADANI.

Sasa, Ibada zitakuwa kama ifuatavyo.
MCHUNGAJI: Bwana asifiweeeee!
WAUMINI: Ameeeeeeeeeni!
MCHUNGAJI: Tafadhalini washarika sasa tuchukue iPad,tablet PC, simu na kindle zetu ili tufungue 1 Wakorintho
13:13. Pia washeni bluetooth zenu ilimuweze kupokea mahubiri. Mnaotumia facebook, twitter, BBM na Whatsapp mnaweza kuendelea kupokea mahubiri haya. Washarika mnaweza kutumia Wi-Fi ya kanisa kwa uhuru kabisa.

WAUMINI: Haleluuuuyaaaaaaaah!
MCHUNGAJI: Wapendwa washarika sasa ni wakati wa sadaka kwa hiyo kadri ya itakavyokupendeza kumtolea
Mungu unaweza kutumia credit ama debit card, pia unaweza
kutoa sadaka kwa njia ya MPesa, Tigopesa, Airtel money
ama ZPesa kupitia namba zinazoonekana kwenye skrini.
WAKATI WA MATANGAZO
KATIBU WA USHARIKA: Wapendwa washarika wiki hii kutakuwa na mikutano ya kiroho kupigia group letu la Facebook. Mada kuu itakuwa uponyaji wa kiroho kwenye ndoa. Washarika wote mnakaribishwa kushiriki.
Siku ya Alhamisi kutakuwa na mafundisho ya Biblia moja kwa moja kupitia Skype kuanzia saa moja jioni. Tafadhali msikose kushiriki. Pia mnaweza kuendelea kufuatilia ibada hii pamoja na mafundisho yote kutoka kwa mchungaji
kupitia akaunti yake ya Twitter.
Haleluyaaaaaah!
WAUMINI
: Ameeeeeen
MCHUNGAJI
: Bwana asifiweeeee!
WAUMINI: Ameeeeeeeeeni!

ZITTO Asema, Ubunge Sasa Basi.

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2015 badala yake anajipanga kuwania urais.Zitto alisema hayo jana alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliokuwa unafanyika maeneo ya Soko la Mwanga, mjini Kigoma.

Zaidi ya watu 200, ambao walihudhuria katika mjadala huo wa wazi walimuuliza maswali mbalimbali mbunge huyo, huku mmoja akigusia kuhusu tetesi za mara kwamba Zitto anataka kugombea urais katika uchaguzi ujao.“Nimefanya kazi kubwa katika kazi yangu ya ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni  mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka kumi.

“Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola,” alisema Zitto.“Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndio msimamo wangu.

“Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi.”
Atangaza kugombea urais
Katika hatua nyingine Zitto alisema ana mpango wa kuwania urais kupitia Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.“Kwanza nataka niwahakikishia watu wa Kigoma msiwe wanyonge…mna uwezo wa kutoa rais wa nchi hii,” Zitto alianza kujibu swali hilo na kuendelea.
 Hata hivyo Zitto alipoulizwa baadaye na Mwananchi kuwa mwaka 2015 atakuwa na miaka 39, hivyo kukosa sifa ya kugombea urais kwa mujibu wa katiba alijibu; “Nadhani nina uwezo wa kuwa rais, sidhani kama Katiba inaweza kumzuia mtu mwenye uwezo asigombee na ndio maana ninaamini kuwa kipengele cha kuwa na miaka 40 kitabadilishwa katika katiba mpya.”

“Nchi za Kidemokrasia lazima vyama vibadilishane utawala wa kuongoza nchi  kama ilivyo katika nchi za Ghana na Zambia. Tanzania inatakiwa kuiga mfano wa nchi hizo,” alisema Zitto
 Katika kukazia hilo, Zitto alisema anashangazwa na umaskini uliopo Tanzania wakati mwaka 1976 uchumi wake ulikuwa sawa na nchi ya Malaysia, lakini mpaka kufikia mwaka 2001, Malaysia ilipunguza idadi ya watu wanaoishi chini ya dola moja kutoka asilimia 56 mpaka kufikia asilimia tatu huku Tanzania ikipunguza kutoka  51 mpaka 46.
Katika hatua nyingine, Zitto alikana kuwa, Chadema ni chama cha udini, ukanda, ukabila  ila akasisitiza kuwa ni chama cha kitaifa.
 “Ndugu zangu naomba mnielewe, Chadema si chama cha ukabila, ukanda wala udini bali ni chama cha kitaifa. Hizo ni propaganda za wapinzani wetu,” alisema Zitto baada ya kuulizwa na mmoja wa washiriki kuhusu tuhuma za chama hicho kuwa cha Kikanda.

“CCM imewahi kudai CUF ni chama cha Waislamu, na sasa wanasema Chadema ni chama cha Wakristo, sasa wao CCM ni chama cha wapagani au cha watu gani?” Alihoji Zitto.
 Alisema ili kuthibitisha kuwa Chadema si chama cha Kikanda, matokeo ya urais wa mwaka 2010, Dk Wilbroad Slaa aliongoza dhidi ya wagombea urais wengine kwa kupata kura nyingi katika Jimbo la Manyovu mkoani Kigoma na hivyo kufanya kupata asilimia nyingi kuliko sehemu yoyote Tanzania.
Habari  kwa hisani ya http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/26305-zitto-ubunge-sasa-basi

Majina Ya Walioteuliwa CCM Haya Hapa...

HALMASHAURI Kuu ya CCM (Nec), imetangaza majina ya wagombea walioteuliwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho, huku ikionyesha kuwa uchaguzi huo utakuwa na mchuano mkali.Katika orodha iliyotolewa jana, baadhi ya makada wake maarufu akiwamo Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono na Salum Londa wametupwa.
Mchuano mkali unaonekana kuwapo kwenye nafasi ya ujumbe wa Nec Mkoa wa Manyara ambako Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye anachuana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk Mary Nagu.

Mchuano huo unatarajiwa kuwa mkali katika nafasi ya uenyekiti kwenye baadhi ya mikoa kutokana na kupitishwa kwa majina ya makada wake maarufu. Mwanza ni miongoni mwa mikoa hiyo kwani Nec imepitisha jina la Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Anthony Diallo ambaye atachuana na Clement Mabina anayetetea nafasi hiyo.
Makada hao watapata ushindani mkali kutoka kwa Zebedayo Athumani, Joseph Yaredi na Mashimba Hussein Mashimba.
Dar es Salaam nako kunatarajiwa kuwa na mchuano mkali kwani mwenyekiti wa sasa, John Guninita atachuana na Mkuu wa Kitengo cha Uchaguzi Makao Makuu ya CCM, Matson Chizzi na kada mwingine, Ramadhan Madabida. Godfrey Mwalusamba, Harold Adamson na Paul Laizer wanawania nafasi hiyo mkoani Arusha.
Vita nyingine kali ipo kwenye Jumuiya ya Wanawake wa Tanzania (UWT), ambako Mwenyekiti wa sasa, Sofia Simba ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto anachuana na Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango Malecela na Mbunge wa Viti Maalumu, Mayrose Majige.
Katika Jumuiya ya Wazazi, Mkono ambaye alikuwa akiwania nafasi hiyo ametupwa na kuwaacha Abdallah Bulembo, Martha Mlata na kada wa siku nyingi, John Barongo kuchuana.
Awali, Mkono alikatwa jina lake na Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo na kutangaza hali ya hatari akisema asipopitishwa patachimbika. Jina lake lilirejeshwa na Kamati ya Usalama na Maadili kabla ya kukatwa tena na Kamati Kuu.
Alipoulizwa jana kuhusu kuondolewa katika kinyang’anyiro hicho, Mkono alisema: “Nimekubaliana na uamuzi wa chama na nitaendelea kuwa mwanachama wa CCM. Nimelelewa na kukulia CCM na nitaendelea kubaki CCM nikiwa mwanachama mtiifu.”

Katika Jumuiya ya Vijana (UVCCM), mchuano mkali unaonekana kuwa katika nafasi ya makamu mwenyekiti kwani mmoja wa wagombea waliopitishwa, Paul Makonda anaaminika kuwa na nguvu kubwa kutoka katika kundi la wabunge na mawaziri wapambanaji wa ufisadi. Makonda anawania nafasi hiyo pamoja na Mboni Mhita na Ally Hapi.
Nafasi ya Mwenyekiti UVCCM inawaniwa na Sadifa Juma Khamis, Rashid Simai Msaraka na Lulu Mshamu Abdallah.
Waziri Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa atachuana na Dk Salash Toure na Nanai Kanina kwenye nafasi ya ujumbe wa Nec kupitia Wilaya ya Monduli.

Wagombea wa ‘kundi la kifo’
Vigogo kadhaa wamepitishwa kuwania nafasi 10 za Nec, wakiwamo baadhi ya mawaziri na viongozi wa juu wa chama hicho.
Miongoni mwao ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo David, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama.
Wengine ni Katibu wa Fedha na Uchumi CCM, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano, Stephen Wassira, Waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Vijana, Dk Fenela Mukangara na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela.
Kwa upande wa Zanzibar, nafasi 10 za Nec kupitia kapu zinawaniwa na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan.
Katika orodha hiyo wamo, Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi, Waziri wa zamani wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, Mohamed Seif Khatib, Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar, Omar Yussuf Mzee na Naibu Waziri wa Fedha wa zamani, Abdisalami Issa Khatib.

Familia ya Kikwete
Katika uteuzi huo wa wagombea, majina matatu ya wagombea kutoka katika familia ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete yamepitishwa.
Waliopitishwa ni pamoja na mkewe Salma Kikwete ambaye anakuwa mgombea pekee katika nafasi ya ujumbe wa Nec Lindi Mjini na Ridhiwan Kikwete ambaye pia ni mgombea pekee wa nafasi hiyo katika Wilaya ya Bagamoyo.
Mbali ya hao, Nec pia imepitisha jina la Mohamed Mrisho Kikwete kuwania nafasi ya uenyekiti wa Wilaya ya Bagamoyo.

Vigogo watemwa
Nec imewatema vigogo kadhaa, baadhi yao ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Azim Premji na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Vicky Nsilo-Swai ambaye alikuwa anagombea ujumbe wa Nec kupitia Wilaya ya Hai na kada wa siku nyingi, Salum Londa.
Pia wamo wabunge, Sarah Msafiri, Munde Tambwe, Deo Filikunjombe na Victor Mwambalaswa.Wengine waliotemwa ni Hussein Bashe na hasimu wake mkubwa kisiasa Dk Hamis Kigwangalla, Jamali Kassim, Anthony Mavunde na Emmanuel Nzungu, ambaye aliomba kugombea Uenyekiti Wilaya ya Ilemela, Mwanza. 
Mgeja chupuchupu
Mwenyekiti wa sasa wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja aliponea chupuchupu kutemwa baada ya Nec kurejesha jina lake kwenye orodha ya wagombea lililokuwa limeondolewa na vikao vya awali.Taarifa za kuondolewa jina la Mgeja zilivuja tangu juzi wakati kikao cha Kamati Kuu kilipoketi ikidaiwa ni kutokana na malumbano kati yake na Mbunge wa Kahama, James Lembeli.
Inadaiwa wakati wa kujadiliwa Mgeja, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alitoka kwenye kikao na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na kumwachia kiti Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa.Baada ya mjadala mrefu wa kumtetea Mgeja kwamba hakutendewa haki, Msekwa alifikia uamuzi wa kurejesha jina.“Baadhi ya waliomtetea ninaokumbuka ni Dk Makongoro Mahanga na Peter Serukamba, lakini wakati wa mjadala wa Mgeja, Mwenyekiti (Kikwete) na Nape walikwenda chemba, kiti akaachiwa Msekwa,” kilisema chanzo chetu.
Awali, kada mkongwe wa chama hicho, Kingunge Ngombale - Mwiru aliituhumu Kamati Kuu kwamba imevunja kanuni za uchaguzi kwa kuteua majina zaidi ya matatu kwenye nafasi moja.
Hata hivyo, inadaiwa Msekwa alimsomea kanuni moja baada ya nyingine zinazohusu uteuzi hali iliyoonyesha kama kumweka darasani na hatimaye ikabainika hakuna kanuni iliyovunjwa.Hoja hiyo ilitokana na baadhi ya mikoa kwenye nafasi moja kusimamisha wagombea zaidi ya watatu kama nafasi ya mwenyekiti mkoa wa Mwanza.
Hatua hiyo inadaiwa inalenga kuondoa matokeo ya kupanga kwa baadhi ya wagombea na kwamba, kwa hali hiyo mshindi hawezi kupatikana kwa mzunguko wa kwanza.
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba anadaiwa kushambulia mtandao uliokuwa umejipanga na kuweka wagombea wao hata kama hawana sifa.“Yule mzee (Makamba) amewachana-chana vibaya, anasema hapa tunasajili timu, kama majina hayafai yaondolewe,” kilidokeza chanzo na kuongeza kwamba hoja hiyo iliungwa mkono na kada mkongwe wa chama hicho, Mzee Peter Kisumo.
Taarifa kwa   hisani  ya  http://www.mwananchi.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/26279-vita-ccm.html

JK Awaapisha Maofisa Wakuu wa JKT na JWTZ

  Rais Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Devis Mwamunyange (kushoto) na maofisa wa Jeshi Luteni Jenerali Samuel Ndomba, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ (wa tatu kutoka kushoto) na Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga mkuu wa JKT walioapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga (kulia) kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) leo Ikulu jijini Dar es salaam.

HEPI BESDEI YA MDAU PETER MATARE GWESSO YAFANA.

 Mdau  GWESSO  akikata    keki    yake maalum  leo  hii  tarehe   26  September.
 Duu  kulishwa  raha , mbethideiwa  akionja keki    taratibu  toka kwa  Bi Isabella.
 Mr  Abdul  aka Baba  Hanifa   akimpongeza  GWESSO  kwa  ishara  ya  kumlisha  keki.
 Blogger  naye   kama  kawa  kama  dawa  kukiwa  na mnuso  sehemu  huwa  hachezi  mbali, akitabasamu kabla  ya  kulishwa  keki.
 Duu  hii  style  mpya  inaitwa  Double Double,   Bi  Rehema  Ndama  akilishwa keki  na  Gwesso.
Taratibu   Mrs  Erick Makoye  aka   Faith Shayo  naye  akilishwa  keki   na  GWESSO
Ukishangaa  ya  Musa  utaona  ya  ....,  Kumbe  keki    inapagawisha  namna  hii cheki  style  hiyo.

JINA JIPYA LA HUU UWANJA WA NDEGE MWANZA UKIKAMILIKA UKARABATI.

 Baada ya mapendekezo ya  kubadili  jina ,  serikali  ya Tanzania imeridhia kubadilishwa kwa jina la uwanja wa ndege wa Mwanza na sasa utaitwa uwanja wa kimataifa wa Serengeti au Serengeti international airport.
Kwa sasa utafanyika ukarabati mkubwa wenye mipango mingi ikiwemo kukuza utalii kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa , hiyo yote itafanikiwa kwa sababu uwanja ukikamilika itakuwa rahisi watalii kufika katika mbuga ya wanyama ya Serengeti wakitokea Mwanza.






MTIKILA Ashinda kesi ya Uchochezi

MWENYEKITI wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ameshinda kesi iliyofunguliwa na serikali, akidaiwa kuchapisha na kumiliki waraka wa uchochezi unaomkashifu Rais Jakaya Kikwete.
Hukumu ya kesi hiyo iliyovuta hisia za wengi nchini, ilitolewa jana na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Elvin Mugeta.
Katika kesi hiyo ya jinai iliyofunguliwa mwaka 2010, Hakimu Mgeta alianza kwa kuikumbusha mahakama kuwa mshtakiwa huyo alikuwa akikabiliwa na makosa mawili.
Mchungaji alikuwa akikabiliwa na makosa mawili.
La kwanza ni kuchapisha kusambaza waraka wa uchochezi kinyume na kifungu cha 32(1),(c) cha Sheria ya Magazeti ya mwaka 2002 na kosa la pili ni la kumiliki waraka huo kinyume na kifungu cha 32(2) cha sheria hiyo.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mugeta alisema Mtikila katika utetezi wake alikiri kuandaa na kuumiliki waraka huo uliotolewa mahakamani hapo kama kielezo cha tatu na jumla ya mashahidi wanne waliletwa na upande wa serikali.
Alisema wakati serikali ikileta mashahidi hao, Mchungaji Mtikila hakuleta shahidi hata mmoja na badala yake alijitetea mwenyewe kwa madai kuwa hakuona sababu ya kuwaleta mashahidi kwani kufanya hivyo ni kumaliza fedha na kupoteza muda wa mahakama.
Hakimu Mugeta alisema kabla ya kutoa hukumu hiyo, alijiuliza maswali kuwa je, ni kweli waraka huo ni wa uchochezi? Je, waraka huo ulileta madhara katika jamii? Je, waraka huo ulikuwa ukitaka kumpindua Rais Kikwete kinyume na sheria za nchi?
“Mimi nimeusoma waraka huo unaodaiwa na upande wa jamhuri kuwa ni uchochezi na nimebaini kuwa si wa uchochezi kwani Mtikila ni mwanasiasa, pia ni kiongozi wa dini na waraka ule ulikuwa umejaa maneno ya kidini ambayo ndani yake Mtikila alikuwa akiwataka Wakristo wenzake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 watumie haki yao ya msingi ya kumpigia kura mgombea ambaye ni Mkristo.
“Na kumng’oa madarakani Rais Kikwete kwa njia ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu si kosa la jinai.
“Mahakama hii kwa kauli moja imeona upande wa jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi unaoonyesha Mtikila alikuwa anataka Wakristo wamuondoe Rais Kikwete Ikulu kwa njia haramu.
“Pia upande wa jamhuri umeshindwa kuthibitisha kwamba kusambazwa kwa waraka huo kulileta madhara, na wameshindwa kuleta ushahidi unaoonyesha waumini wa dini ya Kikristo walishawishika na waraka huo na wakajaribu kumuondoa Rais Kikwete madarakani kwa njia haramu,” alisema Hakimu Mugeta.
Alisema mshtakiwa angeweza kukutwa na hatia kama ingethibitika kuwa alikuwa akitumia karata ya dini kuligawa taifa na kuongeza kuwa mahakama hiyo imejiridhisha kuwa waraka huo haukuibua chuki baina ya waumini wa dini ya Kiislamu na Kikristo na kwa sababu hiyo mahakama imemuona Mchungaji Mtikila hajatenda kosa la uchochezi.
Hakimu Mugeta alisisitiza kuwa hakuna madhara yaliyojitokeza katika taifa kupitia waraka huo na kwa sababu hiyo mahakama yake inamwachilia huru Mchungaji Mtikila.
Baada ya kuachiwa huru, Mtikila alisimama kizimbani na kupaza sauti akisema: “Haleluya, Haleyula… Kesi hii ni ya Mungu na hakuna binadamu yeyote anayeweza kushindana na Mungu.”
Aidha aliwataka Watanzania wakasome Bibilia, Waraka wa Pili wa Timotheo sura 4:2 ambao unasema: “Fanya kazi yako wewe mhubiri wa Injili; onya, karipia na kemea dhambi.”
Mtikila akasema alichokifanya katika waraka ule ni kukemea dhambi na kutangaza neno la Mungu, lakini cha kushangaza serikali ikamfungulia kesi hiyo.
Hii ni kesi ya 43 ya jinai katika zile ambazo Mchungaji Mtikila ameshafunguliwa na serikali tangu aanze kile anachokiita harakati za ukombizi wa Mtanganyika.
Kati ya kesi hizo, serikali ilishinda na kumfunga jela kwa kesi moja tu ya kutoa maneno ya uchochezi ambapo alisema Chama cha Mapinduzi (CCM), kilimuua aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Horace Kolimba.
Kabla ya hukumu ya jana, Mtikila aliwaambia waandishi wa habari nje ya mahakama kuwa angeibuka mshindi dhidi ya serikali katika kesi hiyo.
Hata hivyo wakati Mtikila akiendelea kushangilia ushindi, ghafla aliibuka mtu aliyejitambulisha kuwa mfanyabiashara, Gotem Ndunguru, akiwaamrisha askari wamkamate Mchungaji Mtikila kwa madai kuwa alikuwa na amri ya kumkamata iliyotolewa na Kituo cha Polisi cha Kimara, namba RB/10482/12 ambapo alidai Mtikila alimtishia kumuua kwa maneno.
Askari walishindwa kumkamata Mtikila kwa sababu alianza kumfokea askari mmoja wa cheo cha chini, akimwambia kwa ukali kwamba hana hadhi ya kumkamata kwani yeye ana hadhi ya kukamatwa na mwenye cheo cha mrakibu wa polisi.
“We askari, nani kakuhonga uje unifanyie fujo hapa? Kwa taarifa yako mimi najua sheria, wewe huna mamlaka ya kunikamata na huwezi kunikamata kihuni hivi… hata huyo bosi wako IGP Saidi Mwema kabla ya kunikamata ananipigia simu kwa adabu na mimi mwenyewe ndiye naenda polisi… sasa nakuambia hivi huna hadhi ya kunikamata,” alifoka Mtikila na kusababisha askari huyo kunywea.
Chanzo  kwa  hisani  ya http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=40916 

Semina ya Mwl C. Mwakasege - Viwanja vya Jangwani Dar es Salaam


Utata Wagubika ARV Bandia

UTATA umegubika kuwapo kwa dawa bandia za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARV), baada ya ripoti ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kutofautiana na maelezo ya wizara, kuhusu kiasi kilichosambazwa na madhara yake katika jamii.
Wakati Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ikisema haijajua kiasi halisi cha dawa hizo, lakini ikisisitiza kwamba athari zake ni kidogo, TFDA imeeleza kuwa makopo 1,360 yalibainika katika utafiti wake mkoani Mara kuwa yako mikononi mwa wagonjwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu, Regina Kikula Ijumaa, hadi kufikia Septemba 4, mwaka huu makopo 8,008 ya toleo namba OC.01.85 ya dawa hizo yalikuwa yamezuiwa. 
Taarifa ya TFDA
Taarifa ya jopo la wataalamu wa TFDA waliofanya ukaguzi katika baadhi ya hospitali na vituo vya afya mkoani Mara, inaonyesha kuwa zaidi ya makopo 1,360 yalishatolewa kwa wagonjwa.

Mtaalamu mmoja wa dawa aliliambia Mwananchi kuwa katika makopo hayo baadhi huwa na vidonge 30 na mengine 60.“Kopo lenye vidonge 60 hutumiwa na wagonjwa ambao humeza dawa hizo mara mbili kwa siku, asubuhi kimoja na jioni kimoja, lenye vidonge 30 hutumiwa na wagonjwa wanaomeza kidonge kimoja tu kwa siku,” alisema daktari huyo.

Ukaguzi wa TFDA, katika Hospitali ya Mkoa wa Mara ulibaini kwamba, dawa aina ya TT-VR30 zilizokuwapo katika hospitali hiyo zilikuwa zimeingizwa kutoka nje ya nchi.

Ulibaini pia kuwa, wagonjwa wamekuwa wakitumia dawa hiyo peke yake (monotherapy) kwa muda mrefu badala ya kuchanganywa na nyingine, hivyo kuwapo kwa uwezekano mkubwa wa virusi ya Ukimwi kujenga usugu. “Tulipokagua, tulibaini kuwapo kwa batch (toleo) tatu za dawa hiyo ambazo ni OB.15.85, OB.18.85 na OC.01.85, ambapo batch mbili za kwanza zote hazikuwa na matatizo, isipokuwa batch namba OC.01.85 ambayo ilikuwa na matatizo,” inaeleza sehemu ya ripoti hiyo ya TFDA.

Inaeleza kwamba, katika hati ya malipo ya kupelekwa kwa dawa hizo kutoka MSD, matoleo mawili ya kwanza yaani OB.15.85 na OB.18.85 pekee ndizo zilizoandikwa, toleo namba OC.O1.85 haikuandikwa, ingawa msimamizi wa bohari ya hospitali hiyo, aliwaeleza wataalamu wa TFDA kuwa dawa hizo zilifikishwa hapo Mei, mwaka huu.

“Katika kukagua dawa zilizokuwa ndani ya makopo hayo, tulibaini baadhi ya makopo yalikuwa na vidonge vyenye rangi mbili tofauti, wakati makopo mengine yalikuwa na vidonge vya njano kama aina ya Efavirenz,” inasema ripoti hiyo.Inafafanua kuwa, baadaye wataalamu hao waligundua kuwa vidonge vyenye rangi mbili ni aina ya NEVILAST-30, vilivyotengenezwa na Kiwanda cha Hetero Drugs cha India.

Inabainisha kwamba vidonge vya njano ni aina ya Efavirenz vilivyotengenezwa pia na Kiwanda cha Hetero Drugs, India, vyote vikiwa vimehifadhiwa katika makopo yenye alama ya TT-VR30.“Tulipolinganisha makopo ya dawa hizo, tulibaini kuwa makopo yaliyokuwa na vidonge vyenye rangi mbili, (NEVILAST-30) vidonge vyake vilikuwa katika kopo pana na lenye mfuniko mpana,” inaeleza ripoti hiyo na kuongeza:

“Vidonge vyenye rangi ya njano (efavirenz) vilihifadhiwa katika kopo dogo, jembamba na lenye mfuniko mdogo.”Kwa mujibu wa ripoti hiyo wataalamu hao walifanya ulinganisho huo kirahisi baada ya kufanya ukaguzi katika Kituo cha Afya Nyasho, kilichopo Musoma, ambacho hutumiwa kama kituo kikuu cha Manispaa kwa kusambazia dawa za kupunguza makali ya Ukimwi.

“Katika kituo hicho hakukuwa na dawa aina ya TT-VIR30, isipokuwa NEVILAST-30 na Efavirenz. Kulikuwa na mazingira yaliyoonyesha kuwa dawa hizo zilitoka MSD kama baadhi ya boksi za dawa zilivyoandikwa, kuonyesha kuwa dawa hizo zilikuwa zinakwenda MSD Mwanza na baadaye mkoani Mara,” inaeleza.Inabainisha kuwa, jumla ya dawa zilizobainika kuwa na matatizo hayo na ambazo zilizuiliwa kutumika katika hospitali hiyo zilikuwa katika makopo 216, wakati makopo 800 tayari dawa zake zilishagawiwa kwa wagonjwa.

“Baada ya ukaguzi, tuliandika taarifa ya yale tuliyoyabaini, kuchukua sampuli na kivuli cha invoice (hati ya malipo) ya MSD kilichukuliwa. … Tulielekea wilayani Tarime na kufanya ukaguzi katika Hospitali ya Wilaya,”  sehemu ya taarifa hiyo inaeleza.Inaweka wazi kuwa katika ukaguzi huo walibaini kuwapo kwa dawa aina ya TT-VIR30 inayotengenezwa na Kiwanda cha TPI cha mjini Arusha.

Wataalamu hao pia walibaini kuwapo kwa toleo la nne la dawa aina ya TT-VIR30, la kwanza likiwa namba OB.03.85, la pili OB.06.85, la tatu 0B.18.85 na nne OC.01.85, ambalo lilibainika kuwa na matatizo. Wataalamu hao walipochunguza vidonge vilivyokuwa ndani ya makopo hayo walibaini kuwa vidonge vyote vilikuwa vyenye rangi mbili pekee na hakukuwa na vidonge aina ya efavirenz vilivyoonekana katika makopo hayo. Ripoti hiyo inaweka wazi kuwa, vidonge vingi kati ya hivyo vilikuwa vimeharibika na kuota ukungu na kwamba makopo yote yaliyokuwa yametumika yalikuwa ya dawa aina ya NEVILAST-30.

Inasema kuwa, taarifa ya hospitali hiyo inaonyesha kuwa dawa hizo zilifika hapo kutoka MSD, Mei 8, mwaka huu. "Katika invoice ya MSD batch moja tu yaani OB.15.85 ndiyo iliyoandikwa. Batch nyingine tatu haikujulikana kwa nini hazikuandikwa,” ripoti hiyo inaeleza.

Inafafanua kuwa, makopo yaliyobainika kuwa na matatizo katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime ni 86 na haijulikani ni mangapi yaliyotolewa kwa wagonjwa.Ili kujiridhisha na kuwapo kwa dawa hiyo katika wilaya nyingine, ripoti hiyo inaeleza kwamba wataalamu hao walifanya mawasiliano na mtunza stoo wa Hospitali Teule ya Nyerere wilayani Serengeti na kwamba taarifa walizopewa zilionyesha kuwapo kwa dawa aina ya TT-VR30 katika hospitali hiyo.

Kuhusu dawa toleo namba OC.01.85 katika hospitali hiyo ilielezwa kuwa na matatizo na kwamba msimamizi huyo alipofungua kopo moja moja, alibaini makopo yote yalikuwa na vidonge aina ya NEVILAST-30 vyenye rangi mbili.Mtunza stoo huyo aliwaambia wataalamu wa TFDA kuwa dawa hizo zilipelekwa hospitalini hapo Mei 8, mwaka huu.

Kwa mujibu wa TFDA katika hospitali hiyo ya Nyerere, kulikuwa na makopo 288 ya dawa hizo na kwamba katika Wilaya ya Rorya, Hospitali ya Shirati pia kulikuwa na dawa hizo zilizopokewa kutoka Hospitali Teule ya Wilaya ya Bunda.

“Mei walipokea makopo 596 na kati yake yamebaki 36 tu, walieleza kuwa hawakuwa na invoice ya MSD kwa kuwa dawa hizo hawakupelekewa na MSD moja kwa moja, bali walizipata kutoka Bunda,” inasema ripoti ya TFDA ikiongeza: “Jambo la kusikitisha ni kuwa, baadhi ya makopo yana aina ya Efavirenz ambazo hupaswa kutumiwa mara moja, tena nyakati za usiku tu. Hivyo wagonjwa waliotumia dawa hizo wamekuwa wakitumia dawa moja (monotherapy) kwa muda mrefu na hivyo kuna uwezekano mkubwa wa virusi kujenga usugu.” Inasema kuwa, katika ukaguzi waliofanya mkoani Mara, wataalamu hao walibaini kuwapo kwa dawa hizo bandia kwa kiwango kikubwa.“Vilevile kuna taarifa zinazoonyesha kuwa dawa hizo zilitoka MSD Makao Makuu (Dar es Salaam) na Ofisi ya Kanda ya Ziwa,” inasema taarifa hiyo.

Wataalamu hao katika taarifa yao hiyo, walishauri ukaguzi ufanyike katika kanda nyingine na kwamba lengo liwe kuangalia hospitali na vituo vya afya vilivyogawiwa dawa za ARVs mwezi Mei.

Kauli ya Wizara
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeeleza kuwa haijapata kiwango halisi cha dawa hizo bandia ambacho tayari kilikuwa kimeshasambazwa kwa watumiaji.Kaimu Katibu Mkuu wa wizara ya hiyo, Regina Kikula, alipoulizwa na Mwananchi kuhusu kiwango cha dawa hizo ambacho kilikuwa kimeshasambazwa, alisema kuwa bado wanafanya uchambuzi na kwamba hakuna taarifa rasmi.

Hata hivyo Kikula alisisitiza kwamba wizara bado inaendelea kulifuatilia suala hilo kwa karibu na kwamba baada ya kukamilisha uchunguzi itatoa taarifa kamili.“Baada ya kupata taarifa hizo, tuliwatuma watu wetu katika mikoa yote mitatu ambako taarifa za kuwapo kwa dawa hizo zilipatikana (Mara, Tanga na Dar es Salaam), na hicho ndicho kiwango tulichokipata, lakini bado kuna taarifa hatujazipata vizuri,” alisema Kikula na kuongeza:

"Naomba tupewe muda tuhitimishe uchunguzi wetu kisha tutatoa taarifa kamili, lakini nawahakikishia wananchi waendelee kutumia tu, hali ni salama kwa kuwa dawa hizo tayari zimeshazuiliwa na kuondolewa."Kuhusu wahusika wa dawa hizo alisisitiza kuwa baada ya kukamilika kwa uchunguzi, wale watakaobainika kuhusika kwa namna moja ama nyingine kuingiza dawa hizo sokoni, watachukuliwa hatua za kisheria.
Habari  kwa  hisani  http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/26210-utata-wagubika-arv-bandia

KIBONZO...

Kupenda ni GHARAMA   ni MZIGO kupenda ni RAHA tena ni KARAHA pia ni VITA KALI.
 

SITA: Uchaguzi Ndani ya CCM Umevurugika

WAZIRI  Samuel Sitta
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema kuwa chaguzi zinazoendelea ndani ya CCM zimevurugika kwa kuwa mafisadi wameingilia na kupachika watu wao kwa lengo la kulinda masilahi yao. 

Sitta alisema hayo jana mjini hapa katika mahafali ya 11 ya Shule ya Msingi Kwema yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Shule ya Sekondari Kwema. Alisema watu waliojitokeza kugombea ni mapandikizi na vibaraka wa mafisadi hao. "Hivi karibuni tumepata aibu kubwa ndani ya chama chetu, wakati chaguzi zetu zikiendelea viongozi wamepitisha vipaza sauti vya mafisadi, kazi yao kubwa ni kulinda masilahi ya mabwana zao na kuwafurahisha," alisema na kuongeza: "Wameajiriwa kwa lengo la kupiga kelele, kupiga vijembe, kuwapamba wafalme wao ambao wamefanikisha kuwa wanapata madaraka hayo, lakini kubwa zaidi ni kuwa vibaraka." 

Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki alisema lengo kubwa la mafisadi hao ni kuhakikisha wanashika kila sehemu ya nchi ili iwe rahisi kwao kuendelea kutafuna rasilimali za nchi kwa kupitia watu wao. Alienda mbali zaidi na kutoa mfano wa miaka ya zamani ambapo nchi za Uingereza na Ufaransa kulikuwa na wafalme ambao walikuwa wakiwaajiri watu ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kumchekesha mfalme huyo hata kama atakuwa amekosea. 

"Wachekeshaji wa mfalme wao wanawajibika kwa mfalme, kumsifia, kuremba kupiga vijembe, kuwa vibaraka, kujipendekeza, kumpamba, lakini kubwa zaidi ni kumchekesha mfalme hata kama amefanya mabaya,” alisema. Sitta alisema wachekeshaji hawana aibu kwani lengo lao ni kuhakikisha kuwa mfalme anafurahi kwa kila kitu hata siku akitembea uchi wao wanasema mfalme umependeza na kanzu yako inang'aa dhahabu. Alisema kuwa hali inazidi kuwa mbaya zaidi pale watu hao ambao ni vibaraka wanapojivunia kuwa vibaraka wa watu fulani huku wakipita na kujisifu usiku na mchana wakiwatambia wajumbe. 

Waziri huyo alisema umefika wakati wa chama hicho kuzaliwa upya vinginevyo kitaendelea kupata upinzani hata kutoka katika vyama vidogo. Hata hivyo, Waziri huyo alisema ataendelea kusema na wala hataogopa kitu chochote na atakayenuna na anune kwani yeye ni 'Chuma cha Pua' kwa kuwa anaamini anasimamia katika ukweli. "Ndiyo maana wengine nikisema huwa wananuna, wananuna kwa sababu hawawatendei haki Watanzania. Nchi imejaa mali na rasilmali, lakini zinatumiwa na watu wachache wenye uchu badala ya kuzitumia sote," alisema na kuongeza: "Mimi ni msemakweli ndiyo maana kule kwetu Urambo wananiita 'Chuma cha Pua.' Watu wengine wanasema nailaumu Serikali wakati mimi nipo serikalini na kwamba hiyo ni aibu... Sasa aibu ipo wapi? Hapa mimi nipo ndani ya Serikali lazima niseme vitu hivi kamwe siwezi kunyamaza na kuacha mambo yakiharibika." 

 Sitta alilaani tabia ya baadhi ya viongozi wa Serikali wanaonyamazia maovu kwa kuwa tu wanaogopa kuonekana wabaya ndani ya jamii. Alisema viongozi wengine wamekuwa wanafiki kwa kuwa wako ndani ya Serikali na mambo yanaharibika wananyamaza hivyo nao kuwa kama wachekeshaji wa mfalme. Alisema watu wanatumia vibaya madaraka, kuna watu wazima wanafikiri kwa kutumia matumbo yao badala ya akili wakati mwingine wanajisahau na kuwa na matumbo makubwa mpaka yanawashinda. Aliwataka watu wote wanaohusika kuleta viongozi katika chaguzi hizo watumie fursa hiyo kuweka viongozi bora na si bora viongozi ambao wana masilahi yao binafsi. 

Wakati hali katika chaguzi hizi zikienda ovyo, Waziri Sitta alisema pia kuwa amepata fununu mafisadi hao wanafanya kila njia kuhakikisha wanaweka vibaraka wao katika uongozi wa wilaya hiyo ili kuhakiksha wanaendelea kunufaika na migodi iliyopo katika wilaya hiyo. "Nimepata taarifa kuwa eti umeme unapatikana katika migodi ambayo inazunguka wilaya hii saa 24, lakini cha ajabu wananchi hawafaidiki na umeme huu. Hii inamaanisha nini hasa? Yaani wawekezaji ni bora sana kuliko wananchi? alihoji Sitta. Mahafali hayo pia yalihudhuriwa na Mbunge wa jimbo hilo, James Lembeli ambaye alisema shule hiyo imeujengea sifa mji wa Kahama kwa kuwa mwaka jana ilikuwa ya pili kitaifa na kutoa wanafunzi bora watatu katika 10 bora ambao walishika nafasi ya kwanza, tatu na ya nne.
   
Lembeni ambaye ndiye aliyeonyesha wazi kuanza kuchochea moto huo wa Sitta alisema kuwa wahitimu wa shule hiyo ndio wanaohitajika katika taifa la Tanzania kwa kuwa wamekuzwa katika misingi ya kutokupenda rushwa, kwani hata kujiunga na shule hiyo inahitaji uadilifu wa hali ya juu. Mkurugenzi wa Shule hiyo, Pauline Mathayo alisema hata siku moja hawezi kuruhusu vitendo vya kifisadi katika shule yake kwani anaamini elimu ikitumika vibaya inaweza kuzalisha watu hatari sana katika taifa. "Wote ni mashuhuda, sasa wizi wa benki kwa njia ya mtandao umezidi kuongezeka yote hii inatokana na kutumia elimu vibaya,"alisisitiza Mathayo.
Chanzo  gazeti  la  Mwananchi


EPL RESULTS HIGHLIGHTS OVER THE WEEKEND

Chelsea   1   Stock  City   0




Man  U   2        Liverpool 1


Arsenal  1    Man City 1

More   results    http://www.premierleague.com/en-gb/matchday/results.html

Kimenuka ....Yanga wamtimua Kocha Mkuu.

Fukuza fukuza ya klabu ya Yanga iliyoanza leo mchana baada ya mkutano wa wajumbe wa kamati ya utendaji uliofanyika leo katika makao makuu ya klabu imeendelea imemkumbuka kocha mkuu wa klabu hiyo Mbelgiji Tom Saintfiet.

Taarifa za uhakika kutoka kwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga ni kwamba  uongozi wa timu hiyo umefikia maamuzi ya kumtimua kazi kocha huyo aliyeajiriwa miezi mitatu iliyopita kutokana na kutofautiana sera za namna ya kuiendesha klabu na uongozi wa juu wa mabingwa hao wa Afrika mashariki na kati.

Mchana leo kamati ya utendaji ilisimamisha ajira za viongozi waajiriwa wote wa klabu hiyo akiwemo katibu mkuu Celestine Mwesigwa na msemaji Luis Sendeu huku ikitoa onyo kwa kocha Saintfiet kwa tabia yake ya kuongea na waandishi wa habari bila mpangilio wa klabu. Lakini baada ya taarifa hizo kutoka usiku wa leo kocha huyo akaonekana akiongea kwenye television mojawapo nchini akizungumzia mambo mbalimbali kuihusu Yanga.

Kwa mujibu wa Sanga anasema kwamba sakata lote la jinsi kocha huyo alivyopoteza kazi yake litatolewa ufafanuzi hapo kesho.

Wakati huo huo aliyekuwa katibu mkuu wa Yanga kabla ya Mwesigwa, Lawrence Mwalusako amepewa jukumu la kukaimu nafasi hiyo ya ukatibu mkuu wa Yanga kwa muda, wakati mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Seikolojo Chambua amekabidhiwa majukumu ya kuwa meneja wa timu hiyo akichukua nafasi ya Hafidh Salehe ambaye nae aliondolewa leo mchana.

Nafasi ya usemaji wa Yanga mpaka sasa imekuwa kitendawili, tetesi zinasema kuwa mtangazaji wa Clouds FM NA Clouds TV Abdul Mohamed na Mwanahabari Mahmoud Zubeiry mmojawapo anaweza kula shavu la kumrithi Sendeu
Taarifa  kwa  hisani  ya  Blog  ya  Shaffih 


 YANGA   YAICHEZESHA  KWATA  JKT  RUVU   4 -1  .......


Wachezaji Hamis Kiiza wa Yanga (kushoto), akiwania mpira na Ally Khan wa JKT Ruvu wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo. Yanga ikiwa na kocha wake msaidizi fred minziro imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-1 mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam.
Katika dakika kumi za mwisho wapenzi wa yanga walijikuta wakiomba mchezo umalizike baada ya jkt ruvu kucheza mchezo mkali. Wapenzi wa simba walionekana kushangilia hali hiyo ambayo hata hivyo matokeo yakawa 4-1.

Katika mchezo wa chamazi azam imeibuka na ushindi wa bao 1-0. Bao la azam limepatikana dakika ya 26 ya mchezo kupitia kwa kipre tchetche.
Cledo mwaipopo ameipatia jkt ruvu bao moja baada ya kazi nzuri ya omar changa na sospeter manyasi.
  Yanga imepata bao la nne kupitia kwa didier kavumbangu baada ya kipa jkt ruvu kuutema mpira.
 dakika ya 52 simon msuva aliipatia yanga bao la tatu baada ya kuambaa ambaaa na mpira na kupachika wavuni. mapumziko yanga imetoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-0.

 Bao la kwanza limepatikana dakika ya 4 ya mchezo kupitia kwa nadir haroub canavaro' baada ya kazi nzuri ya haruna niyonzima na athuman idd chuji
Dakika 31 yanga ilipata bao la pili kupitia kwa

didier kavumbagu akimalizia chuji. Katika kipindi cha kwanza yanga iliweza kutawala mchezo kwa kufanya mashambulizi mengi katika lango la jkt ruvu.

 Kwa upande wa jkt ikitumia wachezaji wake sospeter manyasi na omar changa walishindwa kufanya makeke makali hivyo mipira mingi kutoka nje.

  Kesho kuna mechi tatu ambapo mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara msimu uliopita simba itavaana na Ruvu shootingStars mchezo utakaofanyika kwenye uwanja wa taifa dar es salaam. 
Mchezo mwingine utafanyika kwenye uwanja wa chamazi utazikutanisha african lyon dhidi ya tanzania prisons na mechi nyingine itakukuwa kwenye uwanja mkwakwani mkoani tanga mgambo jkt ikiwakaribisha. Kagera sugar. Kilatimu inahitaji pointi tatu ili iweze kukaa sawa katika msimamo wa ligi kuu.

JK Asema Sijamwuzia Kigamboni Rais Bush

 Rais  Dkt Kikwete  jana    aliweka jiwe la msingi katika   mradi  wa  ujenzi  wa  Daraja  la  Kigamboni    unaofadhiliwa   kwa pamoja kati  ya  serikali  ya  Tanzania     na  mfuko wa hifadhi ya Taifa   NSSF , akiweka  jiwe la  msingi   Rais  alikanusha  tuhuma za  kumwuzia  Rais  wa  zamani wa Marekani   G . Bush   eneo la  Kigamboni   na  akiziita  tuhuma  hizo  kuwa ni  mbinu   chafu  za  kisiasa, pichani   
Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli akimpa maelezo Raid Dtk.Jakaya Mrisho Kikwete juu ya Ujenzi wa Daraja la Kigamboni wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa Daraja hilo ulofanyika Kurasini jijini Dar ea Salaam



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akiongea na Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni uliofanyika huko Kurasini jijini Dar es Salaam  jana chana.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadik 

Meneja  mradi wa daraja  la  Kigamboni  Eng: Karim Mataka akimwonyesha  Rais  picha  ya  daraja  linalojengwa  kwa  ushirikianao na  Serikali  ya  Tanzania   na  mfuko  wa  hifadhi  ya  taifa wa  NSSF

Kibonzo...


UEFA Champions League ; Chelsea 2 Juventus 2

Chelsea    Vs    Juventus 



Man   U  Vs    Galatasaray
  
Barcelona  Vs   Spartak

 
UEFA   Champions   League   Results
FTBarcelonaBarcelona3 - 2Spartak M. Spartak Moscow
FTBayern MunichBayern Munich2 - 1Valencia Valencia
FTCelticCeltic0 - 0Benfica Benfica
FTChelseaChelsea2 - 2Juventus Juventus
FTLilleLille1 - 3BATE Borisov BATE Borisov
FTManchester UnitedMan Utd1 - 0Galatasaray Galatasaray
FTShakhtar DonetskShakhtar Donetsk2 - 0FC Nordsjælland FC Nordsjælland
FTSporting BragaSporting Braga0 - 2CFR Cluj CFR Cluj

© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top