Social Icons

Loading...

Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii - Viwanja vya Mwl Nyerere Dar Trade Fair 2012

Mwonekano  wa    Banda  la  Wizara   ya  maliasili    na  utalii   katika  maonesho  ya  36  ya  biashara  ya  kimataifa  Dar  es Salaam  mwaka  huu.

Hapa  ni  mapokezi.








UCC kuendesha mafunzo haya kuanzia July 2012


Breaking Newsssss!!!!Vurugu Kubwa zatokea Tegeta

Kumekuwa na hali ya taharuki katika eneo la Tegeta, Namanga karibu na kituo cha Mafuta cha Big Bon jijini Dar es salaam baada ya wananchi wenye hasira kuanza kurushiana mawe na Mapanga na watu waliotumwa kubomoa Vibanda vilivyo katika eneo hilo.Katika tukio hilo watu Wawili wamejeruhiwa vibaya na wamekimbizwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya matibabu zaidi.Kwa mujibu wa Kamanda KENYELA kikundi cha watu kilifika katika eneo hilo na kuanza kubomoa Vibanda vilivyo katika eneo hilo la Namanga hali iliyowashtua wananchi wa eneo hilo na kisha kuanza kurushiana Nawe na Mapanga na kikundi hicho cha watu.Hata hivyo watu Wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa huo wa Kinondoni kwa mahojiano zaidi kama wana uhalalali wa kubomoa Vibanda hivyo na wametumwa na nani.

Dr: Fenela apata ajali ya gari akielekea Mwanza

Dr: Fenella   Mukangara
Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni Dokta FENELLA MUKANGARA(pichani) amepata ajali ya gari katika Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora akiwa njiani kwenda Mkoani Mwanza kikazi.Habari kutoka Wilayani Nzega zinasema kwamba ajali hiyo imetokea leo asubuhi wakati Waziri huyo akiwa njiani akitokea Dodoma kwenda Mkoani Mwanza kuzindua Mashindano ya Vishale.Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kwamba gari aliyokuwa amepanda Waziri MUKANGARA akiwa na Msaidizi wake imepinduka mara Tatu na inadaiwa kuwa Waziri huyo ameumia Mguu wa kushoto na amekimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega kwa ajili ya matibabu zaidi.
Chanzo:  Uhuru FM.

Chenji ya Rada itaondoa tatizo hili ?



============================================================

Super Mario reduced Germany’s reputation to ashes with a sensational double…

The Manchester City forward  Mario  Baloteli  scored with a 20th minute header and powered in his second 16 minutes later from 20 yards to set up a final showdown with Spain in Kiev on Sunday.
This was the best we have ever seen of Balotelli — and the Germans could not handle him.
Where Italy had failed to take their chances in the quarter-final win against England they were on target this time.They had a late scare when midfielder Mesut Ozil netted a penalty in added time but it was too late for a dramatic comeback.Many had expected a German victory but history was on Italy’s side.
The  First  Goal....

 The   Second Goal....  Fantastic...
Ozil  Penalt.....
 

Waziri Mkuu asitisha kutoa tamko juu ya mgomo wa Madaktari

Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametangaza kusitisha Serikali kutoa tamko lake kuhusu mgomo wa madaktari, ambao ulitakiwa kutolewa leo kama alivyoahidi jana Bungeni.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni na Waziri Mkuu, Pinda, alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe, aliyetaka kujua Serikali ina mipango gani ya dharula ya kuumaliza mgomo huo.

Alisema kwa hivi sasa, Serikali imechukua dharula, kwa kuwaita madaktari wasitaafu kwenda kwenye baadhi ya Hospitali za Serikali, kushika nafasi maeneo ambayo madaktari waliogoma.

Vilevile Serikali imewataka wananchi waende kuhudumiwa kwenye hospitali za Jeshi, ikiwemo Lugalo.

Pinda ameseama kuwa hata yeye alipopokea taarifa kuwa Dk. Ulimboka ametekwa na kupigwa alisikitika sana, na anamuombea apone haraka ili waendelee na suluhisho la mgomo huo wa madakatari.

Alisema kuwa amemuagiza, Waziri wa Mambo ya ndani kuunda jopo la wataalamu kuchunguza kwa haraka kuhusu tukio hilo. 

Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa kuanza leo - TANTRADE yatangaza viingilio





Mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania ( TanTrade) imetangaza viingilio vipya vya watu na magari katika maonyesho ya kimataifa ya Dar es salaam, (DITF) yatakayoanza   leo  tarehe 28 ya mwezi Juni hadi tarehe 8 mwezi ujao.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mdhamini rasmi wa mawasiliano wa maonyesho hayo Vodacom Tanzania, Tantrade imetangaza malipo ya Shilingi elfu 2500 kwa watu mzima na shillingi 500 kwa watoto kila siku isipokuwa siku maalum ya tarehe 7 ambapo viingiio vitakuwa shilingi 3000 kwa watu wazima na watoto shilingi 1000. Tiketi za kupaki magari madogo kwa siku ni 4000/- ma maroli ni 40000/-
  Kwa watakao hudhuria maonyesho hayo na magari madogo watatakiwa kununua tiketi kwa shilingi 4000, kama ambavyo mchanganuo wa malipo unavyobainisha malipo ya huduma nyingine zikiwemo za kupaki magari kama malori na magari makubwa pamoja na huduma nyingine.

Malipo ya ada binafsi.

1. Kwa siku - watu wazima (siku za kawaida) – 2,500/-
2. Kwa siku- watoto (siku za kawaida) – 500/-
3. Kwa siku – watu wazima (siku ya SabaSaba) – 3,000/-
4. kwa siku – Watoto (siku ya SabaSaba) – 1,000/-
5. malipo kwa kipindi chote cha maonyesho - Beji kwa wahusika wa maonyesho - 20,000/-
6. Beji kwa wahusika wa maonyesho (maeneo) – 3,000/-

Tiketi za uegeshaji magari.

1. Kwa siku (magari madogo) - 4,000/-
2. kwa kipindi chote cha maonyesho – 30,000/-
3. Malipo kwa pamoja – 200,000/-
4. Tiketi za maegesho maalum – 400,000/-
5. Maroli na magari makubwa – 500,000/-
6. Malipo ya kuegesha magari nje ya viwanja vya saba saba – 1,500/-
Maonyesho ya kimataifa ya Dar es salaam ni maonyesho pekee yanayoongoza katika huduma za masoko Tanzania, maonyesho hayo yanayodumu kwa siku kumi, huvutia watazamaji zaidi ya laki tatu na nusu na kutoa fursa kwa makampuni kuonyesha bidhaa zao na wanaohudhuria kupata nafasi ya kuuliza maswali na kulinganisha ubora wa bidhaaa kadha wa kadha.

Ronaldo call makes Fabregas spot king Portugal 0 Spain 0 (aet, Spain win 4-2 on pens) - Qualify for Final EURO 2012


Kamanda Kova azungumzia tukio la kutekwa Dr Ulimboka


Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la utekaji nyara na kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari  Dr. Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.

Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezo kuwa msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo.


Askofu Emanuel Lazaro wa TAG afungua kongamano la udhihirisho - Living Water Centre -KAWE




 Bishop Emmanuel Lazaro aliyekuwa Askofu Mkuu wa Tanzania Assemblies Of God kwa zaidi ya Miaka 26 amefungua Kongamano la Udhihirisho siku ya Jana Katika Kanisa la Living Water Centre  (LWC)  almaarufu kama "Makuti Kawe".

Semina hiyo iliyoanza siku ya Jana Mpaka Jumapili itakuwa na Wanenaji kutoka Ndani na Nje ya nchi ya Tanzania chini ya Mchungaji Mwenyeji wa Mahali hapo, Apostle Onesmo Ndegi na Apostle Lilian Ndegi.

Watu Wote Mnakaribishwa katika Semina hiyo inayoendelea leo kuanzia Saa 3 Asubuhi Mpaka jioni kila siku Mpaka siku ya Jumapili  tarehe 01 July 2012, Njoo uone Udhihirisho wa Nguvu za Mungu Kupitia neno lake.



Blogger alasiri hii akiwa na wadau wa UCC tawi la Mbezi Beach

Meneja  wa  Tawi  la  UCC  Mbezi  Beach  Mr  Antony  Karokola



Kutoka  kushoto  ni   Blogger ,Audax  Mujuni,Diana  Akyoo,  Elizabeth Mawi, Antony  Karokola, Nyamama  Machumu, Joyce  Liwa , Omary  Mdakama  ,  Juma  Mwita 




 Hapa ni   mapokezi , kwa  mbali  anaonekana Ms  Diana Akyoo  akiwa  katika  majukumu   yake  ya  kila  siku  tawini.

Hii  ni  office  ya  mameneja  wasaidizi   ,  anaonekana  Ms   Nyanyama  Machumu  na  kwa  mbali  ni   Audax Mujuni   wakichapa  kazi  kama  kawaida.

Breaking News !!! Dr Ulimboka atekwa, aokotwa akiwa mahututi

Dr  Ulimboka  akiwa katika  moja  ya  mikutano na  madaktari wenzake. 

Taarifa iliyonifikia hivi punde ni kuwa jemedari Dr. Ulimboka  Stiven  ametekwa majira ya saa sita usiku  jana na watu watatu waliokuwa na silaha za moto na kumpeleka kusikojulikana! Inasemekana alipigiwa simu na jamaa mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la 'Abeid' ambaye tangu mwanzo amekuwa akiwasiliana naye na kujiita afisa wa serikali na kudai kuwa alitaka aonane naye face to face kwa ajili ya reconciliation.
Taarifa zimekwisha fikishwa polisi na sehemu zingine kwa ajili ya ufuatiliaji

Tizama  picha

Jakob Michelsen atambulishwa rasmi kuwa Kocha wa Timu ya Vijana Tanzania

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtambulisha rasmi   jana  tarehe 26 June  2012   mbele ya waandishi wa habari kocha mpya wa timu za Taifa za vijana, Jakob Michelsen kutoka Denmark ambaye amechukua nafasi ya Kim Poulsen ambaye hivi sasa anainoa Taifa Stars.
 
Michelsen ambaye amepewa mkataba wa mwaka mmoja alitambulishwa na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah na kusema falsafa yake ni kama ile ya Poulsen ya kumiliki mpira na kushambulia muda wote wa mchezo.
 
Kabla ya kuja Tanzania, Michelsen alikuwa kocha wa timu ya daraja la kwanza ya Hobro IK ya Denmark. Ana leseni A ya ukocha kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA), leseni ya ukocha wa vijana kutoka Chama cha Mpira wa Miguu cha Denmark (DBU).
 
Moja ya mafanikio yake ni kuipa ubingwa wa Denmark, timu ya Skovbakken kwenye ligi ya timu zenye umri chini ya miaka 18. Ubingwa huo aliupata msimu wa 2005/2006.


TFF KUZAWADIA WAPIGA PICHA COPA COCA-COLA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litawazawadia wapiga picha za magazetini watakaoripoti mashindano ya Copa Coca-Cola 2012 ngazi ya Taifa yanayoendelea kwenye mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
 
Mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Coca-Cola na kushirikisha mikoa 28 yanafanyika viwanja vya Tanganyika Packers, Kumbukumbu ya Karume mkoani Dar es Salaam, na viwanja vya Tamco na Nyumbu mkoani.
 
Zawadi ya sh. 250,000 itatolewa kwa picha bora katika maeneo matatu; action picture, fair play picture na mpiga picha ambaye ameripoti matukio mengi ya mashindano hayo yanayoshirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 17.
 
Washiriki wanatakiwa kuwasilisha picha zao zilizotumika (cuttings) ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
 
NGORONGORO HEROES KUJIPIMA KWA MISRI, RWANDA
Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) itacheza mechi nne za kirafiki na timu za Misri na Rwanda kabla ya kuivaa Nigeria kwenye mashindano ya Afrika.
 
Ngorongoro Heroes ambayo kwa mara ya kwanza itakuwa chini ya kocha mpya Jakob Michelsen itaanza kwa kucheza mechi mbili za Misri zitakazofanyika Julai 3 na 5 mwaka huu, na baadaye Julai 14 na 16 mwaka huu dhidi ya Rwanda.
 
Mechi zote zitachezwa nchini, na kama ilivyo Ngorongoro Heroes, Misri na Rwanda nazo ziko kwenye kinyang’anyiro cha kusaka tiketi za kucheza Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 zitakazofanyika mwakani nchini Algeria.
 
Katika raundi ya kwanza, Ngorongoro Heroes iliitoa Sudan ambapo katika raundi ya pili imepangiwa Nigeria, na mechi ya kwanza itafanyika jijini Dar es Salaam, Julai 29 mwaka huu. Timu hizo zitarudiana wiki mbili baadaye nchini Nigeria.
 
Iwapo Ngorongoro Heroes itafanikiwa kuitoa Nigeria, katika raundi ya mwisho itacheza na mshindi kati ya Congo Brazzaville na Afrika Kusini.
 
MABINGWA COPA WALALA KWA RUVUMA
Ruvuma imeanza vizuri michuano ya Copa Coca-Cola baada ya kuwafunga mabingwa watetezi Kigoma mabao 2-0 katika mchezo wa kundi A uliofanyika leo asubuhi (Juni 26 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
 
Kigoma ambayo iliifunga Lindi mabao 2-0 katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa juzi, ilishindwa kufua dafu mbele ya Ruvuma na kuruhusu bao katika kila kipindi.
 
Mabao yote ya washindi yalifungwa na mshambuliaji Edward Songo. Mshambuliaji huyo alifunga bao la kwanza dakika ya 34 wakati la pili alilipachika dakika ya 84.
 
Katika mechi nyingine zilizochezwa leo asubuhi, Tanga na Morogoro zilitoka sare ya mabao 3-3 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe, Dar es Salaam.
 
Mkoani Pwani, Mara iliifunga Temeke bao 1-0 kwenye Uwanja wa Nyumbu wakati Kagera ililala bao 1-0 mbele ya Kilimanjaro katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Tamco.
 
Chanzo:
 

Mdau Ezekiel Marco wa The Kilimanjaro Institute of Technology - DSM Campus atangaza nia ..

Mr  Ezekiel   Marco
Mdau    Ezekiel   anakusudia kufunga  ndoa  yake  hapa  Dar  tarehe  19  August  2012  anaomba   maombi   yako   kufanikisha  jambo hili  ukiambatana  na  mchango  wako  wa  hali  na  mali.
   

Tunatoka mbali - Dogo akiendesha Fuso kwa fujo ...

We need to find kids who can play just like Pirlo


England 0 Italy 0 (aet, Italy win 4-2 on pens) 


 We must learn a lesson from this and do our utmost to produce an Andrea Pirlo of our own.
Let’s be fair to ourselves and the Italians and admit it’d have been an injustice had we won. They were by far the better team even though there is no one more patriotic than me.I am pinning a lot of hope on the new St George’s Park development centre and on coaches at every level in England.We must get our kids to play, play, play. Realise it’s not all about being strong, big or fast.Look at Pirlo against England — he had no pace, strength and he’s ancient. But what a fabulous display.

Comments by Harry   Redknapp
 Sources     http://www.thesun.co.uk/sol/homepage/sport/football/euro2012/4392781/Harry-Redknapps-England-verdict.html

© Copyright Daniel Blog in Contemporary News
Back To Top